Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200ยฐC ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari

Mapishi ya Mandazi ya nazi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2
Sukari (sugar) 1/2 kikombe
Hamira (yeast) 1/2 kijiko cha chai
Hiliki (cardamon powder) 1/4 kijiko cha chai
Tui la nazi (coconut milk) kiasi
Baking powder 1/4 kijiko cha chai
Siagi (butter)1 kijiko cha chakula
Mafuta ya kukaagia

Matayarisho

Changanya unga na vitu vyote kasoro tui la nazi na mafuta ya kukaangia. Ukisha changanyika vizuri tia tui la nazi na uanze kuukanda mpaka uwe mlaini. Baada ya hapo usukume na ukate mandazi katika shape uipendayo, Kisha uyawe katika sehemu yenye joto (warm place) ili yapate kuumuka.
Yakisha uumuka yakaange katika mafuta mpaka yaive kisha ipua na uyaache yapoe tayari kwa kuliwa. (Mafuta ya kukaangia yasiwe yamoto sana kwani yatayababua mandazi na hivyo ndani hayataiva vizuri.

Mapishi ya Half cake (Keki)

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2
Sukari (sugar) 1/4 kikombe
Barking powder 1/2 kijiko cha chai
Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

Matayarisho

Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Mkate

Mahitaji

Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2
Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai
Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai
Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula
Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi

Matayarisho

Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada ya hapo ukande tena na uache uumuke tena kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown Na hapo mkate wako utakuwa tayari

Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang’ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.

Mafuta katika mwili yanatengenezwa na โ€˜sebaceous glandsโ€™,kwa hiyo kuna baadhi ya watu wana sebaceous glands ambazo zinatengeneza mafuta kwa wingi sana na hivyo kufanya ngozi zao kungโ€™aa kwa sababu ya hayo mafuta mengi.

Sebaceous gland zipo kwa wingi usoni(face) shingoni(neck), kifuani, kichwani na mgongoni, ndiyo maana hayo maeneo yanakuwa na mafuta kwa wingi.

Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:

  1. Kurithi.
  2. Lishe.
  3. Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
  4. Ujauzito.
  5. Vidonge vya kuzuia mimba.
  6. Baadhi ya vipodozi.
  7. Hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta

Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-

Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.

Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.

Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.

Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.

Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.

Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.

Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1
Yai (egg) 1
Chumvi (salt)
Mafuta (cooking oil)

Matayarisho

Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Sambusa za nyama

Mahitaji

Nyama ya kusaga (minced beef 1/4 kilo)
Vitunguu maji vilivyokatwakatwa(diced onion 2 vikubwa )
Kitunguu swaum/ tangawizi (garlic and ginger paste 1 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt)
Pilipili iliyokatwakatwa (scotch bonnet 1)
Limao (lemon 1/2)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Cinnamon powder 1/4 kijiko cha chai
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Cumin powder 1/4 kijiko cha chai
Unga wa ngano (all purpose flour kidogo)
Manda za kufungia (spring roll pastry)
Giligilani (fresh coriander kiasi)
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho

Changanya nyama na limao, chumvi, pilipili,kitunguu swaum, tangawizi na spice zote, kisha pika katika moto wa kawaida mpaka nyama iive na maji yote yakauke. Baada ya hapo kabla hujaipua nyama tia vitunguu na giligilani na uvipike pamoja kwa muda wa dakika 2 na uipue weka pembeni na uache viipoe. Baada ya hapo tia unga kidogo katika bakuli nauchanganye na maji kidogo kupata uji mzito kwa ajili ya kugundishia manda. Baada ya hapo tia nyama katika manda na kisha zifunge kwa kugundishia na unga wa ngano.Ukisha maliza kuzifunga zote zikaange mpaka ziwe za brown na uzitoe. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Kachori

Mahitaji

Viazi mbatata (potato 4 vya wastani)
Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai)
Kitunguu (onion 1 cha wastani)
Carrot 1
Hoho (green pepper 1/2)
Kitunguu swaum (garlic)
Tangawizi (ginger )
Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai)
Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Limao (lemon 1/2)
Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai)
Giligilani (coriander kiasi)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Unga wa ngano kiasi

Matayarisho

Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni. Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.

