Ujumbe wa mapenzi kwa umpendaye kwa dhati
Nakupenda usiku na mchana Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Nakupenda usiku na mchana Nakuwaza siku zote za maisha yangu
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Mapenzi ni magumu na yatabaki kuwa hivyo, lakini kumbuka
kuna akupendaye naye ni MIMI!.
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu, huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU. Mchana mwema
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo
mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe,
kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
“Mimi sitaki kuwa kila kitu kwa kila mtu, lakini napenda
kuwa kitu kwa mtu.na mtu mwenyewe ni wewe”
nakupenda laazizi
“Kama mimi nilikuwa na maua kila wakati
mawazo yangu
yangekuwa juu yako,nisingefikiri wa kumpa mwingine kabla
yako je wewe ungekuwepo nayo
ungempa nani kwanza? “
, – .(. – .
‘. .’
‘ . . . ‘ Napenda tunda hili likupoze makali uliyo nayo moyoni, Nimeliosha kwa maji safi na salama kwa ajili yako lipo tayari kuliwa.
“APPLE” Ni tunda lenye ishara ya UPENDO, AMANI & FURAHA. napenda liwe zawadi kwako siku hii ya leo.
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Recent Comments