Ujumbe wa mapenzi wa kumpa umpendaye thamani kubwa
Umbo lako kama sayari, lizungukapo umbile la jua
ni kama upendo wa thamani usioweza kuuzika.
Umbo lako kama sayari, lizungukapo umbile la jua
ni kama upendo wa thamani usioweza kuuzika.
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani
nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi
kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali
hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Simu huboa wakati mwingine, kwani ni lazima ufungue meseji
na kuzisoma, kuichaji simu kila mara, lakini usichoke
kwani ndiyo inayotuwezesha tuwasiliane
moyo wangu saafi kama upole wa tausi wingi wa baridi kama maji ya mtungi ,yote ni kutokana na mapenzi unayonipatia. ASANTE KWA KUNIPENDA MPENZI
mahakama ya upendo iliyopo mtaa wa busu imenihukumu
kufungwa kwenye gereza la moyo la mcchana huyo milele kwa
kuutesa mtima wa moyo wa mcchana mmoja ,asiye na
mashauz,mwenye wing upendo ,maneno matamu ,mahaba ya dhat
na mapenz mazito zito,
Naomba upokee zawadi hii ya kiwembe.
Amini ndicho kilichotumika kufanyia operation kwa
kupasuliwa moyo wangu, kwa sababu nimeoza kwa ajili yako,
nimeambiwa ili
nipone maradhi haya nipate:- (1)ushirikiano wako (2)furaha yk, (3)upendo wk, (3)tabasam yk.
Je! uko tayari kuokoa maisha yangu?
kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikukumbukapo kumbato
lako,nakupenda mpenzi
Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jembe la KUSAMEHE, iwekee mbolea ya AMANI, ipige dawa ya NENO LA MUNGU, itakayoua wadudu wote waharibifu kama ubinafsi, chuki, wivu, dharau, unafki, kiburi, choyo, tamaa na fitna kwenye mmea huu, MMEA HUU (UPENDO) UENDELEE KUWA MCHE BORA KULIKO YOTE KTK MAISHA YAKO SIKU ZOTE.
Recent Comments