Yai mmoja hupevuka siku 14 kabla ya hedhi i i inayofuata. Baada ya yai kukomaa ndani ya kokwa la upande wa kulia au wa kushoto, yai husafirishwa kwenye mrija wa kupitisha mayai mpaka kwenye mfuko wa uzazi.
Yai likijiunga na mbegu ya kiume ndani ya mrija wa kupitisha mayai siku zilezile, linaweza kurutubishwa. Yaani, endapo mwanamke anajamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka anaweza akapata mimba.
Kwa sababu wasichana wengi hawapati hedhi ya kawaida, yaani mzunguko wa siku 28 katika kila mwezi, ni vigumu sana kwao kufahamu tarehe ya hedhi i i inayofuata. Hivyo ni vigumu kujua lini litakuwepo yai linalongojea kurutubishwa.
Mzunguko wa hedhi kwa msichana unaweza kuathiriwa na mfadhaiko, huzuni, safari au mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Hata kama msichana ana mzunguko wa kawaida wa hedhi hali hiyo inaweza kubadilika ghafla na ukawa sio wa kawaida. Wanawake wengi na hasa wasichana hawawezi kutegemea kuhesabu siku kama njia ya kuzuia mimba, kwa sababu hawawezi kuwa na uhakika i iwapo lipo yai linalongojea kurutubishwa au la. Hakuna siku salama za kuepukana na mimba!
Recent Comments