MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI

MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.

ORODHA YA MITAGUSO MIKUU

β€’ Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)
β€’ Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)

HISTORIA YA MITAGUSO MIKUU

Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la mashariki na la magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote. Kwa namna ya pekee Mtaguso II wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.

Mtaguso I wa Nisea (325)

Mtaguso I wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa (tangu mwaka 338) mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.
Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia. 2
Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I (314-335) aliwakilishwa na mapadri wawili.
Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria (Misri), ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.
Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa (yaani dhati) ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.
Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya Springi, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.
Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

Mtaguso I wa Konstantinopoli (381)

Mtaguso I wa Konstantinopoli ndio wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene yaliyofanyika wakati wa mababu wa Kanisa. Uliitishwa na kaisari Theodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.
Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, wakathibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso I wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.
Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga dhati ileile ya Baba.
Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Mtaguso wa Efeso (431)

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosi II; Papa Selestini I (422-432) alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.
Patriarki huyo alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani “mbeba Mungu”, na Maria Christotokos, “Mama wa Kristo” si Theotokos, “Mama wa Mungu”.
Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.
Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotamia na kuenea hata Asia mashariki.
Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote. Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila kusaidiwa na neema ya Mungu.

Mtaguso wa Kalsedonia (451)

Mtaguso wa Kalsedonia (leo katika nchi ya Uturuki) unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumeni iliyofanyika katika historia ya Kanisa.
Mtaguso huo uliitishwa na kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.
Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.
Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.
Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake.
Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.
Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I (440-461) aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike. 3
Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo hao hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.
Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

Mtaguso II wa Konstantinopoli (553)

Mtaguso II wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.
Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.
Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.
Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555) na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.
Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa tano kati ya mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa Mtaguso wa Kalsedonia.

Mtaguso III wa Konstantinopoli (680-681)

Mtaguso III wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumeni.
Kaisari Konstantino IV wa Konstantinopoli ndiye aliyeuitisha na kuuendesha kuanzia tarehe 7 Novemba 680 hadi tarehe 16 Septemba 681.
Suala kuu lililosumbua Wakristo wa karne VII lilimhusu Yesu Kristo upande wa utashi. Ulikuwa unaenea mtazamo wa kwamba hakuwa na utashi wa kibinadamu, bali ule wa Kimungu tu.
Lakini wamonaki Sofronio wa Yerusalemu na Maksimo Muungamadini walipinga vikali jaribio hilo la kuleta upatanisho wa Waorthodoksi wa Mashariki (Wamisri n.k.) kwa kumpunguza Yesu katika ubinadamu wake kamili uliosisitizwa na Mtaguso wa Kalsedonia (451).
Vilevile Papa Martin I (649-655), katika mtaguso uliofanyika Laterani, alilaani mtazamo huo, kinyume cha Kaisari na Patriarki wa Konstantinopoli.
Konstantino IV alikubaliana na Papa Agatoni (678-681), na hivyo Mtaguso III wa Konstantinopoli ulilaani rasmi mtazamo wa kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu.

Mtaguso II wa Nisea (787)

Mtaguso II wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787 ili kujadili matumizi ya sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I (772-795).
Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.
Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.
Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Konstantinopoli (717-741) wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake.
Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa hasa na wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.
Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI.
Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.
Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.
Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.
Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

Mtaguso IV wa Konstantinopoli (869-870)

Mtaguso IV wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki linahesabu kuwa Mtaguso Mkuu IV wa Konstantinopoli ule uliofanyika tangu tarehe 5 Oktoba 869 hadi 28 Februari 870.
Uliitishwa na Kaisari Basili I wa Konstantinopoli na Papa Adrian II (867-872), kwa sababu mwisho wa ikonoklastia katika sinodi ya mwaka 843 ulikuwa umeacha athari kubwa katika Kanisa la Mashariki. 4
Patriarki Metodi wa Konstantinopoli (843-847) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III, alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I, mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa mlei msomi Fosyo ambaye kwa siku chache alipewa daraja na kutawazwa, lakini kufikia Februari 859 lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na Papa Nikolaus I (858-867), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika Konstantinopoli kati ya Aprili na Agosti 861 wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za kiutamaduni na za kisiasa pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja umoja kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka 867, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama mzushi na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe 5 Oktoba 869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe 7 Oktoba wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa Papa, lakini wakashindwa na kutengwa (29 Oktoba).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe 12 Februari 870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (28 Februari), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo maaskofu wakuu 37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka 877), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (879-880), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawakubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa Papa Yohane VIII (872-882) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka 886.

Mtaguso I wa Laterano (1123)

Mtaguso I wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.
Mahali pake ni kwenye Kanisa Kuu la Roma (Italia) katika mtaa wa Laterano, alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati, halafu umuhimu wake ukapungua Papa alipohamia Vatikano.
Mtaguso uliitishwa na Papa Kalisti II (1119-1124) mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.
Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.
Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900 kati ya maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi). Papa mwenyewe aliendesha vikao.
Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

Mtaguso II wa Laterano (1139)

Mtaguso II wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II (1130-1143), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi. Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma (Italia).
Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II (1124-1130): hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.
Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.
Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II. Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita Anakleti II.
Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa (1138). 5
Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi, Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.
Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso I wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

Mtaguso III wa Laterano (1179)

Mtaguso III wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.
Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja. Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Mtaguso IV wa Laterano (1215)

Mtaguso IV wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.
Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.
Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.
Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.) na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.
Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Mtaguso I wa Lyon (1245)

Mtaguso I wa Lyon uliitishwa na Papa Inosenti IV (1243-1254) tarehe 24 Juni 1245 akiwa huko Lyon (Ufaransa), alipokimbilia usalama. Waliushiriki karibu viongozi 150 wa Kanisa Katoliki, ambalo linauhesabu kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tatu.
Baada ya mashindano makali kati ya mamlaka ya kiroho ya Papa na ile ya kisiasa ya kaisari huko Ulaya, mtaguso huo uliitishwa ili kumhukumu moja kwa moja kaisari Federiko II kuwa Mpinga Kristo.
Mtaguso ulianza tarehe 28 Juni 1245 wakiwepo maaskofu 144, halafu ukawa na vikao viwili vingine tena tarehe 5 Julai na 17 Julai. Hatimaye maaskofu walikuwa 225.
Mwanzoni papa alitangaza matatizo 5 yanayotesa Kanisa:
β€’ kuharibika kwa imani na maadili;
β€’ kushindwa kuikomboa Nchi takatifu (Yerusalemu ulitekwa tena na Waturuki mwaka 1244);
β€’ kudumu kwa farakano la Waorthodoksi;
β€’ kujitokeza hatari ya kuvamiwa na Watartari;
β€’ kupambana na Federiko II.
Maamuzi yalitangazwa tarehe 25 Agosti tu, baada ya papa na wasaidizi wake kurekebisha miswada, yakapokewa na kufafanuliwa na vyuo vikuu. Lakini uamuzi wa kumuondoa madarakani kaisari haukuweza kutekelezwa hata kwa vita.

Mtaguso II wa Lyon (1274)

Mtaguso II wa Lyon unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na nne. Ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne XIII yote.
Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV (1265-1268).
Ndipo Papa Gregori X (1271-1276) alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.
Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu:
β€’ kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu,
β€’ kuungana tena na Waorthodoksi,
β€’ kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.
Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.
Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.
Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI (1963-1978) tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika Β«bila kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibiΒ». 6
Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa (1282), mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.
Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye (1291) Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.
Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

Mtaguso wa Vienne unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Bonifas VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314) alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa), karibu na himaya ya mfalme huyo.
Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
β€’ suala la Wahekalu;
β€’ vita vya msalaba;
β€’ hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
β€’ urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Kuhusu Wahekalu, mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Kuhusu Vita vya Msalaba, uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Kuhusu imani, ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Kuhusu urekebisho, ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418)

Mtaguso wa Konstanz (Ujerumani) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na sita. Uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).
Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja. Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa β€œkatika kichwa na viungo vyake”.
Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.
Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.
Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Mtaguso wa Firenze (1431-1445)

Mtaguso wa Firenze uliitishwa na Papa Martin V (1417-1431) mwaka wa mwisho wa uongozi wake ili kutekeleza shingo upande agizo la Mtaguso wa Konstanz la kwamba mtaguso ufanyike mara kwa mara.
Mtaguso ulianza Basel (Uswisi) chini ya Papa Eugenio IV (1431-1447), ukiwa na maaskofu wachache kulingana na mapadri na walei wenye haki ya kupiga kura.
Ingawa mtaguso ulifaulu kupatanisha wafuasi wa Hus na Kanisa, na kutoa sheria kadhaa za urekebisho kwa kibali cha Papa, baadaye ulianza kumshambulia yeye pamoja na makardinali, ukionyesha wazi wengi waliuona una mamlaka ya juu kuliko Papa, kinyume cha mapokeo.
Hapo Eugenio IV aliuvunja halafu akauhamishia Ferrara (Italia), ulipokutanika tarehe 8-1-1438, bila kujali upinzani wa wale ambao walibaki Basel na kumchagua antipapa wa mwisho, Felix V.
Huko Italia ulifika ujumbe mkubwa kutoka Konstantinopoli kwa ajili ya kurudisha umoja kati ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Kati ya wajumbe 700 kulikuwa na kaisari na patriarki wa Konstantinopoli, walioogopa Waturuki watateka mji wao (kama ilivyotokea kweli tarehe 29 Mei 1453); hivyo walihitaji msaada wa Wakristo wenzao wa magharibi.
Ferrara iliachwa kutokana na uhaba wa majengo na hofu ya tauni. 7
Mwaka 1439 mtaguso ulihamia Firenze ukafikia makubaliano ya kurudisha umoja (6-7-1439), ingawa uamuzi ukashindwa kutekelezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na upinzani wa waumini wa Konstantinopoli.
Vilevile tarehe 22-11-1439 yalifikiwa makubaliano na Waarmenia na tarehe 4-2-1440 yale na Wamisri.
Hatimaye tarehe 24-9-1443 mtaguso ulihamia Roma kwenye Laterano. Huko yalifikiwa makubaliano ya kurudisha umoja na Wasiria kadhaa (30-4-1444) na Wakaldayo na Wamaroni wa Kupro (7-8-1445).
Hakuna hati kuhusu mwisho wa mtaguso. Lakini waliobaki Basel na kujitenga na Papa, kufikia tarehe 19-4-1449 walimkubali Nikolaus V na siku sita baadaye walifunga mkutano wao.
Mtaguso huo ulichochea Wakristo wa magharibi kutamani mawasiliano na wenzao wa Ethiopia na India, jambo lililowafanya waanze zile safari za mbali kupitia baharini zilizowafikisha Afrika Kusini na Mashariki, China na Amerika.

Mtaguso V wa Laterano (1512-1517)

Mtaguso V wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma. Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.
Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.
Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.
Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.
Kabla yake kilifanyika “Kitaguso” cha Pisa: kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa (Italia) kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon (Ufaransa).
Papa aliitikia β€œkitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.
Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso wenyewe hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.
Upande wa matokeo, utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

Mtaguso wa Trento (1545-1563)

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.
Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne XVI.
Mtu wa kwanza kulilia mtaguso ambao uamue kati yake na papa alikuwa Martin Luther (1517): huko Ujerumani ombi lake liliungwa mkono na wengi, pamoja na kaisari Karolo V aliyeuona kuwa njia ya kurekebisha Kanisa lakini pia ya kujiimarisha kimamlaka. Ndiyo sababu kuu iliyomfanya Papa Klementi VII (1523-1534), aliyesimama upande wa Ufaransa, kukataa kabisa kuuitisha.
Wazo hilo lilipata nguvu tena chini ya mwandamizi wake, Papa Paulo III (1534-1549), ambaye mwaka 1536 aliitia kwanza Mantova halafu Vicenza maaskofu na maabati wote, pamoja na wafalme wadogo wengi wa Dola takatifu la Kijerumani.
Baada ya juhudi mbalimbali kushindikana, mwaka 1542 uamuzi ulifikiwa wa kuitisha mtaguso huko Trento kwa sababu ni mji wa Italia lakini ulikuwa ndani ya mipaka ya dola hilo. Hatimaye (Novemba 1544) papa aliweza kutoa hati ya kuitisha mtaguso inayoitwa Laetare Jerusalem.
Mtaguso ulifunguliwa rasmi tarehe 13 Desemba 1545 katika kanisa kuu la Mt. Vigilio.
Mwanzoni mtaguso ulikuwa na maaskofu wachache, karibu wote kutoka Italia, ukatawaliwa na wajumbe wa papa. Kati ya makardinali wapya (Contarini, Sadoleto, Carafa, Fisher na huyo Pole) wengi walipenda urekebisho.
Zilijadiliwa na kupitishwa hasa dogma dhidi ya mafundisho ya Waprotestanti, kama vile kuhusu utakaso na wokovu. Pamoja na kupitisha tafsiri rasmi ya Biblia katika Kilatini iliyo maarufu kwa jina la Vulgata, kati ya maamuzi muhimu zaidi upo ule wa kudai maaskofu waishi katika majimbo yao ili kufanya uchungaji uliowapasa.
Baada ya mtaguso kuhamishiwa Bologna, Papa Paulo III aliusimamisha mnamo Septemba 1549.
Papa Julius III (1550-1555) aliuitisha tena kuanzia tarehe 1 Mei 1551 na zikatolewa hati juu ya sakramenti za Ekaristi, Kitubio na Mpako wa wagonjwa. Polepole waliohudhuria waliongozeka, 8
wakiwemo Waprotestanti wengi pia, wakidai wanateolojia wao wawe na haki ya kupiga kura na hati zilizokwishatolewa zifutwe. Ndipo ilipoonekana wazi kwamba tofauti katika imani ni kubwa mno.
Majeshi ya Kiprotestanti yalipokaribia Trento, Papa alikubali kusimamisha tena mtaguso tarehe 28 Aprili 1552.
Sehemu ya mwisho ya mtaguso baada ya kuitishwa ilichelewa kuanza hadi tarehe 18 Januari 1562, tena ilikabili matatizo mengi, lakini iliokolewa na kutawaliwa na askofu wa Milano Karolo Borromeo, mpwa wa Papa Pius IV (1559-1565) aliyemalizia haraka mtaguso wakiwemo wajumbe 255.
Katika sehemu hiyo yalitolewa mafundisho rasmi kuhusu Misa, Daraja takatifu na Ndoa, Toharani, sala kwa watakatifu, heshima kwa masalia na rehema. Pia Kanisa la Roma lilikubaliwa kama mama na mwalimu wa makanisa yote. Maaskofu wote walitakiwa kuahidia utiifu kwa Papa, ambaye peke yake ana haki ya kuitisha mtaguso mkuu. Kwa msingi huo, mtaguso ulimuachia Papa kuthibitisha maamuzi yote, naye alifanya hivyo bila kujali upinzani wa maofisa wake huko Roma.
Isitoshe, mwishoni, maamuzi mbalimbali yaliachwa mikononi mwa Papa na ofisi zake, yakachukuliwa miaka iliyofuata; kati yake, urekebisho wa Breviari na Misale, kwa kusawazisha liturujia za majimbo ya magharibi (isipokuwa chache, kama ya Milano na Lyon) kulingana na mapokeo ya Roma. Halafu ikatolewa Katekisimu ya Trento na Orodha ya vitabu vilivyokatazwa (Index librorum prohibitorum).

Mtaguso I wa Vatikano (1869-1870)

Mtaguso I wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870, kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati Dei Filius juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema “ex cathedra”, yaani “kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

Mtaguso II wa Vatikano (1962-1965)

Malengo ya Mtaguso II wa Vatikano

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa Papa, mwenye heri Yohane XXIII alitangaza uamuzi wake wa kuitisha mtaguso mkuu akiamini kwamba utaweza kuandaa na kusababisha ustawi mpya wa maisha ya Kanisa. Lengo kuu la mtaguso lilikuwa kuliamsha Kanisa likumbuke wito wake na kwa kujifanya upya kwa ndani lipate msukumo mpya wa kimisionari ili kuwatangazia watu wote ujumbe wa milele wa wokovu, amani na umoja.
Tangazo hilo lilitolewa tarehe 25-1-1959. Baada ya maandalizi, Mtaguso II wa Vatikano ulifunguliwa tarehe 11-10-1962. Vikao vinne vikafanyika mpaka ulipofungwa tarehe 8-12-1965. Kila kikao kilianza Oktoba na kumalizika Desemba ya miaka hiyo.
Kwa kuwa Yohane XXIII alifariki tarehe 2-6-1963, vikao vitatu vya mwisho viliongozwa na mwandamizi wake, Paulo VI, na hati zote kumi na sita zikatolewa chini yake pia kwa kupigiwa kura ya ndiyo karibu kwa kauli moja. Maaskofu na wakuu wa mashirika kadhaa wenye haki ya kupiga kura walikuwa kama elfu tatu, wakiwakilisha karibu Kanisa lote duniani, isipokuwa nchi zile zenye kuwadhulumu Wakristo.

Mafundisho makubwa ya Yesu Kristo

Heri

Basi Yesu alipoona makutano, alipanda
mlimani akaketi chini, nao wanafunzi
wake wakamjia. 2Ndipo akaanza kuwafundisha,
akisema:
3 β€œWana heri walio masikini wa roho,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
4Wana heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
5Wana heri walio wapole,
maana hao watairithi nchi.
6Wana heri wenye njaa na kiu ya haki,
maana hao watatoshelezwa.
7Wana heri wenye huruma,
maana hao watapata rehema.
8Wana heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
9Wana heri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10Wana heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
11Mna heri ninyi watu watakapowashutumu
na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya
aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini
na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni
kuu.

Chumvi na Nuru

13β€˜β€˜Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini
chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje
kurudishiwa ladha yake tena ? Haifai tena kwa
kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na
watu.
14β€˜β€˜Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji
uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. 15Wala
watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli.
Badala yake, huiweka kwenye kinara chake,
nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani
ya ile nyumba. 16Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze
mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu
mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kutimiza Sheria

17β€œMsidhani kwamba nimekuja kuondoa
Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.
18Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu
na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja
ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo
yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe
kimetimia. 19Kwa hiyo, ye yote atakayevunja
mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri
hizi, naye akawafundisha wengine kufanya
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa
Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na
kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika
Ufalme ya Mbinguni. 20Kwa maana nawaambia,
haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria
na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika
Ufalme wa Mbinguni.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Hasira

21β€œMmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, β€˜Usiue, ye yote atakayeua
atapasiwa hukumu.’ 22Lakini mimi nawaambia
kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake
wa kiume au wa kike, atapasiwa hukumu. Tena,
ye yote atakayemwambia ndugu yake wa kiume
au wa kike, β€˜Raca’a, yaani kumdharau na
kumdhihaki, atapasiwa kufanyiwa baraza. Lakini
ye yote atakayesema β€˜We mpumbavu ulaaniwe!’
Atapasiwa hukumu ya moto wa jehanam.
23β€œKwa hiyo, kama unatoa sadaka yako
madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako
ana kitu dhidi yako, 24iache sadaka yako hapo
hapo, mbele ya madhabahu, uende kwanza
ukapatane na ndugu yako wa kiume au wa kike,
kisha urudi na ukatoe sadaka yako.
25β€œPatana na mshtaki wako upesi wakati
uwapo njiani pamoja naye kwenda
mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia
mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia
mikononi mwa walinzi, nawe ukatupwa
gerezani. 26Amin, nakuambia, hutatoka humo
mpaka umelipa hadi senti ya mwisho”

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Uzinzi

27β€œMmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Usizini’.
28Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote
amtazamaye mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29Jicho
lako la kuume likikufanya utende dhambi, ling’oe
ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam. 30Kama mkono wako
wa kuume ukikufanya utende dhambi, ukate
uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Talaka

31β€˜β€˜Pia ilinenwa kwamba, β€˜Mtu ye yote
amwachaye mkewe na ampe hati ya talaka.’
32Lakini mimi nawaambia, ye yote amwachaye
mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati,
amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na ye yote
amwoaye yule mwanamke aliyeachwa azini.’’

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kuapa

33β€œTena mmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, β€˜Usiape kwa uongo, bali
timizeni, nadhiri zile ulizofanya kwa Bwana’
34Lakini mimi nawaambia,’’Msiape kabisa, ama
kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha
Mungu, 35au kwa nchi, kwa kuwa ndipo mahali
pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu,
kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36Nanyi
msiape kwa vichwa vyenu kwa kuwa hamwezi
kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe
au mweusi. 37β€˜Ndiyo,’ yenu iwe β€˜Ndiyo’ na
β€˜Hapana’, yenu iwe β€˜Hapana.’ Lo lote zaidi ya hili
latoka kwa yule mwovu.’’

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kulipiza Kisasi

38β€œMmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Jicho kwa
jicho na jino kwa jino.’ 39Lakini mimi nawaambia,
msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu
akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na
la pili pia, 40Kama mtu akitaka kukushtaki na
kuchukua shati lako, mwachie achukue na koti
pia. 41Kama mtu akikulazimisha kwenda
kilometa moja, nenda naye kilometa mbili.
42Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie
kisogo yeye atakaye kukukopa.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Upendo Kwa Adui

43β€˜β€˜Mmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Mpende
jirani yako na umchukie adui yako.’ 44Lakini
mimi ninawaambia : Wapendeni adui zenu na
waombeeni wanaowatesa ninyi, 45ili mpate
kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa
maana Yeye huwaangazia jua lake watu waovu
na watu wema, naye huwanyeshea mvua
wenye haki na wasio haki. 46Kama mkiwapenda
wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani?
Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je,
mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu
wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 48Kwa hiyo
iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni
alivyo mkamilifu.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwapa Wahitaji

β€˜β€˜Angalieni msitende wema wenu mbele ya
watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya
hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu
aliye mbinguni.
2β€˜β€˜Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige
panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki
katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na
watu. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha
kupokea thawabu yao. 3Lakini ninyi mtoapo
sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa
kushoto usijue mkono wako wa kuume
unachofanya, 4ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo
Baba yako wa mbinguni, Yeye aonaye sirini
atakupa thawabu kwa wazi.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu kusali

5β€œNanyi msalipo, msiwe kama wanafiki,
maana wao hupenda kusali wakiwa
wamesimama katika masinagogi na kando ya
barabara ili waonekane na watu. Amin, amin
nawaambieni, wao wamekwisha kupata
thawabu yao. 6Lakini wewe unaposali, ingia
chumbani mwako, funga mlango na umwombe
Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye
sirini atakupa thawabu yako. 7β€œNanyi mnaposali
msiseme maneno kama wafanyavyo watu
wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani
kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa
maneno yao. 8Msiwe kama wao, kwa sababu
Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla
hamjamwomba.’’
9β€˜β€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba :
β€œBaba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
10Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa duniani
kama huko mbinguni.
11Utupatie leo riziki zetu za kila siku.
12Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tulivyokwisha
kuwasamehe wadeni wetu.
13 Usitutie majaribuni,
bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu,
kwa kuwa Ufalme ni Wako na nguvu
na utukufu hata milele. Amen.”
14Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine
wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe pia na ninyi. 15Lakini
msipowasamehe watu wengine makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa
yenu.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kufunga

16β€œMnapofunga, msiwe wenye huzuni kama
wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja
nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba
wamefunga. Amin, amin nawaambia wao
wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu.
17Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani
na kunawa nyuso zenu 18ili kufunga kwenu
kusionekane na watu wengine ila Baba yenu
aliye sirini, naye Baba yenu aonaye sirini
atawapa thawabu yenu kwa wazi.”

Akiba Ya Mbinguni

19β€œMsijiwekee hazina duniani, mahali
ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi
huvunja na kuiba. 20Lakini jiwekeeni hazina
mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu
haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.
21Kwa sababu mahali akiba yako ilipo, hapo
ndipo pia moyo wako utakapokuwa.’’

Jicho Ni Taa Ya Mwili

22β€˜β€˜Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni
nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru.
23Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote
utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru
iliyomo ndani yako ikiwa giza, hilo ni giza kuu
namna gani ! ”

Mungu Na Mali

24β€˜β€˜Hakuna mtu ye yote awezaye
kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama
atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine,
au atashikamana sana na huyu na kumdharau
huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia
Mungu na malia.’’

Msiwe Na Wasiwasi

25β€˜β€˜Kwa hiyo nawaambia, msiwe na
wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au
mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa
nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili
zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa
angani, wao hawapandi wala hawavuni au
kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni
huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi
kuliko hao ndege? 27Ni nani miongoni mwenu
ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza
kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha
yake au kuongeza dhiraa mojab kwenye kimo
chake ?
28β€˜β€˜Nanyi kwa nini kujitaabisha kwa ajili ya
mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo.
Hayafanyi kazi wala hayafumi. 29Lakini
nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari
yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo
maua. 30Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi
majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho
yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri
zaidi, enyi wa imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na
wasiwasi, mkisema, β€˜Tutakula nini?’ Au
β€˜Tutakunywa nini?’ Au β€˜Tutavaa nini?’ 32Kwa
maana watu wasiomjua Mungu ndio
wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa
mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo
yote. 33Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa
Mungu na haki yake na haya yote
mtaongezewa. 34Kwa hiyo msiwe na wasi wasi
kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia
yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwahukumu Wengine

β€œUsihukumu ili usije ukahukumiwa. 2Kwa
maana kwa jinsi ile unavyowahukumu
wengine, ndivyo utakavyohukumiwa na kwa
kipimo kile utakachotoa ndicho utakachopokea.
3β€˜β€˜Kwa nini unatazama kibanzi kidogo
kilichomo kwenye jicho la ndugu yako na wala
huoni boriti iliyoko kwenye jicho lako? 4Au
unawezaje kumwambia ndugu yako, β€˜Acha nitoe
kibanzi kwenye jicho lako wakati kuna boriti
kwenye jicho lako mwenyewe ?’ 5Ewe mnafiki,
toa kwanza boriti kwenye jicho lako mwenyewe,
nawe ndipo utakapoona wazi ili kuondoa kibanzi
kilichoko kwenye jicho la ndugu yako.
6β€˜β€˜Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu, wala
msitupie nguruwe lulu zenu. Kama mkifanya
hivyo, watazikanyaga kanyaga na kisha
watawageukia na kuwararua vipande vipande. ”

Omba, Tafuta, Bisha

7β€œOmbeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi
mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
8Kwa maana kila aombaye hupewa, naye
atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa
mlango.
9β€˜β€˜Au ni nani miongoni mwenu ambaye
mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe?
10Au mwanawe akimwomba samaki atampa
nyoka? 11Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua
jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi
sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu
vizuri wale wamwombao ? 12Kwa hiyo cho chote
ambacho mngetaka mtendewe na watu, ninyi
nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii
ndiyo Torati na Manabii.’’

Njia Nyembamba Na Njia Pana

13β€˜β€˜Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba,
kwa maana lango ni pana na njia ni pana
ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa
kupitia lango hilo. 14Lakini mlango ni
mwembamba na njia ni finyo ielekayo kwenye
uzima, nao ni wachache tu waionao.’’

Mti na Tunda lake

15β€œJihadharini na manabii wa uongo,
wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya
kondoo, lakini ndani wao ni mbwa mwitu
wakali.16Mtawatambua kwa matunda yao. Je,
watu huchuma zabibu kwenye miiba au tini
kwenye michongoma? 17Vivyo hivyo, mti
mwema huzaa matunda mazuri na mti mbaya
huzaa matunda mabaya. 18Mti mwema hauwezi
kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya
hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti
usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa
motoni. 20Hivyo, kwa matunda yao,
mtawatambua.’

Mwanafunzi Wa Kweli

21β€œSi kila mtu aniambiaye, β€˜Bwana, Bwana,’
atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni
yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile,
β€˜Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako
na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza
mingi? 23Ndipo nitakapowaambia wazi,
`’Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi
watenda maovu!’

Msikiaji Na Mtendaji

24β€˜β€˜Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya
maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu
mwenye busara aliyejenga nyumba yake
kwenye mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko
yakaja na upepo ukavuma ukaipiga hiyo
nyumba, lakini haikuanguka kwa sababu msingi
wake ulikuwa kwenye mwamba. 26Naye kila
anayesikia haya maneno yangu wala
asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga
nyumba yake kwenye mchanga. 27Mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo
ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo
ikaanguka kwa kishindo kikubwa.’’
28Yesu alipomaliza kusema maneno haya,
makutano ya watu wakashangazwa sana na
mafundisho yake, 29kwa sababu alifundisha
kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama
walimu wao wa sheria.

Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51

Hii ndiyo Sala ya Toba
Zaburi 51
1 Ee Mungu, unirehemu,Sawasawa na fadhili zako.Kiasi cha wingi wa rehema zako,Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa na uovu wangu,Unitakase dhambi zangu.
3 Maana nimejua mimi makosa yanguNa dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,Na kufanya maovu mbele za macho yako.Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe,Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;Uzifute hatia zangu zote.
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
11 Usinitenge na uso wako,Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako;Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13 Nitawafundisha wakosaji njia zako,Na wenye dhambi watarejea kwako.
14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,Uniponye na damu za watu,Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;Moyo uliovunjika na kupondeka,Ee Mungu, hutaudharau.
18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.Ndipo watakapotoa ng’ombeJuu ya madhabahu yako.

Ufafanuzi wa Sala ya Baba yetu

Baba Yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe;
ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike
duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina

Ufafanuzi wake uliotumiwa na Fransisko wa Asizi

BABA YETU mtakatifu kabisa: muumba, mkombozi, mfariji na mwokozi wetu.
ULIYE MBINGUNI: katika malaika na katika watakatifu, ukiwaangazia wawe na ufahamu, kwa sababu wewe Bwana ni mwanga; ukiwawasha wawe na upendo, kwa sababu wewe Bwana ni upendo; ukikaa ndani mwao na kuwajaza furaha, kwa sababu wewe Bwana ni wema mkuu kabisa, wema wa milele, ambaye kwako hutoka mema yote, na bila yako hakuna jema.
JINA LAKO LITUKUZWE: ujuzi wetu juu yako uwe wazi zaidi na zaidi, tuweze kujua upana wa baraka zako, urefu wa ahadi zako, kimo cha ukuu wako, kina cha hukumu zako.
UFALME WAKO UFIKE: utawale ndani yetu kwa njia ya neema yako na kutuwezesha kuingia katika ufalme wako ambapo unaonekana kama ulivyo, unapendwa kikamilifu, unatia heri ya kukaa nawe, unatia raha ya kukufurahia milele.
UTAKALO LIFANYIKE DUNIANI KAMA MBINGUNI: tuweze kukupenda kwa moyo wetu wote, kwa kukuwaza wewe daima; kwa roho yetu yote, kwa kukutamani wewe daima; kwa akili yetu yote, kwa kuelekeza nia zetu zote kwako na kwa kutafuta utukufu wako katika yote; kwa nguvu zetu zote pia, kwa kutumia uwezo na hisia zote za roho na mwili katika kuhudumia upendo wako na si chochote kingine; na tuweze kuwapenda majirani wetu kama tunavyojipenda, kwa kuwavuta wote kwa nguvu zetu zote kwenye upendo wako, tukifurahia mema ya wengine kama tunavyofurahia ya kwetu, na tukihuzunika pamoja na wengine kwa mabaya yanayowafikia, bila ya kumuudhi yeyote.
MKATE WETU WA KILA SIKU: Mwanao mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo.
UTUPE LEO: kwa ukumbusho, ufahamu na heshima ya upendo ule aliokuwanao kwetu sisi na ya mambo yale ambayo alisema na kutenda na kuteseka kwa ajili yetu.
UTUSAMEHE MAKOSA YETU: kwa huruma yako isiyosemeka, kwa nguvu ya mateso ya Mwanao mpendwa, pamoja na stahili na maombezi ya Bikira mbarikiwa daima na ya wateule wako wote.
KAMA TUNAVYOWASAMEHE NA SISI WALIOTUKOSEA: na lolote tusilosamehe kikamilifu, wewe Bwana utuwezeshe kulisamehe kabisa, tuwapende kweli maadui wetu kwa ajili yako, na tuwaombee kwa bidii mbele zako, bila ya kumlipa yeyote ovu kwa ovu, bali tukijitahidi kumsaidia kila mmoja katika wewe.
NA USITUTIE KATIKA VISHAWISHI: kilichofichika au cha wazi, cha ghafla au cha muda mrefu.
LAKINI UTUOPOE MAOVUNI: yaliyopita, ya sasa na yajayo.
ATUKUZWE BABA NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU KAMA MWANZO, NA SASA NA MILELEAMINA.

Maswali na Majibu kuhusu Ufufuko wa wafu

Ufufuko wa wafu maana yake nini?

Ufufuko wa wafu maana yake mwisho wa dunia watu wote watafufuka na miili yao na kwenda nayo katika furaha ya milele au moto wa milele. (Ayu 19:25-26, Mt 22:30-32, Yh 28-29)


Mbinguni ni mahali pa namna gani?

Mbinguni ni makao mema ya heri na furaha (2Kor 5:1, Ufu, 2:17).
Waendao mbinguni ni wale wanaokufa katika hali ya neema ya utakaso na urafiki na Mungu na waliotakaswa kikamilifu


Motoni ni nini?

Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15)


Uzima wa milele ni nini?

Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho.


Toharani ni mahali gani?

Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).


Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?

Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)


Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?

Mambo hayo ni;
1. Kifo
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)


Je, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia?

Ndiyo, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa.
Mwenyewe alisema, β€œMimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele” (Yoh 11:25- 26).
β€œKristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu” (1Kor 15:20-21).
β€œAlitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa haki” (Rom 4:25).


Je, ni muhimu tujiandae kufa?

Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa β€œkufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” (Eb 9:27).
β€œKatika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatima” (YbS 7:36).
β€œHamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka” (Yak 4:14).
β€œKesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” (Math 26:41).


Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?

Ndiyo, β€œina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” (Zab 116:15).
Hasa utiifu wa Yesu msalabani umegeuza laana ya kifo iwe baraka kwa waamini wake.
β€œHeri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” (Ufu 14:13).


Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?

Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake.
β€œNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma” (Yoh 17:3).
β€œKwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet 1:3-4).
Sisi tuliobatizwa tunaitwa β€œwana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!” (1Yoh. 3:1).
Kwa sababu tumesadiki kwamba β€œMungu ni upendo” (1Yoh 4:8) na kwamba β€œhakuna lisilowezekana kwa Bwana” (Lk 1:37).
β€œNa kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu” (Gal 4:6-7).


Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?

Aliyezungumzia moto wa milele ni hasa Yesu: akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee, alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo:
β€œOndokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake” (Math 25:41).
β€œHumo funza wao hafi, wala moto hauzimiki” (Mk 9:48).
β€œNa moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku” (Ufu 14:11).


Toharani maana yake nini?

Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo β€œalichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zao” (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: β€œKama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?” (1Kor 15:29).


Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > β€œhupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo β€œndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (Lk 21:27).
β€œSaa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu” (Yoh 5:28-29).
β€œNa hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele” (Math 25:46).


Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?

Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la.
β€œImetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyopenda, kwamba ni mema au mabaya” (2Kor 5:10).
β€œBasi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu” (1Kor 4:5).
β€œHapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, β€˜Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia… Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi’” (Math 25:31-36,40).
β€œHeri wenye rehema, maana hao watapata rehema” (Math 5:7).


Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?

Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa.
β€œKama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake” (2Pet 3:13).
β€œNa Roho na Bibi arusi wasema, β€˜Njoo!’ naye asikiaye na aseme, β€˜Njoo!’… Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, β€˜Naam, naja upesi’. Amina. Na uje, Bwana Yesu! Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina” (Ufu 22:17,20-21).

Kuhusu Ubatizo, Haya ndiyo mambo ya Msingi unayotakiwa kufahamu

Kwa nini ubatizo unafanyika kwa maji?

Ubatizo unafanyika kwa maji kwa kuwa ndiyo ishara ya usafi na ya uhai unaotupatia kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
β€œNami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu” (Ez 36:26-27).
β€œKisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwanakondoo” (Ufu 22:1).


Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu lini?

Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote.
Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha waamini walivyotekeleza agizo hilo katika mazingira mbalimbali, sio tu yalipopatikana maji mengi. Hivyo Paulo alipokuwa ndani ya nyumba β€œakasimama akabatizwa” (Mdo 9:18).
Kumbe Yohane Mbatizaji hakusogea mbali na mto Yordani, akisubiri watu wamuendee kutoka maeneo yote ya nchi ile kame.
β€œAlikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele” (Yoh 3:23).


Je, ubatizo uliotolewa na Yohane Mbatizaji ulikuwa sakramenti?

Hapana, ubatizo uliotolewa na Yohan Mbatizaji haukuwa sakramenti, kwa sababu yeye alikuwa mtangulizi tu wa Yesu, mwanzilishi wa sakramenti zote.
β€œKweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Math 3:11).
Paulo aliuliza watu, β€œβ€˜Mlibatizwa kwa ubatizo gani?’ Wakasema, β€˜Kwa ubatizo wa Yohane’. Paulo akasema, β€˜Yohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu’. Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu” (Mdo 19:3-5).


Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni zipi?

Tofauti kubwa kati ya ubatizo wa Yohane na ule wa Yesu ni kwamba sakramenti inategemea imani kwa Kristo na kutushirikisha kifo na ufufuko wake.
β€œMaana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo” (Gal 3:27).
Ndivyo inavyoondolea dhambi zote na kuingiza katika uzima wa Utatu Mtakatifu. Kwa sababu hiyo Yesu aliagiza tubatize β€œkwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Math 28:19).
Maneno hayo ndiyo muhimu zaidi katika sakramenti hiyo. Maji peke yake, hasa yakiwa mengi, yanaweza kuosha mwili, lakini si roho. Kumbe ubatizo unaotuokoa
β€œsiyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu” (1Pet 3:21).


Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?

Ndiyo, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake β€œalichukizwa sana, akawaambia, β€˜Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa” (Mk 10:14-15).
Yeremia aliambiwa,
β€œKabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yer 1:5).
Yohane Mbatizaji alitabiriwa β€œatajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye” (Lk 1:15).
Mitume walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu.
Walibatizwa β€œyeye na nyumba yake”, β€œyeye na watu wake wote” (Mdo 16:15,33);
β€œwatu wa nyumbani mwa Stefana” (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.


Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?

Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani.
β€œVinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao umeiweka misingi ya nguvu” (Zab 8:2).
β€œElisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake… kwa shangwe” (Lk 1:41,44).
β€œNakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako” (Math 11:25-26).


Je, watu wazima wanaweza kuelewa sakramenti kwa dhati?

Hapana, watu wazima hawawezi kuelewa sakramenti kwa dhati, kwa kuwa zote ni mafumbo yanayotuzidi. Basi, kama Petro alipooshwa miguu, tumuachie Bwana atufanyie kazi anavyojua yeye.
β€œNifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye” (Yoh 13:7).
Kisha kuoshwa tuzidi kuchimba mafumbo hayo kwa mwanga wa Neno na wa Roho Mtakatifu.
β€œJe, mmeelewa na hayo niliyowatendea?… Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo” (Yoh 13:12,15).


Je, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto?

Ndiyo, imani ya watu wazima inaweza kufaidisha watoto kama wengine pia.
Walimletea Yesu β€œmtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne… Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, β€˜Mwanangu, umesamehewa dhambi zako” (Mk 2:5).
Yesu aliiona imani yao akamponya. Imani ya watu wengine ndio ilivyopelekea kuponywa kwa huyu mtu. Vivyo hivyo Imani ya Mzazi inaweza kumsaidia mtoto.
Kwa ubatizo watoto wanaunganishwa naye na kuanza kuponywa madonda ya dhambi ya asili.
β€œTazama, mimi naliumbwa kati hali ya uovu, mama yangu alinichukua mimba hatiani” (Zab 51:5).
β€œIkiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo” (Rom 5:19).


Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?

Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.
β€œHata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu” (Lk 2:21).
Watu wa mataifa walipoongokea dini hiyo, walioshwa na kutahiriwa pamoja na watoto wao. Mitume pia walipokea katika Kanisa familia nzima, si wazazi tu. Walibatizwa β€œyeye na nyumba yake”, β€œyeye na watu wake wote” (Mdo 16:15,33); β€œwatu wa nyumbani mwa Stefana” (1Kor 1:16).
Kwa hiyo tunaona kuwa tangu wakati wa Mitume sio watu wazima tuu waliokua wakibatizwa bali na watoto pia.
Kwa Kanisa Katoliki, ubatizo sio ukamilifu wa kuwa Mkristo. Ubatizo ni Sakramenti ya kwanza ambayo inakamilishwa na Sakramenti ya Kipaimara ambayo humfanya Mkristo kuwa mkamilifu kwa kukiri na kuahidi mwenyewe kuwa Mfuasi wa Yesu Kristu kwa kumkataa Shetani na Mambo yake yote. Kwa maana hiyo, watoto wanapobatizwa wazazi wanamtoa au wanamwalika mtoto katika Imani ya Kikristu wakiahidi kumtumza na kumwelekeza katika njia ya Imani kwa Yesu Kristu mpaka atakapokua mkubwa na kuwa na ufahamu na Elimu ya kutosha kuhusu Imani yake ndipo na yeye atakiri na kuahidi mwenyewe wakati wa Sakramenti ya Kipaimara.


Je, ubatizo tuu unatosha?

Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula.
Sakramenti hizo tatu kwa pamoja ni msingi wa maisha ya Wakristo wote, kumbe nyingine zinahitajika tu katika hali na nafasi maalumu. Mitume waliwaendea Wasamaria
β€œwakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu” (Mdo 8:15-16).
β€œAmin, amin, nawaambieni: Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndaniyenu” (Yoh 6:53).


Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni ipi?

Sakramenti inayohusiana zaidi na ubatizo ni kipaimara, kinachoendeleza kazi yake.
β€œWaliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao” (Mdo 19:5-6).
Sakramenti hizo ni kama pande mbili za pesa moja. Zinahusiana kama Pasaka na Pentekoste, ambayo ni utimilifu wake, kwa kuwa siku alipofufuka Yesu aliwapulizia Mitume Roho Mtakatifu, ambaye siku hamsini baadaye akawajia kama
β€œupepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote” (Mdo 2:2).


Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi?

Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai.
Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapotulisha na kutunywesha Mwili na Damu yake ili tushiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi.
β€œAulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi” (Yoh 6:56-57).
Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani mwetu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.


Sakramenti ya ubatizo ni nini?

Sakramenti ya Ubatizo ni Sakramenti yenye kuondoa dhambi ya asili pamoja na dhambi nyingine zote tulizotenda, kufufua roho zetu kwa kututia uzima wa Mungu, Kutuandika Wakristu Watoto wateule wa Mungu na wa Kanisa.


Ubatizo ni nini?

Ubatizo ni Sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho Mtakatifu, ni mlango (Kiingilio) kwa Sakramenti nyingine zote na ni ufunguo wa uzima wa milele. (Yoh 3:3, Mt28:19)


Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?

Sakramenti ya Ubatizo yatuletea;
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13)


Kuna Ubatizo wa namna ngapi?

Kuna Ubatizo wa namna tatu;
1. Ubatizo wa maji – Ubatizo wa kawaida
2. Ubatizo wa tamaa – Mfano mtu akifa akiwa na nia ya kubatizwa au akitamani kubatizwa
3. Ubatizo wa Damu – Mtu akiifia Imani japo hajabatizwa


Nani aweza kubatiza?

Mwenye mamlaka ya kubatiza kwa kawaida ni yule mwenye dataja takatifu katika Kanisa, lakini katika hatari ya kufa kila mtu anaweza kubatiza.


Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?

Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu


Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo


Anayebatizwa yampasa nini?

Yampasa kuungama imani yake ama mwenyewe akiwa mtu mzima ama kupitia wazazi kama akiwa mtoto mdogo


Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?

Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni kumwagia maji katika panda la uso na kutamka maneno “Fulani (jina lake linatajwa) nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu” (Mt 28:19)


Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?

Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;
1. Kutoa mfano mzuri wa maisha ya Kikristo
2. Kumuongoza mbatizwa katika maisha ya Ukristo
3. Kumuombea mbatizwa
4. Kushirikiana na wazazi katika malezi

Maswali na Majibu kuhusu Sanamu katika Kanisa Katoliki

Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).
18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.
Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.

Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.

Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.

Kwa nini wakatoliki wanaweka sanamu Kanisani?

Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
“18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.Β (Kutoka 25 :18-22.)
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
“BWANA akamwambia Mose, β€œTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.’’ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.”Β (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.

Sanamu au picha sio haramu bali maana ya hiyo sanamu au picha ndio inaiharamisha.

Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
KumbukaΒ kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwaΒ “Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake”, kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.

Tofauti ya Sanamu za Kikatoliki na za kipagani ni Kwamba,

Sanamu za Kipagani:Β Sanamu hizi huchukuliwa kama Mungu na huabudiwa na kutolewa Sadaka kama Mungu Mwenyewe.

Sanamu za Kikatoliki:Β Sanamu hizi huchukuliwa kama ishara ya kile inachokiwakilisha, haiabudiwi kamwe bali inaheshimiwa tuu.

Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.Β (Kutoka 25 :22).Β Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.

Jifunze kupitia Sanduku la Agano na Msalaba wa Yesu

Kwenye Agano la kale:Β Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hichoΒ Kutoka 25:10-22.Β Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya:Β Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.

Kwa nini tunasali mbele ya Picha/Sanamu na Hasa kufanya Ishara ya msalaba?

Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.

Kwa nini watu wanabusu picha na sanamu?

Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. β€œRoho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39).

Je, ni halali kuheshimu sanamu?

Ndiyo, ni halali kuheshimu sanamu kama viwakilishi vya Yesu, Mama yake na watakatifu wake, ambao zinaleta sura zao.
Kwa msingi huo walimsihi Yesu β€œwaguse hata pindo la vazi lake tu. Na wote waliogusa wakaponywa kabisa” (Math 14:36).
β€œMimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote il msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo” (Gal 6:14).

Maswali na Majibu kuhusu Sala

Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;
β€œNiite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua”.(Yeremia 33:3)
Vile tunavyokuwa na juhudi ya kusali kwa kusema mbele ya Mungu ndivyo hivyo hivyo tunatakiwa tuwe na juhudi ya kumsikiliza Mungu kile anachotuambia.
Tunaweza kumsikiliza Mungu ndani kabisa ya Mioyo yetu, mara nyingine kwa kupitia dhamira zetu, kupitia watu wengine na kupitia neno lake (Biblia). Tuombe neema ya kutambua sauti yake anaposema nasi ili tuweze kumsikiliza na kutengeneza mahusiano mazuri kati yetu na yeye.
Mungu ni Baba yetu, anatupenda sana na yupo tayari kutusikiliza wakati wote ndio maana Mungu anatualika kwa kutuambia;
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Tudumu katika sala daima kwa sababu njia ya sala ndipo tunaweza kusema yale tunayotaka mbele ya Mungu na kusikia yale anayotaka Mungu.


Kwa nini tunasali?

Tunasali ili kudumisha mahusiano yetu na Mungu na ili kutimiza wajibu wetu Mbele ya Mungu. Sababu kuu za kusali ni;
  1. Kumwabudu Mungu,
  2. Kumshukuru Mungu,
  3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu,
  4. Kuomba msamaha,
  5. Kumsifu na kumtukuza Mungu

1. Kumwabudu Mungu

Tunasali ili kumwabudu Mungu, yaani kumpa heshima ya mwisho juu ya kila kitu. Kuonyesha kuwa ni mkuu na wa kipekee kuliko mtu au kitu chochote.

2. Kumshukuru Mungu

Tunasali ili kumshukuru Mungu kwa yale yote aliyokwisha kuyatenda, anayoyatenda na yale atakayoyatenda. Tunamshukuru Mungu kwa yote kwa kuwa yote anayoyafanya anayafanya kwa Mapenzi/ Matakwa yake Matakatifu. Nia ya Mungu ni njema daima ndio maana tunapoona ameruhusu mambo ambayo kwa akili zetu tunayaona ni magumu na sio mema tunapaswa kushukuru kwa sababu ameyafanya kwa makusudi mema.
Biblia inatuambia hivi;
16 Furahini siku zote; 17ombeni bila kukoma; 18shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. (1 Wathesalonike 5:16-18)
Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa Kila jambo na kumshukuru huku ni kwa njia ya sala.

3. Kuomba neema na baraka kwa ajili yetu na wenzetu

Tunasali kwa kuomaba neema na baraka kwa ajili yetu sisi wenyewe na kwa ajili ya wenzetu. Tunamuomba Mungu baraka na Mkono wake katika yale tunayoyafanya na kwa yale wanayoyafanya wengine.
Maombi yetu ili ykubalike mbele ya Mungu ni lazima yawe katika mapenzi yake na yawe na nia njema. Tunafundishwa hivi katika biblia;
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. (Yakobo 4:3)
Tunatakiwa tusali kwa kuomba mema na kwa nia njema ili tuweze kupata yale tunayoyaomba kwa Mungu.

4. Kuomba Msamaha

Tunasali ili kuomba msamaha mbele ya Mungu kwa yote mabaya tuliyoyafanya. Mungu ni mwaminifu hasa kwenye kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu.
9Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. (1 Yohana 1:9)
Vilevile Tunatakiwa kusali katika mapungufu yetu na kuwa na matumaini.
9Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. (2 Wakorinto 12:9)

6. Kumsifu na kumtukuza Mungu

Tunasali ili kusifu na kumtukuza Mungu. Mungu anapenda kusifiwa na kutukuzwa. Kwa njia ya sifa tunapokea neema na baraka hata ambazo hatujaziomba.
1Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Kwa kuwa BWANA ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (Zaburi 100:1-4)


Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali.
Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kudumu katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona hali yetu ya kiroho ipo vizuri. Hatupaswi kuacha kusali kama tumepata neema ya kusimama vyema mbele ya Mungu.
Tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali. Tunasali ili tuweze kurudi katika hali ya neema. Hatupaswi kuacha kusali kama tunajiona tupo katika hali ya dhambi. Kwa njia ya sala ndipo tutakapoweza kutoka katika hali ya dhambi.
Mungu yupo tayari kusikiliza ukiwa katika hali ya neema au kama ukiwa katika hali ya dhambi. Ndio maana tunapaswa kumwelekea Mungu katika hali yoyote tulio nayo.
14Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba. (1 Yohane 5:15)
Tena Mungu anasubiri tumuombe ili furaha yetu itimilike.
24Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. (Yohane 16:24)
Hata kama tuna dhambi Mungu yupo tayari kutupokea na kutusikiliza.
“Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu”. (Isaya 1:18)
Mungu yupo tayari kutusikiliza hata tunapokuwa wadhambi kwa kuwa haziweki dhambi zetu na makosa yetu mbele yetu. Huruma yake ni kubwa kushinda dhambi zetu.
12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. (Zaburi 103:12-13)
Mungu anatuwazia mema daima ndio maana tunapaswa kusali kwake
11Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. 12Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. 13Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. (Yeremia 29:11-13)


Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu.
Tunatakiwa tusali daima Kama Yesu alivyotuhimiza kwa mfano huu;
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.
3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.
4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.
6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?
8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani? 
(Lk 18:1-8)
Kwa hiyo basi, Tusali daima kila siku, kila saa na katika hali yoyote. Tusichoke kusali hata kama maombi Yetu hayajajibiwa. Mungu ni mwenye Hekima na anajua lini hasa akujibu kile unachokiomba kwa manufaa yako wewe. Usipopewa Leo kile ukiombacho unaweza kukipata kwa wakati ufaao tena bila ya Kukiomba.

Sala ni Hazina

Sala ni hazina. Kusali ni kujiwekea hazina. Sala unayosali leo inaweza kukunufaisha wakati usioutarajia.

Maana ya Sala kwa Mkristo Mkatoliki

Maana ya sala kwa Mristu Mkatoliki sio kuomba tuu. Sala kwa Mkatoliki ni zaidi ya kuomba. Kwa Mkatoliki sala inamaanisha kufanya haya;
  1. Tunasali kushukuru,
  2. Tunasali kuomba,
  3. Tunasali kusifu na Kutukuza,
  4. Tunasali kumshirikisha Mungu Furaha zetu na huzuni zetu,
  5. Tunasali kuomba Toba na Msamaha,
  6. Tunasali kumshirikisha Mungu Juhudi zetu na Mipango yetu,
  7. Tunasali kumshirikisha Mungu changamoto zetu.
Tuna kila sababu ya Kusali kila Siku na Kila saa. Maisha yetu yote yanatakiwa yawe Maisha ya Sala. Usifikiri kwamba Wakati wote unaposali lazima utamke maneno Mengi sana ili uwe umesali, Sala haipimwi kwa Maneno. Sala inapimwa kwa nia yake na Kujiweka wazi mbele ya Mungu.
Kila Usalipo Jijengee Tabia ya kunuia, kuwa wazi na kusali kwa ukweli wa Moyo wako. Hata kama ni sentesi Moja fupi Kabisa itamke kwa Upendo na Imani. Kwa Mfano, kuna wakati inatosha kabisa kusema Ee Mungu wangu ninakushukuru kwa hili, hii inaweza kuwa sala Yenye nguvu Kama imetamkwa kwa Imani, Shukrani na Mapendo ya Kweli. Maneno machache yanayotamkwa kwa Imani na Mapendo yanaweza kuzidi Mkesha wa Kusali Usiku Mzima huku unasinzia.
Pamoja na kwamba sala fupi ni nzuri na inafaa sana, kuna haja pia ya kujitengea Muda wa Kutosha Kusali na Kutafakari Huku tukiungana na Mungu. Kila siku tunanye mambo yote mengine lakini tusisahau kuwa Tunahitaji kuwa na Muda wa Kusali.
Tusali daima, Kila wakati na Maisha yetu yawe ni Maisha ya Sala.
Mungu Akubariki sana, Azijibu sala zako na Akujalie Neema ya Kuwa Mtu wa Sala.


Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;
9 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.
11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.
13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. 
Luka 18:9-14
Tunatakiwa tusali kwa nia njema na kwa kufuata Mapenzi ya Mungu ili sala zetu zipate kibali mbele za Mungu. Tunapoomba kwa nia mbaya ya tamaa na majivuno hatuwezi kupata kile tukiombacho.
3Tena, mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa nia mbaya; mnaomba ili mpate kutosheleza tamaa zenu. Yakobo 4:3
Mungu anajibu sala zetu kulingana na nia ya kile tunachokiomba. Watu wote waliofanikiwa Katika sala zao walifanikiwa kwa sababu ya nia ya kile walichokiomba.
Sala sio kutamka manano tuu, sala ni kutamka maneno kwa kunuia. Tena tusalipo yatupasa kujua kuwa tunaongea na Mungu na sio tuu kwamba tunatamka maneno. Tusisahau nia kuu ya kusali ambayo ni mawasiliano Yetu na Mungu.
Tunaposali Tunapaswa Kukumbuka na kuzingatia haya;
  1. Nia na Imani (Kuamini na Kuwa na Uhakika na Unachokifanya)
  2. Unyenyekevu wa Kweli
  3. Ibada na Uchaji
  4. Upendo na Uwazi (Honest)
  5. Matumaini na Saburi (Subira)
Kila unaposali jiulize unasali kwa kwa sababu gani? Kila ubapoomba, jiulize unamuomba Mungu ili nini? Sababu yako ndio kibali cha sala yako.
Mungu Akubariki kwa Kukujalia Imani, Unyenyekevu, Ibada, Uwazi na Matumaini Usalipo. Uwe na Amani.


Sala zipo za namna ngapi?

Sala zipo za namna tatu,
1. Sala ya sauti
2. Sala ya fikara
3. Sala ya taamuli


Sala ya Taamuli ni nini?

Sala ya taamuli ni sala ya kumtazama tuu Mungu kwa upendo mkubwa moyoni


Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno


Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu


Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima


Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila Dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi


Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13)


Je, yatupasa kuombea wengine?

Ndiyo. Yatupasa kuwaombea watu wote hasa wenye shida, wakosefu na hata maadui zetu.


Vyanzo vya sala za Kikristo

Vyanzo vya sala za kikristo ni;
1. Neno la Mungu
2. Litrujia ya kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku


Je, ni sahihi kusali sala kwa kurudia rudia mfano Novena?

