Meseji ya kumkaribisha mpenzi wako
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka.
Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika.
Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka.
Kitale katikati yake ukila utaridhika.
Matamu na maji yake hukata kiu haraka.
Weupe watui lake lina ladha ukipika.
Kupaka mafuta yake mwili hulainika.
Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika.
Hata na upepo wake uvumapo utacheka.
Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani
nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi
kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali
hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
Kumbuka kuwa wewe ni wangu
Kitulizo cha moyo wangu
Kwenye shida na raha
Wewe ni sehemu ya maisha yangu milele
Nakupenda sana P tafadhari usinikasirikie, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu, njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.
Wewe pekee upo moyoni mwangu, nitaendelea kukupenda siku
zote za maisha yangu! Katika siku hii ya wapendanao, wewe
ndiyo ua la moyo wangu!
Chuki huharibu akili; mapenzi huitibu. Umeitibu akili
yangu.
Recent Comments