Mapishi ya bagia na chatney ya machicha ya nazi

Mahitaji

Kunde (Ila mimi nilitumia Nigerian brown beans 1/2 kilo)
Vitunguu maji (onion 2)
Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
Vitunguu swaum (garlic 4 cloves)
Chumvi (salt)
Barking powder (1/2 kijiko cha chai)
Machicha ya nazi (grated coconut 1 kikombe cha chai)
Limao (lemon 1)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka kunde usiku mzima kisha ziondoe maganda na uzitie kwenye blender pamoja na vitunguu maji, vitunguu swaum, pilipili, chumvi,barking powder na maji kiasi. Visage vitu vyote mpaka viwe laini na kisha uutoe na kuweka kwenye chujio ili uchuje maji. baada ya hapo zikaange katika mafuta mpaka ziwe za brown na uzitoe na kuziweka kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta.Baada ya hapo saga machicha ya nazi,limao, pilipili chumvi pamoja na maji kidogo na hapo chatney yako itakuwa tayari kwa kuseviwa na bagia.

Mapishi ya Bagia dengu

Mahitaji

Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Mandazi Matamu

Mahitaji

Unga wa ngano (nusu kilo)
Sukari (Kikombe 1 cha chai)
Chumvi (nusu kijiko cha chai)
Hamira (kijiko kimoja cha chai)
Yai (1)
Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
Butter (kijiko 1 cha chakula)
Hiliki (kijiko1 cha chai)
Maji ya uvuguvugu ya kukandia
Mafuta ya kuchomea

Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya Kujaza nywele kwa njia za Asili

Zingatia mambo haya yafuatayo;

  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
  2. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
  3. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
  4. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
  5. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako

Mapishi ya Viazi vitamu na kachumbari

Mahitaji

Viazi utamu 3
Nyanya 2 kubwa
Kitunguu
Tango
Limao
Chumvi
Pilipili
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Eggchop

Mahitaji

Mayai yaliochemshwa 4
Nyama ya kusaga robo kilo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Limao
Chumvi
Pilipili
Breadcrambs
Carry powder
Binzari nyembamba ya unga
Yai moja bichi
Mafuta

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano 1ย 1/2 Kikombe

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Baking soda ยผ Kijiko cha chai

Chumvi ยฝ kijiko cha chai

Sukari 1 kijiko cha supu

Hamira 1/2 Kijiko cha supu

Yai 1

Maziwa ยฝ Kikombe

Mafuta ya kukaangia

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari 1 Kikombe

Maji ยฝ Kikombe

Iliki au Mdalasini ยผ kijiko cha chai (ya unga)

MAANDALIZI NA JINSI YA KUPIKA

1. Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari na hamira.

2. Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3. Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga ; na ukande kama unga wa maandazi.

4. Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai .

5. Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote mbili.

6. Ipikie shira lakini isiwe nzito .

7. Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote na zitakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta

MAHITAJI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Baking powder – 1 ยฝ Vijiko vya chai

Sukari – 1 Kikombe cha chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Mayai – 2

Maji – kiasi ya kuchanganyia

Tende – 1 Kikombe

ufuta – ยผkikombe

MAPISHI

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
  2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
  3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
  4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
  5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
  6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350ยฐF kwa muda wa nusu saa takriban.
  7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Jinsi ya kutengeneza Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIAMBAUPISHI

Unga – 4 Vikombe vya chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari – 2 Vikombe vya chai

Maji – 1 Kikombe cha chai

Vanilla ยฝ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

JINSI YA KUTENGENEZA

Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.
Changanya vizuri isiwe na madonge.
Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.
Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.
Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .
Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili
Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.
Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai.
Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Uvaaji wa Tai na Maana yake

Wachambuzi wa mambo ya saikolojia wanasema kwamba kwa kuchukua tai na kulivaa ile rangi ndiyo itakayoweza kupeleka ujumbe wa wewe unataka nini au unataka watu wakutambue kwa namna gani.
Wakati Joshua Blue, Makamu mkuu wa shule ya Kennedy mjini Hong Kong, anapoendesha baraza la wanafunzi anavaa tai lenye rangi ya light violet ili kumpa mamlaka.

Tai la rangi ya bluish-purple anasema ni โ€œcolourful yet mutedโ€, anaamini kwamba rangi ya bluu inawafanya wanafunzi wasiboreke wakatiw anasikiliza, anajizuia kutumia brighter purples na pinks wakati akiwa mbele ya wanafunzi.

โ€œHuhitaji kuwa na rangi nyingi zinazongโ€™aa kwani watoto watajivuruga,โ€ anasema Blue mwenye umri wa miaka 35.

Hakika inaweza kuwa kama kichekesho lakini wataalamu wanasema kwamba uchaguzi wa rangi ya tai inasaidia sana kupeleka ujumbe unaotakiwa kwa wahusika. Na hii haijalishi ni mteja, mdau wafanyakazi au watoto.

โ€œRangi hutoa aina Fulani ya ishara,โ€ anasema David Zyla, Mwandishi mwenye makao makuu yake New York anayeandika Color Your Style.

โ€œSuti ile ile inaweza kubadilishwa kimtindo yaani salamu zake kwa kubadili rangi ya tai, na kila mvao ukawa na ishara na salamu tofauti.โ€

Baada ya kusoma maelezo yote hayo, nikuulize je sasa unaweza kufikiria unataka kuvaa tai gani katika mkutano wako ujao.Labda nikusaidie kwa namna hii.:

Rangi nyekundu

Ni rangi Inayotawala

Si bahati mbaya au kitendo cha kubahatisha kwa wanasiasa wengi kuvaa tai lenye rangi nyekundi ndani ya suti zilizo dark na mashati mepesi.

โ€œTai nyekundu inaonesha mamlaka,โ€ anasema Mark Woodman, mchambuzi wa mambo ambaye amejifunza masuala ya huko Laurel, Maryland, Marekani. โ€œKuna kitu Fulani kipo ndani ya rangi nyekundu ambacho mara zote kinajitokeza kumuimarisha mtu na kumpa mvuto wa pekee.โ€

Ofisa Mtendaji wa JPMorgan, Jamie Dimon huvaa tai nyekundu anapozungumza na wananchi
Hata hivyo wataalamu wanasema kwamba kuna rangi nyekundu na rangi nyekundu.Nyekundu iliyokoza kwa miondoko ambayo wazungu wanasema ni burgundy, husaidia kuleta imani na matumaini wakati ile nyekundu nyepesi na pink inakuwa zaidi onesho la ubunifu na namna ulivyo kistaili.Katika miaka michache iliyopita rangi ya pink inaweza kuonesha mshikamano na wamama anasema Woodman.

Wakati unaendesha mradi au unataka kupeleka ujumbe Fulani kwa kruu yako fikiria kuvaa tai la rangi nyekundu iliyokoza ambayo inashaini.Tai la rangi nyekundi unaweza kuwa njia bora ya kuonesha mamlaka.

Royal purples

Ross Znavor, Mtendaji katika moja ya taasisi za kifedha mjini New York yeye huvaa tai la rangi ya purple na si nyekundu katika mikutano ya kibiashara,Rangi hii huonesha kujiamini na humsaidia watu kuendelea kumkumbuka.

Anasema kuvaa tai hilo kunampatia mtu mwingine kukubali kwamba wewe unaweza kushirikiana naye na kujenga uhusiano wa kudumu.

Lindsay anasema purple, kiasili ni rangi ya utiifu na utajiri na kwa sasa inaaanza kukubalika maeneo ya kazi.

Arnold Schwarzenegger huonesha kujiamini kwa kuvaa tai rangi ya purple.

โ€œWanaume wanaovaa mashati ya lighter purple na tai za darker purple, hutaka kutambulika haraka katika kundi bila kuleta ushawishi mwingine wa kipuuzi unaovurugaโ€.

Rangi nyeusi

Inawezekana huvai kila siku au kila mahali lakini ukivaa tai nyeusi katika mikutano ya watendaji, kwenye dhifa unakupa wewe hali ya muondoko mweroro wenye utanashati mkubwa , anasema Zyla.

Muigizaji sinema Leonardo DiCaprio huvaa tai nyeusi katika mikutano au maeneo ambayo ni ya kikazi zaidi.

Lakini ni kweli kuwa rangi nyeusi inakufanya kuwa na ujeuri wa aina Fulani na wengine wanasema kusema kwamba inakuwa overdressed katika mazingira mengi. โ€œRangi hii inafaa kutotumika kama wewe unataka kuendelea kupanda ngazi, wapandisha ngazi wanaweza kufikiria kwamba wewe ni jeuri wa aina Fulani hivi,โ€ anasema Zyla.

Ni vyema sana kama mtu atakuwa amejipatia grey shades, anaongeza Woodman. Tai la rangi ya grey linaweza kukupa mwonekano wenye mvuto mweroro usio na jeuri na usiojinata anasema Woodman.
โ€œGrey iko poa, iliyotulia na ya kisasa zaidi,โ€ anasema.Ili kuifanya iwe imetulia zaidi piga tai hili na shati ambalo ni lighter, pastel-coluored. Tafadhali angalia lighter grey shades na malizia na shaini ili kukupa muonekano ambao ni polished.

Rangi ya kijani

Rangi ya kijani ina maana nyingi kuanzia kuzaliwa upya hadi rangi ya fedha kwa mataifa Fulani.Lakini cha ajabu ni rangi yenye โ€˜keleleโ€™ nyingi katika maeneo ya kazi.
Wakati mwingine kijani inakuwa too much.

