Je, inawezekana kuwa ni hatari kutumia Valium au Klorokwini au dawa nyingine ambazo zinapatikana katika maduka ya dawa?

Ndiyo! Dawa yoyote i itakayotumiwa pasipo mahitaji sahihi au kwa kipimo zaidi ya kinachopendekezwa i inaweza kuwa hatari na pengine husababisa kifo. Mara zote sikiliza kwa makini maelekezo yatolewayo na madaktari au wauzaji wa dawa. Usichanganye dawa na pombe au dawa nyingine kwani kwa hakika kufanya hivyo ni hatari.

Madhara ya dawa za kulevya yanadumu kwa muda gani?

Ni vigumu sana kujibu swali hili kwa sababu muda wa madhara hutegemea sababu mbalimbali kama vile aina za dawa za kulevya, njia za utumiaji, hali ya mtu na mazingira anapozitumia dawa hizo za kulevya. Mtu anaweza kuanza kutumia dawa za kulevya mara kwa mara i ili kukidhi kile anachokihitaji. Kwa baadhi ya dawa za kulevya, na baadhi ya watu, matumizi ya mara kwa mara kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili ni kipimo tosha cha kumfanya aishi kwa kutegemea dawa za kulevya.

Dawa gani za kulevya ni hatari zaidi?

Kwa ujumla dawa zote za kulevya zinaweza kuwa ni za hatari. Kati ya dawa zilizohalalishwa kisheria nikotini, ambayo i ipo kwenye sigara, ndiyo hasa ya hatari. Inawezekana kuwa umeshakuwa tegemezi kwa sigara. Hii i ii ina maana ubongo wako utaizoea nikotini na utahitaji nikotini zaidi na zaidi i i ili kuendelea kuwa na hali nzuri. Nikotini pia ni hatari zaidi kwa sababu vijana mara nyingi huanza kutumia sigara kabla ya kuanza kutumia dawa kali zaidi.

Miongoni mwa dawa zisizoruhusiwa kisheria nchini Tanzania, heroini ndiyo labda yenye kusababisha utegemezi. Vilevile inahusishwa na makosa mengi ya jinai. Utumiaji wa heroini ni hatari hasa katika maambukizi ya UKIMWI. Watu wanaposhirikiana katika kutumia sindano za kujidungia heroini wanajiweka katika hatari na uwezekano mkubwa sana wa kuambukizana virusi vya UKIMWI. Hili hutokea pia pale watumiaji wa heroini wanapojiuza mii li yao katika ngono i ili wapate dawa za kulevya au fedha za kununulia dawa hizo.
Uvutaji bangi husaidia kuondoa aibu na vizuizi. Hii i ii inamaanisha kuwa wavuta bangi wanaweza wakasahau kufanya ngono salama na hivyo kuwa katika hatari zaidi ya kupata au kueneza UKIMWI. Matumizi mabaya ya dawa huweza kuwa hatari sana na pengine kusababisha kifo pale zitakapotumiwa kupita kipimo ama zitakapochanganywa na dawa nyngine au pombe.

Kwa nini kuna Watanzania wanaovuta bangi?

Sababu mojawapo ni kuwa bangi hulimwa hapa nchini na
hivyo hupatikana kwa urahisi. Bangi huuzwa kwa bei
nafuu kuliko dawa nyingine za kulevya. Vilevile, vijana
wengi huwaona wakubwa wao wakitumia na hii huwafanya waone kuvuta bangi ni kitu halali.

Sababu nyingine ni i i imani potofu kwamba ukivuta bangi unaweza kuwa jasiri wa kufanya kazi na kusoma sana. Lakini yote haya ni uzushi na si kweli kwani watu husahau madhara ya muda mrefu yasababishwayo na uvutaji bangi.
Sababu nyingine i inayowafanya Watanzania watumie bangi ni utegemezi wa kisaikolojia, kwani baada ya kuvuta bangi kwa muda, mtu huanza kujisikia hawezi i kuhimili msukumo wa kawaida wa maisha na kuishi bila bangi. Kwa maana hiyo muathirika huendelea na uvutaji bangi.

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika viungo vya
ndani ya mwili kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Watu wengi hufa katika ajali pale wanapokuwa wana kiasi kikubwa cha kilevi katika damu, kwani wanashindwa kutambua mazingira ya hatari.
Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza akafa ghafla kwa kile kinachoitwa kuzidisha dawa, pale mtu atakapotumia dawa za kulevya zaidi ya uwezo wa mwili. Kifo cha ghafla kinaweza kutokea au kutokana na matumizi ya kokaini na vifukishi kama petroli bila hata ya kuzidisha kiwango. Watumiaji wa vifukishi kama petroli mara nyingi hutumia mifuko ya plastiki i i ili kuongeza kiwango cha mvuke wanaovuta. Katika mazingira haya ni rahisi kupoteza fahamu kutokana na kukoseshwa hewa na mifuko hiyo. Kuchanganya baadhi ya dawa za kulevya kama vile heroini na dawa zingine hasa dawa za kutuliza maumivu (mfano valium) au pombe pia huweza kusababisha kifo.

Je, kuna madhara yoyote pale utakapojaribu kutumia dawa za kulevya mara moja tu au utakapotumia kwa kiasi kidogo sana?

Kutumia dawa za kulevya kwa kiasi kidogo kunaweza kusilete madhara i ila mpaka tu pale utakapoyazoea. Mara nyingi watu huanza kuhitaji dawa zaidi pale wanapozizoea na kupata madhara. Hii i ii inaweza kusababishia mtu kutawaliwa na dawa za kulevya. Mtumiaji wa dawa za kulevya anaweza kuwa mtegemezi wa dawa hizo bila ya kujijua. Kujaribu dawa za kulevya kunaweza kukawa na madhara kama β€œutaishia pabaya”. β€œKuishia pabaya” ni jambo la kutisha na si la kufurahisha hata kidogo! Hali hiyo inaweza kutokea mara ya kwanza unapoanza kutumia bangi.

Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali na huwezi ukasema kwa uhakika jinsi zitakavyokuathiri. Madhara ya dawa za kulevya yanategemea aina, kiwango na jinsi zitakavyotumika. Vilevile inategemea na umri, afya ya mwili na ukomavu wa akili, na pia mazoea ya matumizi ya dawa hizo.
Madhara ya muda hutokea mara tu baada ya dawa za kulevya kutumika, wakati madhara ya muda mrefu huonekana baada ya muda kupita, na mara nyingi husababisha uharibifu wa kudumu kwenye mapafu na ubongo.

Kwa mfano, bangi, husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, matatizo ya kumbukumbu ya muda mfupi, pamoja na umakini, kujifunza, kufikiri na kutatua matatizo. Pia inaweza ikasababisha kasoro kwenye utaratibu wa viungo vya mwili. Mara kwa mara wavuta bangi huwa na macho mekundu. Na vijana wengine hupata mihemuko mbalimbali kama uoga na hofu baada ya matumizi ya bangi.
Dawa za kulevya za vichangamsho, kama mirungi na kokaini, inasemekana kuwa huwafanya watumiaji kuwa macho, kujiona wana nguvu na kujiamini. Vichangamsho vikitumika kwa wingi, humfanya mtumaji kujihisi kuwa na wasiwasi au hofu. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya akili au hata kifo i iwapo yatatumika kwa kiwango cha juu.
Dawa za kulevya zinazokufanya upooze kama heroini au dawa nyingine zinazoagizwa na daktari, husababisha kujisikia umetulia, una amani na furaha. Ukizidisha vipimo husababisha usingizi, upungufu wa umakini na uwezo wa kuona, kizunguzungu, kutapika na kutokwa jasho. Vilevile kipimo kingi kinaweza kusababisha usingizi wa muda mrefu, kuzimia na hata kifo.

Pombe za kienyeji kama gongo ni hatari kwa afya na zinaweza kusababisha upofu na hata kifo.
Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa vijana kuhimili na kutatua matatizo yao ya kijamii na kiakili. Hii husababisha vijana kuwa wepesi kujihusisha na ujambazi na mambo ya ngono na ugomvi, mabadiliko hayo ya tabia husababisha ugomvi katika familia na kuvunjika kwa urafiki. Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo sababu kubwa ya ajali za barabarani, kujiua na maambukizo mbalimbali.

Tofauti ya VVU na UKIMWI

Neno VVU ni i virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kii ngereza ni HIV yaani β€œHuman Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa Kii ngereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni β€œAcquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, i ikii manisha kuwa mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi haya huitwa UKIMWI.

Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu anayeumwa UKIMWI i itakuwa tayari i i imepungua. Mwili wake utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.

