Zipo aina mbili za mapacha, wale wanaofanana na wale wasiofanana. Karibu robo ya mapacha wote hufanana. Hii ina maana kwamba wametokana na yai moja lililotungwa mimba ambalo hujigawa katika makundi mawili tofauti ya chembechembe, kila mojawapo hubadilika kuwa kiumbe pekee. Hadi sasa, wataalamu hawaelewi vizuri sababu za yai kujigawa. Mapacha wa aina hii , kwa vile wametokana na yai moja, mara zote huwa na jinsia moja na hufanana sana kimaumbile.
Mapacha wasiofanana hutokea wakati wa yai kupevuka, kokwa za mwanamke hutokea zikawa mayai mawili badala ya moja tu. Mayai yote mawili hurutubishwa na hutungishwa mimba kwa mbegu mbili tofauti za mwanaume. Viumbe viwili hukua wakati mmoja katika mfuko wa uzazi. Mbali ya kukua katika mfuko mmoja wa uzazi na kuwa na umri uleule, mapacha hawa ni sawa sawa na watoto wengine wawili wa wazazi haohao. Wanaweza kuwa wa jinsia na maumbile tofauti kabisa.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments