Karibu AckySHINE

Karibu AckySHINE

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Sababu, dalili na matibabu ya tatizo la kuziba kwa mrija wa mkojo

Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mrija huu unaposinyaa au kuziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa
mashaka na maumivu makubwa. Kusinyaa/ Kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa pia
urethral stricture.

Visababishi na vihatarishi vya tatizo hili

Kusinyaa kwa mrija wa mkojo husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya
mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.

Inaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.
Vihatarishi vya tatizo hili ni pamoja na

Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa

kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au
cystoscope)

  • Kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume
  • Kuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya kinena. Hii hutokea

sana kwa wale wanaopata ajali wakiendesha baiskeli

  • Kupata maambukizi ya mara kwa mara ya mrija wa mkojo (urethritis)
  • Ni nadra sana kwa tatizo hili kutokea kwa wanawake. Aidha ni nadra pia kwa

mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hili (congenital urethral stricture).

Dalili za tatizo hilo.

Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo,

  • Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu.
  • Kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu.
  • Kupungua kwa kiasi cha mkojo kinachotolewa.
  • Kukojoa kwa shida.
  • kutoa uchafu katika mrija wa mkojo.
  • kukojoa mara kwa mara.
  • Kushindwa kumaliza mkojo wote.
  • Kushindwa kuhimili kutoka kwa mkojo (mkojo kujitokea wenyewe/kujikojolea).
  • Maumivu wakati wa kukojoa.
  • Maumivu chini ya tumbo.
  • Maumivu ya kinena
  • Mtiririko dhaifu wa mkojo (hutokea taratibu au ghafla)
  • Mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa
  • Kuvimba uume

Uchunguzi

Daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na namna unavyokojoa. Uchunguzi wa mwili
unaweza kuonesha:

  • Kupungua kwa mkondo wa mkojo
  • Uchafu kutoka katika mrija wa mkojo
  • Kibofu kilichojaa/kuvimba
  • Kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena
  • Tezi dume iliyovimba au yenye maumivu
  • Kuhisi kitu kigumu chini ya uume
  • Uume kuvimba au kuwa mwekundu
  • Hata hivyo, wakati mwingine uchunguzi unaweza usioneshe tatizo lolote lile.

Vipimo

Vipimo ni pamoja na

  • Kipimo cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy)
  • Kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya kukojo (Post-void

residual (PVR) volume)

  • X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram)
  • Vipimo vya magonjwa ya zinaa

Matibabu

Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo
mojawapo ya tiba. Iwapo njia ya kutanua mrija haioneshi mafanikio sana, upasuaji
unaweza kuhitajika. Upasuaji unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo.

Kama tatizo ni dogo/fupi na lipo mbali na bawabu inayotenganisha mrija na kibofu cha mkojo,
linaweza kutatuliwa kwa kukata kasehemu kalikoziba wakati wa kufanya cystoscopy au
kwa kuweka kifaa maalum cha kuzibua na kutanua mrija.

Kama tatizo ni kubwa zaidi, upasuaji wa wazi wa eneo husika unaweza kufanyika.
Upasuaji huu unajumisha kukata sehemu iliyoziba na kisha kukarabati sehemu hiyo.

Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute
retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena
(suprapubic catherization) hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye
bomba lililowekwa chini ya tumbo.

Ifahamike kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya tatizo hili zaidi ya njia za upasuaji na
nyingine zilizoelezwa hapo juu.

Matarajio

Mara nyingi matibabu huleta matokeo mazuri na mgonjwa anaweza kuishi maisha yake
kama kawaida. Hata hivyo wakati mwingine, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya
mara kwa mara ili kuondoa sehemu ya kovu iliyopo katika mrija wa mkojo.

Madhara ya tatizo hili

Tatizo hili halina budi kutibiwa haraka maana kama likiachwa linaweza kusababisha
kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali
ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo
kushindwa kufanya kazi (ARF).
Kinga

Ni muhimu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa kufanya ngono salama au kuacha
kabisa kufanya ngono. Aidha kuwa makini na kazi au mambo ambayo yanaweza
kukusababishia kuumia maeneo ya kinena.

Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho

FROM FR TITUS AMIGU
Siku moja, miaka kama 14 hivi iliyopita, nilimzingua mchungaji wa kikanisa fulani. Alinijia mbio na kuniambia, “Atiโ€ฆ Kadinali wenu amesema kuwa pombe sio dhambi! Kwanini usihame huko? Angalia sasa, hata kiongozi wenu wa juu wa Kanisa amekosea kwa kusema pombe sio dhambi.”
Basi mimi nikamjibu huyo mzee kama ifuatavyo;
Je kisu ni dhambi? Mzee akajibu, “hapana!” Je sumu ya panya? Mzee akajibu tena, “hapana”. Nikampa changamoto hii; Je, kama mtu akimdunga mwenzake kisu na kumuua, hapo dhambi ni kisu au kuua? Au mtu afanyaye kujiua kwa kumeza sumu ya panya, je basi ndio tuseme kuwa sumu ya panya ni dhambi? Mzee akajibu, hapana.
Nikamkumbusha maneno ya Yesu kuwa kitu kimuingiacho mtu hakiwezi kumtia unajisi.
Nikamwambia, “Kanisa lako ni kanisa la walevi.” Mzee akatumbua macho, “โ€ฆ heeโ€ฆ kijana wewe?โ€ฆ” Nikamweleza;
Wengi kama si wote, wa wafuasi katika kanisa lenu ni walevi. Wanatamani kunywa na kulewa, lakini wewe kama mchungaji umewazuia kwa sheria, tena sheria kali yenye vitisho na kuwatia hofu. Umeweka mikono yako machoni pao na kuwaambia kuna shimo mbele, hivyo umewafanya vipofu zaidi. Kila mwanamume amtazamaye mwanamke kwa tamaa amekwisha kuzini naye moyoni , na vivyo hivyo, kila atamaniye ulevi amekwisha kulewa moyoni ; hata kama asipoonja pombe, ni mlevi tu.
Nikazidi kumweleza kuwa mimi niliimarishwa (Kipaimara) kwa kuwekewa mikono na Askofu, nikaombewa ujazo wa Roho Mtakatifu. Kunywa ama kutokunywa nafanya si kwa amri, bali kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Sheria ya usionje, usiguse hainihusu, maana mimi ni mtu huru katika Roho. Kwa hiyo siwezi kujiunga na kanisa la walevi, ambao badala ya kumtii Mungu, wanaitii hofu iliyopandwa ndani yao.
Yule mzee akasema, hapo umenijibu vema kijana, lakini mbona ninyi Wakatoliki mnawaomba wafu, kama Bikira Maria? Nikamjibu,;
Sisi Wakatoliki ni Kanisa lililo katika ushirika wa Watakatifu. Yesu aliwaambia Masadukayo kuwa Bwana ni Mungu wa walio hai, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Ndio maana pale mlimani Yesu alipogeuka sura aliongea na Musa na Eliya walio hai. Katika kikanisa chenu hakuna imani ya kuweza kuongea na Yesu ili muingie katika utukufu wake, na awawezeshe kuongea na Musa na Eliya, Bikira Maria au watakatifu wengine walio hai katika Bwana. Mkifa, mnakufa kama mbwa, na mnakufa kweli kweli. Basi siko tayari kujiunga na kanisa la wafu, tena wasio na imani ya kuona mambo ya rohoni. Japo mnajiita kanisa la kiroho, mambo ya rohoni hamyajui, maana ninyi ni kanisa la wafu.
Yule mzee akazua ghafla safari ya kwenda kunywa chai aliyodai ameitwa na mjukuu wake akanywe, naye faster akasepa.
Je, waijua misingi ya imani yako? Je, unaongozwa na Roho Mtakatifu au na sheria za kidini?
Usiyumbishwe na kila upepo wa mafundisho.

Mambo ya msingi kujua kuhusu ugonjwa wa ngiri

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmengโ€™enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Jinsi wigo wa mimea kwenye shamba unavyoweza kukinga mazao yako na wadudu waharibifu

Wigo wa mimea ni kinga nzuri ya mazao shambani. Mimea ya wigo inaweza kutumika kama kizuizi cha wadudu kuhama hama.

