SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Kisasa
Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi
HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI
jaribu kumwita mpenzi wako “my sweet potato” atakuelewa ila mwite kwa kiswaili ” *kiazi wangu mbatata*”hiyo itakuwa vita ya tatu ya dunia😁😁
Wazo la jioni hii
📢WAZO LA JIONI HII 📢
KAMA MWAKA JANA ULIPIGA HATUA NA HUJAFIKIA MALENGO MWAKA HUU PIGA MSAMBA😝
Mchaga aliyemshangaza Mungu
Mchungaji anawaambia waumini: Fanya jambo moja la kumshangaza Mungu…
Dakika mbili nyingi Mchaga akakimbia na kapu la sadaka
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Cheki nilichomfanyia boss wangu
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallah…!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Dingi kauzu kuliko wote duniani ndiyo huyu hapa
Mtoto: Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.
Baba: Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwanangu…..
Dogo alivyomchomea dada wa kazi kwa mama yake kuhusu baba
Dogo: mama hivi malaika si wanapaa?
Mama: ndiyo wanapaa, kwanini umeniuliza hivyo?
Dogo: nimesikia baba jana anamuita dada (housegir) malaika wangu, kwa hiyo nae atapaa?
Mama: ndiyo atapaa kuelekea kijijini kwao kesho, pumbavu zake.
Wanawake wanavyopenda hela, hadi kutoka kwa nyani na ngedere
Kama Nyani na ngedere wangekuwa na pesa…
Trust me Kuna wanawake wangekuwa wanaishi misituni mda huu…..
Wanavyopenda hela
😂😂😂😂😂😂😂😂
Huyu Baba ni noma, Cheki anachomjibu huyu mtoto wake
Mtoto: baba eti Botwasna ipo wap?
Baba: angalia itakuwa humo humo kabatini maana mama yako nae kwa kuficha kuficha vitu hajambo…
Angalia huyu mwalimu alichokifanya
Mwalimu aliingia darasani akiwa amechoka kinoma
akawambia wanafunzi.
‘leo tutajifunza kipindi cha
dini ” wanafunzi wakiwa wanajiandaa ili kuendelea
na kipindi mwalimu akajiegesha kwenye kiti klichokua
karibuu yake baada ya dakika kadhaa mwalimu alipitiwa
na usingizi, ghafla alingia mkurugenzi na
kusimama pembeni mwa kile kiti alichokalia mwalimu
ghafla kmya kikatawala darasani kiasi cha kunfanya
mwalimu ashtuke usingizini aliamka huku akipiga
miayo alpotupa jicho pembeni alimuona mkurugenzi
kasimama pemben! akiwa anababaika alifungua
kinywa na kusema ‘ Hivi ndivyo walivyolala wanafunzi
wa YESU walipokua wakimsubli kule mlimani, je
kuna mwenye swal? mkurugeni pale alipokua
akapiga makofi na kumsifia mwalimu kwa kufundisha
kwa vitendo.
Je % Ngapi unampa mwalimu kwa
kusolve kibarua chake.????
Angalia Kiingereza kilivyoniponza
Shikamoo kingereza..!
Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!
Price: TSH 44,000/=
Nikaagiza!
Nilipoletewa ndio nagundua kwamba: ni makande na parachichi ..🤔
hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo🤒💨
Angalia walichofanyiana hawa wanadoa, Kati ya huyu mme na mke nani zaidi?
MUME wakati anakata roho huku mkewe akiwa amemshikilia alisema mke wangu, mi natubu kwako, kwani nilifanya mapenzi na dada yako, mdogo wako, rafiki yako na mama yako
MKE akamnong’oneza mume wake na kumwambia mbona mimi nayafahamu yote, ndio maana nimekupa sumu ili na wewe ujue uchungu wake. JE NANI ZAIDI?
Huyu mwanafunzi kweli kiboko
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` 😂😂,😂😂
Kilichotokea baada ya kuzamia sherehe
Pale unapozamia kwenye Dinner Party ya Jumuiya Fulani, sasa Lengo la Jumuiya hiyo ni kupata Fedha za kutunisha Mfuko wa Jumuiya…sasa unakakaa mbele kabisa ili Muda wa Msosi usichelewe na kukuta kwenye Buffee yamebaki maharage!
MC : “Papai zuri kabisa kutoka Newala, Papai Mwendokasi, hili ni Shilingi laki 1..jamani Papai,nipeni ofa!”
MOSHA : “Laki 3 hapaaa!”
“Jamani laki 3 pale kwa Mosha, Papai linaondoka jamani, papai hili ni self contained kabisa….papai jamani”
KIBOLIBO: “Milioni 1 hapaaa”
“Jamani Mambo yanazidi kunoga hapa!…Benedict Kibolibo anataka papai kwa milioni 1 jamani, linaondoka papai!”
RWEYEMAMU : “nitanunua Papai hilo kwa Milioni 5”
Haya sasa jamani Rweyemamu ametoa ofa ya Milioni 5 Jamani, nani mweingineee?”
Kimyaaa…
Haya jamani Papai kama hakuna Ofa basi Papai linakwenda kwa Rweyemamu!……..haya sasa Kuna Kuku hapa Jogoo kabisa, bei yake ni laki 6 jamani Jogoo twitter huyu!”
WEWE “Milioni Mojaaa!”( hapa umejiwahi wa kwanza na wewe uonekane upo huku ukijua kabisa Wakina Mosha na Rweyemamu lazima watampandia Dau Jogoo, tena dau kubwa”
MC: ee sasa Kumekucha Jamani, Kabasele anamtaka Jogoo kwa Milioni 1 jamani!….ofa nyingineeee!”
Kimyaaa…
Jamani Jogoo anakwenda kwa Kabasele jamani!…ofa nyinginee!
Kimyaaa….
Kimyaaa….
😝😝😝…hapa sasa ndio mfukoni kuna Buku jero,..huko kwengineko NMB nill balance…sasa unageuza mimacho kumtazama Mosha kama atapanda dau kwa jogoo👀(mama wee Mosha anachezea Simu!)…..unamtazama Rweyemamu (teh anatafuna Kuku)…..mama weee😝
MC: Haya jamani kama hakuna Mwingine basi zoezi letu liishie hapa na limekwenda kwa Mafanikio, Mpatieni Kabasele Jogoo wake!
Hapa sasa unapokea jogoo wako wa MILIONI kwa Tabasamu la Maiti….kule nyumbani Jogoo wako Mkubwa unauza elfu 20 lakini sasa haka kajogoo kapya Mkononi kanakuwa kazito utadhani umembeba John Cena👀…Mama weee hapa sasa vidari ulivyotafuna unaviona kama vimerudi kwenye Ulimi….Chicken wings zinataka kutokea Masikioni…..Uuuuwiiiii,😝😝😝
Na hapa sasa kabla Dinner haijaisha ndipo unapojikuta Umebuni Cocktail ya Sparetta na Tomato😂😝😝😝😂.
chiel wie okee
Wanaume ni noma, Angalia huyu alivyomdanganya huyu 👧 girlfriend wake
Jamaa kamdanganya girlfriend wake kuwa anasomea HOTEL MANAGEMENT. Siku huyo girlfriend akamkuta jamaa anaosha vyombo kwa MAMA NTILIE.
Girlfriend akamuuliza jamaa “beby vipi mbona uko hapa?” Jamaa bila woga akajibu “NIPO FIELD.
Wanaume hatupendi ujinga sisi 😠😠😠
Wanaume wote ni waaminifu
Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.
Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.
Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?
Jamaa: NDIYO.
Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.
Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?
Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.
Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”
Jamaa: NDIYO.
Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?
Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!
Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.
*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.
WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
😀😀😀😀
Angalia haya mazungumzo ya msichana na mvulana, mapenzi ya ajabu haya
Demu: Hny mambo jamani!
Man: Safi nipe habari wangu wa moyo
Demu:Wafanya kazi gani vile wangu?
Man: Ni fundi wa kufunga ATM
Demu: Wow dont tel me i love you myn mwa mwa mwaaaaah
Man: Mbona wafurahia?
Demu: Nami natamani kuja kufanya kazi za kibenki.
Man: Itakua poa sana nami natamani pia
Demu: Hee si umesema wafanya kazi ya kufunga ATM?
Man: Hukunielewa mie ninafunga mashine na za kunulia condom kwenye bar
Demu: nipishe huko
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.😃😃😃😃
Recent Comments