Madhara ya dawa za kulevya kwa mwili na ubongo

Moja kati ya vitu vinavyotisha kuhusu dawa za kulevya ni kwamba zinaathiri watu kwa njia mbalimbali na huwezi ukasema kwa uhakika jinsi zitakavyokuathiri. Madhara ya dawa za kulevya yanategemea aina, kiwango na jinsi zitakavyotumika. Vilevile inategemea na umri, afya ya mwili na ukomavu wa akili, na pia mazoea ya matumizi ya dawa hizo.
Madhara ya muda hutokea mara tu baada ya dawa za kulevya kutumika, wakati madhara ya muda mrefu huonekana baada ya muda kupita, na mara nyingi husababisha uharibifu wa kudumu kwenye mapafu na ubongo.

Kwa mfano, bangi, husababisha kuongezeka kwa mapigo ya moyo, matatizo ya kumbukumbu ya muda mfupi, pamoja na umakini, kujifunza, kufikiri na kutatua matatizo. Pia inaweza ikasababisha kasoro kwenye utaratibu wa viungo vya mwili. Mara kwa mara wavuta bangi huwa na macho mekundu. Na vijana wengine hupata mihemuko mbalimbali kama uoga na hofu baada ya matumizi ya bangi.
Dawa za kulevya za vichangamsho, kama mirungi na kokaini, inasemekana kuwa huwafanya watumiaji kuwa macho, kujiona wana nguvu na kujiamini. Vichangamsho vikitumika kwa wingi, humfanya mtumaji kujihisi kuwa na wasiwasi au hofu. Matumizi mabaya ya dawa za kulevya kwa muda mrefu huweza kusababisha matatizo ya akili au hata kifo i iwapo yatatumika kwa kiwango cha juu.
Dawa za kulevya zinazokufanya upooze kama heroini au dawa nyingine zinazoagizwa na daktari, husababisha kujisikia umetulia, una amani na furaha. Ukizidisha vipimo husababisha usingizi, upungufu wa umakini na uwezo wa kuona, kizunguzungu, kutapika na kutokwa jasho. Vilevile kipimo kingi kinaweza kusababisha usingizi wa muda mrefu, kuzimia na hata kifo.

Pombe za kienyeji kama gongo ni hatari kwa afya na zinaweza kusababisha upofu na hata kifo.
Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza uwezo wa vijana kuhimili na kutatua matatizo yao ya kijamii na kiakili. Hii husababisha vijana kuwa wepesi kujihusisha na ujambazi na mambo ya ngono na ugomvi, mabadiliko hayo ya tabia husababisha ugomvi katika familia na kuvunjika kwa urafiki. Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo sababu kubwa ya ajali za barabarani, kujiua na maambukizo mbalimbali.

Melkisedeck Leon Shine

Editor: Melkisedeck Leon Shine, Enjoyed? Drop your Comment Below. OR Chat Live here. Download My Books in PDF Format here. More: Legal Guidelines | About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp

Read and Write Comments