Sababu za matumizi ya dawa za kulevya

Zipo sababu nyingi zinazowafanya watu kutumia dawa za kulevya, nazo ni kama zifuatazo:
Watu wengi hutumia dawa wakitumaini kusahau matatizo yanayowakabili, wengine hutumia kama viburudisho na wanataka kujionyesha kwamba ni watu wazima na wenye nguvu. Wengine pia huanza kutumia dawa kiutani na hatimaye hushindwa kujizuia kuzitumia. Wengine hutumia kutokana na msukumo wa rika au kutokana na kushawishiwa na watu wengine kwamba dawa za kulevya huwapa raha. Wengine hutumia kutokana na ukali wa maisha, uchovu pamoja na upweke. Kimsingi, dawa za kulevya hazimpatii mtu ufumbuzi wa matatizo, bali humwongezea matatizo mtumiaji.

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama β€œsukari ya kahawia”.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni i kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.

Je, kuna dawa zozote za kutibu magonjwa ya zinaa?

Magonjwa mengi ya zinaa yana dawa za kutibu, kwa mfano: kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi au utando mweupe. Lakini hata hivyo ni lazima upate matibabu mapema. Ukisubiri muda mrefu bila ya kutibiwa, inawezekana kwamba via vya uzazi vikapata madhara ya kudumu, kwa mfano, kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai.

Ni muhimu sana kwenda kupimwa mapema, wewe pamoja na mpenzi wako. Kwa sababu ukitibiwa peke yako, wakati mpenzi wako bado anaumwa, atakuambukiza tena mara tu ukijamiiana naye.
Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika na kupona kabisa

Inakuaje mwanaume anaonyesha dalili za magonjwa ya zinaa zaidi kuliko mwanamke?

Wanaume mara nyingi huambukizwa sehemu za mrija wa mkojo. Katika sehemu hizi ni rahisi kusikia mwasho au maumivu zaidi kuliko kwenye via vya uzazi vya ndani vya mwanamke. Hasa wakati wa kukojoa, chumvichumvi iliyo kwenye mkojo inagusa vidonda ndani ya mrija. Hivyo, ni rahisi zaidi kwa mwanaume kujua kuwa ameambukizwa.
Vilevile mwanaume akiambukizwa na magonjwa haya, sehemu ya mbele ya njia ya mkojo inashambuliwa na huanza kutoa usaha mzito. Lakini uke wa mwanamke hutoa kemikali ambazo hufanya wadudu kutoweza kushambulia kwa haraka, na dalili hazionekani kwa urahisi. Bahati mbaya, kemikali hizi hazizuii kuingia kwa ugonjwa, lakini dalili huchelewa kuonekana.
Usisahau kwamba kama mwanaume anajitambua kuwa na dalili za kuumwa magonjwa ya zinaa, mpenzi wake pia anatakiwa kwenda kliniki ili apate uchunguzi na tiba.

Magonjwa ya zinaa na dalili zake

Kuna magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana ni kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi, utando mweupe , Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Shida kubwa ya magonjwa mengi ya zinaa ni kwamba dalili zake hazionekani kwa urahisi na kama yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Maelezo kuhusu magonjwa ya zinaa yaliyoenea sana ni kama yafuatayo:

Kisonono:

Huchukua muda wa siku 1 hadi 14 tangu kuambukizwa mpaka kuonyesha dalili za kuumwa. Kwa wanawake dalili za kisonono ni maumivu chini ya tumbo ambayo yanaweza kuambatana na homa na kutokwa uchafu ukeni. Wapo wanawake wengine ambao hawaoni dalili zozote. Kwa wanaume dalili ni kutokwa na usaha uumeni na kupata maumivu wakati wa kukojoa. Athari yake kwa mwanamke ni kuziba mirija ya kupitisha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi, na vilevile ugumba. Kwa mtoto aliye tumboni mwa mama mjamzito kisonono cha mama yake kinaweza kusababisha upofu. Kwa mwanaume athari yake ni kuziba mirija ya kupitisha mkojo.

The ListPages module does not work recursively.

Kaswende:

Dalili ya kaswende kwa mwanamke ni vidonda sehemu za siri hasa kwenye mashavu ya uke na sehemu ya njia ya haja kubwa, pamoja na sundosundo sehemu ya siri. Kwa mwanaume dalili ni vidonda. Mara nyingi kimoja kwenye kichwa cha uume, kwenye kishina cha uume na kuzunguka njia ya haja kubwa. Pia mwanaume anaweza kupata sundosundo sehemu za siri. Ugonjwa huu husababisha matatizo ya moyo, na kuharibu ubongo na kuzaa watoto walemavu.

