Huruma ya mama kwa mwanae ilivyomtesa

Alikuwepo mama mmoja aliyekuwa chongo na mwanae alimchukia kwa sababu ya kuwa chongo. Mwanae alijisikia aibu kutembea na mama yake mwenye jicho moja na hakupenda watu wajue kuwa yule ni mama yake.

Hata alipokuwa shuleni hakupenda mama yake amtembelee, na ikitokea mama yake akamtembelea basi watoto wenzie watamcheka siku nzima na kumtania. Hii ilimfanya mtoto huyu kujisikia vibaya sana na wakati mwingine kujuta kuwa na mama wa aina hiyo.

Lakini mama alimpenda mwanae na hakuonesha kukasirika hata pale mwanae alipomnyanyapaa waziwazi.

Badae mtoto akakuwa akamaliza masomo yake na kupata kazi nzuri. Akafurahi kuwa sasa amepata kazi atakuwa mbali na mama yake ‘chongo’ anayemtia aibu.

Akachagua kufanya kazi mji wa mbali na alipo mama yake. Akafanikiwa kazini kwa kupandishwa cheo na akawa mtu mashuhuri mwenye mali na mwenye heshima kubwa ktk jamii yake.

Siku moja asubuhi akasikia wanae wakilia walipokua nje wakicheza.. Alipowauliza wakasema kuna mtu anawatisha.. Akatoka nje kujua nani anayewatisha wanae. Kufika akamkuta mwanamke mmoja mzee mwenye jicho moja (chongo). Kumbe wale watoto walitishwa na chongo la yule bibi.

Alipomtizama vizuri yule mwanamke akamgundua ni mama yake mzazi. Alikua amechoka na amezeeka sana. Amedhoofu mwili na anaonekana mgonjwa..

Mtoto kwa hasira akamuuliza “mama umekuja kufanya nini hapa? Kama una shida ungenipigia simu sio kuja? kwanza nani kakuonyesha ninapoishi? Na nani kamruhusu mlinzi kukufungulia mlango? Ona sasa umewatisha wanangu kwa chongo lako”

Mama yake akasema “samahani mwanangu, sikujua naomba unisamehe”. Kisha mtoto akamchukua mama yake akamtoa nje na kumpeleka kituo cha basi ili arudi kijijini.

Baada ya siku chache kupita, yule jamaa akapata taarifa kuwa mama yake ni mgonjwa sana na anahitaji kumuona. Akaondoka kwa siri kwenda kijijini ili akasikie mama yake anataka kumwambia nini.

Alipofika akakuta watu wengi wamekusanyika nyumbani kwao. Alipouliza akaambiwa mama yake alifariki baada ya kuugua sana bila msaada wowote.

Alipoingia ndani akakuta barua aliyoandika mama yake.. Barua ilisomeka hivi…

“Kwako mwanangu mpendwa wa pekee,
Naandika barua hii nikiwa kwenye maumivu makali sana na sijui kama nitapona.. Nimeugua nikakosa matibabu kwa kutokuwa na fedha. Sikuwa na mtu mwingine wa kumueleza shida yangu zaidi yako wewe mwanangu wa pekee… Lakini nilipojitahidi kuja kwako angalau unisaidie matibabu ulinifukuza na kudai nawatisha wanao kwa chongo langu ! Uliniumiza sana mwanangu sitisahau maishani mwangu ila nimekusamehe.

Baba yako alifariki ukiwa mdogo sana. Nami sikubahatika kupata mtoto mwingine. Nilikulea kwa nguvu zangu zote na umasikini niliokuwa nao ilikuwa nikitegemea badae utanisaidia lakini umenitelekeza na kunitupa kwa sababu tu mimi mama yako ni chongo ! Hivyo unaona aibu kuwa nami….

Nisamehe kwa kuwatisha wanao kwa chongo langu, nisamehe kwa kuja kwako bila ya taarifa, nisamehe kwa kukufanya uchekwe na wenzio kwa kuwa mimi mama yako ni chongo….

Lakini naomba nikupe siri ambayo hukua unaijua ewe mwanangu, wewe ndiye uliyezaliwa ukiwa chongo. Ulikua na jicho moja tu. Nikaumia sana kuona mwanangu ana jicho moja, atawezaje kuishi na kukabiliana na changamoto za maisha.. Nikaomba madaktari wanitoe jicho langu moja wakupe wewe, Niliona ni heri mimi niwe chongo kwa kuwa nimeshaona mengi sana duniani kuliko wewe..

Na ulipowekewa jicho langu nilifurahi kukuona una macho mawili nikajua utaweza kuzikabili vema changamoto za dunia hii… Na hakika jicho langu limekusaidia kwani wewe ni mtu mashuhuri na tajiri sana kwa sasa…

Lakini kwa jinsi ninavyoumwa najua nitakufa. Ila nafurahi kuwa nakufa nikiwa nimetimiza haja ya moyo wangu. Kwa kutumia jicho langu umeweza kuwa msomi mzuri na tajiri unayeheshimika na jamii yote.. Wasalimie wajukuu zangu na waambie wawe na amani hawataniona tena nikienda kuwatisha na chongo langu.. Please take care of my eye…

Akupendaye,
Mama”

Alipomaliza kuisoma barua hii akalia sana. Akatamani mama yake afufuke amuombe msamaha na amlipe kwa wema wake aliomtendea.. Lakini haikuwezekana, it was TOO LATE.!

MORAL OF THE STORY.!

Nyuma mafanikio ya kila mwanaume yupo mwanamke. Anaweza kuwa mama yako, mke wako, dada yako au mchumba wako.. Je unatambua nafasi yake katika mafanikio yako au unampuuza tu?

Wapo wanawake ambao walijitoa sadaka ili uweze kuwa hapo ulipo. Jiulize mama yako amefanya mangapi kukufikisha hapo.

Hadithi hapo juu inatueleza juu ya mama aliyetoa jicho lake kwa mwanae.. lakini jicho ni kielelezo tu cha yale wanayofanya mama zetu.

Kuna wengine jicho lao ni vibarua alivyokua anafanya ili wewe usome.. Pengine jicho lake ni namna alivyokua akijinyima kwa kuvaa nguo moja mwaka mzima ili upate ada ya shule na mahitaji mengine.. Je umewahi kumshukuru mama yako kwa kutoa jicho lake kwa ajili yako??

Mpende sana mama yako.. Wapende wanawake wote, waheshimu, walinde, wajali. Wanapitia magumu mengi sana ili kutufanya sisi wanaume tuwe kama tulivyo.

Enjoyed? Drop your Comment Below
OR Chat Live with AckySHINE here
Read and Write Comments
Shopping Cart