Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuingia utu uzima,0 yaani kuwa mwanamke. Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka 8 na umri wa miaka 18. Lakini, kuvunja ungo haina maana kwamba unahitaji kuanza kujamii ana. Kwa sababu ukijamii ana kuna hatari ya kupata mimba!
Mwanzoni siku za hedhi zinaweza kuwa na mabadiliko sana. Ni baada ya muda ndipo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo, wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Idadi ya siku katika mzunguko wa hedhi ni siku 21 hadi 35.Ukitaka kuelewa kabisa maana ya kutoka damu za mwezi, lazima nieleze kuhusu mzunguko wa hedhi. Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa.
Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mirija ya kupitisha mayai, i ina maana, kwamba atakuwa amejamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka. Kama yai halikurutubishwa, basi hufa na hutangulia kutoka kama ute, pia utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu. Hii ndiyo hedhi yenyewe.
Endapo msichana amejamiiana na mvulana na yai likarutubushwa, hataona hedhi na aelewe kwamba kuna uwezekano kwamba mimba imetungwa.
Mzunguko wa hedhi kwa baadhi ya wasichana hauna mpangilio mwanzoni, hivyo endapo hupati hedhi inayolingana kila mwezi usijali.
Katika hali ya kawaida usipopata hedhi na hukujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili. Hali hii ikiendelea au ukiwa na wasiwasi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya
Read and Write CommentsReferences:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments