Meseji ya kumsifia mpenzi wako kuwa ni mzuri
Swt ulivyoumbika wengi wanateseka juu yako ,najua
wanakusumbua ni vema usiwakubalie, ukweli umebarikiwa
uzuri umeshushiwa na dhati ya penzi umetunukiwa nakupenda
Swt ulivyoumbika wengi wanateseka juu yako ,najua
wanakusumbua ni vema usiwakubalie, ukweli umebarikiwa
uzuri umeshushiwa na dhati ya penzi umetunukiwa nakupenda
Moyo wangu unajua kupenda katu haujui kutenda
mpz, nakupenda tukwepe fitina mpz.
Natambua ugumu wa mapenzi
Mengi ni matamu, mengine ni machachu
Ila nakusihi usikate tamaa ya kunipenda kimoyo
Ikiwa penzi langu kwako litakufa halitazikwa,ikiwa moyo
wangu ni mwandiko hautafutika na kama dhati yangu ni
machozi daima hayatokauka na wewe kwangu ni damu ngozini
haitochuruzika ila mishipani… .
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee, lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Nakupenda kwa kuwa umegundua thamani ya penzi langu
nakuahidi utafaidi utamu wa mapenzi yangu
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na
furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara
nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa
kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu
anayekujali.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Recent Comments