Ujumbe wa kumwambia umpendaye kuwa ni pengo lisilozibika milele kwa hiyo asikuache
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
nikipoteza kitu cha thamani nitauzunika nitasahau ila
nikikupoteza wewe ni pengo lisilozibika kamwe.
upendo wa moyoni ndiyo dhati niliyoamini amini kwa haya
nisemayo nakupenda wewe ndiyo kaburi nitakalozikwa nalo
mapenzi ni safari,mapenzi ni ahadi,mapenzi ni
ujasiri,mapenzi ni zawadi,mapenzi mitihani,mapenzi
ramani,mapenzi ajali na ndiyo maana nakupenda wewe bila kujali.
Kipepeo kipeperushe kunipenda maamuz yako kamwe usijute
nakupenda mpz moyoni mwako unitulize.
Nakupenda mpz
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Wanasema mtu huanguka katika mapenzi mara moja, jambo
ambalo mimi naliona si la kweli kwa maana kila
ninapokutazama najikuta nakupenda tena na tena.
Tone la mvua huonekana dogo sana, lakini kwa mwenye kiu hulisubiri kwa hamu kubwa. Sms ni kitu kidogo, lakini huonyesha mahali fulani yupo mtu ANAYEKUPENDA, ANAKUKUMBUKA, ANAKUOMBEA,
ANAKUJALI na,
ANAKUTAKIA mafanikio mema
Kama ungekuwa kidonda kwenye moyo wangu, ningekiacha na maumivu yake ndani yangu.
Recent Comments