SMS ya kimahaba kwa mpenzi wako kumwambia unampenda sana hutaki hata sekunde ipite bila kumpenda
Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu,
basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila
kukupenda wewe.
Kama mapenzi huweza kukimbiwa kwa kufumba macho yetu tu,
basi nisingefunika macho kabisa. Sitaki sekunde ipite bila
kukupenda wewe.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Utamu wako ni zaidi ya asali, ni wa asili usiohitaji
kuongezewa ladha ya sukari, nitaumiss endapo
kama ukiwa mbali “NIACHE NIKUPENDE SWEET”
Watu waliniambia ninaweza kufanya chochote kama tu
nitaweka mawazo yangu juu ya hicho kitu. Lakini kila
nikijitahidi unaipoteza akili yangu
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha.
nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.
Dear siku zimekaribia, miaka …… utatimiza katika hii dunia,
hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia,
hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi,
zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi.
Happy Birthday mpenzi.
Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje.
Hodiiiiii, Hodiiiii,
Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Recent Comments