Ujumbe mzuri kwa mpenzi wako kumuonyesha upendo
yapitayo mdomoni yametokea moyoni ,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
yapitayo mdomoni yametokea moyoni ,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kujyatibu,
napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu,
mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu
yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda
nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.
Mpenzi unawafahamu maadui wa mapenzi yetu ? Ni wale rafiki zako wanaokuletea maneno ya uongo, ndugu zako wanaotugombanisha na wachawi wanotuotea mabaya, tujihadhari tusiwape ushindi. Mapenzi yetu yadumu daima.
chekecho la huba ,toka uvunguni mwa moyo wangu
navika moyo wako taji la upendo,na kupulizia marashi ya hubaa ,usimpe mwingine mi ndiye ninayejua kulea.
Hata kama watasema mengi kiasi gani, kwako wewe
nitaendelea kuwa mpole, maana nakupenda sana…
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu,
huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili
mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU.
Mchana mwema
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Recent Comments