SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.

Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.

Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.

Jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha Magonjwa ya moyo

Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo.

Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.

Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa huu vya msongo, ambavyo nimekwisha vielezea hapo awali.

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

Aina kuu ya mizinga bora ya nyuki kwa ajili ya kupata asali nyingi

Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)

Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana na wengi. Gharama yake ni ndogo kiasi kulinganisha na mingine. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga Yya aina hii mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.

 

Mzinga wa Top bar

Faida ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
โ€ข Ni rahisi kukagua asali iliyo tayari.
โ€ข Ni rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji.
โ€ข Ni rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Kwa mfano unaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali.
โ€ข Ni rahisi kurina asali ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu.
โ€ข Aina hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na wadudu/wanyama wanaokula asali kwa kuwa Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa asali kutengenezwa kwa wingi.

Hasara ya Mizinga ya Kifuniko juu (Top bar)
โ€ข Kichane kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama hakitashikwa kwa uangalifu.
โ€ข Masega huvunwa pamoja na asali, kwa hiyo nyuki wanalazimika kutengeneza tena masega mengine ambapo husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.

Mzinga wa Langstroth

Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi kulinganishwa na mizinga mingine Hii ni aina nzuri na rahisa sana ya mzinga. Mizinga hii hufahamika kama mzinga wa fremu, kwa kuwa ina fremu ambazo vichane vya masega hujishikiza. Chumba kikubwa ambacho malkia hutagia mayai. Malkia anazuiliwa kuhama kwenda chumba kingine kwa kutumia waya. Kwenye chemba maalumu ya kutagia juu yake pana chemba ya kuhifadhia asali.

 
 

Mzinga wa Langstroth

Vichane vya masega vinatengezwa kwenye fremu na si kwenye nguzo kama ilivyo kwenye Top bar. Ili kuvuna asali, mfugaji akiwa na masega yaliyojaa asali, hutumia vifaa maalum kwa ajili ya urinaji na kuhifadhi asali bila kupata tabu.

Mzinga wa Langstroth ni gharama kiasi kulinganisha na mizinga mingine.Unaweza kuipata kutoka katika taasisi zinazojiusisha na uuzaji wa mizinga, taasisi na karakana binafsi, au wakala wa Serikali.

SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye

Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.

Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa

Mambo 6 muhimu ya kuzingatia kupata udongo bora mzuri shambani

1. Usiuchoshe sana udongo

Udongo ni kiungo muhimu sana katika uzalishaji wa mazao. Ni mfumo wa uhai kwa mimea. Kwa hiyo, mkulima ni lazima alenge katika kutunza uhai wa udongo na kuepuka usumbufu kwa uhai wa udongo.
Sababu muhimu za kulima/kutifua udongo ni:
โ€ข Hulainisha udongo ili kuruhusu mizizi ya mimea kupenya kwa urahisi.
โ€ข Kutifua kunaboresha uwezekano wa kupenya kwa nitrogen na oxygen kutoka kwenye hewa.

โ€ข Kunawawezesha viumbe hai waliopo kwenye udongo kufanya kazi zao ipasavyo.
โ€ข Kunasaidia Kuandaa sehemu ya kuwekea mbegu.
โ€ข Kutifua kunauongeza uwezekano wa maji kupenya kwenye udongo na kupunguza uyeyukaji wa maji.
โ€ข Kuchanganya mabaki ya mimea na samadi kwenye udongo

2. Acha udongo upumue

Kama ilivyo kwa binadamu, viumbe hai wanahitajika kwa udongo wenye rutuba, pia mimea inahitajika kwa ajili ya binadamu kupata hewa safi ya oxygen. Kuchanganya matandazo,na mboji kwenye udongo ni muhimu sana ili kuboresha mzunguko wa hewa. Viumbe hai wadogo wadogo, wadudu, minyoo, na wanyama wengineo wanapenyeza hewa kwenye udongo.

3. Weka Matandazo kwenye udongo

Huu ni utaratibu wa kufunika udongo kwa kutumia mabaki ya mimea, kwa mfano, matawi madogo madogo ya miti, majani, mabaki ya mimea ya mazao, magugu na kadhalika. Hata hivyo inahitajika nguvu kazi kwa ajili ya kutawanya matandazo.

Matandazo yanazuia mmomonyoko wa ardhi unaotokana na maji na upepo, yanasaidia ardhi kunyonya maji ya mvua, kutunza unyevu unyevu kwenye udongo kwa kuzuia myeyuko wa maji ardhini.

Matandazo yanapo oza hutoa virutubisho vinavyoboresha na kuongeza rutuba kwenye udongo, mbali na hilo pia hubadilika kuwa udongo mweusi wenye rutuba zaidi. Kama kuna uhitaji wa kuharakisha kuoza kwa matandazo ili kuongeza rutuba kwenye ardhi kwa haraka, kinyesi cha ngโ€™ombe kinaweza kuwekwa na kutandazwa juu ya matandazo, hii husaidia kuongeza virutubisho vya nitrogen.

Matandazo yana faida nyingi sana kwenye ardhi, lakini pia yanaweza kusababisha madhara. Mabaki ya mboga za majani yasitumike kama matandazo kwani yanaweza kusababisha wadudu na magonjwa kwa mimea. Viumbe hatari kama bangu (stem borers) wa shina wanaweza kuishi kwenye mabaki ya mimea.

Mabaki ya mimea iliyokuwa imeathiriwa na magonjwa ya virusi au fangasi yasitumike kama matandazo kuepuka uwezekano wa magonjwa hayo kuambukizwa kwa mazao yatakayopandwa msimu utakaofuata. Kilimo cha mzunguko ni njia bora kuepuka athari hiyo.

4. Panda mazao kwa mzunguko

Kupanda mazao kwa mzunguko ina maana ya kuwa na aina mbalimbali ya mazao katika eneo moja kwa msimu.

Kwa mfano, kama shamba lako umepanda mahindi na maharagwe kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkulima anaweza kubadili mzunguko kwa kupanda aina nyingine ya mazao katika eneo hilo kwa mwaka unaofuata.

Mimea iliyo mizuri zaidi katika kilimo cha mzunguko ni pamoja na jamii ya kunde, au malisho kama sesbania ambayo husaidia kuongeza rutuba kwenye udongo.

5. Lisha udongo

Udongo unatakiwa ulishwe ili uwe na virutubisho. Hii ni kazi muhimu sana kwa kila mkulima. Mkulima anaweza Kuulisha udongo kwa kutumia samadi na mboji. Kumbuka udongo uliotumika sana bila virutubisho, umekufa, hauwezi kuzalisha.

6. Kuwa makini na maji

Maji ni mazuri shambani, lakini maji yakizidi ni hatari. Maji yakizidi shambani yanaweza kusababisha mmomonyoko wa udongo. Mmomonyoko wa udongo ni tishio na baa hatarishi kwa rutuba kwenye udongo. Mmomonyoko unaondoa tabaka la juu la udongo, sehemu ambayo ndiyo yenye rutuba zaidi.

Kupanda mimea kwa matuta (kontua) hupunguza kasi ya maji. Baada ya miaka kadhaa, nyasi zinazopandwa zinazopandwa kwenye matuta ya kontua husaidia kuunganisha na kusawazisha sehemu iliyotengwa, kwa kuwa udongo unaomomonyolewa hukusanyika katika sehemu iliyozuiwa na kuunganishwa kwa matuta.

Kwenye mwinuko mkali, kuta au mashimo, ndiyo njia pekee inayoweza kuzuia mmomonyoko wa udongo. Changanya na mimea kama matete, inasaidia kuzuia mmomonyoko na pia kutoa malisho kwa mifugo.

Mbali na matandazo (tazama hatua ya 3) mimea inayotambaa ni mbinu nyingine nzuri zaidi inayoweza kuzuia mmomonyoko wa ardhi. Matone ya maji hufikia ardhi yakiwa na nguvu kidogo sana hivyo kuepuka kumomonyoa ardhi, kwa kuwa yanakuwa tayari hayana nguvu ya kutiririka kwa kasi. Pia mimea inayotambaa hutumika kama kivuli kwa udongo. Mmea wowote unaofunika udongo na kuongeza rutuba unaweza kutumika.

