Vituo vyenye utaalamu na katika hospitali i au Taasisis kama vile Shirika la Amref au CCBRT wana uwezo wa kutoa ushauri nasaha na vipimo vya kuaminika. Ushauri nasaha unakusaidia wewe kuelewa kipimo hicho ni cha nini, ni majibu gani yanayoweza kupatikana au kutopatikana. Upimaji huu hufanywa kwa siri, ni wewe tu pekee yako unaweza kupewa majibu. Katika miji mingi, vituo vya ANGAZA vipo na pia vituo hivi hutoa huduma rafiki kwa vijana.
Huduma za upimaji hazipatikani kwa urahisi sehemu za vijijini kwa sababu vyombo vinavyotumika katika upimaji ni vya gharama kubwa na vinahitaji umeme na uangalizi mkubwa. Mpaka sasa huduma hizi zinapatikana katika hospitali na kwa baadhi ya mashirika yanayojishughulisha na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Jambo nzuri ni wewe kuuliza habari zaidi katika kituo cha afya kilicho karibu nawe.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments