1000+ Vichekesho vipya: Vichekesho vya AckySHINE

Angalia jamaa alivyouweza huu mchepuko wake

Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti ” nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz””!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi “nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!” Akanjbu “elfu 20,000 tu mpenzi” Mtuhurumie jamani ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Maujanja ya kumkalisha mwanamme wako nyumbani weekend haya hapa

Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.

Kumbe wanaenda kunywa supu unasubiri wee mpaka alasiri au jioni

Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.

Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??

Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO

Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.

Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoniโ€ฆ

Mara blenda priiiiiโ€ฆ juiceโ€ฆ ama milk shakeโ€ฆ. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..

Wakati anakunywa juice ama milk shakeโ€ฆAnza kukuna naziโ€ฆ

Chambua mnafuโ€ฆ

Hapo jikoni kuna kanyama kanachemkaโ€ฆ katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..

ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoniโ€ฆ hahahaha kwenye frijiโ€ฆ wala hatumi..

Hahaahhaโ€ฆ utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.

Mmiminie supuโ€ฆ

Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..

Muulize kuna chapatiโ€ฆMpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..

.Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeivaโ€ฆMpe ale..Mshushie na glass ya mtindiโ€ฆHahahaha..

analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipigeโ€ฆ

Hahahahahahaโ€ฆ.Baada ya hapo acha apumzikeโ€ฆ aogeโ€ฆ

Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..

Mkimaliza muombe pesa ya sokoniโ€ฆ

NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.

Hahahahaha.. jamaniโ€ฆ

Hahahahahaโ€ฆ yani kwa raha ya supuโ€ฆ nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu janaโ€ฆ hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njooโ€ฆ unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.

Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwaโ€ฆ

Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongoโ€ฆ. hahahahahahahahahaha.

Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhaziliโ€ฆ
Wali maharage kama jeshi la j

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Angalia Kiingereza kilivyoniponza

Shikamoo kingereza..!

Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:

Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!

Price: TSH 44,000/=

Nikaagiza!

Nilipoletewa ndio nagundua kwamba:ย ni makande na parachichiย ..๐Ÿค”

hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo๐Ÿค’๐Ÿ’จ

Cheki kilichonipata sasa, ungekua wewe ungefanyaje?

Siku moja katika pitapita zangu nikakutana na mtoto mmoja mkali balaa yaani ni mzuri sanaaaa, moyo ukanituma nimuimbishe mtoto akakubali kwamba nitafute siku tukae tuongee vizuri akasema nimpe namba yangu ya simu.

ย 

Ebwana si akatoa simu hiyo inauzwa laki sita mimi hapa nina kisimu cha tochi tena nimefunga na rababendi
Je, wewe ungeendelea kumtajia namba zako!!!

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About