Ujumbe wa meseji wa kumsihi mpenzi wako mdumishe mapenzi yenu
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule
atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi
inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu
laazizi wangu.
Nimekuapata! Kama unanichukia, nipige mshale, lakini
tafadhali si moyoni sababu hapo ndipo wewe ulipo.
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba, nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
Nitafute wakati una huzuni, nitafute wakati hamna wa
kukusikiliza. Sijali kama mimi ni kimbilio lako la mwisho,
bali sipendi ulie peke yako.
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
Nafsi yangu inafurahia ya kwamba
wewe ndio chaguo langu, ubavu wangu
tabasamu usoni mwangu ndio siri ya
pendo lako kwangu
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Imara hautikisiki,kakamavu halishikiki penzi langu kwako
ni nuru daima halizimiki.upo juu katika mapenzi.
Recent Comments