Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako kumuonyesha upendo
yapitayo mdomoni yametokea moyoni ,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
yapitayo mdomoni yametokea moyoni ,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
Kila niamkapo mawazo yangu huwa kwako na upepo uvumapo
huhitaji uwepo wako na hasa nikumbukapo kumbato lako,
nakupenda mpenzi
Wanasema mtu huanguka katika mapenzi mara moja, jambo
ambalo mimi naliona si la kweli kwa maana kila
ninapokutazama najikuta nakupenda tena na tena.
Wewe pekee upo moyoni mwangu, nitaendelea kukupenda siku
zote za maisha yangu! Katika siku hii ya wapendanao, wewe
ndiyo ua la moyo wangu!
mapenzi si pombe lkn yanalewesha, wala si kidonda lakini
yanatonesha,wala si maradhi lakini yanaumiza, wala si
njaa lakini yanakondesha ,mapenzi ni uvumilivu kwa
unaempenda
mpnz wangu ninavyo jua mm huwezi kutupa mawe kwenye mti
usiokuwa na matunda mazuri maana hivyo basi tambua ww ni
mrembo xanandani ya moyo wangu usiniache pekeyangu kwani
na kupenda xana tabua hilo mpnz wangu
hakika kama ni mume MUNGU kanipatia,kuwa nawe najiona
kama malkia ,nakupenda mpz na daima nitaenzi penzi
lako.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki
zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako
wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya,
tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.
Recent Comments