Ujumbe wa salamu kwa mpenzi kumjulia hali
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Unaweza usione kamwe ni kwa kiasi gani ninavyokujali.
Unaweza usisikie ni kwa kiasi gani nilivyokushiba, unaweza
usihisi namna gani ninavyokukumbuka. Sababu ni moyo wangu
tu uliyoyaficha hayo.
Dear siku zimekaribia, miaka …… utatimiza katika hii dunia,
hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia,
hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi,
zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi.
Happy Birthday mpenzi.
Kila unachokifanya natamani niwepo, nikitumainia kila
ndoto yako itimie kila muda na sehemu, niwepo nikikutakia
mafanikio mema kwasababu nakujali.
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda,
macho nayaangaza,
taratibu navuta shuka na kujitanda,
mishumaa pembezoni inaniangaza,
mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa
ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Katika nyuso za dunia, na kati ya miamba ya jangwani,
Kuna SAUTI! Neno la pendo lako liotapo karibu yangu.
Ni zaidi ya roho iendayo safarini.
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Moyo wng mtiifu,2li ume2a kwako,kwang huna upungufu yote nimekupa hekoo,utunze na ulee pia uujali kama mama yako alivyofanya kwako.
Sio Maua yote Huonesha Upendo, “Ni Waridi pekee” sio Miti yote Hustawi Jangwani “ni Mtende pekee” sio watu wote wanaokukumbuka muda huu ni mm pekee. Uhali gani?
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments