Baini Siri za Familia, Mapenzi na Mahusiano

📖Karibu usome Makala Nzuri za Siri za Familia, Mapenzi na Mahusiano. 💑👫💖

📜KUMBUKA: Ukurasa huu haufiki mwisho, unaendelea kujifungua vile unavyoendelea kusoma kushuka chini. 🔄 Kwa hiyo, kama utaona hujapendezwa na Makala, unaweza kuiruka na kusoma zinazofuata chini. ⏭️

🔄ZINGATIA: Kila baada ya Muda, ukurasa huu unajiupdate (unakua mpya) ili kukuwezesha utakapotembelea tena kukutana na Makala mpya. 🆕 Mfano ukitembelea ukurasa huu leo utasoma makala tofauti na utakazoziona kesho. Kwa hiyo, Kila siku unaweza kutembelea ukurasa bila kuuchoka. 📰🎉
Endelea chini au Chagua kati ya hizi kuchuja:

Ujuzi wa Mawasiliano
Upendo na Mapenzi
Ukaribu na Ushirikiano
Familia na Malezi ya Watoto
Ndoa na Kujitoa
Utatuzi wa Migogoro
Afya ya Kihisia
Kuvunjika Mahusiano na Uponyaji wa Majeraha
Pesa na Mambo ya Kifedha Katika Mahusiano

Jinsi ya kuwa Mwanamme wa kipekee: Kujitambua na kujikubali

Mpendwa Msomaji, Makala hii imetolewa kwenye kitabu cha JINSI YA KUWA MWANAMME WA UKWELI NA KIPEKEE. Kama unataka kujitambua na kufahamu uanaume wako, hiki ndicho kitabu cha kusoma.

Namna ya kukubali uanaume wako

Jambo la kwanza la kuzingatia ili uweze kuwa mwanaume wa ukweli na kipekee ni kukubali uanaume wako. Ni kujitambua kuwa wewe ni mwanamme na kuamua kuishi kama mwanamme. Kukubali uanaume ni mchakato wa kujitambua na kujiheshimu kama mwanaume, pamoja na kukubali na kuthamini vipengele vyote vinavyokufanya uwe mwanamme.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia kwenye kukubali uanaume wako:

1. Kufahamu nini Maana ya Kuwa Mwanaume: Tambua na elewa kuwa wewe ni mwanamume na una sifa na uwezo wa pekee ambao unachangia katika jamii yako.

Sifa kuu za mwanamme ni hizi;

  1. Ujasiri: Uwezo wa kushinda hofu na kuchukua hatua katika maisha.
  2. Uadilifu: Kuwa na maadili na kuishi kulingana na kanuni na maadili yanayokubalika.
  3. Uaminifu: Kuwa mwaminifu na kutimiza ahadi zako kwa wengine.
  4. Uwezo wa kulinda na kuhudumia: Kuwa na wajibu wa kulinda na kuhudumia familia na wapendwa wako.
  5. Ukarimu: Kuwa na moyo wa kujali na kusaidia wengine kwa ukarimu.
  6. Uongozi: Kuwa na uwezo wa kuongoza na kuhamasisha wengine kuelekea malengo ya pamoja.
  7. Uvumilivu: Kuwa na subira na uwezo wa kukabiliana na changamoto na misukumo ya maisha.
  8. Uwezo wa kujieleza: Kuwa na uwezo wa kueleza hisia na mawazo yako kwa njia inayofaa na inayosaidia mawasiliano.
  9. Kujitambua: Kuwa na ufahamu wa ndani wa wewe ni nani, nguvu zako, na udhaifu wako.
  10. Ushirikiano: Kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na wengine na kujenga uhusiano mzuri na jamii.

Unaweza kufahamu Zaidi sifa za mwanamme kwa kujifunza kuhusu historia na tamaduni za wanaume. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuona umuhimu wa utambulisho wako wa kiume na itakusaidia kuchukua hatua katika kukubali uanaume wako.

2. Uwe Huru Kuonyesha Hisia: Kukubali uanaume hakumaanishi kwamba unapaswa kuficha hisia zako au kuwa na hisia kali mfano kuwa na ukali usiohitajika. Mimi kama AckySHINE nitakushauri kuwa na ujasiri wa kuonyesha hisia zako, kuwa mnyenyekevu, na kuwa na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha.

3. Kujenga Uhusiano wa Karibu na Wanaume Wengine: Mwanamme unapaswa kuwa na uhusiano wa mzuri na wa kina na wanaume wengine. Ili uweze kujikubali na kujitambua unapaswa kujihusisha katika jamii ya wanaume wengine. Kwa namna hiyo, utaweza kupata msaada, kushiriki uzoefu, na kujenga urafiki wenye msingi wa uaminifu na wanaume wengine.

Haya ni baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kuimarisha mahusiano na ukaribu na wanaume wengine;

  1. Kuwa wazi na mwenye heshima: Kuwa wazi na mwenye heshima katika mawasiliano yako na wanaume wengine. Jenga mazingira ya kuheshimiana na kusikilizana.
  2. Tambua maslahi yanayofanana: Tafuta maslahi yanayofanana na wanaume wengine, kama michezo, shughuli za burudani, au masuala ya kazi. Hii itakusaidia kuwa na mada za kuzungumzia na kujenga uhusiano wa karibu.
  3. Kuwa mkarimu na msikivu: Kuwa tayari kusaidia wengine na kuwasikiliza. Kuwa rafiki anayejali na kusaidia wengine itajenga uhusiano wa karibu na wanaume wengine.
  4. Shughulika na tofauti za kijinsia: Elewa kuwa kuna tofauti za kijinsia katika mawazo, hisia, na uzoefu. Kuwa na uelewa wa hili na kuwa tayari kuelewa mtazamo wa wanaume wengine katika mazingira tofauti.
  5. Unda fursa za kijamii: Jishughulishe katika shughuli za kijamii kama mikutano, hafla, au klabu ambapo unaweza kukutana na wanaume wengine na kujenga uhusiano wa karibu.
  6. Jifunze kutoka kwa wanaume wengine: Wanaume wengine wana uzoefu na maarifa tofauti. Jifunze kutoka kwao na kuwapa nafasi ya kushiriki mawazo yao na uzoefu wao.
  7. Kuwa mwaminifu na mkweli: Kujenga uhusiano wa karibu na wanaume wengine kunahitaji uwazi na uaminifu. Kuwa mwaminifu na mkweli katika mahusiano yako na wanaume wengine.

4. Ondoa Dhana Potofu: Tengeneza uelewa sahihi kuhusu uanaume na kuepuka dhana potofu na ubaguzi wa kijinsia. Fanya kazi kwa bidii kuondoa mitazamo hasi kuhusu wanaume ambayo inaweza kuzuia kukubali uanaume wako kwa ukamilifu.

5. Kuwa Mfano wa Kuigwa: Mwanamme anapaswa kuwa mtu anayeheshimu wengine, anayejali na kuunga mkono usawa wa kijinsia, na kuwa na ushiriki mzuri katika familia na jamii yako, na watu wote wanaokuzunguka. Kuwa mfano mzuri wa uanaume maana yake ni kujenga maadili na tabia chanya. Kukubali uanaume ni safari ya kibinafsi ambayo inahitaji ufahamu, uelewa, na ujasiri wa kuamua wewe mwenyewe. Kumbuka kuwa kila mtu ni tofauti, na njia yako ya kukubali uanaume itakuwa ya kipekee kwako. Jitahidi kupambanua mambo, kukua, na kuongeza ufahamu mzuri juu ya wewe ni nani kama mwanaume.

Mtazamo wa jamii na tamaduni kuhusu uanaume

Baada ya kusoma namna ya kujikubali kama mwanamme, sasa tuangalie Mtazamo wa jamii na tamaduni kuhusu Mwanamme. Kwa sababu mtazamo wa jamii na tamaduni kuhusu uanaume una mchango mkubwa katika namna wanaume wanavyojiona, wanavyotenda, na jinsi wanavyoshiriki katika jamii.

Hii ni baadhi ya Mitazamo ya jamii na tamaduni kuhusu uanaume:

1. Matarajio ya Jinsia na Maumbile: Jamii inatarajia wanaume kuwa wenye nguvu, wasioonyesha hisia nyingi, wakali, wazalendo, na wenye mafanikio. Wewe kama mwanamme unapaswa kufahamu haya kwa sababu yanaweza kusababisha shinikizo la kuishi kulingana na matarajio hayo. Unapaswa kufahamu mipaka yako na kuishi kama unavyotaka.

2. Ubaguzi wa Kijinsia: Jamii inaweza kuwa na mfumo wa ubaguzi wa kijinsia ambao unaweza kudhuru wanaume. Hii inaweza kuonekana katika uhusiano wa kijinsia, upendeleo katika mfumo wa haki, na dhana potofu kwamba wanaume hawawezi kuwa wahasiriwa wa unyanyasaji au matatizo ya kijamii, kiafya ya akili.

3. Wajibu wa Familia na Baba: Katika baadhi ya jamii, wanaume wanaweza kuwa na jukumu la kuwa watoaji wa kifedha katika familia na kuwa viongozi wa kaya. Hii inaweza kuleta shinikizo na majukumu makubwa kwa wanaume katika jukumu lao la baba na mwenzi wa ndoa. Kama mwanammez unapaswa kufahamu majukumu yako na kuyatimiza inavyotakiwa.

4. Unyanyapaa wa Kijinsia: Mfumo wa jamii unaweza kuweka unyanyapaa au vizuizi kwa wanaume kuhusiana na mambo kama kutafuta msaada. Hii inaweza kufanya wanaume kujizuia kuomba msaada na kuhisi wanaume ni dhaifu wanapopambana na changamoto hizo. Jamii inaamini kwamba mwanamme anapaswa awe anajiweza mwenyewe. Jamii inatengeneza mazingira ya ugumu kwa mwanamme kuomba msaada hasa kwa mwanamke.

5. Ushiriki katika Huduma ya Jamii: Katika jamii nyingi, wanaume wanaweza kuwa na jukumu kubwa katika masuala ya kijamii na uongozi. Wanaweza kutarajiwa kushiriki katika huduma za kijamii kama vile ulinzi, usalama, na uongozi wa kisiasa. Hii inaweza kujenga shinikizo la kudumisha hadhi na kusimama kwa utu wa kiume. Ili uweze kuwa mwanamme wa ukweli na wa kipekee unapaswa kufahamu naa kushiriki huduma za kijamii hizi zinazomlenga mwanamme.

Ni muhimu kutambua kuwa mitazamo hii inaweza kutofautiana kulingana na tamaduni, dini, na mazingira ya kijamii. Kuelewa mitizamo hii ni muhimu ni muhimu ili kuweza kuishi na kukubalika katika jamii kama mwanamme.

Utambulisho na Sifa za Mwanamme halisi

Kuna vipengele tofauti vya utambulisho wa kiume ambavyo huunda sehemu ya uanaume wa mtu. Ukiwa kama mwanamme unapaswa kufaaha vipengele hivi ili kujitambulisha inavyotakiwa na kuwa na sifa za kiume.

Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo;

1. Utambulisho wa Kijinsia: Utambulisho wa kijinsia unahusisha kujitambua kama mwanaume na kuhisi kujaliana na jinsia yako ya kuzaliwa. Ni ufahamu wa ndani na hisia ya kipekee ya kuwa mtu wa kiume.

2. Nguvu na Uwezo wa Kimwili: Wanaume mara nyingi huwa na sifa za kimwili kama nguvu, ukubwa wa mwili, na uwezo wa kimwili unaohusiana na jinsia yao. Hii ni moja ya vipengele vya kipekee vya utambulisho wa kiume.

3. Uwezo wa Kuongoza: Utambulisho wa kiume mara nyingi hujumuisha wajibu wa kuwa kiongozi na mtu wa maamuzi katika jamii, familia, au eneo la kazi. Uwezo wa kuongoza na kufanya maamuzi yenye msingi ni vipengele muhimu vya utambulisho wa kiume.

4. Uhusiano na Ubaba: Uwezo wa kuwa baba na kushiriki katika malezi ya watoto ni vipengele muhimu vya utambulisho wa kiume. Jukumu la kuwa mlezi na kuwa mfano mzuri kwa watoto ni sehemu muhimu ya uanaume.

5. Nafasi ya Kijamii na Utambuzi: Utambulisho wa kiume unaweza pia kuhusisha nafasi ya kijamii na utambuzi. Hii inajumuisha jukumu la kuwa na mchango wa kifedha na kimawazo katika familia, mtetezi wa haki na usawa, na mshiriki muhimu katika jamii.

6. Ujasiri na Uhodari: Wanaume mara nyingi wanakabiliwa na shinikizo la kuonyesha ujasiri na uhodari katika hali mbalimbali. Uwezo wa kushughulikia changamoto na kusimama imara ni sifa muhimu ya utambulisho wa kiume.

7. Kujieleza na Kuonyesha Hisia: Ingawa kuna dhana potofu kwamba wanaume hawapaswi kuonyesha hisia, sehemu ya utambulisho wa kiume ni uwezo wa kujieleza kwa ufasaha na kuonyesha hisia kwa njia sahihi.

Ni muhimu kutambua kuwa vipengele hivi havina umuhimu sawa kwa kila mtu na kwamba kila mtu anaweza kuwa na utambulisho wa kiume unaofanana au tofauti. Utambulisho wa kiume ni uzoefu wa kibinafsi ambao unaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Kuenzi Maadili, Majukumu na Wajibu wa Mwanamme

Kuenzi Maadili, Majukumu na Wajibu wa Mwanamme ni kipengele muhimu kumuwezesha mwanamme Kuukubali uanaume wake. Kuenzi nguvu na maadili yanayojitokeza katika wanaume ni muhimu katika kujenga utambulisho chanya wa kiume na kukuza maendeleo bora ya mwanamme na jamii kwa ujumla.

Haya ni baadhi ya maadili na nguvu kadhaa ambazo zinaweza kuenziwa na mwanamme katika kuukubali uanaume wake:

1. Uadilifu: Kuwa na uadilifu ni msingi muhimu wa maadili yanayoheshimiwa katika uanaume. Kuishi kulingana na kanuni na maadili ya haki, ukweli, na uwajibikaji ni ishara ya nguvu ya kimaadili katika wanaume.

2. Uongozi: Wanaume wanaweza kuenziwa kwa uwezo wao wa kuwa viongozi na watu wenye ushawishi katika familia, jamii, au maeneo yao ya kazi. Uongozi unaoheshimika na wenye msingi wa maadili huwezesha wanaume kuleta mabadiliko chanya na kuleta mafanikio kwa wengine.

3. Ujasiri: Ujasiri ni sifa ambayo mara nyingi hufahamishwa kwa wanaume. Uwezo wa kukabiliana na changamoto, kushinda hofu, na kuwa na uhodari katika maisha ni ishara ya nguvu na maadili katika uanaume.

4. Uwajibikaji: Wanaume wanaweza kuonyesha nguvu na maadili kwa kuwa watu wa uwajibikaji katika majukumu yao. Uwezo wa kuheshimu ahadi, kushughulikia majukumu kwa uaminifu, na kuwa na nidhamu katika matendo yao huwapa wanaume sifa nzuri na kuwafanya kuwa viongozi wa kuigwa.

5. Ukarimu: Kuwa na moyo wa ukarimu na kujali wengine ni maadili muhimu katika uanaume. Uwezo wa kusaidia wengine, kugawana rasilimali, na kuwa na nia njema katika matendo yao hujenga uhusiano mzuri na kuimarisha jamii.

6. Uvumilivu na Ustahimilivu: Uvumilivu na ustahimilivu ni maadili yanayosaidia katika kuendeleza uhusiano mzuri na kushughulikia tofauti na changamoto kwa busara. Mwanaume anapaswa kuwa na uwezo wa kusikiliza na kuelewa maoni tofauti, na kuwa na subira katika kipindi cha mafadhaiko ili kuchangia nguvu na maadili katika uanaume.

Kuenzi nguvu na maadili haya katika wanaume ni muhimu katika kujenga jamii yenye usawa na yenye mafanikio. Mimi kama AckySHINE nasisitiza kwamba ni jukumu la kila mwanamume kuishi kulingana na maadili haya na kuwa mfano mzuri kwa wengine.

Jinsi ya kuwa Mfano na kuwasaidia wanaume wengine kujitambua

Baada ya kujitambua kama mwanamme ili uwe mwanamme wa ukweli na wa kipekee una wajibu wa kuwa mfano wa kuigwa na kuhamasisha wanaume wengine kujitambua. Kuhamasisha na kuwasaidia wanaume wengine kukubali na kujieleza wenyewe kwa uhuru ni jambo muhimu kwa wanaume, kwani inawawezesha kuishi maisha yenye furaha, afya na kujenga uhusiano wa kina na wengine.

Zifuatazo ni njia unazoweza kutumia za kuhamasisha wanaume wengine kukubali na kujieleza wenyewe kwa uhuru kama wanaume:

1. Elimu na Uhamasishaji: Toa elimu na uhamasishaji kuhusu umuhimu wa kukubali na kujieleza wenyewe kwa uhuru kwa wanaume. Fanya mazungumzo, shiriki na changia kwenye semina, na programu za elimu zinazolenga kukuza ufahamu wa wanaume juu ya umuhimu wa kuonyesha hisia zao na kuwa wazi kuhusu mahitaji yao na hisia zao.

2. Kuunda Nafasi Salama: Hakikisha kuna nafasi salama na mazingira yasiyo na hukumu kwa wanaume kuweza kujieleza. Weka mazingira ya kuaminiana, kama vile vikundi vya msaada au vikao vya majadiliano ambapo wanaume wanaweza kujisikia huru kuzungumza kuhusu hisia zao na changamoto wanazokabiliana nazo.

3. Kuwa Mfano Bora: Kama mwanaume, kuwa mfano bora kwa kujieleza kwa uhuru na kukubali nafasi yako ya kuwa binadamu. Onyesha ujasiri kwa kuonyesha hisia zako, kuzungumza kwa uwazi, na kushiriki katika mazungumzo ya kina na wengine. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuhamasisha wanaume wengine kuiga tabia hiyo.

4. Kujenga Ushirikiano: Kuwa sehemu ya uhusiano wa kina na wanaume wengine. Kwa kushiriki uzoefu, kuunga mkono na kusikiliza wengine, unaweza kuhamasisha wanaume wengine kujieleza na kukubali wenyewe kwa uhuru. Kujenga mtandao wa msaada na urafiki na wanaume wengine unawawezesha kushiriki na kujifunza kutoka kwa wengine.

5. Kuelimisha Juu ya Umasikini wa Jinsia: Elimisha juu ya umasikini wa jinsia na madhara yake kwa wanaume. Wanaume wanaweza kuathiriwa na shinikizo la kijinsia na dhana potofu kuhusu jinsi wanavyopaswa kuwa. Kwa kuhamasisha uelewa juu ya umasikini wa jinsia, unaweza kusaidia kujenga jamii inayokubali zaidi na yenye nafasi ya kujieleza kwa uhuru kwa wanaume. Kuhamasisha kukubali na kujieleza wenyewe kwa uhuru kwa wanaume ni mchakato endelevu. Ni muhimu kuwa na subira, uelewa, na kusaidiana katika safari hii. Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kujenga jamii inayojali na inayowaheshimu wanaume kama watu wanaostahili kuwa huru kujieleza na kukubali nafasi yao katika ulimwengu huu.

Unaweza kuendelea kusoma Mada nyingine nyingi Kama hii kwenye kitabu cha JINSI YA KUWA MWANAMME WA UKWELI NA KIPEKEE. Angalia maoni ya wasomaji wengine pamoja na listi nzima ya Yaliyomo hapa>>>

Click Download Now kukichukua

WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila wakati.
3.Ukimuomba simu yake ghafla lazima akwambie hebu kwanza…….
4. Kamwe haiiti always vaibration.
5. Namba nyingi ha save.
6. Kuna simu hapokei hata iweje….anapenda sms zaidi
7.Majina mengi kwenye simu yameseviwa kwa majina ya kufikirika.
8.Muda mwingi ni mtu wakujihami.
9.Anapenda password na anabadili mara kwa mara.
10.Akiazima simu yako, akitumia tu anafuta deal no haraka.
11.Always yuko na simu…..hadi bafuni ikibidi.
12. Anajazba ukimuuliza chochote kuhusu simu….anajishtukia.
13. Akiwa anachati anakuangalia mara kwa mara kiwiziwizi
14. Hana jeuri ya kukuweka profile picture na akikuweka humalizi masaa anakudampu huko Hapa kuna ukweli asilimia millioni moja kabisa Share na washikaji zako😜😜i

Download Kitabu hiki Kifuatacho cha SIRI ZA MWANAMKE kuwafahamu zaidi Wanawake

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Dalili za mahusiano feki, mahusiano ya kichina

Ukitaka kujua Simu ya Kichina utajua tu jinsi ilivyo na makelele mengiiiii sana wakati wa kuita….

Sasa ukitaka kujua relationship feki ya kichina utaona tu makelele yalivyo mengi kama ile simu…

Watu hawatulii kwenye wall,mara I miss my baby,mara baby come back,mara baby this,ooh my man/Girl is special,mara picha…

Mi and my baby,full kujishaua..ukiona wall zenye hayo makelele asilimia 90 ni penzi la kichina na lazima lina double line.

Relationship serious na Original hazina makeke wala mikelele mingi kama hiyo yako na milio mikubwa ya ajabu na vibration ambazo zinaweza kufyeka hata majani.

TULIA, hatuhitaji kujua who is ur baby au umemmiss, ukimmiss mpigie simu hukooo! Ebooo!!!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake

Mambo 7 ambayo mwanaume apaswi kumfanyia mke wake..
1. Usimpige.
2. Usimtukane na kumshushia heshima.

3. Usimfanye ajihisi hapendwi na anamkosi.
4. Usimbake.
5. Usimsaliti na kujionyesha kabisa kwamba una saliti.
6. Msikilize pale anapokua na stress, mpe muda wako, mkumbatie na mpe maneno ya faraja.
7. Mpe zawadi, hata kama ni ndogo kiasi gani kwake ni alama tosha.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE ili kuwafahamu zaidi Wanawake

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema “sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema “we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema “ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!” Kisha akamgeukia mke wake na kusema “mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

Sababu 5 zinazosababisha wanawake warembo wazuri wasiolewe

Wanawake wengi warembo husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti.

Wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa
Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa? Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake warembo kusalia wapweke.

1. Tabia mbaya

Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya na kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.

2. Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana

eti hawawezi kuosha nyumba kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawaju kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.

3. Ghali kuwatunza

Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.

4. Wabinafsi na wenye chuki

Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa “wanapendwa” na wanaume wengi.

Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.

5. Hawataki kuwa wazazi

Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.

Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

 

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

 

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE

Jinsi ya kuamsha mahaba na mapenzi katika mahusiano

Hizi hapa njia za kuamsha na kudumisha uhusiano mzuri kati yako na mpenzi wako hasa baada ya kuwa mmeshazoeana sana na kuhisi kuchokana.

Dumisha faragha katika mahusiano yenu

Hakikisha kunakua na faragha katika mahusiano yako na mpenzi wako. Vile vile itahakikisha kuwa wewe na mpenzi wako mnakuwa na wakati wa kutosha kustarehe bila wasiwasi. Usiruhusu siri zako na mwanamke zitoke nje kati yenu.

 

Tenga muda wa kustarehe pamoja

Ili kudumisha mahusiano na mwanamke lazima kuwepo na mda wa kuwa pamoja na kufanya mambo yenu mnayoyataka kwa kuridhika bila kupungukiwa na muda. Kwa mfano ni muhimu kupumzika mapema kitandani ili kuhakikisha mnakuwa na wasaa wa kutosha wa kufanya mapenzi.

Ongeeni pamoja kwa uhuru kuhusu suala la tendo la ndoa

Ni muhimu kujadili na kukubaliana na mwanamke kuhusu swala la kufanya mapenzi. Ni vyema muongee kuhusu suala la mapenzi na jinsi ya kuwasha moto wa mapenzi baada ya kuchokana. Mwanamke anatakiwa apewe uhuru wa kusema kile anachokihitaji.

 

Pangeni miadi ya usiku

Mwanamke huridhika zaidi katika mapenzi kwa kuandaliwa ipasavyo hii ikiwa ni pamoja na kuwa na utayari wa kufanya mapenzi. Hivyo ni vyema kupanga miadi ya usiku ili mwanamke awe tayari na ili kumridhisha mwanamke.

Badilisha mazingira

Njia nyingine ya kuamsha mapenzi ni kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi. Kwa mfano mnaweza kuacha kitanda chenu cha nyumbani na kulala katika chumba cha hoteli iwapo uamuzi huo utaboresha mapenzi kati yenu.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Mchumba anayefaa kufunga naye ndoa

Maisha ya ndoa yanahitaji maandalizi mazuri, kama waswahili wasemavyo nyote njema huonekana asubuhi, asubuhi ya maisha ya ndoa ni kipindi cha uchumba. Ndugu zangu, kipindi cha uchumba ni lazima tukitumie vizuri na kwa makini na kila jambo, ukitambua hakuna jambo dogo wa kubwa, kila jambo uliangalie katika mapana yake na katika uzito wake.

Hivyo basi huyo anayetaka kuwa na wewe jiulize maswali haya juu yake;

1. Je anamtambua Mungu na kuishi maisa ya kumpendeza Mungu, katika matendo yake na maneno yake?
2. Je huyo mchumba wako yupo tayari kukusaidia wewe kufikia malengo yako katika maisha?
3. Je huyo mchumba wako anakuheshimu na kukusikiliza au mtu anayekudharau?
4. Je mchumba wako anakushirikisha kila jambo kuhusu maisha yake na pia kuwa na utayari wa kupokea mawazo yako?
5. Je mchumba wako ana mawasiliano na wewe kwa kiasi kikubwa na kukujulia hali mara kwa mara?
6. Je mchumba wako yupo tayari kujitoa kwa ajili yako kwa hali na mali ili kufikia malengo yenu ya pamoja?
7. Je unatambua mazuri na mapungufu ya mchumba wako, hasa tukitambua hakuna mtu ambaye ni mkamilifu na namna gani mnasaidiana katika madhaifu yenu
8. Je mchumba wako ni msikivu au ni mtu ambaye anapoamua jambo ndilo analotaka hawezi kukusikiliza wala kupokea mapendekezo yako?
9. Je mchumba wako ni mwaminifu na anajitunza kwa ajili yako wewe tu au ni mtu ambaye haeleweki heleweki?
10. Je mchumba wako yupo tayari kukusamehe unapomkosea au kuomba msamaha anapokosea, au ni mtu mbishi
Haya ni mambo machache ambayo ni lazima kuyatafakari kuhu mchumba wako kama anakufaa kuunga naye NDOA? Usikurupuke.

Ushauri wa ukweli Ili Uwe mwanaume wa Ukweli

1. Ukija kijiweni au pub au kwenye nyama choma acha zile stori za sijui umesoma wapi hadi wapi, sijui una madigirii mangapi. Piga stori nyingine, mbona ziko nyingi tu. Kujielezea sana shule yako ni ushamba fulani hivi, dizaini kama hujiamini so lazima ujivishe nyota. Unaboa.

2. Tembea na keshi mfukoni kama vipi, stori za kadi yangu ya benki imegoma sio ishu.

3. Punguza mambo yako ya kuvaa sana kipapaa. Sometimes ibuka na pensi na jinsi tu mwana.

4. Punguza kukesha nje mfululizo, iwe umeoa, una mpenzi au upo upo. Kikanuni kabisa usikae nje hadi usiku wa manane siku tatu mfululizo labda uwepo mchongo wa maana sana. I mean wa maana sana.

5. Epuka sana mchezo wa kujipiga tattoos. Kuna watu wamekosa wake au michongo hevi in life kisa hizo mambo.

6. Nasisitiza sana epuka kumtaka mpenzi wa zamani wa mshikaji wako. Pigia mstari hii pointi. Kwani lazima upite palepale? Tusiishi kikondoo bro.

7. Jiunge walau na mtandao mmoja wa kijamii. Keep in touch na washikaji. Kuna wana toka mmemaliza primary hamjachekiana, utawakuta mitandaoni. Unaweza kupata mchongo au kujifunza ishu mbili tatu, au kuwa fala zaidi ukiamua.

8. Maisha mafupi sana, jitahidi kupunguza kukunja ndita. Jiachie mara moja moja.

9. Ukifika baa uwe tayari unajua unakunywa nini. Sio Mhudumu anakuja kukusikiliza unawaaaaaza. Inaonyesha hujisomi na huna mipango. Samahani lakini.

10. Kama hujaalikwa kwenye ishu, usiende mwanangu. Sometimes hata ukialikwa usiende pia. Unaweza kualikwa ili useme no, kiushahidi tu.

11. Halafu tumechoka wewe kuwa kituko ukilewa. Kama pombe huziwezi ziache, piga juisi tu au maji wakati wana tunapiga monde, sio kesi, ni uwezo tu wa kuhimili.

12. Toa tip bila kuomba namba ya baamedi basi mwanangu. Jifanye kama umetoa tu msaada. Hata simba sio swala wote huwa anawala porini, wengine anawacheki anapita zake.

13. Punguza kutumia simu sana, tena wakati mwingine kwa ishu ambazo hazina mpango.
Ukumbuke juzi juzi hapa wataalamu wamesema simu zinaleta ugumba.

14. Nunua tumiwani twa jua twa bei bei hivi, inakupa mwonekano wa kijentlomani sometimes.

15. Piga push-ups walau 50, sit ups na dips kabla ya kuoga asubuhi, hii afya tumeazimwa tu, jiweke fit.

16. Toka out na washikaji zako at least mara moja kwa mwezi mpige msosi na kinywaji. Wife au demu wako na wanao waache home! Sio kila kona kila siku uko nao kama mkoba, kichwa kitatia kutu.

17. Julikana walau hata baa mbili tatu au sehemu mbili tatu. Baa, basketball ground, soccer ground, acha kujikunyata home. Wewe mtoto wa kiume man.

18. Jifanye mjuaji sometimes, then jifunze baadaye. Sio kila kitu wewe ni “I don’t know”.

19. Beer moja au glass moja ya wine baada ya mlo haiwezi kukuvurga, kama hutaki, kunywa majuisi yako basi ulete inzi, au misoda ujijazie magonjwa.

20. MTOTO WA KIUME HAPIGI SELFIE OVYO OVYO NA KUBINUA MIDOMO na KULAMBA LIPSI. PIGA SELFIE KWENYE ISHU MUHIMU. FAMILIA HIVI, DEMU MKALI, etc. Umenisoma?

21. Ukiweza miliki hata panga ghetto, maana bastola najua ngumu. Sio nyumba nzima huna hata kasilaha kadogo.

22. Ridhika. Hamna hata siku moja utakuwa na kila kitu. Jifunze kushukuru kwa ulicho nacho.

23. Sometimes agiza matunda badala ya chipsi.

24. Ukikutana na demu mzuri kiwanja yuko peke yake, muongeleshe.

25. Miliki walau suti moja kabla hujapitisha miaka 30 bro. Please. Na tupafyumu.

26. Kuwa na mpenzi moja
kwa wakati mmoja. Anatosha sana. Trust me.

27. Ukitaka kujilinganisha, jilinganishe wewe wa jana na wewe wa leo. Utafika mbali. Ukijilinganisha na wana utapasuka kichwa.

28. Piga picha nyingi kwa camera (again, sio selfies) tunza kumbukumbu.

29. Ukialikwa kwenye party usiende mikono mitupu. Nenda walau na kachupa kamoja ka mvinyo.

30. Date demu nje ya wale unaokutana nao club au baa mara wa mara. Utakuja kuniambia faida zake.

31. Huwezi kuwa mpenzi wa pombe au sigara kwa sababu hivyo vitu havitakaa vikupende.

32. Hata siku moja usirudiane na demu aliyekuacha kisa huna mkwanja. Kaenda kutafuta kakosa ndio maana kakurudia labda baada ya kuona umepata. Siku akikutana na mwenye chambi kukuzidi? Jibu kaa nalo.

33. Sometimes jitoe out mwenyewe, kaa mahali piga msosi wako na kinywaji chako, tafakari ishu zako. Alone.

34. Jisomee ukiwa na time. Inakupa chance kuazima ubongo wa mtu mwingine lakini pia inakupa matirio kwenye maongezi, ila stori za kuja kwenye joint na washikaji na kuanza kusema oh nimesoma kitabu hiki na kile kausha!

35. Puuza wanaozomea. Huwa wamekaa viti vile vya bei rahisi.

36. Hata siku moja usiseme “Ndo hivyo bwana, hamna namna tena”. Ipo namna bro.

37. Usi-bet kama ukipoteza buku 5 we ni mtu wa kulia lia kindezi.

38. Muombe na Mshukuru Mungu wako. Kama huna Mungu jishukuru mwenyewe, kiazi wewe.

39. Kumbuka, sheria hufuatwa na wajinga lakini huwaongoza wenye busara.

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Ushauri kwa vijana wenye miaka 22 nakuendelea

Ikiwa wewe ni kijana na Una umri wa kuanzia miaka 22 na Kuendelea
Soma hapa ujifunze maisha ya hekima na namna bora ya kuishi na kufanikiwa ungali kijana

1. Kama uko shule au chuo soma na usicheze ukifeli unajipotezea muda. Soma sana utafanikiwa…

2. Jifunze kuweka akiba ya pesa. Pia jifunze kuwa na matumizi mazuri ya pesa,bajeti vizuri na jiwekee akiba bank au popte unapoona panafaa.

3. Jitengenezee good character yaani tabia yako njema ili uwe tofauti na wengine.. Jitofautishe na wengine, uwe mfano bora

4. Jifunze kufanya kazi tofauti tofauti. Fanya hiki ama kile ili angalau uweze kuishi popote kwani dunia inabadilikaa na huwezi jua kesho yako

5. Anza kununua na kumiliki vitu kama kitanda godoro vyombo na ardhi au kiwanja. Kumbuka msingi mzuri wa maisha ni fikra za ujana na kujiwekea mali

6. Kama utaweza kapange ujifunze maisha. Anza kujitegemea ili kujipa confidenece na maisha.

7. Weka falsafa yako katika maisha na uiishi. Falsafa ni dira ya kukuongoza. Mfano unataka kumiliki nini katika maisha? Unataka mke au mume wa aina gani? Aina gani ya maisha unaipenda? Hiyo ndiyo falsafa…

8. Tengeneza mahusiano yaliyotulia na weka malengo. (Kwa wale wa ndoa) Jichagulie kijana au binti aliyemzuri katika wengi, kijana au binti wa moyo wako, mpende… Kipindi hiki ni cha kuwa na mwenza aliyetulia kama unafikiri kuoa au kuolewa. Ukicheza ukafikisha 30 bila kuwa na mtu maaalumu basi utaoa au kuolewa bora mradi ila siyo na mtu wa ndoto yako..

9. Kuwa na marafiki imara, jichagulie katika wengi marafiki kadhaa waliotulia wenye nidhamu ya maisha na wanaopenda uende mbele. Kijana chunga marafiki ulionao wengi leo wanajuta kwaa urafiki m’baya uliowapoteza… a

10. Kumbuka ibada na kumshukuru Mungu. Kipindi hiki ni cha misukosuko na mihemko mingi. Usiache mafundisho ya imani yako, usimsahau Mungu. Mshukuru Mungu kwa uhai na kila jema au baya likupatalo.

11. Jitume katika kazi, watu waliofanikiwa wanajua thamani ya juhudi na kujituma. Usikate tamaa hata kama unapata kidogo. Fanya kazi kama vile kesho haipo. Matunda utayaona

12. Zingatia kujiweka safi. Kuwa msafi na mtanashati huanza na ubongo, muonekano wako ndivyo watu watakavyo kuchukulia. Jiweke safi na jitunze..

13. Kula kwa afya, wengi wanachukia miili yao. Wanauchukia aidha unene au wembamba, ila ukila kwa afya, ukafanya mazoezi unatengeneza afya bora ya sasa na baaadae..

14. Vaa kwa heshima, usivae kama mcheza disko au teja. Kumbuka thamani yako kwa Mungu. Kwanini uvae nguo za machukizo mbele yake! Kwanini ukubali kuwa wakala na kutumiwa na shetani kuwaaangamiza wengine kwa kuvaa ovyo? Vaa kwa heshima..

15. Pendelea kusafiri maeneo tofauti na ujifunze! Asafiriye hupata maarifa na hujifunza mengi. Penda kusafiri, tembelea maeneo tofauti utakuwa na mengi ya kujifunza.

16. Kumbuka kupumzisha mwili. Kuishi kwetu kupo katika chembe ya uhai iliyopo mwilini. Upe mwili na ubongo chakula chake cha kupumzika. Nenda maeneo yatakayofanya mwili na akili vipumzike angalau kila baada ya miezi kadhaa..

17. Jifunze kuamua mwenyewe. Usisubiri kila kitu kumshirikisha mtu ndio uamue. Jifunze kuwa mwamuzi wa mambo yako mwenyewe haijalishi kwa gharama ipi. Watu wawe washauri ila ubaki kuwa mwamuzi mwenyewe.

18. Kuwa mtu wa kutunza siri. Jitahidi kuwa na shingo nzito na akili yenye kuweka siri. Usiwe mtu wa kusema kila uonacho au uambiwacho.

19. Jfunze na zitawale hisia zako. Hisia ziwe za hasira, mapenzi au ugomovi zitawale na utaishi miaka mingi. Asiye tawala hisia zake hata awe mkubwa bado ni mdogo…

20. Jitolee kwaajili ya wengine, fundisha kemea saidia. Unaweza kufundisha kupitia facebook wasap nk. Kemea ukiona mtu anafanya kitu kibaya, saidia wenye shida wakumbuke wagonjwa yatima wazee na wenye mahitaji. Wewe ni yatima, mzee, au muhitaji wa kesho.. Weka akiba ya wema

21 Jenga mazingira ya kuishi na watu vizuri. Usijione mzuri au HB sana ukadharau wengine. Ishi na kila mtu kwa upendo hata kama wanakuchukia..

22. Tunza muda, muda ni mali huwezi kuurudisha, kuusimamisha au kuuzuia. Ukishapotea ndio basi tena. Tambua thamani ya muda na fanya vitu kwa wakati..

23. Pendelea kusoma hasa vitabu vya dini, kuhusu mali, elimu, mchumba, afya, maisha, uongozi, hekima, busara, utu, uchaji, utii, maarifa, utajiri, heshima, uvumilivu, matumaini, upendo, na kila kitu vimo katika Biblia na Qur’an ..soma uchote hekimaa…

24. Acha kujifunza matumizi ya pombe, sigara , dawa za kulevya. Kama unatumia jitahidi uache, kama unajifunza acha na kama kuna mtu anakushawishi kataa. Afya ni mali na mtaji usichoshe na kuumiza uhai wako kwa pombe sigara na madawa ya kulevya…

Inafaa ukishare kwa wengine wajifunze maarifa haya..
*Maisha ni maamuzi yako wewe*
Kuamua kufanikiwa au kushindwa,
kuamua utajiri au umasikini yote ni mipango na hutokana na fikra zako..

Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa

Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara. Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.

2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia “Mimi ni mume wa mtu” au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, “wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao”

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
MBARIKIWE SANA WANAUME WOTE WENYE BUSARA..

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE ili uweze kuwafahamu zaidi wanawake

Jinsi ya kumjua mwanamke ambaye hajatulia a.k.a kicheche

Kumjua mwanamke ambaye hajatulia unaangalia mambo haya yafuatayo

Siyo rahisi kupenda

Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.

 

Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha

Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote

Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka. Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

 

Anamarafiki wakiume kwa manufaa

Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale. Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.

 

Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka

Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake. Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.

