Ujumbe wa kimahaba kwa umpendaye sana
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Kama ningeweza kubadili herufi, ningeweka yangu na yako
kuwa pamoja
Nakupenda mpenzi wangu, sifikirii kitu chochote zaidi yako
na kwa kuwa nakupenda sipendi kuwa na urafiki hata na
mwingine kwani atakuwa anabana nafasi niliyokuwekea wewe.
Noamba unipende nami nakupenda kila sikunde inayopita
maishani mwangu. Mwaaaaaaaaa
Mpenzi wangu kukutana nawe ilikuwa ni bahati, kukuchagua kuwa rafiki yangu ilikuwa ni maamuzi yangu, lakini kuanguka kwenye penzi lako haikuwa hiyari yangu. Umeniteka moyo na akili yangu pia.
Penzi lako ndiyo pumzi yangu nawezaje kukuacha laazizi,
ina maana nife??? Siwezi kukuacha nakupenda. Nitakupenda
mpaka mwisho wa uhai wangu.
Penzi langu kwako ni la milele, nitakuhifadhi moyoni
mwangu siku zote za maisha yangu, uwe wangu nami niwe wako
daima, nakupenda dear…
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda, macho nayaangaza, taratibu navuta shuka na kujitanda, mishumaa pembezoni inaniangaza, mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Ingawa mwaka umekwisha, mawazo yangu katu sitobadilisha, amini ni wewe pekee unayenipagawisha, hakika kwa penzi lako kiu yangu katu haitakwisha!
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! “NAKUPENDA MALAIKA WANGU”
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako,
naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments