Meseji ya pongezi kwa mpenzi wako
pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la
mapenzi,ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili
chumbani.penzi lako halichakai daima huzaliwa upya.
pongezi kwako mpenzi kuwa wangu mtetezi kwenye jahazi la
mapenzi,ufundi na ujuzi unao hasa tuwapo wawili
chumbani.penzi lako halichakai daima huzaliwa upya.
Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na
maumivu yake ndani yangu.
Imani hufanya mambo yote yawezekane, Matumaini hufufua
yaliyopoteza uhai, lakini mapenzi hufanya mambo yote
yaonekane mazuri. Sina linalonihuzunisha maishani mwangu
kwa kuwa tunapendana!
Kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikumbukapo kumbato lako,
nakupenda mpenzi
Uzuri wako hung’ara kuendana na matendo yako,
Ushupavu, upole, ujasiri na uchambuzi wa kweli,
kwa yote yajayo mbeleni mwako.
Tone la mvua huonekana dogo sana, lakini kwa mwenye kiu hulisubiri kwa hamu kubwa. Sms ni kitu kidogo, lakini huonyesha mahali fulani yupo mtu ANAYEKUPENDA, ANAKUKUMBUKA, ANAKUOMBEA,
ANAKUJALI na,
ANAKUTAKIA mafanikio mema
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo, suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni, nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!
mapenzi ni utoto,deka ulie nitakubembeleza,mapenz ni
zawadi,tabasamu,nibusu niambie kiasi gani
unanipenda,naweza kusema asilimia kubwa jina lako
limezunguka ukuta wa moyo wangu,na kamwe jina lako
haliwezi futika.
NAKUPENDA
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
Recent Comments