Ujumbe wa kumwambia umpendaye kuwa ni pengo lisilozibika milele kwa hiyo asikuache
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo ningetelemka
na kuishia midomoni mwako, lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
Utakuwa wangu wa maisha daima na penzi le2 litakuwa km
mfuko wa hazina,2talitunza km zaidi ya mboni la jicho.
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
Kusumbuliwa na mlio wa simu yako, humaanisha kuwa muda
fulani, mahali fulani, kuna mtu anakufikiria muda huu, na
huyo ni mimi mara zote nakujali.
Mapenzi mazuri yanasifa zifuatazo, kuridhishana, kupeana
bila kubaniana, kubusiana, kuheshimiana, kujaliana, kusubiriana, kusikilizana. je utaweza kunifanyia yote hayo? nijibu mpenzi.
Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia
Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli
Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana
Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki
zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako
wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya,
tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.
Recent Comments