Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi.

Kanuni ya Mungu kuhusu mema

Unapoona mtu, jambo, kitu ni chema na kinakupendeza, Mungu naye anakifanya chema. Kwa maana anapenda kile tunachokipenda kama tuu hakina mawaa. Mfano. Mungu anakubali mtu unayetaka kufunga nae ndoa kama unampenda na unaona ni sawa

Utatu Mtakatifu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu

Mungu ni nani? Sifa za Mungu

Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote, katika mbingu na nchi, Mkubwa wa Ulimwengu mwenye kuwtunza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya. (Mt: 6:8-9, Yoh 20: 17) Sifa za Mungu Mungu ni Muumba wa vitu vyoteMungu ni Muumba wa vyote maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tuu pasipokutumia kitu chochote…

Kushinda ulimwengu ni kushinda mwili na akili yako

Maana ya Kumuamini Mungu

Kumuamini Mungu ni kuwa na uhakika na uwepo na uwezo wa Mungu. Ni kutambua na kukubali kwa uhakika kuwa Mungu yupo na anaweza kutenda. Unaweza kuwa na Imani lakini ukakosa kuamini yaani unaamini kwa Mungu lakini huamini kama atakutendea. Kuamini kunakua na sifa zifuatazo 1. Kutokuwa na mashaka kama Mungu…

Moyo wa Yesu

Ahadi kumi na mbili za Moyo Mtakatfu wa Yesu

Bwana Yesu mwenyewe kwa kutumia kinywa cha Mtakatifu Margareta Maria Alakoki aliahidi Baraka na neema zifuatazo kwa wale wote watakaouheshimu Moyo wake Mtakatifu. Na kwa maneno yake mwenyewe, Bwana Yesu aliahidi: 1. “Nitawajalia neema zote watakazozihitaji katika hali yao ya maisha 2. Nitawajalia amani katika familia zao 3. Nitawafariji katika…