SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜‚

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi ya Kufuga vizuri kware Kwa Faida

Kware au Kwale au Kereng’ende ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana.

Ndege hawa ni wadogo 280gm – 300gm, rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano.

Chakula

1. Kware anakula chakula chochote anachoweza kula kuku ikiwemo chakula cha broiler. Kama utaamua kuwapa chakula cha broiler unawapa โ€œstarterโ€ kware wenye umri kuanzia siku moja hadi wiki ya tatu baada ya hapo unawapa Falcon au hill.

2. Ukiweza kuwatengenezea chakula chako mwenye kutumia pumba nk. Ni vizuri zaidi kwa mayai yenye lishe 100%

3. Kware 100 wenye umri wa mwezi hutumia kiroba cha kilo 20 kwa wiki 3.

4. Kware hawamalizi chakula kama kuku.

5. Pia kware hupewa majani kama mchicha nk.

Kutaga na kuatamia kwa Kware

Kware dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).

Mayai ya Kware huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.

Njia bora ya kutotolesha mayai ya Kware ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.

Utunzaji wa vifaranga vya kware na chakula

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 1 โ€“ 7

Vifaranga wapatiwe chakula โ€œSTARTER PELLETโ€ na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee โ€˜GLUCOSEโ€™ kwenye maji, Packet moja kwa lita 20 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wawekee Amin Total kwenye maji, Wape maji pekee siku ya sita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle. Utawapatia joto kwa njia ya umeme kwa โ€˜BULBโ€™ mbili (2) za 200watts kwa kila vifaranga 300, ama unaweza kuweka taa ya โ€˜Energy Serverโ€™ pamoja na jiko la mkaa uliofunikwa na majivu ambao utakidhi kuwapatia joto sawia kwa masaa 24 kwa siku 7. (Majivu yanasaidia moto kukaa kwa muda mrefu)

Banda/box lako liwe la ukubwa wa 1.5m x 1.5m (au eneo la ukubwa huo ndani mwa banda kubwa la kufugia kuku) lazima uzingatie usalama wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka magazeti au mabox chini kwenye sakafu yatakayosaidia usafi. Kwa week ya kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri utumie chakula cha pellet ili kusaidia vifaranga wasiteleze na kuathiri miguu. NOTE: Weka gololi au mawe kwenye drinkers zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 8-14

Vifaranga wataendelea kupewa chakula โ€œSTARTER PELLETโ€ na maji safi. Wataendelea kuhitaji โ€˜mwangaโ€™ wa kutosha muda wote na joto la wastani bulb 2 za watts 100 au moja ya watts 200

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 15-21

Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakayowawezesha kula mchana na usiku.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 21 na Kuendelea

Kware wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua.

UTAGAJI WA KWARE

WIKI YA SITA

Wiki ya sita kuelekea ya saba Kware wako wataanza kutaga mayai kila siku, kwa wastani Kware mmoja hutaga mayai 300 kwa mwaka.

Magonjwa ya Kware

Kware ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata Kware ni typhoid, mafua na kuharisha .

Tiba za asili za kware

Waweza kuwatibu vifaranga au Kware wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama.

Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa Kware na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.

Mwarobaini na Aloe Vera:

Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya Kware. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).

Kitunguu swaumu:

Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya kware wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.

Maziwa:

Maziwa yanayotokana na ngโ€™ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu Kware waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo Kware anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ngโ€™ombe wanaotibiwa kila mara.

Angalizo

Siyo lazima Kware waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.

Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu Kware kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia; Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis), Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid).

ZINGATIA:

Wanapokosa madini ya kutosha kwenye chakula huweza kupata madhara yafuatayo:-
1. Kuharisha
2. Kunyonyoka manyoya
3. Kupunguza kasi ya kutaga mayai.

Chanjo Ya kware

Siku ya 7 lazima vifaranga wapatiwe chanjo ya โ€œkideri/mdondoโ€
(respiratory & digestive diseases) kwa dawa inayoitwa โ€˜newcastleโ€™. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 14 lazima wapewe chanjo ya โ€œgumboroโ€. Chanzo cha
maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya โ€œNewcastle (aina ya IBDL)โ€. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 35 lazima wapate chanjo ya โ€œNduiโ€.