Mfano maharage na mimea mingine ya jamii ya kunde, ambayo ina virutubisho vya nitrogen kwa wingi. Mimea inayopendekezwa ni ile ya jamii ya kunde. Inastahimili ukame, inatoa virutubisho vya naitrojeni, inatoa chakula, na pia inaweza kutumika kama chakula cha mifugo kilicho na protini nyingi. Kwa kuongezea inaweza pia kukabiliana na wadudu waharibifu.

BareFoot Sprayer: Pampu imara ya kunyunyiza dawa – Mabomba ya kupulizia dawa mepesi kubeba na yenye nguvu

BareFoot Sprayer ni Pump Imara na yenye Nguvu Maalumu kwa ajili ya kunyunyiza/kupuliza dawa mashambani, kwenye mifugo nakadhalika.

BareFoot Sprayer imetengenezwa kwa Muundo mzuri kwa kurahisisha ubebaji na upigaji wadawa.

BareFoot Sprayer ina dumu imara lisilopasuka kirahisi na linaloweza kudumu kwa muda mrefu.

Bidhaa hii inaletwa Kwako na Kampuni ya BareFoot International Limited. Wauzaji na wasambazaji wa bidhaa Bora za Kilimo Tanzania.

Mawasiliano

Simu:

+255 756 914 936

โ€”

WhatsApp:

+255 756 914 936

โ€”

Email:

info@bfi.co.tz

โ€”

NB: Tunapatikana Mikoa Yote Tanzania

Meseji nzuri ya kumwambia mpenzi wako kuwa wewe ndiye unayempenda wa kwanza

โ™ฅWatu wanao pendana daima hukumbukana!!! Na salamu
kusalimiana!!! Afya njema kutakiana!!! Huruma
huoneana!!! Kwenye shida husaidiana!!! Makosa
husameheana!!! Katika dhiki huvumiliana!!! Kila
jambo zur hupeana!!! Maneno mazur yaliyo jaa upendo
huambiana!!! Ushaur mwema hushauriana na njia
za mafanikio huonyeshana!!! Mbele ya madui hulindana!!!nai
ni mmoja katia ya wakupendao,hakika ni
mm wa kwanza kwanza wengine wanafataโ™ฅ

Madhara ya Kuvaa/ Kuweka Kope Za Bandia

Mapokeo ya urembo wa kisasa katika nchi zinazoendelea ni sehemu ya mchango wa urembo na mvuto tunaouona kwa baadhi ya wasichana na wanawake ambao kwa hakika unaleta hamasa ya kuangalia.
Hata hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza kutolewa ushahidi kwa sasa.

Moja kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi.

Wataalam wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.

Gundi hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa โ€˜kuonaโ€™. Endapo mtumiaji ataendelea kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae.

Hata hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa gharama ama kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye hatari zaidi.

Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.

Faida za kuogea maji ya Moto

Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.
Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo.

Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo.

Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji ya moto angalau mara tatu kwa wiki

Kulainisha na kutunza ngozi

Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.

Usingizi

Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usinngizi.

Kukuweka katika hali nzuri

Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.

Kuchangamsha ubongo

Unapooga kwa kutumia maji ya moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.

Kushusha shinikizo la damu

Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.

Kusaidia mzunguko wa damu

Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.

Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kuto oga kwa maji ya moto sana kwani huathiri ngozi.

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu hujulikana kama kitu cha kushangaza katika tiba huko mashariki ya mbali, Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe.

Kina nguvu za kuua bakteria mbalimbali na kuzuia magonjwa ikiwemo kutibu chunusi. Kuna namna 2 za kutumia kitunguu swaumu kutibu chunusi; namna ya kwanza ni kukitumia kitunguu swaumu kwenye vyakula vyako unavyopika kila siku, namna ya pili ni kukitwangwa kitunguu swaumu na kukipaka moja kwa moja katika sehemu yenye chunusi.

Ukiacha harufu yake isiopendwa na wengi, kitunguu swaumu kinaweza kukupa afya na urembo unaouhitaji.

Kitunguu swaumu husaidia kupunguza ukubwa wa chunusi. Hata hivyo uwe makini kwani kitunguu swaumu kinaweza kuunguza ngozi yako usipokuwa makini na ili kuepuka hili jaribu kuchanganya kidogo na maji baada ya kukitwanga ili kupunguza makali yake.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About