Ekaristi Takatifu

Mambo ya Msingi unayopaswa kufahamu kuhusu Ekaristi

Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ipi? Sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai. Sisi ambao tulishiriki kifumbo kifo na ufufuko wake tukapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, tunaalikwa kukaribia mara kwa mara…