Meseji ya kumuomba mpenzi wako akwepe fitina kwani unampenda sana
Moyo wangu unajua kupenda katu haujui kutenda
mpz, nakupenda tukwepe fitina mpz.
Moyo wangu unajua kupenda katu haujui kutenda
mpz, nakupenda tukwepe fitina mpz.
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo
mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe,
kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
mapenzi ni safari=unifanye nauli ya moyo, mapenzi ni
maradhi=unifanye daktari ni kutibu maradhi yako,mapenzi ni
kiu=niwe maji jangwani,mapenzi ni chakula=nikulishe
maishani mwako na uwe asali moyoni mwangu
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
Nakupenda mpenzi wangu, sifikirii kitu chochote zaidi yako
na kwa kuwa nakupenda sipendi kuwa na urafiki hata na
mwingine kwani atakuwa anabana nafasi niliyokuwekea wewe.
Noamba unipende nami nakupenda kila sikunde inayopita
maishani mwangu. Mwaaaaaaaaa
Recent Comments