Soko la kware

Mayai ya Kware ni bidhaa adimu sana hapa nchini kwa kuwa ni wafugaji wachache waliojikita katika ufugaji huu, Ufuatao ni muhtasari wa wastani wa bei ya bidhaa za Kware sokoni

1. Trei ya (mayai 30) ya KWALE inauzwa shilingi 30,000 .
2. Kifaranga wa Kware wa siku moja anauzwa shilingi 2500 โ€“ 3000
3. Kware wa week 4 (mwezi mmoja) anauzwa kwa shilingi 10,000โ€“ 12,000
4. Kware aliyeanza kutotoa (week 6) huuzwa shillingi 20,000 โ€“ 25,000
5. Kware kwa aliyekomaa kwa ajili ya kitoweo huuzwa kwa shilingi 25,000
6. DROPING za Kware huuzwa kwa shilingi 10,000 kwa 50kg kwa wafugaji wa samaki

Soko la KWALE liko juu sana kwa mayai na nyama. KWALE pia hutofautiana bei kwa jike na dume.

FAIDA ZA KUFUGA KWALE

Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine

ยท Chanzo cha kipato kwa wafugaji.
ยท Hawana gharama sana katika suala kufuga.
ยท Hawataji utaalam sana katika kuwafuga.
ยท Mayai yake ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
ยท Mayai yake hayakosi soko.

Tatizo la kutoka majimaji kwenye matiti

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba. Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu.

Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa. Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji katika matiti pia huweza kuwatokea wanaume watu wazima, vijana walio katika umri wa balehe, wa kike na wa kiume, watoto wachanga wa kike na wa kiume.

Chanzo cha tatizo

Matiti yanaweza kutoa majimaji endapo chuchu zitachezewa au kunyonywa mara kwa mara na kusababisha kuvuruga baadhi ya homoni mwilini.

Homoni zinazohusika zaidi na tatizo hili ni homoni ya โ€˜prolactineโ€™.
Vilevile katika hali hii ya kutokwa na majimaji asilimia 50 ya matatizo chanzo chake bado hakijulikani.

Mama anayenyonyesha homoni zinazochangizwa na kusababisha matiti yatoe maziwa ni โ€˜Prolactinโ€™, Estrogenโ€™ na Progesterone.

Dawa nyingine zinazoweza kumfanya mtu atokwe na majimaji katika matiti ni dawa kama Methyldopa, madawa ya kulevya na dawa za magonjwa ya akili.

Pamoja na matatizo katika mfumo wa homoni, hali ya kusuguasugua kifua mara kwa mara, hali ya kuwa na hofu na wasiwasi au shauku fโ€™lani, mfano ya kuhitaji kupata ujauzito husababisha kuamsha homoni za uzalishaji wa maziwa au hayo majimaji.

Vyanzo vingine ni matatizo kichwani kwenye tezi ya โ€˜pituitary au pituitary adenomaโ€™.
Dawa nyingine zinazoamsha tatizo hili ni kama vile โ€˜Cimetidineโ€™ ambazo hutibu vidonda vya tumbo.
Pia zipo dawa nyingine za asili ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha zinazoweza kusababisha tatizo hili.

Dalili za tatizo

Mwanamke mwenye tatizo hili la kutokwa na maziwa kwenye matiti wakati si mjamzito na wala hana historia ya kuwa na mimba, huwa hapati ujauzito.
Mwanaume mwenye tatizo hili hupungukiwa na nguvu za kiume, uzalishaji wa mbegu za kiume huwa mdogo.

Kwa ujumla tatizo hili husababisha ugumba.

Kwa vijana na watoto wa kiume au wa kike ni vema uchunguzi wa kina ufanyike.
Maziwa yanaweza kutoka tu yenyewe au kwa kuminyaminya matiti au chuchu.

Uchunguzi

Hufanyika hospitalini kwa madaktari wa masuala ya uzazi. Vipimo vya damu kuangalia homoni, matatizo katika matiti, na ikibidi CT-Scan vitafanyika kuangalia matatizo katika tezi ya Pituitary.

Ushauri

Wahi hospitali kwani athari ya tatizo hili ni kupoteza uwezo wa kuzaa.
Epuka kuchezea chuchu ziwe zako mwenyewe au za mpenzi wako au za mtoto kwani unaamsha homoni ambazo katika wakati huo hazitakiwi.

Namna ya kuvaa vizuri kwa mwanamme upendeze na kuwa mtanashati

Nimeona leo nitoe darasa kidogo kuhusu mavazi sababu na mimi ni kipaumbele changu katika maisha.

1.Epuka kuvaa marangirangi

Wakati unamatch mavazi jitahidi kupunguza idadi ya rangi, rangi 3 tu zinatosha kukutoa bomba.

2. Vaa kulingana na mazingira/sehemu

Mtu mjanja anajua kubadilika kulingana na mazingira, sio kuvaa jezi la Man utd lenye jina la Wazza kwenye sherehe

3. Masharti ya kuchomekea

-Marufuku kuvaa oversize/undersize
-Usivae mlegezo
-Hakikisha singlet haionekani
-Usivae mkanda mrefu
-Usivae makubanzi/sandals

4. Kama umevaa pensi /kaptula.

-Hakikisha unavaa soksi fupi zisizoonekana
-Piga raba au makubanzi/sandals bila soksi
-Haipendezi kuchemekea

5. Usivae shati jeupe kama la mwanafunzi

Shati nyeupe ni nzuri kama unaijulia wakati unanunua hakikisha ina urembo wa aina yoyote ile au ni ya kimtindo sio kuvaa shati la shule

6. Hakikisha una suruali nyeusi

Mwanaume yoyote yule wa kijanja anajua umuhimu wa suruali nyeusi sababu inamatch mashati ya rangi nyingi.

7. Saa

-Kama umevaa jeans/kadet unaruhusiwa kuvaa saa ya aina yoyote
-Kama umevaa suti/suruali ya kitambaa epuka kuvaa saa ya mkanda wa plastic.

8. Miwani

Duh hapa pagumu kidogo lakini cha msingi zingatia muundo wa kichwa chako pamoja na aina ya macho uliyonayo na aina ya pamba ulizovaa pia.Sio umepiga jeans kali,kichwa kama madenge na macho kama bundi kisha unapiga miwani ndogo ya njano,ni

9. Vaa kofia za kijanja

Kofia pia huongeza mvuto,chagua kofia kulingana na aina ya kichwa na mavazi uliyovaa,haipendezi kuvaa suti na kapelo.Kanzu sharti ivaliwe na barakashia ndo utaeleweka la sivyo ni sawa na kuvaa dera tu

10. Mkanda

-Usivae mkanda mrefu km vile umefunga nyoka kiunoni
-Mikanda ya vitambaa au madoidoi inafaa kuvaliwa na jeans/kadeti/kaptula
-Jitahidi mkumatch rangi ya mkanda na viatu kama umevaa nguo za kuchomekea
-Zingatia upana wamkanda na rux za nguo yako

11.Tupia cheni za ukweli

Mikufu ya kiume pia huongeza mvuto
-Kama umevaa nguo za kuchomekea au suti itapendeza ukivaa cheni ndogo ambayo haitokezi nje ya shati
-Kama umepiga pamba za kishua mfano T.shirt na jeans hapa tupia cheni kubwa lakini hata cheni ndogo zinakubali

12.Uvaaji wa Tai

-Vaa kulingana na urefu wako
-Kama wewe mwembamba inapendeza kuvaa tie nyembamba
-Jitahidi kumatch tie na rangi ya shirt/suruali
-Hakikisha tie yako imefungwa vizuri shingoni

13.T.shirt na Jeans

Wanaume wajanja wa mjini hupenda kupiga t shirt na jeans na chini kutupia raba Kaliโ€ฆ..Vazi hili lina mvuto wa aina yake hasa likivaliwa kitaani na sehemu za mitoko kama vile kwenye Club za starehe.

14. Vaa viatu kijanja

Hapa pia Kuna changamoto
-Usivaa suruali ya kitambaa na Raba
-Usivae suruali ya kuchomekea na makubanzi
-Ukipiga jeans unaweza kumatch t.shirt/shirt na rangi ya viatu
-Ukivaa suti yakupasa upige kiatu kikali โ€ฆ.ulikosea itakuwa sawa na Toyota Mark X yenye matairi ya Fuso !!!

Umuhimu wa kufanya Masaji

Kufanya Masaji kuna faida hizi zifuatazo;

Masaji uongeza kinga ya mwili

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama โ€˜cytokinesโ€™ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama โ€˜cortisolโ€™.

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Kufanya masaji huondoa tatizo la kukosa usingizi

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.

Kuondoa mfadhaiko wa akili au Stress

Masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Masaji huondoa huzuni

Watafiti wanasema kuwa masaji kuongezeka homoni ijulikanayo kama โ€˜oxytocinโ€™ na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo โ€˜adrenocorticotropinโ€™.

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini

Masaji hupunguza maumivu hasa ya mgongo na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.

Masaji huongeza uwezo wa kujiamini

Masaji hutuliza mwili na kuongeza concentration

Mambao ya saluni ni shida, cheki kilichotokea kwa huyu

DADA alienda Salon wakati anasukwa akaingia
MKAKA mtanashati,
DADA akaamua kujaribu bahati yake.
DADA:Mambo? KAKA:Poa.
DADA:Mimi na wewe tunaweza kuongea baade?
KAKA:Kuhusu nini?
DADA:Nimekupenda nataka nikutoe out.
KAKA:Sawa ila nitamwambia nini
MKE wangu?
DADA:Aah ilo sio tatizo mdanganye tu,mwambie unakwenda kumtembelea rafiki yako hospitalini.
KAKA:Mwambie mwenyewe huyo hapo anayekusuka.

ย 

Unajua nn kiliendelea?

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia aloe vera

Mshubiri au Aloe Vera kama ilivyozoeleka na namna nzuri kwa wale wote wanaotaka kubaki na ngozi nyoro na ya kupendeza kila siku.

Chukua kipande cha mshubiri freshi na ukikate kasha chukua maji maji yake (jeli) na upake moja kwa moja kwenye uso wako na ujisuguwesuguwe kwa dakika 15 hadi 20 hivi pole pole kasha jisafishe na maji safi.

Tumia dawa hii mara 2 au 3 kwa wiki. Hii ndiyo njia rahisi ya kutibu chunusi bila kukuacha na madhara mengine mabaya.

Hizi ndizo faida za kiafya za kuota jua

Kuna mambo ambayo huwa tunayachukulia ya kawaida na wala hatuko tayari kufahamu umuhimu wake. Jua ni kitu mojawapo ambacho huwa tunakiona kila siku, lakini ni mara chache tumelichunguza.

Kwa hakika kuna umuhimu mkubwa wa jua kwa mimea na viumbe vingine akiwemo binadamu. Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya, zimebaini kuwa kuna manufaa makubwa ya kuota jua angalau kwa kiasi fulani kila siku.

Kwa kuwa najua unapenda afya bora, basi fahamu faida 10 za kuota jua kiafya.

Kuua bakteria

Jua linaweza kutumiwa kuua bakteria mbalimbali katika majeraha na ngozi. Tiba hii iligunduliwa na mshindi wa tuzo ya Nobel Niels Finsen. Tiba hii ilitumiwa kuponya vidonda vya wanajeshi wa Kijerumani baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Huondoa msongo wa mawazo

Inakadiriwa mtu anapokuwa kwenye jua hupata takriban kiasi cha kemikali ya lux kipatacho 100,000. Hivyo kukosa jua kunasababisha tatizo linalofahamika kama vile Seasonal Affective Disorder (SAD) ambayo ni aina fulani ya msongo.

SAD hutokea mara nyingi kwa watu wengi kipindi cha masika au kwa wale wanaokaa ofisini muda mrefu. Hivyo kuoata jua kutakuongezea kemikali ya lux na kukuepusha na tatizo la Seasonal Affective Disorder (SAD).

Huzuia shinikizo la damu

Utafiti uliofanyika katika chuo cha Edinburgh ulibaini kuwa kemikali ya nitric oxide ambayo hukabili shinikizo la damu, huingia kwenye damu pale mwili unapopigwa jua.

Watafiti waliendelea kueleza kuwa kutokana na utafiti huo ni wazi kuwa jua haliboreshi afya pekee, bali hurefusha maisha kwa kumwepushia mtu hatari ya kifo kinachoweza kutokana na shinikizo la damu.

Huimarisha mifupa

Inafahamika wazi kuwa jua ni chanzo cha upatikanaji wa vitamini D ambayo huuwezesha mwili kufyonza madini ya calcium na phosphorus yanayoimarisha mifupa.

Inaelezwa pia vitamini D3 inayozalishwa wakati wa uzalishaji wa vitamini D, husaidia kuzuia kuvunjika kirahisi kwa mifupa hasa kwa watu wenye umri mkubwa.

Huponya matatizo ya ngozi

Katika utafiti mmoja uliofanyika kwa watu wenye matatizo ya ngozi, ulibaini kuwa asilimia 84 ya magonjwa hayo yalipona baada ya kukaa kwenye jua kwa muda uliopendekezwa na daktari.

Inashauriwa kukaa kwenye jua kwa kiasi au kwa kutegemea ushauri wa daktari ili kuepusha madhara na kuhakikisha tiba hii inafanya kazi ipasavyo.

Huzuia baadhi ya saratani

Wakati watafiti wa saratani wakieleza kuwa zipo saratani hasa za ngozi zinazosababishwa na mionzi ya jua; kwa upande mwingine jua huzuia baadhi ya saratani.

Inaelezwa kuwa vitamini D inayozalishwa kutokana na jua, hupunguza aina mbalimbali za saratani kwa takriban asilimia 60.

Huboresha kinga ya mwili

Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kukaa kwenye jua la wastani huwezesha uzalishaji wa seli nyeupe za damu ambazo huukinga mwili dhidi ya maradhi.

Hupunguza lehemu (cholestrol)

Jua linapopiga ngozi ya mwanadamu hubadili lehemu iliyoko kwenye ngozi na kuifanya kuwa homoni ya steroid pamoja na baadhi ya homoni nyingine muhimu kwenye uzazi.

Hivyo kukaa kwenye jua hakupunguzi tu lehemu bali huzalisha pia homoni muhimu katika mwili wa binadamu.

Husaidia ukuaji wa watoto

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa jua ni muhimu sana hasa kwa ukuaji wa watoto wadogo. Hivyo kumweka mtoto nje ili apate angalau kiasi fulani cha jua kutaboresha afya na ukuaji wake.

Huongeza kiwango cha oksijeni mwilini

Jua linapoupiga mwili wako, linafanya seli nyekundu za damu kuweza kubeba na kusafirisha kiwango kikubwa zaidi cha oksijeni. Hili litapelekea kuwepo kwa kiwango kizuri cha oksjeni kwenye mwili wako.

Kumbuka! Kila kitu kinatakiwa kuwa cha kiasi ili kiwe na manufaa kwako. Kukaa muda mrefu sana kwenye jua kunaweza kukuletea madhara. Inashauriwa kukaa angalau dakika 10 hadi 15 ili upate manufaa kiafya.

Jinsi ya kulima vitunguu (vitunguu maji) kwa mbinu za kilimo bora na kwa faida

Vitunguu ni zao la mbogamboga na hulimwa kwa ajili ya balbu zake ambazo hutumika kama kiungo cha chakula. Vitunguu vina matumizi mengi sana na vina madini joto, chuma, vitamin A, vitamin B, vitamin C na vitamin E.
Vitunguu hulimwa na hukubali zaidi nyanda za baridi. Nyanda zenye joto vitunguu hulimwa pia. Vitunguu vinaweza kulimwa mwaka mzima endapo maji yanapatikana.

Aina za vitunguu vinavyolimwa Tanzania

  • Red Creole
  • Bombay Red
  • Hybrid F1

Hali ya hewa

Joto linatakiwa sana kwa ajili ya ukuaji wa balbu ila joto likizidi vitunguu hukomaa mapema kabla balbu hazijafikia ukubwa unaostahili, hivyo mkulima anaweza kupata mazao kidogo.

Udongo

Vitunguu huweza kupandwa kwenye udongo wowote wenye rutuba, usiotuamisha maji na usionata sana. Hufanya vizuri kwenye udongo wenye asidi kidogo japo udongo wenye alkali kidogo sio mbaya sana. Kwenye udongo wenye mchanga mchanga umwagiliaji ni lazima. Udongo mzuri sana kwa ustawi wa vitunguu ni tifutifu-kichanga.

Mbolea

Epuka matumizi ya mbolea mbichi isioiva vizuri kwani husababisha vitunguu kuwa na shingo pana sana majani hukua sana badala ya balbu.

Umwagiliaji

Umwagiliaji ni muhimu sana hasa wakati wa kuanza kutengeneza balbu. Unyevu uliozidi ni hatari sana kipindi cha ukuaji.

Kitalu cha vitunguu

Ni muhimu kumwagilia maji ya kutosha siku kumi za mwanzo tangu kusia mbegu kitaluni. Vitunguu hukaa kitaluni kwa wiki 6-8 na miche ifikiapo upana wa penseli na urefu wa sm 15 ni tayari kwa kuhamishia shambani/bustanini.

