Ujumbe wa kuasa kuhusu upendo wa kweli
Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia
Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli
Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana
Rafiki wa kweli hudhaminiwa kama familia
Pendo la kweli humaanisha, kupenda kweli
Kumlinda, kumjali, kuvumilia na kusameana
Mpenzi huwa unanipagawisha unaponipumulia pumzi masikioni
nasikia raha.
Niliandika upendo wangu kwako kwenye majani ng’ombe
akala,nikaandika kwenye jiwe mvua ikafuta ,nikaandika
kwenye sms likafutwa lakini nimeandika moyoni mwangu
halitafutika kamwe.
Mpenzi wangu T tambua kuwa ulimwengu tunaoishi una mambo
muhimu matatu. Jambo la kwanza ni kumpata umpendaye, la
pili ni kupata atakayekupenda la tatu ambalo ni kubwa
kuliko yote ni kwa jambo la kwanza na la pili kuungana
pamoja.Nashukuru nimekupata wewe nikupendaye, naomba unipende na uungane name
Watu husema kwamba, awapo mtu mmoja tu akupendaye, maisha
hayajapoteza maana, kwa hiyo, ukijihisi mpweke hauhitaji
kuishi nikumbuke mimi.
Fungua macho yako uone kopa za mahaba ninazokumwagia,
fungua mikono yako na upokee mapenzi yangu,
fungua simu yako uone ni jinsi gani ninavyokukumbuka japo
kwa kukutumia sms mpenzi wangu,
Nakutakia usiku mwema
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Nakupenda sana P tafadhari usinikasirikie, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu, njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu,
huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili
mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU.
Mchana mwema
Kumbuka kuwa wewe ni wangu
Kitulizo cha moyo wangu
Kwenye shida na raha
Wewe ni sehemu ya maisha yangu milele
Usikimbie nyuki ukakosa asali, utamu wa samaki ni kula na wali, usizidishe siki akawa mkali. Ni mimi niliye na dhiki nakujulia tu hali.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments