Ujumbe wa kimahaba kumwambia mpenzi wako kuwa mnafiti kuwa pamoja
Mvua na jua haviwezi kuwa pamoja, usiku na mchana
hazigongani, lakini mimi na wewe, hata wasemaje,
‘tunafiti’ kuwa pamoja.
Mvua na jua haviwezi kuwa pamoja, usiku na mchana
hazigongani, lakini mimi na wewe, hata wasemaje,
‘tunafiti’ kuwa pamoja.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu
usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee,
lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
mapenzi ni utoto,deka ulie nitakubembeleza,mapenzi ni
zawadi tabasamu nibusu niambie kiasi gani unanpenda,naweza
kusema asilimia kubwa jina lako limezunguka kuta wa moyo
wangu.kamwe jina lako haliwezi kufutika.nakupenda sana.
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikumbukapo kumbato lako,
nakupenda mpenzi
Ni ngumu kwa watu wawili kupendana wanapoishi Dunia
tofauti, lakini Dunia hizo zikutanapo na kuwa kitu kimoja,
hiyo ndiyo maana ya kuitwa wewe na mimi.
Uamkapo nitakupa langu tabasamu
Ukweli wa moyo utawale roho yako
Kwani macho yako ndo uzuri kwangu
Nakupenda sasa na milele kipenzi changu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Kumbuka kuwa wewe ni wangu
Kitulizo cha moyo wangu
Kwenye shida na raha
Wewe ni sehemu ya maisha yangu milele
Recent Comments