SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Cheki hawa wachungaji

CHEKA KIDOGO

Wachungaji watatu walikutana kwa siri na kuelezana matatizo yao ili waweze kuombeana.

MCHUNGAJI WA KWANZA: mimi tatizo langu ni wizi, kila nikimaliza ibada lazima niibe pesa za sadaka.

WA PILI: Mimi tatizo langu ni wanawake yani nimeshalala na wana kwaya wote pamoja na mke wa ASKOF.

WA TATU akaanza kulia badala ya kuongea.WENZAKE:

We vp unatatizo gani mbona unalia???

AKAJIBU: jamani mimi tatizo langu ni “umbea” haya yote tuliyoongea lazima nikaseme!

😂😂😂😂😂👆🏻😂😂

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawake tunaokwenda na wakati hupenda kuvaa viatu virefu ilikuongeza muonekano wa umbile lako nikiwa na maana kuwa miguu huonekana yenye kuvutia zaidi unapo kuwa umevaa viatu virefu.

Kutokana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku.Visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku vikikunyima raha ya kutembea kwa uhuru kiasi kwamba wengine hufikia hatua ya kuvua na kutembea peku.

Leo hii napenda kukujuza madhara ya uvaaji wa wa viatu virefu.Kwa kawaida, miguu ya binadamu hasa visigino, vimeumbwa ili kuuzuia uzito wa mwili juu ya ardhi.Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa mwili kubebwa na kisigino, hivyo uzito wa mwili kushindwa kuhimili uzito wote.

Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito.Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino.Tatizo hilo hupelekea kiuno,Miguu na mgongo kuwa katika hatari ya matatizo ya kiafya pamoja na kuteguka na kuvunjika miguu.

Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo hupelekea magoti na misuli ya mapaja kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili usawa.Kwa kuwa misuli inafanya kazi kubwa, uwezekano wa kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za baadae huwa mkubwa zaidi. Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya mapaja kuuma, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi yake.

Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu, magoti, na mifupa ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea na hivyo kusuguana wakati wa kutembea.

Jambo la kuzingatia kwa wale wanaopenda kuvaa viatu virefu,ni vema kama unapenda kuvaa viatu virefu hakikisha hutembei umbali mrefu kama una usafiri sio mbaya ukivaa viatu virefu,na kwa wale wanao kwenda ofisini jitahidi kuwa na viatu flati ndani ya mkoba wako ili unapokuwa umechoka unavua na kuvaa viatu vyako pia ukiwa ofisini waweza kuvua viatu virefu.

Mpenzi msomaji kama huwezi kutembelea viatu virefu nivema ukipitwa na wakati kuliko kujiabisha barabarani na kuonekana rimbukeni ikiwa wewe ni mjamzito epuka uvaaji wa viatu virefu.Usikose kujumuika nami katika safu hii ya urembo na mitindo.

Namna ya kuondoa Mikunjo ya ngozi

MIKUNJO katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi.
Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mablimbali.
Katika kupambana na tatizo hilo, wadau wa urembo wa asili wamegundua njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutatua tatizo hili.

Wadau hao wanashauri kumwona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi wa matumizi ya njia hizo za asili kabla ya kuanza kutumia njia za asili kwani hata kama ni vipodozi asilia, haina maana kama ni salama kwa watu wote.

Kwa mujibu wa wadau hao, unaweza kutumia viungo vinavyopatikana jikoni kwako kupambana na mikunjo katika ngozi. Baadhi ya viungo hivyo ni pamoja na:

Karoti
Tumia juisi ya karoti kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika.
Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako. Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi.

Si hivyo tu, karoti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya
ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maeneo kama hayo.
Namna ya kufanya

Chukua karoti, saga kwenye mashine kisha kamua ili kupata juisi yake.
Tumia pamba kupaka katika maeneo yaliyoathirika, fanya hivyo mara kwa mara, itakusaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

Maziwa
Maziwa yana virutubisho vinavyochochea kunawiri kwa ngozi. Pia yana chembechembe za ‘Alfa-Hydroxide Acid’ ambazo zina uwezo mkubwa kuondoa seli zilizokufa mwilini.

Yote haya husaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la mikunjo katika ngozi.

Unachotakiwa kufanya
Kuchukua maziwa kiasi na chovya pamba ndani yake, kisha paka maeneo yaliyoathirika.

Aloe Vera
Jeli ya Alovera ndiyo hasa inayotakiwa katika zoezi hili. Chukua jani lake na kisha likate ili kupata utomvu wake.

Chukua utomvu au jeli hiyo kama wengine wanavyoita na kisha pakaa sehemu iliyoathirika, itapunguza ama kuondoa kabisa tatizo hilo.

Parachichi
‘Mask’ ya Parachichi husaidia kuifanya ngozi iwe na mng’ao. Siyo hivyo tu, bali huchangia kwa kiasi kikubwa pia kuifanya ngozi iwe laini na nyororo.

Unachotakiwa kufanya
Chukua parachichi liloiva vizuri, kisha saga hadi lilainike.

Baada ya hapo pakaa sehemu iliyoathirika na acha kwa muda wa dakika 10, kisha osha sehemu hiyo uikaushe.

Papai
Mask ya Papai pia husaidia kuondoa tatizo hili.

Unachotakiwa kufanya
Chukua kipande cha papai kilichoiva na kuchanganya na kijiko kimoja cha unga wa ngano.

Pakaa sehemu iliyoathirika na kaa nayo kwa muda usiopungua dakika kumi. Mbali na kupaka pia unaweza ukatumia kula kwani lina vitamin E kwa wingi, ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa ngozi.

Danzi
Juisi ya tunda hili husaidia katika uzalishaji wa sehemu ya juu ya ngozi ‘collagen’. Danzi lina kiwango kikubwa cha vitamini C. Na kwa kawaida aina hii ya vitamin husaidia kuchochea ukuaji wa ‘collagen’, hivyo kuifanya ngozi yako kunawiri.

Maji
Kunywa maji mengi kwani husaidia kuifanya ngozi yako iwe na unyevu muda wote.
Ikiwa utazingatia zoezi hili mikunjo kati ngozi yako itakuwa ni historia.

Umasikini isiwe sababu wala utajiri isiwe sababu ya kuwa mchafu au kutokuwa na usafi

Katika maisha, umasikini siyo sababu ya mtu kuwa mchafu au kutokuwa na usafi. Hali ya umasikini inaweza kuathiri uwezo wa mtu kumudu bidhaa za usafi au kuishi katika mazingira safi, lakini hii haimaanishi kuwa mtu mwenye utajiri automatically ni mtu mwenye usafi.

Kinyume chake, utajiri haujazi hakika mtu kuwa na kila kitu ambacho hahitaji. Utajiri ni kuwa na uwezo wa kununua au kumiliki vitu vingi, lakini ukweli ni kwamba tunahitaji tu vitu vichache sana katika maisha yetu. Tunapojikuta tukiwa na wingi wa vitu visivyotumiwa, tunaweza kujikuta tukichafua mazingira yetu na kutopenda kila kitu tunachomiliki.

Sasa angalia nyumbani kwako! Je, kuna vitu ambavyo haujahitaji kwa muda mrefu au vinachafua tu nafasi yako? Kufanya maamuzi ya busara na kujiondoa na vitu visivyohitajika, vitakuwezesha kuishi katika mazingira safi na yenye upangaji mzuri. Usafi sio lazima uendane na utajiri, bali ni suala la utaratibu na umakini katika kusimamia mazingira yetu.

Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri Sio kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. Hebu angalia hapo nyumbani kwako!

Vitu msivyovihitaji Leo wala kesho mmeweka vya nini? Umenunua makochi mapya Yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya.

Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwa secondary mpaka Leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua.

Jikoni ndo shida iliposhika hatamu! Mivyombo ya plastiki imepaukiana imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto. Mahotpot yamekata roho imebaki kuwa sufuria we unalo tuu. Mxiuuu

Ndoo hata hazitumiki zipozipo tu, hata maua hazifai kupandia we unazogo tu huchomi, hutupi wala huzihitaji.. Sa zanini hapo?? 😡😡

Vyombo vya udongo vina mapengo na magego kama vinang’atwaga au vinapiganaga vyenyewe. 😂😂. Isitoshe kila kimoja na dizaini yake havifanani coz seti imeshavunjikavunjika hivo ndo vimebaki. Unaboa… 😏😏😏

Dressing table imejaa mikopo na mibox haina Kazi, perfume ya mwaka 2000 unayo hapo kisa ukumbusho wa zawadi. Ushamba huooo… 😫😫

Stoo yako mwenyewe ila unaiogopa kuingia coz imejaa vitu visivyohitajika imekuwa ghetto la panya na nyoka kama sio nge badala Ukiweka mnavyohitaji. Ipo siku mtakuta mamba humo.. 🐲🐲🐲

Nje ya nyumba kuna gari la urithi la babu lipogo tu hapo linafuga ndege na vibaka… Aaalaaaa 😡😡😡

Kutupa vitu visivyohitajika hamtupi eti Dhambi na kugawa hamgawi coz mmeviharibu hadi mwisho mtampa nani? Kutwa mnapishana mahospitalini mnaumwa mafua na vifua kila siku.

Kwann msiumwe na mnakaa dampo ? Hivi mnajua km huu ni ugonjwa? Unaitwa hoarder disorder. Tena mnawaambukiza watoto wenu kwani wanajua kwao hata kikopo cha icecream hakitupwagi kinaoshwa kinawekwa hapo.

Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa?

Kwa kweli, mtazamo wa kuridhika na hali ilivyo sio tu hatari kwa maendeleo binafsi, lakini pia kwa jamii kwa ujumla. Mazingira tunayoishi yanahitaji uangalizi na uhusiano wa moja kwa moja na afya zetu, usalama, na hata uchumi wetu. Kama ilivyosemwa awali, kila mmoja wetu – bila kujali hadhi yetu kifedha – ana wajibu wa kuchukua hatua za makusudi katika kudumisha usafi wa mazingira yetu.

Tunapaswa kuzingatia kuwa usafi na umakini wa mazingira yanatuhusu sote na yana faida zinazoonekana na zisizoonekana. Uchafuzi wa mazingira, kwa mfano, unaweza kuathiri ubora wa hewa tunayopumua na maji tunayotumia, na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya. Kwa upande mwingine, mazingira safi na yenye kuendelezwa vizuri yana uwezo wa kuongeza thamani za mali, kuboresha uzuri wa jamii, na kuvutia uwekezaji na utalii ambao unaweza kukuza uchumi wa eneo husika.

Kila mtu anapaswa kuchukua hatua, iwe ni katika kutupa takataka mahali pake, kushiriki katika shughuli za kusafisha mazingira, kupanda miti, au kufunza wengine umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. Serikali na asasi zisizo za kiserikali zinaweza kusaidia kwa kutoa elimu, rasilimali na sera zinazosaidia usafi na utunzaji wa mazingira.

Ni muhimu kutambua kwamba uamuzi wa kutunza mazingira unapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku na sio tu wakati wa maadhimisho au mikakati ya muda mfupi. Uendelezaji wa mazingira safi na salama ni jukumu letu la kudumu, linalohitaji kujitolea na ushirikiano kutoka kwa watu wote katika jamii.

Mambo madogo hayapaswi kupuuzwa – matumizi ya mifuko inayoweza kutumika tena badala ya plastiki zinazotupa sana, kutumia njia mbadala za nishati zinazoweza kujazwa upya ili kupunguza uchafu, na hata kusimamia taka za kielektroniki – yote haya ni sehemu muhimu ya kujenga mazingira endelevu. Hivyo basi, hebu tuchukue hatua, kila mmoja wetu, kwa mustakabali mzuri zaidi. Tunalo jukumu hilo, kwa ajili ya kizazi chetu na vizazi vijavyo.

Mambo ya kuzingatia kujikinga na chunusi | Jinsi ya kuzuia

Mambo mhimu ya kuzingatia

1. Fanya mazoezi ya viungo kwa saa moja kila siku
2. Kunywa maji mengi kila siku
3. Ondoa mfadhaiko (stress)
4. Weka homoni sawa kama hazipo sawa
5. Kuwa msafi wa mwili wote kila mara
6. Usiziguse chunusi au kuzitoboa na mikono yako au na chochote kuepuka makovu yasiyo ya lazima
7. Epuka vyakula vifuatavyo kama unasumbuliwa na chunusi kila mara, navyo ni pamoja na:

a)Vyakula vyenye mafuta sana

b)Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi

c)Kahawa

d)Chai ya rangie)

e)Pombe na vilevi vingine

f)Chokoleti

g)Popcorn

h)Maziwa

i)Mapera

j)Vyakula vya kwenye makopo

k)Pizza

Jinsi ya kujisaidia unapotokwa na damu Puani

Unapotokwa na damu puani fanya yafuatayo;
1. Simama wima na inamisha kichwa kwa mbele, kusimama itakusaidi kupunguza kasi na presha katika mishipa ya damu puani wakati unapoinamisha kichwa kwa mbele huzuia kumeza damu ambayo italeta shida tumboni.

2. Weka pamba au kitambaa chenye uwezo wa kufyonza damu nje ya pua na bana pua kwa muda wa dakika 15 huku ukitumia mdomo kupumua, kubana pua hurudisha damu katika mishipa ya pua na kuzuia kuvuja.

3. Kuzuia damu isitoke tena usichokonoe pua wala kuinamisha kichwa mbele kwa nguvu na kwa muda mrefu.

4. Kama damu inaendelea kutoka bana pua kwa kutumia kitambaa chenye ubaridi au barafu itasaidia kusinyaa kwa mishipa ya damu na kuzuia damu.

5. Nenda hosipitali kama damu puani inatoka na kuumia kichwani, haijakata kwa muda wa dakika 20 na kama pua imeumia au kuvunjika

KUMBUKA: Kutokwa na damu puani ni jambo la kawaida sana kwa kila mtu na mara nyingi huwa sio hatari sana isipokuwa kama linaambatana na dalili nyingine hatari. Tatizo ili huweza kusababishwa na kuumia ndani au nje ya pua, kuchokonoa pua mara kwa mara, shinikizo la damu, matumizi dawa za aspirini, ukosefu wa vitamini K, pombe kupita kiasi, na mabadiliko ya hormoni kwa wajawazito

Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake

BABA OYEEEEEE💪💪
Soma hii…

Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-

MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor

MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by Ngũgĩ wa Thiong’o

MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie

MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.

MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe

Baba mtu akawatazama kisha akasema

BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli

MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!

BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!

Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED” by Wole Soyinka.

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa vya mpira.
7.Misumari midogo.
8.Jiko.

MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.
2.Caustic soda
3.Mshumaa.

KAZI ZAKE:

1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

JINSI YA KUTENGENEZA.

(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c)KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About