SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Dunia haijali mazuri yako ila ubaya wako, jiamini songa mbele

Siku moja mwalimu wa shule aliandika ubaoni kama ifuatavyo:
9ร—1=7
9ร—2=18
9ร—3=27
9ร—4=36
9ร—5=45
9ร—6=54
9ร—7=63
9ร—8=72
9ร—9=81
9ร—10=90
Alipo maliza kuandika tu, akaona wanafunzi wote walikua wanamcheka, kwasababu alikua amekosea swali la kwanza.

Mwalimu aliwatazama wanafunzi, kisha akawaambia yafuatayo:
`”Nimejikosesha lile swali la kwanza makusudi, kwasababu nilihitaji mjifunze kitu kimoja muhimu sana. Mnapaswa kujua namna ambavyo dunia inaweza kuwachukulia. Unaona hapo, nimeandika kwa usahihi mswali tisa (9), lakini hakuna kati yenu aliyenipongeza kwa hilo; wote mmecheka na kunilaumu kwasababu ya kosa moja tu nililofanya.”`
Hivyo, hili ni somo kwenu:
`”Dunia haijali mazuri unayofanya hata ukiyafanya mara milioni, lakini fanya baya moja uone jinsi watakavyo kulaumu…”`
“`Hata hivyo usikatetamaa, MARA ZOTE SIMAMA IMARA NA USHINDE VIKWAZO VYOTE.” `
JIAMINI

Jinsi ya kutibu tatizo la kukosa choo bila kutumia dawa

Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.

Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku, lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.

Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.

Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(Vyakula vyenye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.

Vifutavyo ndivyo vyakula ambavyo husaidia kutibu tatizo la kukosa choo.

Tende

Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitolโ€“aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.

Maji

Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.

Wataalamu wa afya wanashauri kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)

Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.

Kahawa na Vinywaji Vingine vya Moto

Kahawa na vinywaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.

Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo

Ulaji wa Matunda au Saladi

Matunda yanasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.

Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.

Ulaji wa Mboga za Majani

Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.

Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.

Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.

Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo la Kukosa Choo Pia:

Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.

Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako. Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).

Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.

Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibu tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.

Kilichotokea kati ya mkaka na mdada walipokutana hotelini

Mkaka aliingia kwenye hoteli moja akaketi meza moja na mdada mrembo maarufu sana;
MKAKA: Samahani dada sijui saa ngapi?
MDADA: Nani kakwambia saa yangu ndio ya kuangalia kila mtu?

MKAKA: Samahani sanaโ€ฆ.jamaa akachukua Galaxy yake akapiga simuโ€ฆ.aise saa ngapi saa hizi? mi ndio nimeingia toka USA nataka kurekibisha saa yangu ifwate muda wa huku. Na wewe uwahi kuchukua iPad nimekuja nazo tatu tu za zawadi. Halafu ntafutie mtoto mzuri nimumwagie midola niliyokuja nayo, ok ciao tuonane badae.
MDADA: Kaka samahani saa hizi ni saaโ€ฆ..
MKAKA: Achana na mimi wewe

Ha ha ha ha haaaaa!!

Hii ndio sababu kwa nini huwezi kufanikiwa kibiashara

HUWEZI KUFANIKIWA KIBIASHARA KAMA UNAPENDA KUJIHURUMIA HURUMIA!
๐Ÿ’ฅMama mmoja Mzungu alitembelea mlima Kilimanjaro miaka iliyopita. Alikuwa amepanga kupanda mlima Kilimanjaro mpaka kileleni, yaani Kibo na Mawenzi, ili hatimaye apewe cheti cha kupanda mlima mrefu Afrika.

๐Ÿ’ฅLakini kwa bahati mbaya akiwa amefika katikati ya mlima alizidiwa kiafya na hatimaye akashushwa mlimani akiwa amezirai hadi hospitalini.

๐Ÿ’ฅSiku ya tatu alipozinduka hospitalini huku marafiki zake wakimpa pole, aliwajibu kuwa โ€œMlima Kilimanjaro hauwezi kuongezeka urefu, lakini mimi mwanadamu nina uwezo wa kuongeza maarifa, nguvu na mbinu za kupanda milima wowote duniani. Kwa hiyo nitarudi tena wakati mwingine mpaka nipande mlima Kilimanjaro hadi kileleni, ingawa nimepata changamoto wakati huu.โ€.

๐Ÿ’ฅAlivyorudi kwao Marekani, alianza kufanya mazoezi tena ya kukimbia na kupanda vichuguu na vilima kwa muda wa mwaka mzima, na kisha mwaka uliofuata alirudi tena Tanzania, akapanda mlima Kilimanjaro mpaka kilele cha Kibo na mawenzi, na hatimaye akapewa cheti cha kupanda mlima Kilimanjaro!.

๐Ÿ’ฅJe huyo mzungu angeamua kusubiri mlima Kilimanjaro upungue urefu ndipo aje Tanzania kuupanda, jambo hilo lingewezekana?

๐Ÿ’ฅJe unataka maisha yawe rahisi ndipo uyamudu? Je unataka viwanja vishuke bei ndiyo ujenge nyumba yako? Je unataka ada za shule ziwe chini ndipo usome? Je unataka gharama za hospitali ziwe chini ndipo utibiwe? Je unataka mahari iwe chini ndipo uoe? Je unataka vitabu vya mafunzo ya biashara viwe bei chee ndiyo ununue? Unataka mshahara wako uwe mkubwa ndipo ufanikiwe? Je unataka shetani auwawe ndiyo umche Mungu? Je unataka dunia irudi nyuma, ndipo uweze kuyamudu maisha? Je, unataka urudi tumboni mwa mama yako ili uwe unakula na kulala bure? Ebo!๐Ÿ™Š

๐Ÿ’ฅKama nia yako ni kufanikiwa hutakiwi kujionea huruma, nenda kwa wakati na ujitoe hadi kieleweke.

Kila la kheri na pia nakutakia MAFANIKIO makubwa sana wewe na kizazi chako! Siri ya utajiri ni ubahil asikudang’anye mtu tumia hela ikuzoee hakuna aliyezaliw kuwa maskin!

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mtaalamu wa nyuki

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya nyuki. Unapoanza ni lazima uulize mtaalamu wa nyuki, wafugaji wenzako ambao wana uzoefu wa kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya ufugaji wa nyuki.

Sehemu salama kwa ajili ya mzinga

Unahitaji kutafuta mahali pazuri, salama, na penye sifa ya kufugia nyuki. Vifaa vyote vikishapatikana kinachofuata ni kuchagua mahali gani pa kuweka mzinga. Hakikisha sehemu hii ni mahali ambapo makundi ya nyuki hukusanyika mara kwa mara.

Uwekaji Bora wa Mizinga

Ukishatafuta ya sehemu ya kuweka mizinga, kinachofuata ni kuandaa mizinga kwa ajili ya kuweka panapotakiwa.

Mambo ya muhimu ya kuzingatia
โ€ข Kwanza Safisha mzinga kuondoa uchafu wote, utando wa buibui na aina nyingine za wadudu.
โ€ข Kisha Weka chambo kwenye mzinga (maranyingi nta hutumika kama chambo) kwa kuipaka katika kuta za mzinga kwa ndani.
โ€ข Halafu Mzinga unaweza kutundikwa kwenye mti, kwenye nguzo, kuweka kwenye jukwaa au kwenye miamba. Hii inategemea wewe mwenyewe anapendelea njia ipi.

JINSI YA KUTENGENEZA BATIKI

Batiki inatengenezwa kama ifuatavyo

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.
2.Sponji zenye urembo mbalimbali.
3.Brash kubwa/ndogo.
4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.
5.Sufuria.
6.Vitambaa vya mpira.
7.Misumari midogo.
8.Jiko.

MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.
2.Caustic soda
3.Mshumaa.

KAZI ZAKE:

1.Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2.Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

JINSI YA KUTENGENEZA.

(a)JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoekidogo.Andaa kitambaa cha cotton na kukitandika mezani,chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo.Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b)JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita.Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano.Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja.Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu.Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano.Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c)KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu.Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile.Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d)JINSI YA UFUA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.
PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.

Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe na mvuto na kuvutia zaidi

Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Miongoni mwa maswali ambavyo huwa tunaulizwa na wasamoaji wetu ni pamoja ni kwa jinsi gani naweza kutengeneza nywele zangu ili ziwe za kuvutia?

Basi nasi bila ya haiana yeyote ile tunakuletea somo hili maalum kwa ajili ya watu wote ambao wanatamani kujua namna ya kuzifanya nywele zako zivutie. Kwanza kabisa kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto

Hivyo zifuatazo ndizo njia ya kufanya nywele zako zivutie:

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

Usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.

Jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

Kula vyakula venye protin na matunda

kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

Kata ncha za nywele zako

kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

Osha nywele zako angalau mara moja kwa wiki

kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. Hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuonsha nywele zako.

Zifunge nywele zako kabla ya kulala

Unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

Tumia mafuta asili

Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.

Zilinde nywele zako na jua

W akati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. Pia unaweza kuzipaka sunscreen.

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hiviโ€ฆ”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipoโ€ฆ!!!

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoโ€ฆ..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!โ€ฆkamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?โ€ฆkwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!โ€ฆsasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,โ€ฆhakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,โ€ฆ.hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!โ€ฆSasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!โ€ฆMy God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimyaโ€ฆ

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimyaโ€ฆ

Dogo ana dharau huyu!โ€ฆSasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!โ€ฆ.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!โ€ฆDogo hakuwepo!โ€ฆ.na Mabegi pia hayapo!โ€ฆlap top haipo!โ€ฆ.NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!โ€ฆ.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!โ€ฆyaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!โ€ฆniitieni Ambulance!

๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About