Klamdia:

Dalili yake kwa mwanamke mara nyingi siyo rahisi kuonekana. Kwa mwanaume dalili ni kupata maumivu wakati wa kukojoa, na kukojoa mara kwa mara. Athari kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Mimba hizi kuhatarisha maisha ya mama na kuleta ugumba vinaweza kutokea. Kwa mwanaume athari ni kuziba mirija ya kupitisha mbegu na utasa.

The ListPages module does not work recursively.

Kankroidi:

Dalili yake ni vidonda sehemu za siri vinavyokuwa na maumivu makali, maumivu wakati mkojo unapopita kwenye vidonda na kuvimba tezi sehemu za siri. Tezi huweza kupasuka na kutoa uchafu na maumivu makali.

Utando mweupe:

Dalili kwa mwanamke ni kutokwa na uchafu ukeni (kama maziwa yaliyoganda), kuwashwa na kuwa na michubuko sehemu za siri. Kwa mwanaume ni kuwashwa sehemu za siri na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Athari ni maumivu wakati wa kujamiiana.

The ListPages module does not work recursively.

Virusi vya UKIMWI:

Katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa hakuna dalili maalum. Hatua hii inaweza kuchukua mpaka miaka kumi. Lakini mara mtu anapoanza kuugua UKIMWI dalili zinakuwa nyingi. Pamoja na kupungua kinga ya mwili, kupungua uzito na kuumwa mara kwa mara. Matokeo ya kuugua UKIMWI baada ya muda fulani ni kifo.

Magonjwa ya zinaa yanavyoenea

Magonjwa ya zinaa husababishwa na vijidudu vya magonjwa na huambukizwa kwa kukutana kimwili na mtu mwenye vijidudu hivyo.
Katika Tanzania magonjwa haya yameenea sana haswa kwa vijana.. Hivyo kama una wasiwasi wewe au mpenzi uliyekutana naye kimwili kuwa na ugonjwa kama huo, muhimu mwende kupimwa. Magonjwa hayo yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Magonjwa ya zinaa mara nyingi yanasababisha ugumba.

Nifanyeje kujiepusha na vishawishi vya mpenzi wangu vinavyoweza kunifanya nisitumie kondomu?

Mara nyingine siyo rahisi kujiepusha na vishawishi vya kujamiiana bila kutumia kondomu kutokana na msukumo wa mpenzi wako. Lakini kumbuka kwamba siyo rahisi kumtambua mwenye magonjwa ya zinaa na mara nyingi huwezi kujua kama mpenzi wako hana ugonjwa wowote wa zinaa au hata virusi vya UKIMWI.
Huwezi kufahamu ni watu wangapi ameshajamiiana nao maishani mwake na mpenzi wako vilevile hawezi kufahamu kama wewe umeshajamiiana na mtu mwingine. Kila unapojamiiana kuna uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Kwa hiyo jadiliana na mpenzi wako na mkubaliane juu ya umuhimu wa kutumia kondomu wakati wa kujamiiana kwa nia ya kuwakinga wote wawili. Kama mpenzi wako anakuambia kwamba hana ugonjwa kama huo, mwambie kwamba hana uhakika wa kufahamu kutokuwa na virusi vya UKIMWI bila kupimwa damu. Na kama mmoja kati yenu hajapimwa, basi uwezekano wa kuwa na virusi upo. Usikubali kushawishiwa kutotumia kondomu, kwa sababu inaweza kuhatarisha maisha yako.
Matumizi ya kondomu inazuia ujauzito ambao wewe bado hauko tayari kuwa nao

Je, mwanamke anajisikiaje akijamiiana na mwanaume aliyevaa kondomu au aliye β€œpeku”?

Hatuwezi kusema mwanamke husikia raha gani akijamiiana na mwanaume aliyevaa kondomu au na mwanaume asiyevaa kondomu. Kila mtu ana upendeleo wake, lakini jambo la msingi katika kujamiiana ni hisia, hali ya kuelewana katika mapenzi na kiwango cha msisimko.
Wanawake wengine wanapendelea kujamiiana na mwanaume aliyevaa kondomu, kwa sababu hofu ya kupata mimba au kuambukizwa magonjwa ya zinaa haipo. Wanawake wengine wanapendelea kujamiiana bila kondomu. Lakini, pamoja na hatari ya kupata mimba, siku hizi kujamiiana bila kondomu kuna hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa na hasa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa hiyo ni vizuri zaidi kutomwamini mtu yeyote mpaka mpimwe kliniki wote wawili kuwa ni wazima wa afya na kuendelea kuwa waaminifu wote wawili.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About