1000+ Vichekesho vipya: Vichekesho vya AckySHINE

Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe

Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi

PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!

Angalia kile kitabia cha kufuta namba kwenye simu kilivyomponza huyu jamaa

Jana nilijipa kazi ya kufuta vitu visivyo na umuhimu kwenye sm yangu. Katika futa futa si nimefuta namba ya bosi wangu. Halafu boss mwenyew wa kike. Mida ya Saa mbili usiku nikawa chumbani kwangu. Mara simu ýäñgù ikawa inaita. Kucheki namba ngeni. Nikapokea baada ya salamu. Me→nani mwenzangu?? Boss→we hunijui me ?? Me→usinijbu swali kwa swali Nita kublacklist sasa hiv. Sipendagi ujinga.. Kwa sasa nazurura tu mtaani na roba langu La machupa

Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari

Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!

Madhara ya kubeba nauli kamili tuu. Cheki kilichonipata

Kubeba nauli kamili nayo ni shida
Yani nimepanda daladala
Kondakta mmoja akaingia kwenye Gari amevaa suti za blue za daladala na miwani Kisha akakusanya pesa Gari Zima alafu akakaa siti ya nyuma baade Kondakta mwingine akaanza kukusanya pesa watu wakalalamika na kusema tayari tumelipa na kumuonyesha tuliemlipa Kondakta akacheka na kusema huyo tuliemlipa ni kipofu na alikuwa anaomba msaada..!!

SOMA HII: Kama wewe ndo baba au mama hapa ungefanyaje!???

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit,
boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?

Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu! Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
Mama akasema msinizingue nyie…Mbona siwaelewi..
Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.

Mama akaenda jikoni..
Bakari: akaita mamaa
Mama : bee bakari
Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.?
Mama kimya
Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.

Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tu…..😄😄😄😄😄

Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Alifanya hivi;
Siku ya kwanza

MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

Shopping Cart
27
    27
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About