Mvulana hawezi kuthibitisha ubikira wa msichana kwa njia ya kumwangalia wala kwa njia ya kumwingilia kimwili. Hii ni kwa sababu ubikira ni kutowahi kujamii ana na hautegemei kuwepo kwa kizinda ndani ya uke. Yaani msichana ambaye hajawahi kujamii ana, lakini ambaye kizinda chake kimepasuliwa kwa sababu nyingine, bado ni bikira. Njia pekee ya kufahamu kama msichana ni bikira ni kufahamu kile alichofanya maishani, na hii , kwa kweli haiwezekani.
Msichana anaweza kujifahamu kuwa bikira kama hajawahi kujamii ana, yaani kuingiliwa kimwili na mwanaume au mvulana.
Jamii nyingi hutilia mkazo kuhusu ubikira wa wasichana wakati wa kuolewa. Lakini suala la kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa au kuoa ni muhimu kwa wote, wasichana na wavulana. Kutofanya mapenzi mpaka siku ya kuolewa kuna maana ya kujiepusha na shida zinazoweza kutokea, kama mimba isiyotarajiwa, magonjwa ya zinaa na hata maambukizi ya VVU na UKIMWI. Iwapo huwezi kustahimili ashiki ya kujamii ana, basi huna budi kuhakikisha kuwa unajikinga wewe na mpenzi wako asipate ujauzito na magonjwa kwa kutumia kondomu.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Recent Comments