Ujumbe wa kumwambia umpendaye kuwa ni pengo lisilozibika milele kwa hiyo asikuache
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
Nakupenda kwa kuwa umegundua thamani ya penzi langu
nakuahidi utafaidi utamu wa mapenzi yangu
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli,
lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe.
nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.
Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
moyo wangu saafi kama upole wa tausi wingi wa baridi kama maji ya mtungi ,yote ni kutokana na mapenzi unayonipatia. ASANTE KWA KUNIPENDA MPENZI
Recent Comments