Kwa kawaida mtu anapoamua kwenda kupima mara nyingi anakuwa na sababu za kumfanya ahisi kuwa au kutokuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo mtu akipata jibu kuwa hana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, i itabidi ajiulize huo wasiwasi ulitokea wapi.
Pale mtu anapojua ni kitu gani kilimfanya aende kupima, ni vyema mtu huyo kukaa mbali / kuacha kurudia hilo jambo au tabia i iliyomweka katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa mfano, kama alifanya ngono na mtu zaidi ya mmoja na kwa nyakati zote hakutumia kondomu. Baada ya kupima, mtu huyu anatakiwa aache tabia ya kuwa na wapenzi wengi na pia awe anatumia kondomu kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ni muhimu kuchukua tahadhari zote i ili kujikinga na maambukizi ya Virusi na UKIMWI na UKIMWI.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments