SMS Nzuri: Meseji za Vituko Vya Kukupa Mudi Mpya

Ndege ya Tanzania

Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:

Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!

Kuna watu makauzu ila huyu kazidi.. Soma hii!

Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli.
Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye……
Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji.
“Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!”
Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..

Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.

“CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5”

Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji.
“BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI”

#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……

Cheki nilichomfanyia boss wangu

Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..

Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamake😀😀😀😀😀😀😀

Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli

Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma barua
Ikisema yan.mwanangu tumapata shida maana shamba halijalimwa na jatujii litalimwaje na msimu ndio huo nataman.ungekuwepo ningepata msaada wa kulimiwa hili shamba

Yule kijana alijibu tafadhal baba usilime hilo shamba maana pesa zote nilizo ibwa nimeficha.huko

Kwakuwa barua zote laxima zipite kwa mkuu wa gereza ndio xiende kwa muhusika kesho yake mzee alikuwa shamba lote limelimwaa na polisi

Akatuma ujumbe tena yule kijana
Nashukulu umepata msaada sasa nazan unaweza ukaendelea kupanda mazao shamban.kwetu😂😂😂😂😂

Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake

Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.

Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?

Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.

Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Shopping Cart
21
    21
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About