SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Kukubadilisha Mudi

Angalia huyu secretary anavyomjibu bosi wake

Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:

SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwako…

Boss akabaki anashangaa… Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.

Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:

BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki au…?

SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili

Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!

JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.

Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,

Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…

MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…

MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…

MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!

MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.

Chezea mawaifu walokole wewe!

Stori za simu za wavulana na wasichana

STORY ZA WASICHANA KTK SIM

Mary… Hallow mpenzii
Lily…. Niambie my dear
Mary..Pouwaa za siku jamani
Lily…Nzuri rafiki Yangu wa damu
Mary…Jioni nakuja kwako tule Na
kunywa japo wine wanguu
Lily…Nakusubiri kwa hamuu
mpenziiii

BAADA YA KUKATA SIMU…KILA
MMOJA ANAWAZA

Lily…Huyu mchawi wa kike Leo
anataka kuja kwangu wala hanikuti.
Mary..Hahahahaaaa Uwiiiiiiiiii huyu
kahaba eti nakusubir Kwa hamuu
nani aende!!!

STORY ZA WAVULANA KATIKA SIMU

John…Niaje we mbwaa
Sam…Pouwa kichaa wanguu
John..Upo wap mpumbavu wewe
Sam…Niko hom, we fala Uko wap?
John..Baadae nakuibukia jambaz
langu tukale bata
Sawa… Pouwaa we ms**nge
nakusubiri

BAADA YA KUKATA SIMU…KILA
MMOJA ANAWAZA

John…Dah baadae nikakae na
mwanangu Sam sijamuona long
time
Sam…John bwana akiwa Na pesa
lazima anitafute mwanaeee.

FUNZO..

Baadhi ya Wasichana
hujifanya wanapendana Kwa
maneno lkn ni Kwa nje tu!! lkn
WANACHUKIANA
WAVULANA unaweza Kudhani
hawapendani Kwa Maneno lkn
WANAPENDANA..

Mpe TANO mchizi wako kudumisha upendo wetu wavulana…
High 👊👊👊👊👊 boys

hiyo apo

Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki

Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea…”

“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?”

Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”

Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”

“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?”

Kimyaa….
“Padri yesu atanisamehe?”
kimya….

Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.

Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu…….”

Utani wa wahindi, cheka kidogo

Mhindi afaulu mtihani wa Kiswahili

(1) Mfa maji ?……………….. Tampa life jacket.
(2) Mwenda pole?………… Tachelewa fika.
(3) Usipoziba ufa ?……….. Mizi taona mpaka dani.
(4) Usilolijua ?……………… Uliza google.
(5) Mbio za utelezini ?……. Chafua guo yako.
(6) Ukipenda boga ?……… Ngoja mezi ya ramzani tapata.
(7) Ukiona vinaelea ?…….. iko nyepesi hiyo.
(8) Maji yakimwagika ?…… Mambie dada tapiga deki.
(9) Chelewa chelewa ?……… Takosa guo ya sikukuu…
(10) Kila ndege ?………….. …Hutua Airport
(11) Bandu bandu ?….. …….Rafiki yake Jecha
(12) Mtaka cha Mvunguni ?… Ondoa tanda
(13) Simba mwenda kimya?….Kama sio gonjwa basi haina njaa.
(14) Aisifuye mvua ?………. Najua iko Mkulima hiyo
(15) Barabara ndefu ?…….. Ongeza mwendo au tachelewa fika.
(16) Mlanawe hafi nawe ila?…. Takimbia
(17) Asie sikia la mkuu ? …….. Tapeleka jela
(18) Hasira za mkizi ? …………..Tatafuna veve
(19) Mchamba wima ?…….. Karibu ya Hurumzi
(20) Akumurikae mchana ?….Kipofu hiyo
(21) Mficha maradhi ?…….. Taenda Loliondo
(22) Mkataa wingi ? ……….Taenda Chadema
(23) Bendera ?……………. Kama sio ya CCM, ya CUF
(24) Baniani mbaya ?……. Peleka Bombay Lakini sio HB kweli, naonea tu
(25) Akili nyingi ?………. Tapasi mtihani yote
(26) Penye kuku wengi ? …….. Chija bili tatu ivi, hapana mtu najua.

Unakumbuka hizi enzi za utoto?

Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika

1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : 🗣Joniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule

2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: 🗣 we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama

3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: 🗣 Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
😂😂😂😂😂😂

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About