Ndiyo, Hii ni kwa sababu sala nyingi za kurudia ni za Ahadi na zinasaliwa ili kutimiza ahadi ile. Mfano Novena husaliwa kwa siku 7 au 9 kwa nia ya kupata kile kilichoahidiwa au kinachodhamiriwa. Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli wafanye Ibada maalumu kwa kurudiarudia mfano wakati walipoangusha kuta za Yeriko walifanya Ibada maalumu kwa siku 7 (Saba).
“Waisraeli walipopita waliagizwa na Mungu kuzunguka Mji wa Yeriko 2Kisha BWANA akamwambia Yoshua,β€œTazama, nimeitia Yeriko mikononi mwako, pamoja na mfalme wake na watu wake wa vita. 3Zunguka mji mara moja pamoja na watu wako wote wa vita. Fanya hivi kwa siku sita. 4Uwe na makuhani saba wakibeba mabaragumu ya pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Siku ya saba, mzunguke mji mara saba, nao makuhani wakipiga baragumu hizo. 5Utakaposikia makuhani wamepaliza sauti kubwa ya baragumu, watu wote wapige kelele kwa sauti kuu, kisha ukuta wa mji utaanguka na watu watakwea, kila mtu aingie ndani moja kwa moja kutokea pale alipo.’’ (Yoshua 6:2-5).
Naamani aliambiwa na Nabii Elisha aoge mara saba kwenye mto Yordani ili apone.
14Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya mto Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo. (2 Wafalme 5:14)
Yesu alisali sala ya kurdia rudia kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, β€œBaba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, β€œJe, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41β€˜β€˜Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, β€œBaba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Je ni makosa kurudia sala maneno yale yale kwa Mfano Rozari?

Hapana sio Makosa. Kwa Mfano Biblia inatuambia kuwa Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia.
“8Kila mmoja wa hawa viumbe wenye uhai wanne, alikuwa na mabawa sita na kujawa na macho pande zote, hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kusema: β€˜β€˜Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.’’ (Ufunuo 4:8).
Vile vile tunasoma katika kitabu cha Isaya kuwa malaika walikua wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa sala/ maneno ya kurudiarudia. “Katika mwaka ule mfalme Uzia alipokufa, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu na kilichotukuzwa sana, nalo pindo la joho lake likajaza hekalu. 2Juu yake walikuwepo maserafi, kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Kwa mabawa mawili walifunika nyuso zao, kwa menngine mawili walifunika miguu yao na kwa mawili walikuwa wakiruka. 3Nao walikuwa wakiitana kila mmoja na mwenzake: β€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni BWANA Mwenye Nguvu, Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Kama Malaika humtukuza Mungu kwa maneno ya kurudia rudia kwa nini sisi tukifanya hivyo tuwe tunakosea? Na sisi tunaweza kumuomba, kumsifu na kumtukuza Mungu kwa sala au maneno ya kurudiarudia kama walivyofanya malaika. Kwa hiyo sala za kurudia rudia sio makosa.
Tukiangalia Zaburi ya 136 inarudia maneno “kwa maana fadhili zake zadumu milele” mara 26 yaani kwenye mistari yake yote. (Zaburi 136:1-26)
Yesu pia allimuomba Mungu Baba kwa kurudia maneno yale yale kama tunavyosoma,
39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, akisema, β€œBaba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki na kiniepuke, lakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo Wewe.’’ 40Kisha akarudi kwa wanafunzi wake na kuwakuta wamelala. Akamwuliza Petro, β€œJe, hamkuweza kukesha pamoja nami kwa saa moja? 41β€˜β€˜Kesheni na mwombe, msije mkaanguka majaribuni. Hakika roho iko radhi lakini mwili ni dhaifu.’’ 42Akaenda tena mara ya pili na kuomba, β€œBaba yangu, kama ikiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisikinywe, mapenzi yako yafanyike.’’ 43Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. 44Hivyo akawaacha akaenda zake tena mara ya tatu na kuomba akisema maneno yale yale. (Mathayo 26:39-44)

Sala kwa Mkatoliki ni nini hasa? Tunaposema sala tunamaanisha nini hasa?

Sala ni kuongea na Mungu. Sala kwa Mkatoliki inajumuisha maombi, tafakari, ibada, taamuli, shukrani na sifa. Maana ya sala kwa Mkristo Mkatoliki sio kuomba tuu kama wanavyotafsiri watu wasio wakatoliki. Wengi wa wasio Wakatoliki wanaposema Sala wanamaanisha Maombi.
Kwa hiyo kwa Mkatoliki, Sala ni zaidi ya Maombi. Ndiyo maana kwa mkatoliki kuna sala za namna mbalimbali kama vile za Tafakari, za Maombi za Sifa na za kushukuru. Mfano sala ya Atukuzwe Baba sio maombi bali ni sala ya kumtukuza Mungu kwa maana hiyo sio Maombi, ndiyo maana husaliwa baada ya sala au matukio fulani kama ishara ya kumtukuza Mungu na kutambua ukuu wa Mungu

Yesu alifundisha tusali vipi?

Kisha Yesu akawapa wanafunzi Wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.
2Akawaambia, β€œKatika mji mmoja alikuwapo hakimu ambaye hakumwogopa Mungu wala kumjali mtu. 3Katika mji huo alikuwako mjane mmoja ambaye alikuwa akija kwake mara kwa mara akimwomba, β€˜Tafadhali nipatie haki kati yangu na adui yangu.’ Wa Mjane Asiyekata Tamaa 4β€œKwa muda mrefu yule hakimu alikataa. Lakini hatimaye akasema moyoni mwake, β€˜Japokuwa simwogopi Mungu wala simjali mwanadamu, 5lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ” 6Bwana akasema, β€œSikilizeni asemavyo huyu hakimu dhalimu. 7Je, Mungu hatawatendea haki wateule Wake wanaomlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasaidia? 8Ninawaambia, atawapatia haki upesi. Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:1-8)


Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo


Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu


Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu

Kwa nini watu wengi wanaomba kwa Bikira Maria?

Watu wengi wanaomba kupitia Bikira Maria kwa sababu wanashuhudia sala zao kujibiwa kirahisi zaidi wanaposali kupitia Bikira Maria kwani Bikira Maria anatuombea kile tunacho mwomba. Bikira Maria anasimama Kama mwombezi wetu mbele ya Mungu hasa pale tunaposhindwa kusali Inavyotakiwa.

Bikira Maria anatuombea kwa jina na mamlaka ya nani?

Bikira Maria anatuombea kwa jina la Yesu Kristu na kwa mamlaka ya Yesu Kristu aliye mwanaye. Hakuna Sala yoyote inayotolewa kwa Bikira Maria moja kwa moja kwani Sala zote kwa Bikira Maria zinatolewa kwa kusema utuombee ikimaanisha kuwa utupelekee Maombi yetu kwa Mungu. Bikira Maria hatusaidii sisi moja kwa moja bali anatusaidia kwa kutuombea msaada kutoka kwa Mungu.

Je ni halali au ni sawa kwa Bikira Maria kutuombea kwa Jina la Yesu? Na Je tunajuaje kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu?

Ni halali na nisawa kabisa Bikira Maria kutuombea. Tunajua kuwa Bikira Maria anaushirika na Yesu kwa kuwa Yesu mwenyewe alituambia kuwa “asiyepingana na sisi yupo upande wetu”. Biblia iintuambia…
“Yohane akadakia na kusema “Umemwona Mtu mmoja akifukuza pepo kwa kutumia jina lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa si mmoja wetu.” Lakini Yesu akawaambia, “Msimkataze kwani asiyepingana nanyi yupo upande wenu” (Luka 9:49-50).
Kwa hiyo Bikira Maria anapolitumia jina la Yesu bila kupingana na sisi wala Yesu ni ishara tosha kuwa ni mshirika wa Mungu (Yesu)

Je ni kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo?

Sio kweli kwamba Bikira Maria ni Malkia wa Kipepo/Kishetani
Sababu hizi zifuatazo zinadhihirisha kuwa Bikira Maria sio Malkia wa kipepo;
1) Kuomba kwa jina la Yesu: Angekua ni Malkia wa Kipepo asingeomba kwa Jina la Yesu. Kama ilivyoelezwa hapo juu. Biblia iintuambia linapotamkwa Jina la Yesu mapepo hukimbia. Sasa iweje yeye alitumie Jina hilo kutuombea Kama yeye ni pepo? (Luka 10:17)
2) Hafundishi uovu/dhambi: Mbali na kuomba kwa jina la Yesu, vilevile Yesu alituambia tuzichunguze roho na tutazitambua roho hizo kwa matendo yake. Kwa lengo hili tukichunguza kuhusu Bikira Maria tutaona kuwa Bikira Maria ni Mtakatifu aliye upande wa Mungu kwa sababu Mara zote alipowatokea watu amekuwa akifundisha na kuelekeza watu kuishi maisha ya utakatifu na kumfuata Mungu kweli kwa kutii amri zake na kufuata mafundisho ya mwanae ambayo ni yakuelekea katika utakatifu. Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalihusishwa na vitendo viovu au vya kuvunja Amri za Mungu.
3) Mafundisho yake yanaendana na Neno la Mungu (Biblia): Bikira Maria hajawaji hata mara moja kufundisha na kuelekeza vitu vilivyo nje ya Mafundisho ya neno la Mungu (Biblia). Hakuna hata Mara moja mafundisho ya Bikira Maria yalikinzana na Mafundisho ya Neno la Mungu.
4) Anahubiri Wema, Unyenyekevu, Upole na Utii: mambo ambayo ni alama ya kudhihirisha Utakatifu.
5) Anasisitiza Upendo kwa Binadamu wenzetu na kwa Mungu: Anahubiri Upendo hasa kwa Maadui zetu na wale wanaoipinga Imani ya Kikristu na wanaomkataa Yesu Kristu. Anasisitiza mara zote Tumpende Mungu na kumtii.
6) Anahubiri Amani: Anahubiri Injili ya Amani na Mara zote anasisitiza tuombe amani ambapo amani ndio Ishara ya Utakatifu.
7) Hajitukuzi mbele ya Mungu bali anajinyenyekesha: Hajawahi kufundisha kwamba tumtukuze yeye au tumuheshimu yeye. Mara zote anahubiri tumheshimu Mungu pekee na kumtukuza Mungu. Amekua akijishusha kwa unyenyekevu huku akituelekeza tuige mfano wake wa unyenyekevu wa kumuelekea Mungu aliye Baba wa huruma na upendo.
8) Anaongeza imani kwa Mungu: Kwa sala na Ibada za Bikira Maria waumini wanapata kuongezewa Imani na Uchaji wao kwa Mungu. Wengi wanabadili maisha yao ya dhambi na kuelekea Maisha mema ya utakatifu ya Kumtumikia Mungu.
9) Sala Ibada yake inachanganyika na Ibada nyingine za Kikristu: Hakuna mgongano/ushindani wa Ibada kwa Bikira Maria na Ibada nyingine za Kikristu. Kama angekua ni pepo kamwe Ibada yake isingechanganyika na Ibada Takatifu.
10) Ibada kwa Bikira Maria Imedumu: Haikufifia wala kupotea bali ilizidi kuendelea vizazi hata vizazi. Hii inadhihirisha kwamba kuna Neema ya Mungu.
Kwa sababu hizi unaweza ukaona kwamba Bikira Maria anaushirika na Mungu na ni Mtakatifu.


Ni zipi sala Muhimu kwa Mkristo?

Sala muhimu kwa Mkristo ni;
1. Misa Takatifu
2. Baraka ya Sakramenti Kuu
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari Takatifu
6.Novena


Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala


Mahali gani panafaa kwa sala?

Mtu anaweza kusali mahali popote lakini Kanisani ndipo mahali Rasmi pa sala


Mwenye kusali anakutana na majaribu gani?

Anakutana na Majaribu haya;
1. Mtawanyiko wa Mawazo
2.Ukavu wa moyo
3. Uvivu na Uregevu
Ndiyo maana kwa Wakatoliki sala nyingi zimeandikwa ili kutuongoza hasa tunapokuwa majaribuni katika sala.


Neno “Amina” katika sala lina maana gani?

Neno “Amina” katika sala lina maanisha “Na iwe Hivyo” (Hesabu 5:22)


“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maana gani?

“Aleluya” katika sala, hasa zaburi ina maanisha “Msifuni Mungu”


Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”


Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili


Kwa kugusa kifua tuna maana gani?

Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.


Kwa kugusa mabega tuna maana gani?

Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote


Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?

Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu


Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?

Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.


Sala zina faida gani? Kwa nini watu tunasali?

Sala zina faida hizi;
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili kushinda vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema


Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao.
β€œEwe pepo mchafu, mtoke mtu huyu” (Mk 5:8).
β€œEwe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena!” (Mk 9:25).
Yesu ameliachia Kanisa mamlaka yake juu yao.
β€œAliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu” (Mk 6:7).
β€œPaulo alisikitika, akageuka akamwambia yule pepo, β€˜Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu’. Akamtoka saa ileile” (Mdo 16:18).


Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tufanye nini?

Ikiwa sala ni maongezi ya Mungu na mtu, kwanza tumsikilize kwa makini na kutafakari alichosema ili tukifanyie kazi. Tukisema peke yetu si sala, kwa kuwa ukisema upande mmoja tu si maongezi.
β€œNena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia” (1Sam 3:10).
β€œNakutafakari Wewe makesha yote ya usiku” (Zab 63:6).
β€œSheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa” (Zab 119:97).
β€œManeno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu” (Yer 15:16).


Kielelezo cha sala yetu ni nani?

Kielelezo cha sala yetu ni Yesu Kristo.
β€œIkawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, β€˜Bwana, tufundishe sisi kusali” (Lk 11:1).
Yeye kama binadamu alichota humo uaminifu kwa wito wake wa pekee.
β€œBaba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe” (Yoh 17:1).
β€œAba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Mk 14:36).


Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa nani?

Kama binadamu Yesu alijifunza kusali kwa Mama yake na kwa mapokeo yote ya Israeli, yaliyojitokeza hasa katika Zaburi.
β€œWazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu” (Lk 2:41-42).
β€œSaa tisa Yesu alipaza sauti yake kwa nguvu, β€˜Eloi, Eloi, lama sabakthani?’” (Mk 15:34).
β€œEe Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu” (Lk 23:46).


Je, sala ya Yesu inatokana na utu wake tu?

Hapana, sala ya Yesu haitokani na utu wake tu, bali katika huo Mwana wa milele ndiye anayemuelekezea Baba yake sala kamili ya kitoto.
β€œSaa ileile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, β€˜Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, umewafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza” (Lk 10:21).
β€œBaba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote” (Yoh 11:41- 42).
β€œBaba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Lk 23:34).


Yesu alisali vipi?

Yesu alisali kila mahali na kila wakati, akidumisha ushirika wa upendo kati yake na Baba katika Roho Mtakatifu.
β€œSaa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu” (Yoh 4:23).
Pamoja na kushiriki kiaminifu ibada za taifa lake, mara nyingi alijitafutia mahali pa faragha.
β€œAliongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani” (Lk 4:1).
β€œAlikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba” (Lk 5:16).
β€œAliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” (Lk 6:12).
Ndiyo sababu ametuambia,
β€œWewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini” (Math 6:6).
Tusipojua kuongea na Baba moyo kwa moyo, tutawezaje kuongea naye kati ya umati?


Yesu ametufundisha kusali vipi?

Yesu ametufundisha kusali akitueleza misimamo ambayo tuwe nayo.
β€œUpatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako… Waombeeni wanaowaudhi… Msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu” (Math 5:24,44; 6:5).
β€œMtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipigapiga kifua akisema, β€˜Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi’. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki” (Lk 18:13-14).
Hasa ametutia Roho Mtakatifu atuongoze kama alivyomfanyia yeye.


Je, Yesu ametufundisha maneno ya sala pia?

Ndiyo, Yesu ametufundisha maneno ya sala ya β€˜Baba Yetu’, kamili kuliko zote. Maombi yake saba yanategemea utangulizi ambao tunamuendea Mungu kwa ujasiri na furaha kama watoto wake, ndugu kati yetu.
Maombi matatu ya kwanza yanalenga atukuzwe, atawale, apate ushirikiano wetu. Maombi manne ya mwisho yanalenga tupate chakula cha roho na cha mwili, msamaha wa dhambi, ushindi katika vishawishi, usalama dhidi ya yule Mwovu.
β€œBaba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi…” (Math 6:8-9).


Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga
β€œjuu ya imani… na kuomba katika Roho Mtakatifu” (Yud 20).
β€œMkiwa katika kusali, msipayukepayuke, kama watu wa mataifa; maana hao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi” (Math 6:7).
Hii haituzuii tusirudie maneno yetu kwa dhati zaidi na zaidi.
Yesu β€œalikwenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yaleyale” (Math 26:44).
Tunaweza kusali kimoyomoyo pia.
β€œHana alikuwa akinena moyoni mwake, midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe… β€˜Nimeimimina roho yangu mbele za Bwana’” (1Sam 1:13,15).
β€œManeno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana” (Zab 19:14).


Je, sala yetu inasikilizwa daima?

Ndiyo, sala yetu inasikilizwa daima kwa kuwa imeunganika kwa imani na ile ya Yesu, njia pekee ya kumuendea Baba.
β€œHata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata, furaha yenu iwe timilifu” (Yoh 16:24).
Lakini Baba, kwa ujuzi na upendo usio na mipaka, anaweza akatupatia mambo tofauti na yale tuliyomuomba.
β€œKama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, β€˜Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai” (Yoh 4:10).
β€œIkiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je, Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” (Lk 11:13).
Imani yetu ikubali kwamba aliyotupatia ni bora zaidi.


Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani.
Mhalifu alisema,
β€œβ€˜Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako’. Yesu akamwambia, β€˜Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi” (Lk 23:42-43).
Stefano aliomba,
β€œβ€˜Bwana Yesu, pokea roho yangu’. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, β€˜Bwana, usiwahesabie dhambi hii’” (Mdo 7:59-60).
β€œRoho na Bibi arusi wasema, β€˜Njoo!’. Naye asikiaye na aseme, β€˜Njoo!’… Na uje, Bwana Yesu!” (Ufu 22:17,20).


Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
β€œMungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’” (Gal 4:6).
β€œRoho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa… huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, β€˜Njoo, Roho Mtakatifu!’ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.


Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
β€œYeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Ef 3:16-19).
β€œHuyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.


Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote.
β€œKwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Rom 8:38-39).
β€œKwangu mimi kuishi na Kristo, na kufa ni faida… Ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo” (Fil 1:21,23)
.
Kwa kuwa hao wako na Kristo mbinguni, wanatuombea mfululizo pamoja naye.
β€œNiliona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, β€˜Ee Mwenyezi, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini…’” (Ufu 6:9-10).
Tunawaomba wazidi kutuombea kwa Mungu, kama tunavyowaomba wenzetu waliopo duniani.
β€œMkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi” (Ef 6:18-19).


Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Mafundisho ya Msingi kuhusu Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika sala?

Roho Mtakatifu ndiye Mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu

Majina mengine ya Roho Mtakatifu ni yapi?

Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji wa kweli, Roho wa Bwana, Roho wa Kristu

Ni alama zipi zinawakilisha Roho Mtakatifu?

Alama zinazowakilisha Roho Mtakatifu ni hizi; Maji, Mpako wa mafuta, Moto, wingu, tendo la kuweka mikono, njiwa

Neno Manabii maana yake ni nini?

Neno Manabii maana yake ni waliovuviwa na Roho Mtakatifu waseme kwa jina la Mungu

Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku gani?

Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume siku ya Pentekoste, yaani siku ya hamsini toka Pasaka. (Mdo 2:1-4)

Roho Mtakatifu aliwafanyia nini Mitume?

Roho Mtakatifu aliwatia Mitume Mwanga wa nguvu ili waweze kuhubiri Injili na kueneza Kanisa kote duniani

Roho Mtakatifu anatufanyia nini sisi Wakristo?

Roho Mtakatifu anatufanyia haya;
1. Anatuangaza tufahamu mafundisho ya dini
2. Anatuimarisha tutende mema na kuacha mabaya
3. Anatutakasa na kutututia uzima rohoni mwetu
4. Analiongoza Kanisa. (Yoh 16:13-15)

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa namna gani?

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa;
1. Neema ya utakaso
2. Fadhila za Kimungu na vipaji vyake

Maandiko Matakatifu ndiyo nini?

Maandiko Matakatifu ndiyo vitabu vyote 73 ambavyo viliandikwa na watu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu vikakusanywa na Kanisa kwa jina la β€œBiblia”, yaani β€œVitabu”.
Hao β€œwanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Pet 1:21).

Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana.
β€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Rom 5:5).
Ametumwa kwetu atufanyie kazi pasipo kuonekana.
β€œUpepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yoh 3:8).
β€œWote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rom 8:14).

Je, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu?

Ndiyo, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu na kulenga hasa kuandaa watu wampokee, wamfuate na kumshuhudia katika umoja wa kundi lake, Kanisa.
β€œAjapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. Nanyi pia mnashuhudia” (Yoh 15:26-27).

Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake nini?

Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake ni kuja kuongozwa naye badala ya kutawaliwa na shetani.
β€œKwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanae mioyoni mwetu, aliaye, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu… Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho” (Gal 4:6-8; 5:25).
β€œIkiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake” (Rom 8:9).

Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia nini?

Tukimpokea Roho Mtakatifu papo hapo tunapokea pia adili kuu la upendo:
β€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Rom 5:5).
Tena tunapokea vipaji vyake ambavyo Yesu alikuwa navyo kikamilifu.
β€œRoho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana. Na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana” (Isa 11:2-3).
Mambo hayo, tofauti na karama, ni ya lazima kwa yeyote apate wokovu wa milele.

Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?

Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo.
β€œWengi wataniambia siku ile: Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri: Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” (Math 7:22-23).
β€œNijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu” (1Kor 13:1-3).

Je, karama ni zile za kushangaza tu?

Hapana, karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi:
β€œMungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha” (1Kor 12:28).
β€œBasi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha” (Rom 12:6-8).

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kufanya nini?

Karama nyingine muhimu zinatuwezesha kuishi kwa useja kama Yesu na Paulo, au kwa ndoa:
β€œNipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane; ni heri wakae kama mimi nilivyo” (1Kor 7:7-8).
β€œSi wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa” (Math 19:11).
Tunavyoona katika historia ya watawa, mara nyingi karama ya useja inaendana na nyingine katika maisha ya sala, ya kijumuia na ya kitume. Hivyo Filipo β€œalikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri” (Mdo 21:9).

Karama zinagawiwa vipi?

Karama zinagawiwa na Roho Mtakatifu jinsi anavyotaka, si kwa sifa au faida ya binafsi, bali kwa ustawi wa taifa la Mungu.
β€œKazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye… Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote wanatenda miujiza? Wote wana karama za kuponya wagonjwa? Wote wanena kwa lugha? Wote wafasiri?… Kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za roho, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa… Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani” (1Kor 12:11,29-30; 14:12,33). Kwa ajili hiyo mitume walipambanua na kuratibu karama katika ibada na katika maisha ya jumuia zisije zikavuruga Kanisa.

Karama za kushangaza zina hatari gani?

Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete majivuno, kijicho na mafarakano.
β€œIkiwa kwenu kuna husuda na fitina, je, si watu wa tabia ya mwili ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?… Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki… Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 3:3; 4:8; 10:12).
Katika mambo yasiyothibitika ni rahisi kudanganyika kuwa yametoka kwa Mungu, kumbe sivyo. Kisha kudanganyika ni vigumu kuachana nayo hata yakiwa na madhara kwa mhusika au kwa Kanisa.
β€œWapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani” (1Yoh 4:1).

Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni lipi?

Tunda la kuongozwa na Roho Mtakatifu ni umoja wa Kanisa unaotokana na ustawi wa upendo na vipaji ndani ya waamini.
β€œWote walijaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja” (Mdo 4:31-32).
β€œTunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria” (Gal 5:22-23).
β€œLakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. Maana hapo palipo wivu na ugomvi, ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi; tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki” (Yak 3:14-17).
Madhehebu yanapozidi kufarakana ni lazima tujiulize kama kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu anatusaidiaje kusali?

Roho Mtakatifu anatusaidia tusali kama Yesu, akiwa mlezi wa ndani na kutumia vipaji vyake saba.
β€œMungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’” (Gal 4:6).
β€œRoho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa… huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu” (Rom 8:26-27).
Ndiyo sababu Kanisa linatuhimiza tumtamani na kumualika kila mara, β€˜Njoo, Roho Mtakatifu!’ yaani kumuomba Baba kwa njia ya Mwana amtume zaidi na zaidi ndani mwetu.

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu.
β€œYeye awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Ef 3:16-19).
β€œHuyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yoh 16:13).
Safari hiyo inategemea sana sala isiyoishia katika maneno bali inalenga kupenya mafumbo kwa imani na upendo.

Sakramenti ya Kipaimara ni nini?

Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa

Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26)

Je, Roho Mtakatifu Katika mfano wa ndimi za Moto Maana yake nini?

Maana yake ni kupata nguvu ya Kuhubiri Injili, Neno la Mungu linalopenya kwenye Moyo Kama Moto.

Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini nini?

Roho Mtakatifu anawafanyia Waamini haya.
1. Anawatakasa
2. Anawaangaza na kuwavuta ili waende kwenye uzima wa milele

Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu Anatutakasa?

Roho Mtakatifu anatutakasa kwa njia ya Sakramenti, Visakramenti, Fadhila za Kimungu na vipaji vyake. (Yoh 16:8)

Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anatenda kazi zake?

Roho Mtakatifu anatenda kazi zake kwa njia hizi;
1. Anatuangaza kwa Mwanga wake tupate kuelewa mafundisho ya dini
2. Anatupatia neema za msaada za kutusaidia kutunza utakatifu wetu
3. Anatuvuta kwa mapendo yake tuzitumie Neema na kufika kwenye uzima wa milele.
4. Anatufariji katika shida zote. Ndio maana Roho Mtakatifu huitwa pia Mfariji

Kwa nini Sakramenti hii inaitwa Kipaimara?

Inaitwa Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu inaimarisha na kukamilisha neema ya Ubatizo

Roho Mtakatifu anakuja kufanya nini rohoni mwetu kwa Kipaimara?

Anakuja kufanya yafuatayo;
1. Anakuja kutuongezea Neema ya Utakaso
2. Anatuletea pia ukamilifu wa mapaji yake saba na msaada wa kuungama imani yetu mbele za watu

Mapaji Saba ya Roho Mtakatifu ndio nini?

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni msaada wake wa kuimarisha na kuzoesha akili na moyo wetu kwa mambo ya utumishi wa Mungu

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni yapi?

Mapaji Hayo ni;
1. Hekima
2. Akili
3. Shauuri
4. Nguvu
5. Elimu
6. Ibada
7. Uchaji wa Mungu (Isaya 11:2)

Hekima ni nini?

Ni upendaji wa Mambo ya Mungu na Machukio ya Mambo ya Dunia

Akili ni nini?

Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu

Shauri ni nini?

Ni utaratibu wa Kuchagua Siku zote mambo yenye kufaa kwa sifs ya Mungu na kwa Wokovu wetu

Nguvu ni nini?

Ni moyo wa kushika sana Amri za Mungu na mambo ya utumishi wake tusiogope watu, matukano, mateso wala kufa. (Rum 8:38-39)

Elimu ni nini?

Ni maarifa ya kutambua werevu na udanganyifu wa shetani; anaposhawishi mwenyewe au kwa kutumia vitu au watu. (1Pet 5:8-9)

Ibada ni nini?

Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima

Uchaji wa Mungu ni nini?

Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake.

Roho Mtakatifu hutajwa wapi katika Rozari?

Roho Mtakatifu hutajwa katika fungu la tatu la Matendo ya Utukufu tusemapo; Aliyepeleka Roho Mtakatatifu. (Mdo 2:1-4)

Kabla ya Kupaa mbinguni Yesu aliwaahidi nini Mitume?

Kabla ya kupaa mbinguni Yesu aliwaahidia Mitume kuwapelekea Roho Mtakatifu; ndiye nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu. (Yoh 16:7)

Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Matunda ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ni yapi?

Matunda ya Roho Mtakatifu ni;
1. Upendo
2. Furaha
3. Amani
4. Uaminifu
5. Uvumilivu
6. Utu wema
7. Fadhila
8. Upole
9. Kiasi
(Wagalatia 5:22, 23)

Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu.

Je, Biblia ilipatikanaje? Nini chanzo na asili ya Biblia.

Biblia iliundwa kwa kukusanya vitabu vya dini vya wakristo hapo awali na kuunda kitabu kimoja. Kwa maana hii, Biblia ni vitabu teule vya dini vilivyoonekana vinafaa kutumika kwa waumini Wakristo ili kusaidia Imani yao. Hivyo basi, kama Biblia ni vitabu teule tuu vipo vitabu vingine vya dini ambavyo havikuwekwa Kwenye Biblia.
Wakristo wa kwanza walichagua vitabu kadhaa na kuviweka pamoja na kisha kuvita Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu muhimu tuu vya dini mpaka kufikia Enzi za Mitume.

Je, Biblia ndicho kitabu pekee cha neno la Mungu?

Hapana, Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu isipokua Biblia ni kitabu kilichoidhinishwa rasmi kutumika Kama kitabu kikuu cha Wakristo. Hii ni kwa sababu Biblia imeundwa na vitabu muhimu tuu vilivyochaguliwa na wakristo wa kwanza vilivyoonekana vinafaa kwa kufundishia, Ibada na kukuza Imani. Kwa hiyo basi vipo vitabu vingine ambavyo haikuwekwa Kwenye Biblia ambavyo ni Maneno ya Mungu.
Hii ndiyo sababu kwa nini Wakatoliki wana vitabu vingi kuliko madhehebu Mengine. Yaani sababu ni kwamba madhehebu Mengine walivitoa vitabu vingine vilivyounda Biblia. Na Wakatoliki waliweka vitabu vingine vya dini Kwenye Biblia walivyoona vinafaa pia kutumika.

Je nje ya Biblia hakuna Neno la Mungu au Maandiko matakatifu?

Nje ya Biblia kuna Neno la Mungu na Maandiko Matakatifu. Hii Inamaanisha kuwa Biblia sio kitabu pekee cha neno la Mungu. Zipo nyaraka na Vipo vitabu vingine vingi ambavyo viliandikwa na Manabii na Mitume ambavyo havikuwekwa kwenye Biblia lakini ni mafundisho ya Mungu. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vikuu vya Mungu.
Kumbuka kuwa sio nyaraka zote za Mitume ziliandikwa Kwenye Biblia. Vile vile manabii walikuwa ni wengi kuliko waliowekwa Kwenye Biblia.

Je Biblia ndiyo mafundisho ya Mungu pekee?

Hapana, Biblia sio mafundisho pekee ya Mungu. Hii ni kwa sababu sio mambo yote aliyofanya na kusema Mungu yaliandikwa na vilevile Mitume hawakua watu wa Mwisho kupokea Roho mtakatifu na kupokea neno la Mungu.

Biblia inatuthibitishia yenyewe kuwa haijakamilika na Si mambo yote yameandikwa Kwenye Biblia

Biblia inatuthibitishia kuwa haijakamilika tunaposoma (Yohane 21:25)
Biblia inatuambia hivi…”Kuna mambo Mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo Kama yangeandikwa yote, moja baada ya jingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.”…Kwa mstari huu Biblia inatuthibitishia kuwa haikuandikwa vitu vyote.

Je Biblia ni mwisho wa Maandiko ya Mungu?

Biblia sio mwisho wa Maandiko ya Kimungu.
Biblia ni sehemu ya maneno ya Mungu mpaka miaka ya Mitume
Hata sasa Mungu anafanya kazi na watu wake kupitia Roho Mtakatifu na kwa kwa sababu hii Biblia sio mwisho wa kazi ya Mungu ya kusema na watu wake.
Mungu yu hai na anafanya kazi na watu wake mpaka sasa kwa kutumia vinywa vya watu Kama aliyofanya hapo awali.
Hata maneno unayohubiriwa sasa yanaweza kuwa ni kutoka kwa Mungu kwa maana hata waandishi wa Biblia walitumiwa na Mungu Kama wahubiri wa sasa. Mungu ni yule yule, Roho Mtakatifu ni yuleyule na Neno ni lile lile.
Kwa hiyo Biblia ni maneno yaliyochaguliwa mpaka enzi za Mitume. Vitabu vilivyofwata Baada ya Mitume japokuwa viliandikwa kwa Roho Mtakatifu havikuwekwa Kwenye Biblia.

Sababu ya Kanisa katoliki kutumia mapokeo na Maandiko ya Watakatifu

Kanisa katoliki linatumia mapokeo na Makala za watakatifu kwa Imani kuwa Mungu yule yule aliyefanya kazi tangu zamani anafanya kazi na watu wake mpaka sasa na hivyo Maandiko ya watu wa Mungu yanafaa kutumika kama yalivyotumika ya watu wa kale.

Yesu alituambia nini kuhusu Neno la Mungu na Mwendelezo wa kazi ya Mungu ya kusema na watu?

Yesu alituambia hivi katika (Yohane 16:12-15)..”Ninayo mengi ya kuwaambieni Ila kwa sasa hamuwezi kuyastahimili. Lakini atakapokuja huyo Roho wa Ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote. Maana hatasema kwa Mamlaka yake mwenyewe bali atasema atakayoyasikia na kuwajulisheni yatakayokuja. Yeye atanitukuza Mimi kwa kuwa atawajulisheni Yale atakayoyapata kutoka kwangu β€œβ€¦
Sasa basi,kama Roho Mtakatifu ni yuleyule na kazi zake ni Zile Zile za tangu Mitume, kwa nini hatukubali kuwa Anafanya kazi mpaka sasa kupitia watu wa Mungu? Kwa nini tunakataa mafundisho yao? Kwa nini tunashindwa kuelewa kuwa Biblia haikuwa mwisho wa Neno la Mungu? Kwa nini tunakana Mapokeo ya Watakatifu? Kwa nini hatuwaamini watumishi wake wa sasa?

Mambo ya Msingi kufahamu kuhusu Ndoa ya Kikatoliki

Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu gani?
Daraja na ndoa ni tofauti na sakramenti nyingine kwa sababu hazilengi hasa faida ya mtu anayezipokea, bali huduma zake kwa ajili ya Kanisa na jamii. Daraja inatia uwezo wa Kristo kwa ustawi wa Kanisa, Bibi arusi wake. Ndoa inatia upendo wake mwaminifu kwa ustawi wa familia, kanisa dogo la nyumbani.
β€œJitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe” (Mdo 20:28).
β€œHakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa” (Ef 5:29-32).

Kadiri ya mpango wa Muumba, ndoa halisi ina sifa ngapi?
Kadiri ya mpango wa Muumba, ndoa halisi ina sifa tatu: umoja, uimara na utayari wa kuzaa.
β€œHamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, β€˜Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja?’ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Math 19:4-6).
β€œMungu akawabarikia, Mungu akawaambia, β€˜Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha’” (Mwa 1:28).
Mitara, uzinifu, talaka, ushoga na kukataa uzazi ni kinyume cha mpango huo.

Yesu aliweka sakramenti ya ndoa kwa sababu gani?
Yesu aliweka sakramenti ya ndoa kwa sababu ya umuhimu wa familia kwa ustawi wa mume na mke, watoto, jamii na ufalme wa Mungu, na kwa sababu ya uzito wa majukumu yanayohusika.
β€œSiku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwepo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake” (Yoh 2:1-2), akaleta divai bora ya ndoa sakramenti badala ya ndoa ya kimaumbile.
Hivyo ametuandalia neema tuweze kushinda β€œugumu wa mioyo” (Math 19:8) unaohatarisha daima uzuri wa mpango wa Mungu kuhusu upendo mwaminifu katika ndoa. β€œMungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana” (Mwa 1:31).

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya nani?
Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake.
β€œNjoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwanakondoo” (Ufu 21:9).
Wakiwa na ndoa halisi, mume na mke waliobatizwa ni ishara wazi ya hao wanaarusi wawili wasioonekana.
β€œKama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake” (Ef 5:24-25).
Ndiyo sababu Mkatoliki hawezi kufunga ndoa bila ya kuhusisha Kanisa na kufuata taratibu zake.

Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?
Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa

Sakramenti ya ndoa ni nini?
Sakramenti ya ndoa ndio yenye kuwaunganisha wakristo wawili mume namke waliopendana kwa hiari bila shuruti au vitisho au kizuizi kwa kuwapa neema ya kuishi pamoja kitakatifu wakiwalea watoto wao katika utakatifu

Je, ndoa halali yaweza kuvunjwa?
Sakramenti ya ndoa iliyofungwa kihalali hudumu milele kwani Yesu anafundisha kuwa “Alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe” (Mt 19:6)

Ndoa imewekwa na nani?
Ndoa imewekwa na Mungu mwenyewe na Yesu Kristo ameeinua na kuifanya Sakramenti. (Mwz 2:18; Mt 19:1-12)

Kabla ya kupokea Sakramenti ya Ndoa hutakiwa nini?
Kabla ya kupokea Sakramenti ya Ndoa hutakiwa;
1. Uhuru wa kila mmoja
2. Matangazo ya ndoa
3. Wachumba wawe na nia ya kweli ya kuoana
4. Mafundisho na semina ya ndoa
5. Wasiwe na kizuizi chochote cha ndoa
6. Wasikae suria na wapokee Sakramenti ya Kitubio

Mtu aweza kupokea Sakramenti ya ndoa zaidi ya mara moja?
Ndiyo, mwenzi akifa yule aliyebaki yupo huru kufunga ndoa tena (1Kor 7:39)

Vizuizi vya ndoa ni kitu gani?
Vizuizi vya ndoa ni vile vinavyofanya ndoa isiwe halali tangu mwanzo

Vizuizi vya ndoa ni vipi?
Vizuizi vya ndoa ni;
1. Upungufu wa umri
2. Uhanithi
3. Ndoa awali halali
4. Tofauti za dini au upagani
5. Daraja Takatifu
6. Nadhiri
7. Utekaji au kutumia nguvu
8. Taksiri au Jinai au Mauaji ya mwenzi wa ndoa
9. Uhusiano wa damu
10. Uhusiano wa ndoa
11. Ugoni au uhawara
12. Kuasili mtoto au Uhusiano wa kisheria

Ndoa mchanganyiko maana yake ni nini?
Ndoa mchanganyiko ni ndoa kati ya Mkristo Mkatoliki na Mkristo asiye Mkatoliki

Ndoa ya utofauti wa Imani maana yake ni nini?
Ndoa ya utofauti wa Imani ni ndoa kati ya Mkristo Mkatoliki na mtu ambaye hajabatizwa kwa mfano Mpagani, Mwislamu, Yehova, Mlokole tangu kuzaliwa n.k

Mkristo Mkatoliki awezaje kufunga ndoa mchanganyiko au utofauti wa dini kwa uhalali?
Aweza kufunga ndoa hiyo kwa uhalali baada ya kupata ruhusa maalumu ya Askofu kwa Barua.

Ili Askofu atoe ruhusa ya kufungisha ndoa ya mchanganyiko au dini tofauti kuna Masharti gani?
Ndiyo, Askofu atatoa ruhusa baada ya Mkristo Mkatoliki kuahidi kwamba;
1. Atabaki Imani Katoliki mpaka kufa na isiwe amedanganya
2. Watoto wote watabatizwa na kulelewa katika Kanisa Katoliki
3. Huyo anayefunga naye ndoa akubali bila masharti yoyote

Je, Mchumba Mkatoliki aweza kuiacha Imani yake kwa sababu ya Ndoa?
Hapana, Kwa kuwa Kanisa Katoliki limeasisiwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo kama la lazima kwa kupata wokovu, wanaokataa kuingia au kuhudumu ndani yake hawawezi kuokolewa.

Kuna kosa gani kama mmoja wapo atakuwa amedanganya ili aruhusiwe kufunga ndoa mseto au mchanganyiko
Kama mmoja amedanganya basi ndoa hiyo ingawa imefungwa haitakuwa halali kabisa mpaka mwisho. Watadumu katika dhambi mpaka kufa au watubu.

Kanisa linatoa ushahuri gani kuhusu ndoa halali au ya mseto?
Kanisa linatambua hatari kubwa kwa Imani linashauri watoto wake wawe na busara kubwa wanapoamua kupendana kwa lengo la kufunga ndoa.

Je, ndoa halali inaweza kuvunjwa?
Hapana, Hakuna yeyote anayeweza kuvunja ndoa halali isipokuwa kifo. (Mt 19:4-6)

Anayevunja ndoa na kuoa au kuolewa anaweza kupokea Sakramenti?
Hapana, Anayevunja maagano ya ndoa na kuoa au kuolewa hawezi kupokea Sakramenti ya Ekaristi wala Kitubio hadi afanye toba na kurekebisha hali hiyo. (Mk 10:11-12)

Ni nani wahudumu wa Sakramenti ya ndoa?
Wahiudumu rasmi wa Sakramenti ya ndoa ni wachumba wenyewe, Padri kama shahidi rasmi wa kanisa. Tena ni lazima ifungwe mbele ya mashahidi wengine wawili.

Watu wa jinsia moja waweza kuoana?
Hapana, watu wa Jinsia moja hawawezi kuoana na wakifanya hinyo wanatenda dhambi kubwa inayomlilia Mungu. (Wal 18:22)

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu Mungu

Je, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani?

Ndiyo, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani kila wakati hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu

Nani ameumba vitu vyote?

Mungu ameumba vitu vyote

Mungu ni nani?

Mungu ndiye muumba wa kila kitu katika uwingu na nchi, Mkubwa wa ulimwengu mwenye kuwatuza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya.
“8Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla hamjamwomba.’’ 9β€˜β€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba : β€œBaba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe.(Mt. 6:8-9).
17Yesu akamwambia, β€˜β€˜Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie, β€˜Ninapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu ambaye ni Mungu wenu.’ ’’ (Yoh 20:17)

Mungu ni Muumba vyote maana yake ni nini?

Mungu ni Muumba vyote Maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tu pasipo kutumia chochote. (2Wamakabayo 7:28, Yoh 1:3)

Mungu ni nini?

Mungu ni Roho kamili na ukamilifu wake hauna mipaka. (Yoh. 4:24, Kut.3:13-15, Zb. 144:3)

Mungu ni Roho maana yake ni nini?

Mungu ni Roho maana yake haonekani wala hashikiki. (Lk: 24:39)

Mungu ni mweza wa yote maana yake ni nini?

Mungu ni mweza wa yote maana yake kila atakalo hufanya. (Zab 135:6)

Mungu ni wa Milele maana yake ni nini?

Mungu ni wa Milele maana yake hana mwanzo wala mwisho, amekuwapo kabla ya nyakati, yupo na atakuwapo baada ya nyakati, yupo daima. (1Tim, 1:17)

Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10)

Mungu ni Mwenye haki maana yake ni nini?

Mungu ni Mwenye haki maana yake kila mtu hupata kwa Mungu haki yake kadiri anavyostahili

Mungu aenea pote maaana yake ni nini?

Mungu aenea pote maaana yake yupo kila mahali mbinguni na duniani wala hakuna mahali asipokuwepo?. (Zab, 139:7-12)

Mungu ajua yote maana yake nini?

Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu

Mungu ni mwenye huruma maana yake nini?

Mungu ni mwenye huruma maana yake anawasamehe watu dhambi zao wakitubu.

Mungu ni mwenye subira maana yake ni nini?

Mungu ni mwenye subira maana yake mara nyingi akawia kuwaadhibu wakosefu maana ataka kuwapa nafasi ya kuongoka. (Eze, 33:11, Zb, 102;1-5)

Mungu wako wangapi?

Mungu yupo mmoja tuu Mkubwa wa wote na Baba wa wote. (Is: 44:6)

Katika Mungu mmoja kuna nafsi ngapi?

Katika Mungu mmoja kuna nafsi tatu nazo ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; nafsi zote ni sawa.

Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?

Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22)

Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?

Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu kwa ajili yetu wanadamu na wokovu wetu ili atupatanishe na Mungu na kutushirikisha tabia ya umungu. (2Pet, 1:4)

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria ni ipi?

Nafasi ya Heshima kwa Bikira Maria inafuata baada ya Heshima kwa Utatu Mtakatifu

Tunaanzaje kumjua Mungu?

Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu.
β€œKwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake” (Rom 1:20).

Je, tunaweza kusema juu ya Mungu?

Ndiyo, tunaweza kusema juu ya Mungu kuanzia wema, ukweli na uzuri wa viumbe vyake na kumsifu kiasi chetu kwamba ndiye wema, ukweli na uzuri wenyewe.
Lakini tukiri pia kuwa maneno yetu duni hayawezi kutosha kamwe kufafanua fumbo lake.
β€œKwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua” (Ayu 42:3).
Tungemuelewa, asingekuwa Mungu.

Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote.
β€œTazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; hesabu ya miaka yake haitafutiki” (Ayu 36:26).
β€œMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. β€œRoho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39).

Je, Mungu amewasiliana nasi?

Ndiyo, Mungu amewasiliana nasi, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katika urafiki naye na hatimaye tushiriki heri yake.
β€œNikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshima” (Zab 8:3-5).
β€œSiwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu” (Yoh 15:15).

Hasa Mungu amejifunua kuwa nani?

Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe.
β€œBwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6).
β€œMungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake” (1Yoh 4:16).
β€œYeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo” (1Yoh 4:8).

Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?

Ndiyo, Mungu amejitambulisha pia kwa majina mbalimbali. Katika Agano la Kale jina muhimu kuliko yote liliandikwa β€œYHWH” yaani, β€œMimi Ndimi”. Tangu zamani Wayahudi hawalitamki, hivyo wakilifikia wanasoma kwa kutafsiri, β€œBwana”.
Ndiyo sababu katika Agano Jipya halitumiki kamwe, isipokuwa Yesu alifunua Umungu wake kwa kujisemea, β€œMimi Ndimi” na kwa kukubali kuitwa, β€œBwana”. Pamoja na hayo, alisali na kufundisha kusali kwa kumuelekea β€œABA” yaani, β€œBaba”. Ndilo jina ambalo linampendeza zaidi na kutuingiza katika fumbo lake kama wana ndani ya Mwana pekee ambaye β€œMungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba” (Fil 2:9-11).
β€œMsalipo, semeni, β€˜Baba, jina lako litakaswe’” (Lk 11:2).
β€œMlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, β€˜Aba!’ yaani, β€˜Baba!’” (Rom 8:15).

Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu.
Amefanya hivyo kwa maneno na matendo yanayoshikamana sana kwa kuwa maneno yanafafanua matendo, nayo matendo yanathibitisha maneno.
β€œMungu hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (1Tim 2:4).
β€œMungu si mtu, aseme uongo” (Hes 23:19).
Yeye hadanganyiki wala hadanganyi.

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Kwa nini dhambi zipo?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani.
β€œMimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu… Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo” (Mwa 45:4-5; 50:20).

Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?

Mungu aliwahi kujifunua kwa wazazi wetu wa kwanza, akaendelea hasa kwa taifa la Israeli, hadi alipomtuma Mwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule.
β€œMungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana” (Eb 1:1-2).

Je, ufunuo wa Mungu unaendelea hata leo?

Hapana, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani Neno wake wa milele.
β€œKwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” (Yoh 1:17-18).
Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema,
β€œMbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Math 24:35).
β€œIjapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!” (Gal 1:8-9).

Ufunuo wa Mungu unatufikiaje miaka elfu mbili baada ya Kristo?

Ufunuo wa Mungu unatufikia kupitia Kanisa lake, lililokabidhiwa Mapokeo ya Mitume na linaloongozwa na Roho Mtakatifu hadi ukweli wote.
Yesu aliahidi kwamba,
β€œYeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yoh 16:13).
β€œMaana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” (1Kor 2:10).

Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?

Hapana, Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima ni Umoja kamili.
β€œBwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” (Mk 12:29).
Tumuabudu yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine.
β€œMimi na Baba tu umoja” (Yoh 10:30).

Tumejuaje kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu?

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu.
β€œYesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, β€˜Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye’” (Math 3:16-17).
Naye akaagiza, β€œBasi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu” (Math 28:19).
Ni nafsi tatu zenye jina moja, yaani Umungu mmoja tu.

Umoja wa Mungu unategemea nini?

Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu.
β€œBaba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu” (Yoh 17:24).

Je, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji?

Ndiyo, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji, kila nafsi akiuchangia kulingana na sifa yake maalumu ndani ya Utatu. Baba Mwenyezi sifa yake ni Uwezo. Mwana kama Neno la Baba sifa yake ni Hekima. Roho kama Pumzi ya uhai ya Baba sifa yake ni Upendo.
Katika Uwezo wake Baba anafanya yote kwa Hekima na Upendo, hasa katika utume wa Mwana aliyefanyika mtu na katika utume wa Roho kama paji.
β€œAmin, amin, nawaambia: Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vilevile” (Yoh 5:19).

Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake.
β€œMaana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote” (Rom 11:32).

Yesu ni Mungu au mtu?

Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. β€œKwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1Tim 2:5). β€œKatika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli.

1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: β€œHuyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, β€˜Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu. Yohana 1:1-6:37

5 Tomaso akamwuliza, β€œBwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaam bia, β€œMimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”
8 Filipo akamwambia Yesu, β€œBwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.” 9 Yesu akamjibu, β€œFilipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, β€˜Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. Yohane 14:5-10

29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, β€œNimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, β€œTunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.” Yohane 10: 29-33

Yesu anapatikana wapi? Yesu anakaa wapi? Yesu Yupo wapi kwa sasa?

Yesu kama Mungu yupo kila mahali, hakuna mahali asipokuwepo. Yesu kama mwanadamu yupo Mbinguni kwa Baba na anakaa nasi duniani katika Maumbo ya Mkate na Divai Katika Ekaristi.


Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake.
β€œBasi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, β€˜Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu’” (Mk 15:39).

Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele.
β€œHayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” (Yoh 14:10).

Kwa nini Maria anastahili kuitwa β€œMama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa β€œMama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa:Β β€œUmebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.Β Limenitokeaje neno hili, hataΒ mama wa BwanaΒ wangu anijilie mimi?
” (Lk 1:42-43).

Je, Bikira Maria ni kama Bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu Duniani au anayo thamani zaidi?

Bikira Maria sio kama bahasha au chombo cha kumleta Yesu tuu duniani. Yesu ametokana na Bikira Maria katika ubinadamu wake. Mwili wa Yesu wa kiubinadamu ni sehemu au uzao wa Bikira Maria. Bikira Maria anayo uhusiano wa damu na Yesu Kristu. Ndiyo maana Mungu alimtakasa Bikira Maria Ili atakayezaliwa kutoka kwake awe na yeye mtakatifu.
Mungu alimtakasa Bikira Maria kabla ya Kuamua kuzaliwa kupitia yeye kwa kuwa Mungu ni Mtakatifu. Ubinadamu wa Yesu (MWILI – Nyama na Damu) asili yake ni Bikira Maria.

Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, β€œhata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8).
β€œKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rom 5:19).

Je, Mungu Baba alihusika na sadaka ya Mwanae?

Ndiyo, Mungu Baba alihusika sana na sadaka ya Mwanae, kwa sababu;
β€œMungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake… Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye” (2Kor 5:19,21).

Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana.
β€œPendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Rom 5:5).
Ametumwa kwetu atufanyie kazi pasipo kuonekana.
β€œUpepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” (Yoh 3:8).
β€œWote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu” (Rom 8:14).

Je, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia?

Ndiyo, tumuadhimishe Mungu katika Nafsi zake tatu pia: Baba kama asili ya umungu na ya uhai wote, Mwana kama Neno wake aliyejifanya mtu atukomboe, tena Roho Mtakatifu kama Upendo wao ambao unawaunganisha na kututakasa.
Pamoja na viumbe vyote tuwaimbie usiku na mchana,Β β€œMtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja!” (Ufu 4:8).
β€œMungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli” (Yoh 4:24).

Hamu kuu ya binadamu ni ipi?

Hamu kuu ya binadamu ni kumwona Mungu

Je, Yatupasa kumwomba Roho Mtakatifu?

Ndiyo, kwani twataka kwake maonyo na msaada. Tusipokuwa na neema yake hatuwezi kutenda jambo jema la kufaa kutuokoa. (Yoh 16:13)

Mafundisho kuhusu Binadamu, Mtu na Utu

Mungu alisema nini alipotaka kumuumba mtu?

Mungu alipotaka kumwumba mtu alisema;
“Tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu” (Mwa 1:26-27)


Mtu ni nani?

Mtu ni kiumbe chenye mwili na roho kilichoumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. (Mwa 1:26)


Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu maana yake ni nini?

Tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu maana yake tuna roho zenye akili na utashi yaani uwezo wa kutofautisha mema namabaya, na zitakazoishi milele.


Watu wa kwanza kuumbwa na Mungu ni akina nani?

Watu wa kwanza kuumbwa na Mungu ni Adamu na Hawa (Eva). (Mwa 1:27)


Mungu alimwumbaje Adamu?

Mungu aliufanya mwili wa Adamu kwa udongo, akaupulizia roho yenye uhai. (Mwa 2:7)


Mungu alimwumbaje Eva (Hawa)?

Mungu alimwumba Eva kwa mfupa wa ubavu kutoka kwa Adamu, akamtia roho. (Mwa 2:21-24)


Kwa nini Mungu alituumba? Kwa nini Mungu aliumba mtu?

Mungu ametuumba tumjue, tumpende, tumtumikie tulipo wazima hapa duniani, hata mwisho tukisha kufa tuende kwake Mbinguni katika katika makao ya raha milele. (Mwa 2:7; Mt. 19:17; Yoh 14:1-3 na Yoh 17:24)


Ni kipi cha kutunza kwa makini zaidi kati ya mwili na roho yako?

Yatupasa kutunza roho zetu zaidi kwni Yesu mwenyewe alisema:
“Itamfaa nini mtu ikiwa ataupata ulimwengu wote na kuupoteza ufalme wa Mungu.” (Mk 8:38)


Mungu aliwapa watu wa kwanza mapaji gani?

Mungu aliwapa watu wa kwanza neema ya utakaso na neema nyingine nyingi, na kukaa paradisini wenye heri bila kufa. (Mwa 28-30; 3:7)


Mungu aliwaamuru nini watu wa kwanza?

Mungu aliwaamuru watu wa kwanza wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasije wakafa. (Mw 2:16-17)


Je, Adamu na Eva walimtii Mungu?

Hapana, Adamu na Eva walitenda dhambi ya kutotii, wakataka kuwa kama Mungu lakini bila Mungu na pasipo kufuata maagizo ya Mungu. (Mwa 3:1-16)


Dhambi ya asili ndio nini?

Dhambi ya asili ambayo binadamu wote wanazaliwa nayo, ni hali ya kukosa utakatifu na hali ya asili ya urafiki na Mungu


Adhabu gani walipewa Adamu na Eva?

Adamu na Eva kwa ukubwa wa dhambi yao ya kiburi na ya uasi:
1. Walipoteza neema ya utakaso
2. Walifukuzwa paradisini
3. Walipungukiwa akili na kushikwa na tamaa ya kutenda dhambi
4. Walipitia mahangaiko na taabu nyingi
5. Kupaswa kufa. (Mwa 3:16-20: 5:5)


Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi nini?

Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi kuwaletea Mkombozi. (Mwa 3:15)


Alipokwisha umba watu Mungu aliwafundisha nini?

Alipokwisha umba watu Mungu aliwafundisha Dini (Mwa 2:15-17)


Dini ni nini?

Dini ndio mambo yatupasayo kwa Mungu Bwana wetu na Baba yetu. (Mk 16:15-16)


Mungu alinena na nani?

Alinena na;
1. Adamu na Mababu
2. Musa na Manabii
3. Mwishowe Mungu alimleta mwanawe atufumbulie kabisa dini. (Waebr 1:14-45)


Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi.


Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?

Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46)


Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kufanya nini?

