Cheki huyu mtoto anachosema
sijui hili toto langu nilipeleke wapi, Leo limetoka shule eti nikaliuliza BIBILIA kwa kingereza inaitwaje likaniambia GRANDMOTHER CRY
π π π sijui nikabadilishane na kijiko cha chumviπ€π€π€
sijui hili toto langu nilipeleke wapi, Leo limetoka shule eti nikaliuliza BIBILIA kwa kingereza inaitwaje likaniambia GRANDMOTHER CRY
π π π sijui nikabadilishane na kijiko cha chumviπ€π€π€
Trafik mlevi alisimamisha gari Mama akapaki pembeni akaona trafik anakuja akiwa anayumba! Alipofika akasema, “naomba leseni yako.”
Mama akasachi mkoba Wake akatoa kioo kidogo cha kujtazama akampatia! Trafik akakiangalia kwa dakika 2
Akasema sasa si ungesema kama wewe ni trafik mwenzangu!
Haya nenda
Ulevi sio mzuri
ππππ
Angalia kilichotokea
Walevi wawili waliokota kioo, mlevi wa 1 akaangalia muda mrefu kisha akasema “hii sura sio ngeni machoni mwangu sema jina tu silikumbuki..! !!
Mlevi wa pili akamnyang’anya kisha nae akaangalia kioo akasema “wee kweli huna akili, si mimi huyu? halafu unajidai hunikumbuki β¦!!!
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
π² π²
Akikuta PESA wakati anafua atapiga kimya kimya, sasa ngoja akute umeacha CONDOM ndo utajua kama umeoa KIPAZA SAUTI ππππππ
Ndio maana mimi nafungaga condom na hela kwa pamojaβ¦ akivikuta anachukua hela na kuishia kusonya tu.. πππππππ
Huwa sipendagi ujinga Mimi
ππ kweli nimeamin mitandao inahribu watu
Leo kuna jamaa kamuona Dada akipita barabaran kapendeza jamaa kamwendea Dada akamwambia!
Dada nice photoΒ ππππ
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!β¦
MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”
MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”
MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”
HABARI MPASUKO..
jana katika taasisi ya wanyama pori ya Nat Geo ilitangazwa kuwa ametokea Nyoka hatar san Ambaye hajawah kutokea duniania.. wanadai kwamba nyoka huyo anaongezeka ulrefu wa 0.5sm kila akila chakula na huwa anakula chakula kuanzia sekunde 30 kurudi nyuma.. mpaka sasa hakuna siraha ya kuweza kumuua nyoka huyo isipokuwa akiji uma mwenye ndo anaweza kufa, wanasayansi hao walieleza japo uchunguz zaid bado unaendelea⦠huyu ni nyoka anayeua kuliko nyoka wote waliowah kutokea katika historia ya maisha ya mwanadam..
nyoka huyu hupatikana katika simu pekee za nokia toch katika sehem ya game inaitwa snake xenzia..
asanteni kwa kufurah na umakin mkubwa katika usomaji wa matini hiiβ¦
haya ni mambo ya wikiend jaman na iwe njema kwenu wote
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJEβ¦
mke wa laki sita
unalala nae ndaniβ¦.
BANGI SI NZURI JAMAN
ππππππππ
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enheeβ¦
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesomeβ¦
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kulaβ¦.
GIRL: Enheeβ¦na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamasβ¦.halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheartβ¦halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Mchumba wangu amenialika kwao nikawaone wazazi wake lakini akaniambia nisiende mikono mitupuβ¦
Nikaamua kuvaa glovesβ¦
Sipendagi aibu ndogo ndogo ukweni.πππ
USIJIONE MJUAJI SAAAAβ¦NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani.
kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia “hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani”
mama”hee embu tuoneshe mwanangu”
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu “ngapi?”
wazazi”moja” akainua wa pili “ngapi?” wazazi “mbili”
akawarudisha akisema”wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani”
baba”mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA”
Recent Comments