โ€œJe unataka kukumbukwa akwa ajili ya tai au kama wewe binafsi?,โ€ anauliza Woodman .Anasema kuchagua rangi ya kijani inayostahili ni kazi kubwa.Kijani inayowaka inavuruga kutokana na mwako wake na pia inakuwa na taabu sana kupata suti inayoambatana nayo au hata shati. Hata hivyo tai la light green likiwa na subtle print linaweza kuwa jema katika shati ambalo rangi yake ni neutral.
Tai ya rangi ya njano, ni tai la kiasili kwa nchi nyingi hata waingereza wanaliheshimu kwa sababu linakupa uhakika, kukuweka mngโ€™avu na mwenye siha hasa ya kufaa.

Ni rangi inayoonesha jua, hivyo watu wengi wanaweza kuwa na kishawishi cha kuzungumza nawe kwa sababu ya ukweli kuwa ni rangi yenye mvuto wa kipekee. Kwa wengi kuvaa tai la rangi ya njano kunaonesha kwamba maisha yeye anayaangalia katika dunia chanya zaidi, anasema Eve Roth Lindsay, mshauri wa masuala ya muonekano wa Hong Kong.

Lakini kiukweli kuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukafanya kosa la uasili na utamaduni wa eneo lenu inapokuja suala la rangi.

Mathalani rangi ya njano nchini india ina maananisha kwamba wewe ni mfanyabiashara wakati rangi nyeupe nchini China inamaana upo katika kipindi cha maombolezo.

Rangi ya bluu

Unahofu ya kupeleka ujumbe ambao uhuhitaji kwa kutumia tai uliyovaa yaani rangi yake?basi ni vyema ukafikiria kutumia tai ya rangi ya bluu.

Rangi hii hutumika katika matukio yote.
Rangi ya bluu ni rangi bomba kwa kuwa inawakumbusha watu anga na bahari, vitu vyenye kutuliza maisha ya binadamu anasema Lindsay.

โ€œRangi ya bluu hakika ni salama zaidi kuivaa,โ€ anasema.

Bluu inaonekana dhahiri ni rangi ya nguvu ya kimataifa

Tai ya Patterned blue hutoa hali ya kutulia na kitaalamu zaidi na inaweza kutumiwa katika mikutano ya kimataifa ya kibiashara na mazingira bila kupeleka ujumbe usiotakiwa.

Tai ya subtle blue inaweza kuwa na mvuto na kujionesha undani wakati cobalt au royal blue hukufanya ujiachie ndani ya kundi kwa namna Fulani. โ€œBluu iliyokoza ni rangi ya marubani watukuka. Bluu bahari ni rangi inayoaminika, inayokupa imani na kiburi cha uwezo,โ€ anasema Lindsay .

Kuwa rafiki na asili

โ€œKabati lako likiwa na rangi rafiki za asili kama tan, kahawia, earthy colours, salmon na njano hufaa sana kwa watu wanaojishughulisha na wengine kama wafanyabiashara (mauzo), walimu na watu wa huduma mbalimbali,โ€ anasema Lindsay.

Hakikisha kwamba tai la rangi ya kahawia haiku pekee kwani inaweza kuonesha ugoigoi katika wajihi. Hata hivyo tai la beige linaweza kukuonesha kwamba huna matatizo, yuko huru.
Epuka kuvaa tai la rangi ya udongo na shati linalofanana nalo. Na kama unataka kujishebedua na kuonekana kweli katika eneo la kazi rangi hizi za asili achana nazo kabisa.

Mapishi ya visheti vitamu

VIAMBAUPISHI

Unga – Vikombe 2

Samli au shortening ya mboga – 2 Vijiko vya supu

Maziwa ยพ Kikombe

Iliki – Kiasi

Mafuta ya kukarangia Kiasi

VIAMBAUPISHI :SHIRA

Sukari – 1 Kikombe

Maji ยพ Kikombe

Vanila ยฝ Kijiko cha chai

Zafarani (ukipenda) – Kiasi

JINSI YA KUPIKA

Katika kisufuria pasha moto maziwa na wakati huo huo chemsha Samli katika kisufuria kengine.
Tia unga katika bakuli na iliki, kisha mimina samli iliyochemka na huku unachanganya.
Tia maziwa na uwendele kuchanganya vizuri isiwe na madonge, ikiwa maziwa haitoshi ongeza maji kidogo.
Kisha uwache unga ukae mahali pa joto kwa muda wa dakika 10 hivi.
Halafu fanya viduara vidogo vidogo, kisha finyiza kwenye greta yenye vishimo vidogo ili upate umbo lake.
Kisha karanga kwenye mafuta yaliyopata moto hadi vibadilike rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta.
Chemsha shira, ikiwa tayari mimina visheti na upepete na kuzichanganya zipate shira kote.
Weka kwenye sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa na kahawa.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About