SMS nzuri ya kumtumia umpendaye kumwambia unavyompenda na kumridhia
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhia… .nakupenda daima mpenzi!
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhia… .nakupenda daima mpenzi!
Kuna bahari kati yetu. Misitu na milima inatutenganisha,
mimi si ‘Supamani’ lakini nipe sekunde moja nitavuka nchi
nyingi kukutumia mapenzi yangu. Umeipata hiyo? Pokea mapenzi yangu japo uko mbali.
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na
furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara
nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa
kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu
anayekujali.
Maji hunitosha nisikiapo kiu, chakula hinitosha nisikiapo njaa, lakini wewe hunifaa kwa kila kitu!
Je unakubali au unakataa kwa mujibu wa sheria ya mahakama
ya mapenzi kifungu cha mahaba unahukumiwa kuwa na mimi
milele,unaweza kukata rufaa kama hujatendewa haki.sawa?
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako
Safarini nitajenga hekalu la pendo letu
Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako
Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Imani hufanya mambo yote yawezekane, Matumaini hufufua
yaliyopoteza uhai, lakini mapenzi hufanya mambo yote
yaonekane mazuri. Sina linalonihuzunisha maishani mwangu
kwa kuwa tunapendana!
Kama safari tumeianza,kama chakula sinto kusanza,kama
nyumba wewe kibaraza na kama ukingo wewe kiambaza.
Wanafiki tusiwaombee kifo daima na milele washuhudie penzi
letu linavyozidi kukua,na tunavyopambana na mapito.
Recent Comments