Ikiwa Mungu anatushughulikia, tunapaswa kujiachilia mikononi mwake kwa moyo wa kitoto, tukiwajibika bila ya mahangaiko yanayowapata watu wasiomjua.
β€œWaangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je, si bora kupita hao?” (Math 6:26).
β€œNawe una nini usichokipokea?” (1Kor 4:7).
β€œNimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?” (Zab 116:12).


Kwa kuwa tumetoka kwa Mungu na tutarudi kwake, tunapaswa kuishi vipi?

Kwa kuwa tumetoka kwa Mungu na tutarudi kwake, tunapaswa kuishi kulingana na hakika hiyo, kwa kumpa daima nafasi ya kwanza katika mawazo na mapendo yetu, tusijali kiumbe chochote kuliko yeye wala badala yake.
β€œBwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote” (Kumb 6:4-5).
Tusipoitikia upendo wake na kuambatana naye, basi, tumeshindikana kabisa.


Tunaanzaje kumjua Mungu?

Tunaanza kumjua Mungu kwa kuzingatia viumbe vyake, hasa dhamiri yetu.
β€œKwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake” (Rom 1:20).


Je, Mungu amewasiliana nasi?

Ndiyo, Mungu amewasiliana nasi, akijitambulisha na kujitoa kwetu, tuweze kuishi katika urafiki naye na hatimaye tushiriki heri yake.
β€œNikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; umemvika taji ya utukufu na heshima” (Zab 8:3-5).
β€œSiwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu” (Yoh 15:15).


Mungu ametufunulia nini?

Mungu ametufunulia pia ukweli juu yetu wenyewe akijibu kabisa maswali yanayotusumbua kuhusu maana na lengo la maisha yetu.
Amefanya hivyo kwa maneno na matendo yanayoshikamana sana kwa kuwa maneno yanafafanua matendo, nayo matendo yanathibitisha maneno.
β€œMungu hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli” (1Tim 2:4).
β€œMungu si mtu, aseme uongo” (Hes 23:19).
Yeye hadanganyiki wala hadanganyi.


Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Kwa nini dhambi zipo?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani.
β€œMimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu… Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo” (Mwa 45:4-5; 50:20).


Viumbe vyenye hiari ni vipi?

Malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye hiari ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la.
β€œNazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” (Kumb 30:19-20).


Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?

Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele.
β€œKulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” (Ufu 12:7-8).
Chaguo letu binadamu linafanyika siku kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu dini na maadili.
β€œMwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (Yoh 5:39-40).


Sisi binadamu tukoje?

Sisi binadamu ni umoja wa mambo mawili: roho iliyoumbwa na Mungu moja kwa moja, na mwili ulioumbwa naye kwa njia ya wazazi.
Maumbile hayo yanatakiwa kukamilika kwa kupokea na kutimiza upendo wa Mungu aliyesema,
β€œβ€™Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi’. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba” (Mwa 1:26-27).


Je, mwili wetu ni muhimu?

Ndiyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa na Mwanae ili atuokoe, umehuishwa na Roho Mtakatifu atakayeutukuza siku ya ufufuo kwa mfano wa Yesu.
β€œMwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. Je, hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye?… Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?” (1Kor 6:13-16,19).


Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?

Mungu aliwahi kujifunua kwa wazazi wetu wa kwanza, akaendelea hasa kwa taifa la Israeli, hadi alipomtuma Mwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule.
β€œMungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana” (Eb 1:1-2).


Je, Mungu aliumba watu wa kwanza katika hali ya mateso na mauti tuliyonayo sasa?

Hapana, Mungu aliumba watu wa kwanza katika hali ya heri, wakiwa na upendo wake, utakatifu na uadilifu.
Mateso na mauti yametokana na uasi wetu ambao tangu mzazi wetu wa kwanza tunajaribu kuboresha maisha yetu mbali na Mungu.
β€œMungu hakuifanyiza mauti, wala haimpendezi walio hai wakipotea… Ila ulimwengu uliingiwa na mauti kwa husuda yake Shetani” (Hek 1:13; 2:24).
β€œDhambi iliingia ulimwenguni kwa mtu mmoja, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Rom 5:12).


Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi?

Ndiyo, Mungu angeweza kuzuia watu wasitende dhambi, lakini aliwaacha watende kwa hiari yao awaonyeshe ukuu wa huruma yake.
β€œMaana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote” (Rom 11:32).


Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?

Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu.
Lakini Mungu aliwahi kumuambia Shetani:
β€œNitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako, na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwa 3:15).
β€œHata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4).


Dhambi zimetuathiri vipi tena?

Dhambi zimetuathiri kwa ndani zaidi, zikitutia udhaifu katika mwili, ujinga katika akili na uovu katika utashi; madonda hayo yanatufanya tuzidi kushindwa.
β€œKwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii” (Rom 8:7).


Katika unyonge wetu tutumainie nini?

Katika unyonge wetu tutumainie huruma ya Mungu aliyetutumia Mkombozi hata β€œdhambi ilipozidi, neema ikawa kubwa zaidi” (Rom 5:20).
Ushindi wake juu ya dhambi umetupatia mema makubwa kuliko tuliyoyapoteza kwa dhambi.
β€œMungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu; alituuhisha pamoja na Kristo; yaani, mmeokolewa kwa neema” (Ef 2:4-5).


Yesu ni Mungu au mtu?

Yesu ni Mungu na mtu kwa pamoja, ndiyo sababu ni mshenga pekee kati ya Mungu na watu. β€œKwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, mwanadamu Kristo Yesu” (1Tim 2:5). β€œKatika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol 2:9). Hivyo ni Mungu kweli na mtu kweli.

1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hiyo huangaza gizani na giza haliwezi kamwe kuizima.
6 Mtu mmoja aitwaye Yohana alitumwa na Mungu 7 awaambie watu kuhusu hiyo nuru, ili kwa ushuhuda wake wapate kuamini. 8 Yohana mwenyewe hakuwa ile nuru. Yeye alitumwa kuishuhudia hiyo nuru. 9 Nuru halisi ambayo inawaangazia watu wote ilikuwa inakuja ulim wenguni. 10 Neno alikuwepo ulimwenguni, lakini japokuwa aliumba ulimwengu, watu wa ulimwengu hawakumtambua! 11 Alikuja nyumbani kwake, lakini watu wake hawakumpokea! 12 Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu. 13 Hawa hawakuwa watoto wa Mungu kwa kuzaliwa kwa njia ya asili, wala kwa mapenzi au mipango ya watu bali wamezaliwa na Mungu mwenyewe.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba. 15 Yohana alishuhudia habari zake, akatangaza: β€œHuyu ndiye yule niliyewaambia kuwa, β€˜Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi kwa kuwa alikuwapo kabla sijazaliwa.”’ 16 Na kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema tele. 17 Musa alitule tea sheria kutoka kwa Mungu, lakini Yesu Kristo ametuletea neema na kweli. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee, ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha Mungu kwetu. Yohana 1:1-6:37


5 Tomaso akamwuliza, β€œBwana, hatujui unakokwenda; tutaijuaje njia?” 6 Yesu akawaam bia, β€œMimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”
8 Filipo akamwambia Yesu, β€œBwana, tuonyeshe Baba yako nasi tutaridhika.” 9 Yesu akamjibu, β€œFilipo, imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu? Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje unasema, β€˜Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya yote. Yohane 14:5-10


29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, β€œNimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, β€œTunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.” Yohane 10: 29-33


Yesu anapatikana wapi? Yesu anakaa wapi? Yesu Yupo wapi kwa sasa?

Yesu kama Mungu yupo kila mahali, hakuna mahali asipokuwepo. Yesu kama mwanadamu yupo Mbinguni kwa Baba na anakaa nasi duniani katika Maumbo ya Mkate na Divai Katika Ekaristi.


Je, Umungu na utu wa Yesu vinachanganyikana?

Hapana, Umungu na utu wa Yesu vimeunganika katika nafsi moja visichanganyikane, kwa kuwa ndani yake hali hizo mbili zinatenda kila moja ya kwake.
β€œBasi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, β€˜Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu’” (Mk 15:39).


Je, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu?

Ndiyo, Mwana wa Mungu tangu atwae mwili ni mtu kamili mwenye akili na utashi wa kibinadamu. Katika umoja wa nafsi yake vipawa hivyo vinatenda kulingana na Umungu anaouchanga na Baba na Roho Mtakatifu milele.
β€œHayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake” (Yoh 14:10).


Kwa nini Yesu alishawishiwa/alijaribiwa na Shetani?

Yesu alishawishiwa na Shetani kwa kuwa ni mtu kweli, akamshinda kwa niaba ya watu wote, akituonyesha namna ya kumtii Mungu moja kwa moja, β€œhata mauti, naam, mauti ya msalaba” (Fil 2:8).
β€œKwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” (Rom 5:19).


Tutakapofariki dunia itatutokea nini?

Tutakapofariki dunia roho yetu isiyokufa, mbali na mwili unaooza, itapewa tuzo au adhabu tuliyostahili kwa maisha yetu. β€œIkawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake” (Lk 16:22-23). β€œKwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” (Fil 1:21,23). β€œNasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni β€œmavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu 12:7). Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele. β€œPumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno” (Ez 37:10).

Je baada ya kufa ni hapo hapo roho inaenda motoni au mbinguni, Au ni mpaka Siku ya hukumu Yesu Atakaporudi?

Ni siku ile ile Roho ya mtu aliyekufa inaenda Mbinguni, toharani au Motoni. Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
“Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” (Luka 23:42-43)
Sauli aliweza kuongea na Samweli hata baada ya kufa na Samweli alimbashiria mambo yatakayotokea kwa Sauli maanake ni kwamba Japokuwa alikuwa amekufa bado anayomuungano na Mungu ndio maana aliweza kumwambia Sauli mambo yatakayompata,
“7Basi Sauli akawaambia watumishi wake, β€œNitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi ili nimwendee nipate kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, β€œYuko mwanamke mmoja huko Endori.” 8Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, β€œNibashirie na unipandishie huyo nitakayekutajia,” 9Huyo mwanamke akamwambia, β€œWewe unajua lile alilofanya mfalme Sauli. Amewakatilia mbali wapunga pepo, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?” 10Sauli akamwapia huyo mwananmke kwa Jina la BWANA, akasema, β€œKwa hakika kama BWANA aishivyo, hutaadhibiwa kwa ajili ya jambo hili.” 11Ndipo yule mwanamke akauliza, β€œJe unataka nikupandishie nani? Sauli akasema, β€œNipandishie Samweli.” 12Yule mwanamke alipomwona Samweli alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamwuliza Sauli, β€œMbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.” 13Mfalme akamwambia, β€œUsiogope. Unaona nini? Yule mwanamke akasema, β€œNaona Mungu anapanda kutoka ardhini.” 14Sauli akamwuliza, β€œNi mfano wa nini?” Yule mwanamke akasema, β€œNi mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.” Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi uso wake hadi ardhini. 15Samweli akamwuliza Sauli, Kwa nini unanitaabisha, kunipandisha juu?” Sauli akasema, β€œMimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe lakufanya.” 16Samweli akamwuliza, β€œKwa nini uniulize mimi, maadam BWANA amekuacha na kuwa adui yako? 17BWANA ametenda lile alilotangulia kusema kwa kupitia kwangu. BWANA ameurarua ufalme kutoka mikononi mwako, naye amempa mmoja wa jirani zako, yaani, Daudi. 18Kwa sababu wewe hukumtii BWANA, wala hukumtimizia ghadhabu yake kali juu ya Waamaleki, BWANA amekutendea mambo haya leo. 19Zaidi ya hayo, BWANA atawatia Israeli pamoja na wewe mkononi mwa Wafilisti na kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia atalitia jeshi la Israeli mkononi mwa Wafilisti.
Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro Yesu alisimulia hivi
19 Akasema, β€œPalikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake. 22 β€œHatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, β€˜Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, β€˜Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, β€˜Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, β€˜Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 β€˜Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’ 31 β€œIbrahimu akamwambia, β€˜Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’ (Luka 16:19-31)
Wakati Yesu anabadilika Sura walitokea Musa na Eliya.
“Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu. 2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang’aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye. 4 Hapo Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya.” (Mathayo 17:1-5)
Yesu alituambia kuwa Mungu sio wa wafu bali wa walio hai ndio maana akaitwa Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo kwa kuwa Wote wako hai kwake.
37Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila keteketea, alipomwita Bwana β€˜Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki na Mungu wa Yakobo.’ 38Yeye Mungu si Mungu wa wafu bali wa walio hai, kwa kuwa Kwake wote ni hai.” (Luka 20:37-38)
Yesu alimwahidi yule mtu waliyesulubiwa pamoja kuwa watakuwa peponi pamoja siku hiyo hiyo na sio siku ya hukumu.
“Kisha akasema, “Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akamwambia, “Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi.” (Luka 23:42-43)
Angalia pia wakati Stefano akipigwa Mawe aliikabidhi roho yake kwa Mungu baada ya kuona mbingu zimefunguka hii ni kama Yesu alivyokuwa pale msalabani aliikabidhi Roho yake kwa Baba yake.
55Lakini yeye Stefano akiwa amejazwa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, naye Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 56Akasema, β€œTazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kuume wa Mungu.’’ 57Lakini wao wakapiga kelele kwa sauti kubwa, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja. 58Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni mwa kijana mmoja aitwae Sauli. 59Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, β€œBwana Yesu, pokea roho yangu” 60Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, β€œBwana usiwahesabie dhambi hii.’’ Baada ya kusema haya, akalala. (Mdo 7:55-60)
Kwenye Ufunuo tunasoma (Ufunuo 6:9-10) β€œNa alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.”
Kwa hiyo mtu akifa anaenda mbinguni au motoni kulingana na alivyoishi.
β€œNasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” (2Kor 5:8). Kwa kuwa kifo ni β€œmavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” (Mhu 12:7).
Siku ya ufufuo roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya uzima au moto wa milele.
β€œKwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” (Fil 1:21,23).
Mtume Petro ameandika hivi…
“18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.” (1Petro 3:18-20)


Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?

Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > β€œhupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika” (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo β€œndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi” (Lk 21:27).
β€œSaa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu” (Yoh 5:28-29).
β€œNa hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele” (Math 25:46).


Haki gani ya Binadamu ni ya msingi kupita zote?

Haki ya binadamu iliyo ya msingi kupita zote ni uhai wake ambao ni lazima uheshimiwe na kulindwa tangu siku ya kutungwa mimba


Hamu kuu ya binadamu ni ipi?

Hamu kuu ya binadamu ni kumwona Mungu

Maswali na majibu kuhusu Mpako wa wagonjwa au Mpako wa Mwisho

Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu gani?
Yesu aliweka Kitubio na Mpako wa Wagonjwa kwa sababu alijua udhaifu wa binadamu hauishi mara anapopokea uzima wa Mungu kwa sakramenti tatu za kuingizwa katika Ukristo. Hivyo alipanga kusaidia mpaka mwisho wa dunia waamini wake watakaopatwa na dhambi na ugonjwa, kama alivyowasaidia wengi aliokutana nao katika maisha yake.
β€œYesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, β€˜Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako’… β€˜Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi’ – amwambia yule mwenye kupooza – β€˜Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako’. Akaondoka, akaenda zake nyumbani kwake. Makutano walipomwona, walishikwa na hofu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu amri ya namna hii” (Math 9:2,6-8).


Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na nani?
Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa β€œkupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (Math 10:1). Nao
β€œwakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza” (Mk 6:13).
β€œMtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa, nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa” (Yak 5:14-15).


Mafuta ya mpako wa wagonjwa yanamaanisha nini?
Mafuta ya wagonjwa yanamaanisha lengo la kuwaponya na kuwarudishia nguvu na uzuri.
Kama kawaida, maneno yanaweka wazi zaidi kuwa lengo si kuponya mwili tu, bali hasa roho kwa kuitia msamaha na faraja katika mateso ambayo huenda yakaendelea. Kwa kuwa Mungu haponyi mwili kila mara, isipokuwa kwa faida na wokovu wa mgonjwa na wa wengine. Kama ndiyo mapenzi yake, kila mmoja ajifunze kufaidika vilevile na ugonjwa:
β€œMakusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke. Naye akaniambia, β€˜Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu’. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu” (2Kor 12:7-9).
β€œSasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake” (Kol 1:24).


Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ni nini?
Ni Sakramenti ambayo Padri humuombea neema ya Mungu na kumpaka Mafuta Matakatifu mgonjwa aliye katika hatari ya kifo kwa ajili ya neema ya roho na mwili. (Yak 5:14-15, Mk 6:13)
Sakramenti ya Mpako wa wagonjwa ilianza lini? Je, wakati wa Yesu kulikuwa na sakramenti hii?
Sakramenti ya mpako wa wagonjwa ilikuwepo tangu wakati Yesu akiwa hai. Tunaweza kuiona Kwenye Biblia tunaposoma Yesu alivyowatuma wanafunzi wake waliwapaka watu mafuta. “Waliwatoa pepo wengi Wabaya, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta wakawaponya. (Marko 6:13)


Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?
Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu.


Sakramenti ya Mpako Wa Wagonjwa inamanufaa gani rohoni mwa mtu?
Manufaa ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni
1. Nguvu ya kuvumilia mateso na kuyaunganisha na mateso ya Yesu Kristo
2. Maondoleo ya dhambi zote asizoweza kuziungama
3. Nafuu ya mwili, hata uzima ikifaa kwa wokovu wa roho yake
4. Neema ya kujiandaa kuaga dunia na kuingia katika uzima wa milele


Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri


Padri aitwe kwa mgonjwa lini?
Padri aitwe kwa mgonjwa mara inapoonekana Hatari ya Kifo na kamwe isisubiriwe mpaka mgonjwa apoteze fahamu.


Ni nani aweza kupokea Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?
Ni kila Mkatoliki aliyefikia umri wa kufikiri na aliye katika hatari ya kufa kwa ugonjwa au uzee aweza kupokea Sakramenti hii.


Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa yaweza kupokelewa mara ngapi?
Sakramenti hii yaweza kupokelewa mara nyingi ugonjwa ukizidi au akipatwa na ugonjwa mwingine mkubwa


Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni nini?
Alama wazi ya Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni tendo la kupaka Mafuta Matakatifu wagonjwa na kutamka maneno
“Kwa mpako huu Mtakatifu na kwa pendo lake kuu, Bwana Akujaze na nguvu ya Roho Mtakatifu. Amina Akuondoe katika enzi ya dhambi, akuweke huru. Kwa wema wake akupe nafuu katika mateso yako na kukujalia neema. Amina”


Kama padri hatapatika na mgonjwa afanye nini?
Kama padri hatapatikana mgonjwa aweke nia ya kuungama na afanye majuto kamili


Komunyo pamba ndio nini?
Komunyo pamba ndio Ekaristi inayopokelewa na wale wanaokaribia kuaga maisha ya duniani na wanaojiandaa kuvukia uzima wa milele

Faida ya kuabudu Ekaristi Takatifu

1.Kila saa moja tunayotumia kuabudu, inafurahisha moyo wa Yesu na hivyo majina yetu huandikwa mbinguni kwa ajili ya uzima wa milele (Mama Thereza wa Calcuta)
2.Maisha ya kiroho ya familia zetu yanaimarishwa kwa njia ya saa ya kuabudu (John Paul II)
3. Saa takatifu ya kuabudu ni ya muhimu sana kiasi kwamba roho za waamini wengi huenda kwenye uzima (mbinguni) badala ya motoni (ufunuo wa Yesu kwa Dina Belanger)
4. Wakati pekee ambao Yesu aliwaomba kitu wanafunzi wake ni wakati anakaribia mateso na hakuomba chochote isipokua saa moja ya kukesha nae (Askofu Mkuu Fulton Sheen)
5.Saa moja takatifu ya kuabudu ni kushiriki katika harakati za ukombozi (Askofu mkuu Fulton Sheen)
6. Neema ya kuabudu Ekaristi iko juu ya watu wote (St Peter Julian Eymard)
7.Bwana wetu Yesu husikia maombi yetu yote na popote lakini amewafunulia watu wake kuwa wale watakaokwenda kukaa nae katika kuabudu Ekaristi wanapata neema zaidi (Mtakatifu Alphonsus Ligoria)
8.Kila saa unapokwenda kuabudu kumbuka kwamba Yesu amekusubiria wewe binafsi kwenda kumtembelea kwa karne ishirini (St Josemaria scavia)
9.Kuabudu kwa dhati kuna neema na manufaa makubwa ambayo huzidi kwa wale wanaoabudu, hupanuka na kugusa nyumba zao familia zao na mpaka katika parokia zao (Pope Paul VI)
10. Saa moja takatifu mbele ya Ekaristi ni muhimu kuliko miaka elfu moja ya utukufu wa mwanadamu (Mtakatifu Padre Pio)

Asili na matumizi ya Neno “AMINA” kama kiitikio muhimu katika Liturujia

Kiitikio hicho tunakifahamu sisi sote; tunaitikia mara nyingi lakini je, tunaelewa umuhimu wake? Binafsi nikichunguza wakati wa maadhimisho mbalimbali ya Liturujia hasa Adhimisho la Ekaristi, ni baadhi tu ya waamini wanaoitikiaAmina sehemu mbalimbali wakati wa Misa. Waamini wengine huitikia  kwa sauti  ya kuungama dhambi na wengine hawaitikii kabisa.

Asili yake 

Kwa asili Amina ni neno la kiebrania na maana yake ni: ni kweli kabisa.  Neno hilo lililotumika kukubali au kuthibitisha ukweli wa maneno au jambo lililokuwa limesemwa. Kwa hiyo mtu aliyesema Amina alitakiwa kusikia nini kilichosemwa na ndipo akubalie:    Amina.
Neno hilo limetumika katika Agano la Kale hasa katika Zaburi. Katika Agano Jipya Bwana Yesu alilitumia mara nyingi alipotaka kusisitiza siyo tu ukweli wa lile alilolisema bali pia uzito wake. Kwa namna hiyo Bwana Yesu alidhihirisha pia mamlaka yake katika lile alilosema.
Katika kitabu cha Ufunuo Yesu mwenyewe anaitwa Amina, kwani yeye ni mwaminifu kabisa katika maneno yake na kwamba yale anayosema kwa uhakika yatatimia. Tunasoma hivi: β€œHaya ndiyo anenayo yeye aliye Amina. Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli…” (Ufu 3:14). Yesu mwenyewe anajiita  β€œnjia, na  ukweli na  uzima”(Yn 14:6).

Katika Liturujia

Katika Liturujia yetu Amina ni kiitikio muhimu sana. Tunapoanza Sala zetu na kuhitimisha tunafanya Ishara ya Msalaba na kuitikiaAmina.Tunaposema Amina tunasisitiza umuhimu wa kuanza Sala au Liturujia tunayoadhimisha kwa jina la Utatu Mtakatifu. Kwa Sala hiyo msingi tunautukuza Utatu Mtakatifu na kuomba utuongoze katika Liturujia yetu tunayoadhimisha au Sala yetu tunayoitoa. Kwa kupiga Ishara ya Msalaba tunajiweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu tunapoanza Sala zetu au kuadhimisha Liturujia, na tunapomaliza tunapiga tena Ishara ya Msalaba na kusemaAmina. Katika Adhimisho la Liturujia kwa kawaida kuhani huhitimisha kwa Baraka ndipo waamini hujiandika Ishara ya Msalaba.
Hata hivi katika Adhimisho moja la Liturujia kuna Sala mbalimbali ambazo kuhani au atazitamka kwa sauti peke yake kama mwongoza Adhimisho ili waamini wasikie na hatimaye waitikie Amina lakini kuna Sala ambazo kuhani hutakiwa kusali pamoja na waamini na wote watazihitimisha kwa pamoja kwa kiitikio hichohicho Amina. Tufuatane kuangalia Aminakatika Adhimisho la Ekaristi, yaani Misa.

Mwanzo wa Misa  

Mwanzoni kuhani huanza: Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Kama tulivyosema hapo juu hii ni Sala ya msingi ambayo inatuweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu tunapoanza kuadhimisha Liturujia yetu. Kuhani akishasema vile Wakristo wote wanatakiwa kuitikia Amina. Wale wasioitikia wanafanya kosa kubwa la kutokukiri imani kwamba tunajiweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu. Wanatakiwa kujiuliza wamefika kanisani kufanya nini?
Kuhani huwasalimu waamini na kisha hutualika kukiri dhambi zetu. Hapo kuna namna mbalimbali za kukiri dhambi, lakini zote huishia na Sala anayotamka kuhani: Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Waamini wote hutakiwa kuitikia  Amina. Kwa nini wengine basi hawaitikii?
Hata hivi tukumbuke tendo hilo ni la kukiri dhambi na kuomba msamaha wa jumla katika kujiweka tayari kuadhimisha mafumbo matakatifu kama mwaliko wa kuhani unavyosema. Hiyo siyo nafasi ya Sakramenti ya Kitubio na Upatanisho. Mkristo mwenye dhambi kubwa lazima aende kuungama kwa kuhani yaani padri au Askofu.
Baada ya tendo la kukiri dhambi na kuomba msamaha hufuata Utenzi wa Utukufu ambao huimbwa au kusemwa siyo na kwaya peke yaobali na waamini wote pamoja na kuhani. Utenzi huishia na Amina. Waamini wote pamoja na kuhani hukiri kwamba walivyoimba au kusali ni ukweli kabisa.
Sehemu ya Mwanzo wa Misa huhitimishwa na Sala iitwayo Kolekta, kutokana na neno la kilatini lenye maana ya kukusanya. Kuhani akishasema: Tuombe, inampasa kunyamaa kitambo ili kila Mkristo na kuhani mwenyewe wasali kimya ndipo kuhani ahitimishe maombi yao kwa sala iliyomo katika kitabu cha Misa. Sala anayosali kuhani ni kama inakusanya na kuhitimisha maombi ya Wakristo wote wanaoshiriki Misa hiyo. Mwishoni mwa Kolekta hiyo wote hutakiwa kuitikia Amina. Asiyeitikia huwaza nini moyoni mwake?

Liturujia ya Neno

Wakati wa Liturujia ya Neno, kabla ya Injili, kuhani hujiandaa kwa Sala fupi  ili kutangaza Injili. Iwapo Misa huongozwa na Askofu, shemasi au padri iwapo shemasi hayuko huomba Baraka kwa Askofu. Anapopata Baraka hupiga ishara ya Msalaba na kutikia Amina.
Baada ya mahubiri, siku za Dominika na Sherehe hufuata Kanuni ya Imani ambayo, kama utenzi wa Utukufu kwa Mungu juu, huimbwa au husemwa na Wakristo wote, na mwishoni wote humaliza kwa Amina.
Tunapomaliza sehemu ya Liturujia ya Neno kuhani huwaalika waamini kusali: Salini ndugu, ili sadaka yangu na yenu ikubalike kwa Mungu Baba mwenyezi. Wakristo wakishasali hawasemiAmina kwa sababu kuhani huendelea mara na Sala iitwayo Sala juu ya Vipaji (oratio super oblata) ambayo ni ya kuombea dhabihu. Baada ya Sala hiyo ndipo Wakristo wote huitikia Amina.Tujibidishe kufanya vile.

Sala Kuu ya Ekaristi

Sala ya kuombea vipaji huhitimisha sehemu ya kuandaa vipaji. Hufuata Sala Kuu ya Ekaristi inayoanza na dayalojia: Bwana awe nanyi,… Inueni mioyo .. Mwishoni mwa Sala Kuu ya Ekaristi hufuata kiitikio cha Amina, ambayo huitwa Amina Kuu. Waamini wote hutakiwa kuitikia kwa nguvu Amina hiyo Kuu. Katika Sherehe  waamini wote siyo kwaya peke yao, waimbe Amina mara tatu. Wanamuziki wazingatie hilo wakitunga muziki.
Baada ya Amina kuu hufuata sehemu ya kujiandaa kwa Komunyo Takatifu, inayoanza na Sala ya Bwana: Baba yetu uliye mbinguni. Baada ya sala hiyo hatuitikii Amina kwa sababu kuhani huendelea`mara :Ee Bwana, tunakuomba utuopoe β€¦hatimaye wote huitikia: Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu…
Hufuata mara Sala ya kuomba Amani ambayo kuhani husali na mwishoni wote huitikia Amina. Wakati wa kupokea Ekaristi kila Mkristo hutakiwa kuitikia Amina kabla ya kupokea Mwili wa Bwana. Ni tendo la kukiri imani kwamba unasadiki huo ni Mwili wa Kristo. Wote huitikiaAmina mwishoni mwa Sala baada ya Komunyo.

Hatima

Mwishoni mwa Misa wakati kuhani anapowabariki waamini ndipo wote wakiinamisha vichwa vyao, hupiga Ishara ya Msalaba na kuitikia Amina ya mwisho.Wito kwa Wakristo wote: Tuitikie AMINA wakati wa Liturujia, bila kusita.Kwa kufanya vile tunashiriki na kusali  na kuhani tena tunakiri imani yetu kwamba alivyotamka kuhani ninakubali, ni kweli kabisa na Sala hiyo huwa Sala yetu pia.

MATATIZO YANAYORUDISHA UIMBAJI WA KWAYA KATOLIKI NYUMA

1.Kuwaimbia binadamu.Yaani tupo kwa ajili ya kuimba ili tusifiwe na watu.
2.Kuimba bila tafakari.Mara nyingi tunaimba tu bila kuzingatia ujumbe Wa ule wimbo
3.Kuimba bila kusali!Yasemekana Kuimba ni kusali Mara mbili.Waimbaji wengi hukariri wimbo na nyimbo nyingi zimetungwa kwa njia ya sala lakini wanakwaya wengi huimba tu wala hali ya sala haimo ndani yao!
4.Walimu wenye hasira na ubinafsi.Mkufunzi Wa kwaya ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya uimbaji.Iwapo choirmaster ni mwenye vurugu, mchochezi na mpenda fitina, bila shaka itakuwa vigumu kwa kwaya kupiga hatua kiuimbaji!
5.Sheria Kali zisizoenda na maadili ya kanisa.Kila jamii INA sheria zake na sheria ni nzuri.lakini tukiwa na sheria zinazowakandamiza wengine, tutapoteza kondoo wengi badala ya kuwaleta kwa Mungu!
6.Utoaji Wa albamu au kurekodi nyimbo kwa nia ya kutafuta pesa au kigezo kwa kwaya.Kwaya nyingi zimeanguka pindi tu wanapotoa albamu ya kwanza!Maana tunakosa kufahamu kuwa sisi ni wainjilisiti na tunawasaidia mapadri wetu kuhubiri injili.
7.Kutotii viongozi Wa kanisa.Wanakwaya wanaokosa kufahamu kuwa wapo chini ya viongozi na kanisa husika Mara nyingi hujipata wakiwa kwa makosa bila kunuia!
8.Kutoishi kwa hali ya sakramenti!Kama kuna jambo kubwa ambalo ibilisi hufurahia, ni yule MTU anayeishi katika maisha ya ndoa isiyo halali mbele za Mungu.Yaani Maana yake unaishi na mke au Mme bila ndoa ya kanisa na huna kizuizi chochote kinachokufanya usipate sakramenti hiyo.
9.Kitubio.Wengi tunapokea sakramenti ya ekaristi katika hali ya dhambi na hatushughuliki kabisaa kwenda kitubio.Hii inachochea zaidi kuwepo kwa dhambi za mazoea katika maisha yetu!
10.Kutosali kila siku.Inakuwa rahisi kwetu sisi kujaribiwa tukiwa hatusali.Kuimba kwako kunawasha hasira za shetani kwa hivo usiposali, bila shaka atarudi kulipiza kisasi.

Nifunge nini Kwaresma? Mambo ya kufunga kipindi cha Kwaresima

NIFUNGE NINI?
FungaΒ huzuniΒ upateΒ furaha,
FungaΒ ulabuΒ upateΒ siha,
FungaΒ majivunoΒ upataΒ utukufu,
FungaΒ uzinziΒ upateΒ wongofu,
FungaΒ kisiraniΒ upateΒ utakatifu,
FungaΒ umbeaΒ upateΒ fanaka,
FungaΒ wivuΒ upataΒ baraka,
FungaΒ unafikiΒ upateΒ uchaji,
FungaΒ kinyongoΒ upateΒ faraja,
FungaΒ kwaresimaΒ wakati ni huu
FungaΒ kiburiΒ ujazweΒ hekima,
FungaΒ jeuriΒ ujaweΒ rehema,
FungaΒ hofuΒ ujazweΒ imani,
FungaΒ kinywaniΒ ujazweΒ moyoni,
FungaΒ kisiraniΒ ujazweΒ rohoni,
FungaΒ dharauΒ ujazweΒ heshima,
FungaΒ majungu,Β ujazweΒ neema,
FungaΒ usiriΒ ujaweΒ wafuasi,
FungaΒ tamaaΒ ujazweΒ kiasi,
FungaΒ kwaresima wakati ni huu.

Maana kamili ya Kwaresma

Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu.
Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake.
Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu.
Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi pamoja na kufuata kielelezo cha Yesu kristo ambae alifunga siku arobaini (usiku na mchana) huzingatia maagizo ya YESU mwenyewe na nabii Isaya ambao kwa kiasi kikubwa hufafanua aina ya funga ambayo wakristo wanapaswa kuizingatia.
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo ya namna ya kufunga kupitia kwa nabii isaya akisema hivi
“Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu ; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao. Hutaka kwangu sheria za haki, humkaribia Mungu. Husema, mbona tumefunga lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je, kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je, ni siku ya mtu kujitabisha nafsi yake? je ni kuinamisha kichwa kama unyasi na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? je utasema ni siku ya kufunga na ya kukubaliwa na BWANA? Je, saumu niliyoichagua sio ya namna hii? Kufunguo vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaachia huru walio onewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia, utukufu wa BWANA (Mungu) utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na BWANA ataitika, utalia nae atasema mimi hapa…” (Isaya 58: 2-9).
Mwenyezi Mungu alitoa maagizo haya baada ya kuona watu wengi wakipoteza muda mwingi na kujitabisha kuacha kula na kujitesa miili yao ili kumpendeza Mungu, huku wakisahau mambo muhimu zaidi ambayo Mungu anawataka wafanye ili kumpendeza. (Katika kipindi hicho wayahudi walikuwa wakifunga kwa kujitesa sana ikiwa ni pamoja na kuacha kula, kuvua nguo zao za thamani na kuvaa magunia, kujipaka majivu na wengine kujipiga na kujikata miili yao ili waone maumivu zaidi.
Aidha, watu walikuwa wakitumia kipindi cha kufunga kuuonesha umma jinsi walivyo wacha Mungu na hivyo kupewa heshima mtaani. Mtu asiyefunga alionekana mjinga, mtenda dhambi na asiyefaa katika jamii. Kufunga ilikuwa sehemu ya maisha na si suala la uhusiano binafsi kati ya mtu na Mungu).

Kwa vile Mwenyezi Mungu wetu ni wa upendo na huruma, alimtuma nabii isaya kuwaambia watu hao kuachana na funga hiyo isiyo na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika mambo muhimu ambayo Mungu anaangalia katika kutathimini utu wa mtu. Mambo hayo ni upendo, huruma na kujitoa kama ilivyoelezwa hapo juu na kuachana uovu wa aina zote.. Kwa msingi huo, mtu mwenye upendo na anaejitoa kusaidia wengine ana thamani kubwa mbele za Mungu kuliko mtu anaeshinda njaa siku 300 za mwaka pasipo kuonesha upendo wa kweli kwa wengine.
Yesu kristo alipokuja ulimwenguni, alisisitiza maneno ya nabii Isaya kwa kutaka watu waache tabia ya funga za kujionesha kwa watu, na badala yake wajitahidi kumpendeza Mugu.
Yesu alisema “Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako (Mungu) aliye sirini; na baba yako aonae sirini atakujazi” (Mathayo 6:16)
Kumbe tabia ya kujionesha mbele za watu kwamba tumefunga inamuudhi Mungu na kutufanya tukose thawabu. Mtu anaejionesha au kujisifu kwamba anafunga huambulia kusifiwa na watu wa kidunia ambao wanadhani mtu huyo ni mtakatifu sana, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu huyo anajisumbua na kupoteza muda wake bure kwani hakuna thawabu anayo pata kwa Mwenyezi Mungu.
Tumuombe Mungu sana atuongoze na kutusaidia katika kipindi hiki cha Kwaresma na baada ya hapo.Ni wajibu wetu kujitahidi kuachana na maovu yote, kufanya toba ya kweli na kumpokea Yesu katika mioyo yetu badala ya kumuabudu kwa midomo tu. Tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu wetu ni yule yule kabla, wakati na baada ya kipindi cha Kwaresma na hivyo kipindi hiki kiwe kipindi cha kutukumbusha na kutuandaa kwa ajili ya wakati mrefu ujao baada ya Kwaresma.

Ijue Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa paji la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka ‘Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina’.
Kugusa paji la uso tuna maana kukubali kwa akili, kugusa kifua maana yake ni kupokea na kuupenda msalaba moyoni na kugusa Mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba Msalaba kwa nguvu zetu zote.
Tunafanya njia ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu Mmoja katika Nafsi tatu. Pia Msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu.
Ishara ya Msalaba Juu ya Paji la uso, mdomo na kifua kabla ya injili:
Hii ina maana kwamba Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu Kwa Akili yangu,
Nitalitangaza kishujaa kwa midomo yangu, na Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu Wote.

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu
Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.
Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13.

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema
Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.
Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About