Wigo hutatiza vidukari kuhama na kuingia bustanini. Kwa mfano, mimea kama tithonia ni kizuizi kwa aina nyingi sana za wadudu.

Safu za mbaazi zimekuwa zikitumika kulinda nyanya, viazi, kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharage yanaweza kupandwa kati ya mistari ya kabichi yakiwa kama mitego kwani yanasaidia kulinda kabichi dhidi ya buibui wekundu.

Maharagwe yanapandwa kama mtego kwenye kabichi lakini yanafanya kazi ya kudhibiti wadudu (mtego), kuboresha udongo, chakula cha mifugo, matandazo au kutengenezea mbolea.

Vile vile wigo wa mimea ni makazi ya wanyama/wadudu wanaowinda.

Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya

Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!

Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzakoโ€ฆ..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!

Madhara ya Kuvaa viatu virefu

NI wazi kuwa viatu virefu huvutia sana vinapo kuwa vimevaliwa.Tulio wengi hasa mabinti au wanawake tunaokwenda na wakati hupenda kuvaa viatu virefu ilikuongeza muonekano wa umbile lako nikiwa na maana kuwa miguu huonekana yenye kuvutia zaidi unapo kuwa umevaa viatu virefu.

Kutokana na utafiti wa kitaalamu, mwanamke ana uwezo wa kutembea wastani wa hatua 10,000 kwa siku.Visigino virefu hufanya nguvu inayotumika kutembea hatua moja kuwa kubwa kuliko kawaida, huku vikikunyima raha ya kutembea kwa uhuru kiasi kwamba wengine hufikia hatua ya kuvua na kutembea peku.

Leo hii napenda kukujuza madhara ya uvaaji wa wa viatu virefu.Kwa kawaida, miguu ya binadamu hasa visigino, vimeumbwa ili kuuzuia uzito wa mwili juu ya ardhi.Uvaaji wa viatu virefu hufanya uzito wa mwili kubebwa na kisigino, hivyo uzito wa mwili kushindwa kuhimili uzito wote.

Matokeo yake husababisha misuli na mishipa ya miguu, kiuno, mgongo na shingo kufanya kazi kubwa ya kujaribu kusawazisha uzito.Kazi ambayo kwa kawaida hufanywa na visigino.Tatizo hilo hupelekea kiuno,Miguu na mgongo kuwa katika hatari ya matatizo ya kiafya pamoja na kuteguka na kuvunjika miguu.

Visigino virefu hubadili muundo wa mifupa ya miguu, hivyo hupelekea magoti na misuli ya mapaja kufanya kazi ya ziada ili kuupa mwili usawa.Kwa kuwa misuli inafanya kazi kubwa, uwezekano wa kupatwa na maumivu makali ya miguu na kushindwa kutembea katika siku za baadae huwa mkubwa zaidi. Visigino virefu husababisha maumivu ya visigino, damu kuvilia ndani ya miguu, mpangilio wa mifupa ya vidole kuvurugika, mishipa na misuli ya mapaja kuuma, neva za fahamu kufungana na kushindwa kufanya kazi yake.

Tatizo huendelea kwa vifundo vya miguu, magoti, na mifupa ya kwenye mapaja kushindwa kujivuta na kulegea na hivyo kusuguana wakati wa kutembea.

Jambo la kuzingatia kwa wale wanaopenda kuvaa viatu virefu,ni vema kama unapenda kuvaa viatu virefu hakikisha hutembei umbali mrefu kama una usafiri sio mbaya ukivaa viatu virefu,na kwa wale wanao kwenda ofisini jitahidi kuwa na viatu flati ndani ya mkoba wako ili unapokuwa umechoka unavua na kuvaa viatu vyako pia ukiwa ofisini waweza kuvua viatu virefu.

Mpenzi msomaji kama huwezi kutembelea viatu virefu nivema ukipitwa na wakati kuliko kujiabisha barabarani na kuonekana rimbukeni ikiwa wewe ni mjamzito epuka uvaaji wa viatu virefu.Usikose kujumuika nami katika safu hii ya urembo na mitindo.

MALAIKA WA MUNGU

Hapo Mwanzo Mungu aliumba Malaika katika hali ya njema na Heri kubwa. Kisha aliumba mbingu na nchi, na viumbe vyote vinavyoonekana na visivyoonekena. (Kol, 1;16, Mwa, 1;31)
Malaika ni viumbe vilivyo Roho tuu vyenye akili na utashi. (Zab 91:11, Ebr 1:7, Uf, 12:7-9).
Malaika wengine walikosa kwa kumkaidi Mungu, wakatupwa motoni na ndio Mashetani ambao Mkubwa wao ni Lusiferi. (Yn, 8:44: Uf 12:7-9,).
Mungu aliumba Malaika ili Wamtukuze, Wafurahi nae Mbinguni na wawe Matarishi/wajumbe wake kwa Wanadamu. (Tob 12:12, Lk. 16:22).
Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika walinzi. (Ebr, 13:2). Ambapo kila Mwanadamu ana Malaika wake wa kumlinda na kumuongoza Roho na Mwili, ndie Malaika wake mlinzi, (Zab, 91:11, Mt. 18:10).
Malaika wote sio sawa, wapo Malaika Wakuu, Malaika wanaomtumikia Mungu Mbinguni kwa mfano Makerubi na Maserafi, na pia wapo Malaika walinzi.
Malaika wakuu ni Mikaeli, Gabrieli na Raphaeli (Dn, 10:13, Tobiti 12:15, Lk 1:26).
Mashetani kazi yao ni kuteswa Motoni na hutaka kudhuru Roho na Miili ya wanadamuna kutupoteza milele. (1 Petro, 5:8, Yoh, 8:44).

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa uwezo wa kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake baada ya kuona kile anachokitaka hakipati kwa mpenzi wake.

 

Yafuatayo ni mambo ambayo wanawake wanapenda wanaume wayajue hata kabla ya kuambiwa;

1. Wanawake wanapenda ufuate anachokitaka

Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu. Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanya vile wanavyovipenda.

2. Hupendelea tendo la ndoa lidumu muda mrefu

Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda kuungana na wewe kihisia kupitia kushikana, kubusu nakadhalika. Wakati wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka. Kwa hiyo wanapenda tendo la ndoa lidumu lakini lisichoshe.

 

3. Wanataka mwanaume jasiri sio anayetumia nguvu

Wanawake wanataka wanaume walio jasiri wa kufanya nasio wanaotumia nguvu na ubabe. Wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu na mwisho kuwaumiza wapenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. Wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri kwamba sio kutumia nguvu na ubabe.

4. Wanawake hawafanani

Wanawake wanapenda wanaume wajue kuwa sio wanawake wote hupenda vitu sawa. Wanaume wengine hufikiri kuwa kwa sababu mpenzi wake wa zamani alikua anapenda kufanyiwa alikuwa basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta njia ya kukukwepa. Kwa hiyo mwanamme anatakiwa amjue mpenzi wake kibinafsi yeye kama yeye na sio kumjua kwa kumfananisha na wanawake wengine. Mwanamme amfanyie mpenzi wake kama anavyopendelea na sio kama anavyofikiri wanawake wanapendelea.

 

5. Kumfurahisha mwanamke sio ufundi tuu bali ni mapenzi

Wanawake wanapenda kuonyeshwa upendo au mapenzi ya dhati. Wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi na uzoefu katika haya mapenzi, ila wanasema hiyo sio kitu bora zaidi, wanachokitaka ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Mapenzi ni kichocheo kikubwa cha kumridhisha mwanamke.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa mojakirahisi kabisa kwenye simu yako.

Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ngโ€™ombe

Mahitaji

Mpunga – 4 vikombe

Nyama – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 3

Mbatata/viazi – 7 vidogodogo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu

Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 3 vipande

Hiliki – 7 punje

Pilipili manga nzima – 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Mafuta – ยฝ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele weka kando
Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye ufugaji wa nyuki wa asali

Mtaalamu wa nyuki

Unapohitaji unahitaji kufuga nyuki ni lazima uwe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya nyuki. Unapoanza ni lazima uulize mtaalamu wa nyuki, wafugaji wenzako ambao wana uzoefu wa kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya ufugaji wa nyuki.

Sehemu salama kwa ajili ya mzinga

Unahitaji kutafuta mahali pazuri, salama, na penye sifa ya kufugia nyuki. Vifaa vyote vikishapatikana kinachofuata ni kuchagua mahali gani pa kuweka mzinga. Hakikisha sehemu hii ni mahali ambapo makundi ya nyuki hukusanyika mara kwa mara.

Uwekaji Bora wa Mizinga

Ukishatafuta ya sehemu ya kuweka mizinga, kinachofuata ni kuandaa mizinga kwa ajili ya kuweka panapotakiwa.

Mambo ya muhimu ya kuzingatia
โ€ข Kwanza Safisha mzinga kuondoa uchafu wote, utando wa buibui na aina nyingine za wadudu.
โ€ข Kisha Weka chambo kwenye mzinga (maranyingi nta hutumika kama chambo) kwa kuipaka katika kuta za mzinga kwa ndani.
โ€ข Halafu Mzinga unaweza kutundikwa kwenye mti, kwenye nguzo, kuweka kwenye jukwaa au kwenye miamba. Hii inategemea wewe mwenyewe anapendelea njia ipi.

Jinsi ya kufanya nywele zako ziwe na mvuto na kuvutia zaidi

Mwanamke unywele hasa ukiwa nao, hii ni kauli upya ambayo Muungwana blog inakupa siku ya leo. Miongoni mwa maswali ambavyo huwa tunaulizwa na wasamoaji wetu ni pamoja ni kwa jinsi gani naweza kutengeneza nywele zangu ili ziwe za kuvutia?

Basi nasi bila ya haiana yeyote ile tunakuletea somo hili maalum kwa ajili ya watu wote ambao wanatamani kujua namna ya kuzifanya nywele zako zivutie. Kwanza kabisa kuna vitu vingi vinavyoweza kufanya nywele zako zikakosa afya na mvuto, vitu kama vumbi, upepo, mvua, jua, maji na madawa tunayoweka kwenye nywele zetu pamoja na vyakula tunavyokula ni chanzo kikuu cha nywele zetu kuharibika na kukosa afya na mvuto

Hivyo zifuatazo ndizo njia ya kufanya nywele zako zivutie:

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako

Tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.

Usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.

Jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.

Kula vyakula venye protin na matunda

kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.

Kata ncha za nywele zako

kukata ncha za nywele zako kunasaidia kufanya nywele zako kujizaa upya, mara nyingi seli katika ncha za nywele hufa. seli zinapokufa huzui nywele zinazozaliwa kushindwa kustawi vyema na hivyo kuzifanya nywele zako kukosa afya. japo wanawake wengi huwa hawapendi kukata ncha za nywele zao wakihofia nywele zao kuonekana fupi. lakini ukweli ni kwamba unapokata ncha za nywele zako unasaidia nywele zako kupata nafasi ya kukua vizuri na kuwa zenye afya nzuri na kuvutia.

Osha nywele zako angalau mara moja kwa wiki

kuosha nywele zako angalau mara moja kwa wiki kutasaidia kuzifanya nywele zako ziwe na afya. Hata kama uko busy sana basi jitahidi isipite wiki mbili bila kuonsha nywele zako.

Zifunge nywele zako kabla ya kulala

Unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika

Tumia mafuta asili

Badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.

Zilinde nywele zako na jua

W akati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. Pia unaweza kuzipaka sunscreen.

Kutibu chunusi kwa ute mweupe wa yai

Hii inaweza kuchukuliwa kama njia rahisi na isiyo na gharma katika kutibu chunusi. Kwa mjibu wa wanasayansi kutumia mchanganyiko wa ute mweupe wa yai na maji maji ya limau ni namna nzuri ya kutibu chunusi.

Changanya ute mweupe wa mayai matatu na kijiko kidogo kimoja cha maji maji ya limau na ukoroge vizuri. Pakaa mchanganyiko huu usoni na uache kwa dakika 15 hivi kisha jisafishe na maji moto.

Fanya zoezi hili mara 1 au 2 tu kwa wiki

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About