Ujumbe wa kimahaba kumwambia mpenzi wako kuwa mnafiti kuwa pamoja
Mvua na jua haviwezi kuwa pamoja, usiku na mchana
hazigongani, lakini mimi na wewe, hata wasemaje,
‘tunafiti’ kuwa pamoja.
Mvua na jua haviwezi kuwa pamoja, usiku na mchana
hazigongani, lakini mimi na wewe, hata wasemaje,
‘tunafiti’ kuwa pamoja.
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?
Mapenz hayana msimu walam majira isipokuwa ni kama majani yaotayo popote kwani siyo mimi ni msukumo na hisia zangu. Nakupenda sana
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na maumivu yake ndani yangu.
Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.
Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa wakwe zangu,
unajua ni kwa nini? Ni siku waliyokuleta kwenye hii dunia,
happy birthday mpenzi!
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua
furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu
nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu
tabibu ,we ndo wangu wa manani.
Tambua kuwa nakujali
Furahia kwamba nitakuwa na wewe
Katika siku zote za maisha yangu
Nitakupenda bila kikomo milele
Recent Comments