Upandaji

Kabla ya kupanda udongo ni lazima utifuliwe vizuri na reki kuondoa mabaki ya mimea na mawe ama Vipande vikubwa vya udongo. Matuta yawe na upana wa mita moja. Vitunguu hupandwa kwa mstari mojakwamoja ama kutokea kitaluni. Pia huweza kupandwa kwa mstari pacha. Vitunguu hupandwa sm 10-15 kutoka mmea hadi mmea na sm 10-15 kutoka mstari hadi mstari, kama inavyoonekana kwenye mchoro hapa chini. Pia epuka kupanda vitunguu mahali palipopandwa mboga jamii ya vitunguu siku za nyuma. Mfano Vitunguu saumu na vitunguu majani.

Utunzaji wa shamba

Kutandazia shamba na majani yaliyooza vizuri ama mabua inashauriwa ili kuongeza ruba ya ardhi, zuia magonjwa yatokanayo na udongo na magugu. Kupanda vitunguu kwenye matuta yaliyoinuka ni muhimu sana kuzuiya utuamishaji wa maji na mlipuko wa magojwa ya miche. Kungoa magugu na uvunaji ufanywe kwa mkono.
Vitunguu hufanya vizuri kama shamba litawekewa mbolea ya samadi ama mboji ilioiva vizuri. Kiasi cha tani 25-40 kwa heka kinashauriwa. Hii ni sawa na kilo 7.5 -12 kwa tuta lenye urefu wa mita 3 na upana wa mita 1.

Uvunaji

Vitunguu huvunwa kuanzia siku 90-150 tangu kusia mbegu. Dalili za kukomaa ni kuanguka kwa majani. Vitunguu huvunwa kwa kuvuta kwa mkono na kuhifadhiwa siku kadhaa shambani vikiwa vimefunikwa na majani. Baada ya hapo majani hukatwa na balbu hupakiwa kwa ajili ya kuhifadhi kusubiria bei nzuri. Vitunguu huweza kuhifadhiwa hadi miezi 9 tangu vivunwe bila kuharibika. Vitunguu vihifadhiwe kwenye nyuzijoto chini ya 4.4 ยฐC ama juu ya nyuzijoto 25ยฐC ili visiharibike.

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Namna ya kuondokana na tatizo la kunuka Kikwapa

Harafu ya jasho inakera, kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe husikii harufu hiyo ila wale walio karibu yako. Kwa upande mwingine kujaribu kuzuia kutoka jasho ni hatari kwa afya yako na kujaribu kuondoa harufu kwa kutumia pafyumu husababisha madhara mengine ya kiafya na kwa bahati mbaya perfume zina jaribu poteza harufu kwa mda mfupi tu na sio kutokomeza tatizo hilo.

Dawa rahisi ya kuondoa harufu kwenye kwapa o ni kutunza mwili wako ikiwa ni pamoja kuoga mara kwa mara hata ikibidi mara tatu kwa siku kwa kuanzia, kwani harufu mbaya ya kwapa inatokana na kuwepo kwa bakteria katika kwapa hasa kukiwa na unyevu au maji maji kwapani.

Ili kukomesha tatizo hili ni lazima kuoga mara nyingi pia wakati unaoga mkazo utiliwe kwenye kwapa tumia dodoki na sabauni unaposafisha kwapa lako, pili ni lazima ukaushe kwapa barabara ili kuondoa unyevu ambao unakaribisha bakteria ambao wanajaribu kuvunja vunja jasho lako na ndiyo maana linatoa harufu kali.

Vile unashauriwa mara baada ya kuoga tumia potassium alum au sulphur.

Vile vile jitahidi kuepuka nguo za polista (polyster) vaa nguo za pamba 100%

Punguza kula vyakula vyenye viungo vikali kama vitunguu swaumu nk.

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoidoโ€ฆ..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!โ€ฆkamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?โ€ฆkwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!โ€ฆsasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,โ€ฆhakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,โ€ฆ.hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!โ€ฆSasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!โ€ฆMy God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimyaโ€ฆ

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimyaโ€ฆ

Dogo ana dharau huyu!โ€ฆSasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!โ€ฆ.ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!โ€ฆDogo hakuwepo!โ€ฆ.na Mabegi pia hayapo!โ€ฆlap top haipo!โ€ฆ.NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!โ€ฆ.sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!โ€ฆyaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!โ€ฆniitieni Ambulance!

๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ๐Ÿ™†๐Ÿผ

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About