Ubikira ni nini?: Maana halisi ya neno “bikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kujamii ana hapa i ina maana kwamba uume wa mwanaume unaingia katika uke wa mwanamke.
Watu kadhaa wanasema kwamba kuwepo kwa kizinda, ambacho ni ngozi nyembamba laini i i iliyoko kwenye uke i inayokaa kama kiwambo, ndiyo ubikira. Lakini wanawake wengine huzaliwa bila kiwambo au ngozi hii , i inawezekana kwa wengine kuchanika kwa kiwambo hiki i wakati wakifanya mazoezi mazito kama vile kupanda baisikeli, kukwea miti na kadhalika. Pia, i inaweza kutokea wakati wa uchunguzi wa kiafya au tiba i inayohusisha sehemu za ndani sana ukeni. Kiwambo hiki kinatofautiana baina ya msichana na msichana.
Kwa hiyo, kizinda siyo kipimo kizuri kwa ajili ya kumtambua bikira. Njia pekee ya kumtambua bikira ni kufahamu kama mtu hajawahi kujamii ana (yaani bikira) au kama ameshajamii ana (siyo bikira). Wewe si bikira kama umewahi kushiriki ngono na utakuwa umepoteza ubikira na hamna njia ya ubikira kurudi tena, hata ukisubiri muda mrefu. Lakini hii haimaanishi wewe uendelee kufanya ngono ovyo.
Msichana ambaye hajawahi kujamiiana anaitwa bikira, je mvulana huitwaje?
Neno “bikira” ni mtu yeyote ambaye hajawahi kujamii ana maishani mwake, awe mwanamke au mwanaume.
Zamani, watu walimtambua msichana bikira kwa njia ya kuhakikisha kwamba kile kiwambo chembamba ndani ya uke kipo. Lakini kwa sababu ngozi hii huweza kuchanika kwa njia nyingine zaidi ya kujamii ana, siyo kipimo kizuri cha kumtambua msichana ambaye hajajamii ana kabisa (yaani bikira).
Katika jamii nyingi ni kawaida kuwaita `bikira` wanawake ambao hawajawahi kujamii ana. Pia, jamii nyingi wanasisitiza umuhimu wa mwanamke kuwa bikira mpaka siku ya kuolewa. Hata hivyo, neno “bikira” hutumiwa kwa wanawake na wanaume.
Je, mvulana atajuaje kama msichana ni bikira? Na pia, msichana anaweza kujitambua vipi kama ni bikira?
Mvulana hawezi kuthibitisha ubikira wa msichana kwa njia ya kumwangalia wala kwa njia ya kumwingilia kimwili. Hii ni kwa sababu ubikira ni kutowahi kujamii ana na hautegemei kuwepo kwa kizinda ndani ya uke. Yaani msichana ambaye hajawahi kujamii ana, lakini ambaye kizinda chake kimepasuliwa kwa sababu nyingine, bado ni bikira. Njia pekee ya kufahamu kama msichana ni bikira ni kufahamu kile alichofanya maishani, na hii , kwa kweli haiwezekani.
Msichana anaweza kujifahamu kuwa bikira kama hajawahi kujamii ana, yaani kuingiliwa kimwili na mwanaume au mvulana.
Jamii nyingi hutilia mkazo kuhusu ubikira wa wasichana wakati wa kuolewa. Lakini suala la kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa au kuoa ni muhimu kwa wote, wasichana na wavulana. Kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa kuna maana ya kujiepusha na shida zinazoweza kutokea, kama mimba isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa na hata maambukizi ya VVU na UKIMWI. Iwapo huwezi kustahimili ashiki ya kujamii ana, basi huna budi kuhakikisha kuwa unajikinga wewe na mpenzi wako asipate ujauzito na magonjwa kwa kutumia kondomu.
Kizinda ni nini na kinawezaje kuharibika
Kizinda ni kiwambo laini kinachokuwepo ndani ya uke. Kiwambo hiki kina tundu katikati i i ili kuwezesha damu ya hedhi kupita kiurahisi. Ukubwa na unene wa kiwambo hiki hutofautiana kati ya msichana na msichana. Wakati wa tendo la kwanza la ngono, huchanika na kwa wengi i i inasababisha kutokwa damu. Lakini pia inawezekana kutokuwepo na tendo la kutokwa damu. Hii ni kwa sababu kiwambo hiki kina asili ya kunyumbuka sana na wakati mwingine tundu lake ni kubwa. Inawezekana pia kuwa kiwambo hiki tayari kilikuwa kimeharibiwa na sababu nyingine.
Read and Write CommentsReferences:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments