SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Mchana Huu
Jamaa amkomesha boss wake
Kuna jamaa alifutwa kaziβ¦
Ikawa kila siku anaenda nyumbani kwa boss wake na kunya mlango wa mbeleβ¦ Ikawa hvβ¦
boss: _mbona waja kunya kwangu?_
jamaa: _nataka kukuonesha kuwa silali njaa_
πππππππππππππππππ
Kilichompata huyu anayependa kusoma SMS za watu kwenye daladala
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochatiβ¦
Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyuβ¦. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext:Β “Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomuπ£ lilipukeβ¦ najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sana⦔ Yule jamaa akajirusha dirishaniβ¦β¦ππ
βkwani mi napenda ujinga xx πππππππ
Ndege ya Tanzania
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Angalia Kiingereza kilivyoniponza
Shikamoo kingereza..!
Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!
Price: TSH 44,000/=
Nikaagiza!
Nilipoletewa ndio nagundua kwamba:Β ni makande na parachichiΒ ..π€
hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezoπ€π¨
Angalia mchezo wa kutuma message mara zikubali mara zikatae.. Lilishakukuta hili???
GARLFREND»»hellow sweetheart
BOYFREND»»hellow darling(SENDING FAILED)
GARLFREND»»kwanin hutaki kujibu sms yangu,au huna mda»??
BOYFRENDΒ»>najitahid kukujibu lakin mtandao unasumbua,imefika??(SENDING FAILED)
GARLFREND»»kama hunipend bhas usinijbu,kama unanipenda kwel bhas nijibu
BOYFREND»»i love you (SENDING FAILED)
GALFREND»»do you lov me????
BOYFREND»»i lov you baby(SENDING FAILED)
GARLFREND»»usiongee na mimi tenaaaaa
BOYFREND»»i love you sweetieeee(SENDING FAILED)
GARLFREND»»unataka mim na wew tuachaneee????
BOYFREND»»nshachoka mie na huu upUmbavu,shenz (MESSAGE SENT)
πππππππππππππππππππππππππππ
Cheki hawa wachungaji
CHEKA KIDOGO
Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.
MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.
WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.
WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:
We vp unatatizo gani mbona unalia???
AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!
πππππππ»ππ
Je, Chuoni kwako Kukoje?
FACT!
1.Ukiona geto lina feni, sabufa, meza ya plastic na kitanda ch sita kwa sita na Pc UJUE ni jamaa wa UDSM.
2. Ukaona geto lina nguo nyingi za watu tofauti tofauti, unga mwingi, vtunguu vng, nyanya halaf pembeni, Vitabu vya kutosha na lundo la karatasi za betting ujue huyu JAMAA ni wa SAUT.
3. Ukaona geto halina kitu ndani zaidi ya mkate wa bakheresa na kopo la maji UJUE huyu jamaa ni wa UDOMπβ
4. Ukaona geto lina visamaki vikavu mezani, Notes za kutosha mezani na jaba pembeni UJUE huyu ni MJAMAA WA MWENGE/MWECAUππ€
5. Ukaona geto lina Mawigi mengi na dressing table pembeni, ngazi ya kuwekea viatu UJUE huyu mjamaa ni wa RUCO IRINGAπ
6. Ukaona geto lina spray za kila aina, Nguo nyingi hasa za mitumba ambazo zimemodolewa mpaka tight UJUE huyu MJAMAA ni wa USHIRIKA MOSHI.
7.Ukiona geto lina Nyanya na mikungu ya ndizi halafu halafu nje kuna jiko la Mkaa UJUE huyu mjamaa ni wa TEKU mbeyaπ³
8. Ukiona geto lina tranka na nje wamevulia buti, viatu vya matope UJUE huyu Mjamaa ni Wa SMUCO MWIKA.
9. Ukaona geto ndan mashuka ya kimasai kinabao, hapa usipatwe na Mashaka, Jua huyu ni Mjamaa wa MAKUMIRA. ππππ
10. Ukaona geto lina vimodo, vimini, miwani za tittled, jiko la mafuta ya taa, kitandani mito zaidi ya Minne,Visarafu kwenye meza, Tshirt nyingi za semina za family planning, Ukimwi n.k halafu chini tv ya chogo na king’amuz cha continental Ujue huyu MJAMAA ni wa TIA DSM π±π±π±π±π±π±π±
β¬β¬β¬β¬β¬β¬β¬β¬β€΅β¬ππππ
JE, KWAKO KUKOJE? ???
πππππππππππ
Kwa nini watu hawapendi hesabu!! Sababu hii hapa!
Sababu ni hii
AL-SHABAB
AL-QAEDA
Kwenye MATHEMATICS pia kuna kundi linaitwa
“AL-GEBRA”
ππππ
πΆπ»πΆπ»πΆπ»πΆπ»πΆπ»πΆπ»
Kumbe ndo maana wengine hawapendi hesabu coz kuna element za ugaidi
Angalia huyu mvulana anachomwambia huyu daktari baada ya rafiki yake wa kike kupata ujauzito
ππππ
MVULANA:Β Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?
DAKTARI:Β Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!
MVULANA:Β Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.
DAKTARI:Β Nashukuru umeelewa somo!!π
πππππππππππππππππ
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Huyu mme ni shida
MKE..mume wangu unaweza kuua simba kwasababu yangu???
MME: Hapana mke wangu, sema kingine
MKE:unaweza kunipa nione watsapp yako nione msgs?
MME: Haya sema huyo simba yukwap nikamuue
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupoΒ kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskiaΒ i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
πππ
Β
Angalia anachokisema Madenge sasa
MWALIMU kaingia darasani na kusema. “Wanaojijua wajinga wasimame”.
MADENGE akasimama peke yake.
MWALIMU: Wewe ndio mjinga?
MADENGE: Hapana, ila nimeona umesimama peke yako nikaona usijisikie vibaya angalau tuwe wawili.
Hizi sifa zimezidi sasa
MADEM KWA SIFA..
kuumwa aumwe yeye lakn kujifanya anajali sana bas utamsikiaΒ BABY KARIBU TUMEZE DAWAΒ πππ
Cheki kilichotokea baada ya kufumaniwa
Nimefumaniwa hapa na jamaa ameniambia nitulie tuyamalize kishikaji, yaani nisijali sasa ametoka nje nasikia ananoa kisu nadhani anataka anichinjie kuku!
WATU WENGINE WANA ROHO NZURI!ππππ
Status za Whatsapp za Wazungu na Wabongo
STATUS ZA WAZUNGU kwenye Whatsapp vere vere kliaaaβ¦
πsick
πat movieΒ π in a meeting2
π kind of happy,, πbusy,,
πavailable
πDriving
πsleeping
STATUS ZA WABONGO SASA MBUTA NANGA MBONGO NGAFU
“Akutake nani una shepu la Kitorondo utaishia kumegwa na kuachwa
“Watu tuna nyota za Chips Mayai sio wewe mwenye Nyota ya Punda,halulaaa”
πKantangazeee ndo Kwanza naanza na ntakukomesha Mwanaharamu we!
π I love yu so much ur my only one,No one lyk yu and I mean it πΆ Yu ma numba1 ma sweet sweet namba1 roho yangu mama,,
π Asante π vimenitoshaaa tena kama ulijua πππππ,
πͺ unajifanya simba kumbe nyau mimi ndo maji kama hujanioga utaninywaa,
π nauza Ubuyu kwa bei nafuuu kama unataka inbox me plz
π poleee jaman utapona wangu,,,
πͺ utalijua jiji na chuki zako walingia na tako wakati hadi nyani analo kitu sura dadaβ¦
π‘ usinisemeshe usiniongeleshe tena utaniambia vizur ulikuwa wapi..
π· mdomo kaumbiwa mwanadamu ongeeni nyie me sijali ya wanafiki nafanya yangu huna hadhi ya kujibiwa na mimi
pamoja na ya kwako ulowekaππππ
Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka machoπ, akaenda hospital akawekewa macho ya pakaππ±,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
πππππ
Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!
Angalia hivi
-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi
-Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave
kichwani.
-Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima
itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji
Magari.
-Lazima waende Kununua nguo.
-Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani.
-Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi
ama kitandani.
-Actress huwa hawapiki hata chai.
-Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima
avae nguo inayoishia mapajani.
-Actress even after 5 yeas utakuta staili ya
nywele na rangi za kucha ni zile zile.
-Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea.
-Movie zote wapenzi huitana Baby..
-Main actor wote ni wafanya biashara na lazima
wataongelea mizigo kutoka bandarini.
-Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.
Angalia uhuni wa huyu dereva
Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,”nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?” Trafki akamwmbia, kwanin ucngeenda upande ambao una watu wachache ili uokoe wengi? Jamaa akajibu, “nilifanya hivo, huku kushoto alikua m1 na kulia walkua wa4, nikamfuata uyu wa kushoto et akakambilia upande wakulia akazani cjamwona, nikamfata huko huko alipoenda, nikampa kitu mbwa yule”
Recent Comments