Meseji ya kumkumbusha mpenzi wako kuwa unampenda
Mapenzi ni magumu na yatabaki kuwa hivyo, lakini kumbuka
kuna akupendaye naye ni MIMI!.
Mapenzi ni magumu na yatabaki kuwa hivyo, lakini kumbuka
kuna akupendaye naye ni MIMI!.
Licha ya upole ulionao! Pia upendo wako ndio kishawishi cha kunifanya nikukumbuke siku zote. Jiulize! nina namba za watu wangapi ktk cmu yangu,na bado sijatamani kujua hali zao ila wewe! kwa kuwa, nakuthamini nakukujali, ndiyo maana nakutakia, SIKU NJEMA
Si vibaya mimi kukusifia kwani wewe ni wangu, nivingi umejaaliwa, vinavyouvutia moyo wangu, ama hakika uzuri wako umedhibiti matamanio yangu “SINTOMPENDA MWINGINE ZAIDI YAKO”
Mpenzi wangu T tambua kuwa ulimwengu tunaoishi una mambo
muhimu matatu. Jambo la kwanza ni kumpata umpendaye, la
pili ni kupata atakayekupenda la tatu ambalo ni kubwa
kuliko yote ni kwa jambo la kwanza na la pili kuungana
pamoja.Nashukuru nimekupata wewe nikupendaye, naomba unipende na uungane name
Mawingu yametanda napanda kwenye kitanda,
macho nayaangaza,
taratibu navuta shuka na kujitanda,
mishumaa pembezoni inaniangaza,
mziki laini wanibembeleza kitu pekee nilichokikosa
ni joto lako na vijimambo vyako kunako kitanda!
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
kiangazi aumasika
kukupenda nitawajibika kwenye chupa au birika chai yako
ya uhakika ,iwe ndoo au pipa ujazo wa penzi kimiminika.
Tambua kuwa nakujali
Furahia kwamba nitakuwa na wewe
Katika siku zote za maisha yangu
Nitakupenda bila kikomo milele
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Recent Comments