Meseji ya kumtumia mpenzi wako anapoonyesha kukupenda
Nakupenda kwa kuwa umegundua thamani ya penzi langu
nakuahidi utafaidi utamu wa mapenzi yangu
Nakupenda kwa kuwa umegundua thamani ya penzi langu
nakuahidi utafaidi utamu wa mapenzi yangu
Umbo lako kama sayari, lizungukapo umbile la jua
ni kama upendo wa thamani usioweza kuuzika.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
ni bora mnara ukitikisika kuliko kupata pengo lisilozibika
moyoni umeniachia jeraha lisilotibika na ufa
usiozibika.rudi mpenzi unautesa mtima wa moyo wangu.
tunda langu laangaliwa hawajui nilipoli chuma,
utamu wake maridhawa,hakika utalipenda.si mpi tunda langu mwingine na lila mwenyewe.
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
Pendo la kweli ni hisia zilizomo moyoni ambazo sauyi yake haisikiki isipokuwa kwa akupendae kwa dhati. Nakupenda mpenzi wangu.
Recent Comments