Unaweza kuwafahamu wanawake zaidi kupitia Kitabu hiki cha SIRI ZA WANAWAKE. Unaweza kudownload kitabu hiki moja kwa moja hapa

Mbinu 9 za kuwavutia na kuwateka wanawake kimapenzi

Kati ya wanawake na wanaume wote wawili wanahitaji kuvutiwa na wenza wao ili wadumu katika mahusiano. Kama mwanaume lazima upate wakati wa kujua unatakiwa kufanya nini kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua.
Hali kadhalika kama bado haupo Kwenye mahusiano kuna mambo ambayo ni ya msingi kufanya au kuwa nayo ili uweze kuwa na mvuto zaidi kwa wanawake.

Yafuatayo ni mambo yakufanya ili kumvutia mwanamke.

1. Kuonyesha kuwa unamjali

Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali wao kama wao, wanaojali kile wanachokifanya na watu wao wa karibu kama ndugu na wazazi. Wanapenda wanaume wanawaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa amjali mpenzi wake kwa kila hali. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Vile vile kuonyesha kujali mambo yake na watu wake wa karibu kunamvutia mwanamke.

2. Kuonyesha kuwa karibu na kupatikana unapohitajika

Mwanamke huvutiwa sana na mtu ambaye yupo karibu nae na ambaye anapatikana wakati anapohitajika. Kati ya vitu vinavyowapa wapendeza sana wanawake ni pamoja na kusogezwa karibu. Hapa ni kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku na kushiriki katika mambo yake hata kwa mawazo kama ukishindwa kwa matendo. Ni vizuri kuwa naye au kuwasiliana naye wakati wa kula, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie. Ni mambo madogo sana lakini yanayoongeza nakshi katika mapenzi na ambayo ni muhimu sana kwa wanawake. Yapo mengi sana ambayo kwa kuyafanya utakuwa umemsogeza mpenzi wako karibu yako, mfano kutembea pamoja, kuangalia movie pamoja, nakadhalika. Tumia ubunifu wako ili uweze kuteka hisia za mwenzi wako kisawasawa kwani mwanamke anavutiwa sana na mtu aliye karibu nae.

3. Kumsifia na kumuonyesha kuwa ni bora

Wanawake wanapenda kusifiwa na kuonekana kuwa bora. Mwanamke akisifiwa anahisi kupendwa kupita kiasi. Anajiona kamili, peke yake na mwenye nguvu kwako. Anajiamini na unamfanya azidi kukupenda kwa kuwa anaamini yupo na mwanaume ambaye anajivunia kuwa naye. Vilevile kumsifia mwanamke kwake ni njia ya kuonyesha upendo na Ishara ya kuonyesha kumjali kupita kiasi.

4. Kupewa kipaumbele

Mwanamke anavutiwa zaidi na mtu anayeonyesha kumpa kipaumbele na kupewa nafasi. Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mwanamke akawa katika hali hiyo, msikilize.
Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumani kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’.
Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kazini kwako au kifamilia, mshirikishe.
Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaendelea vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.

5. Usafi binafsi

Wanawake wanapenda mwanamme ambaye ni msafi, hii ni kwa sababu kiasili wamejaliwa kupenda usafi ndio maana ni nadra sana kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebuleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele.

6. Anavutiwa na mwanamme anayejiamini

Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini yaani mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia pale anapotakiwa kufanya hivyo au wakati wowote ule. Siyo anayebabaika na kuyumba yumba. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia nguo mpya.
Mwanamke anapenda kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba.
Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha.
Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwanamke hapendi mtu anayebadilikabadilika Kwenye maamuzi na misimamo yake.

7. Malengo ya maisha

Mwanamke anapenda mwanaume mwenye malengo na anayemshirikisha katika mipango yake. Mwanamke anavutiwa na mwanamke mwenye malengo katika maisha yake. Vilevile anapenda mtu anayemshirikisha katika malengo yake na kumuweka katika mipango yake. Faida ya kumshirikisha katika malengo yako ni pamoja na kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Msaidizi kamili wa nyumba yenu. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia.

8. Anayeweza kujitetea

Mwanamke hupenda mwanamme anayeweza kujitetea. Mwanaume aliye ‘fiti’ ni chaguo la wanawake wengi. Si mnyonge. Mpole kupitiliza na aliye tayari kuonewa! Huyu hana nafasi.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi. Hili si suala la kutetea tu haki yako pekee kama mwanaume, bali inapobidi kusimamia haki ya mwanamke wako. Nisieleweke vibaya katika hili, lakini mwanaume imara ni yule ambaye ana nguvu – anafanya mazoezi na ambaye yupo tayari kwa lolote! Inapowezekana, uwe na uwezo wa ‘kuzichapa’ ikiwa mtakutana na vibaka au watu wabaya wenye lengo wa kukudhuru/kuwadhuru au kumdhuru mpenzi wako.

9. Anayemtosheleza tendo la ndoa

Mwanamke anavutiwa zaidi na mwanamme anayeweza kumridhisha katika tendo la ndoa. Anataka mwanamme anayeweza kufanya kile anachotaka yeye na kile anachokipenda. Mwanamke hapendi mwanamme anayemkomoa katika tendo la ndoa au anayefanya mambo asiyoyapenda. Mwanamke anataka kuridhishwa na kujaliwa katika tendo la ndoa.

Ili kufahamu mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu wanawake, Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Maisha ya Wasichana Wa facebook na instagram

Wiki ya kwanza
Status:”Location flani amazing”
“Having fun”
“I love my life”
“sijali mnayosema nafanya nachotaka”

BAADA YA MIEZI MIWILI
STATUS:”Binadamu wengi ni wasaliti”
“trust nobody”
“Na hili nalo litapita”
BAADA YA MIEZI SITA
Status:”Yesu wewe ndio rafiki wa kweli”
“Bwana ndiye mchungaji wangu”
BAADA YA MIEZI TISA NA KIDOGO
STATUS: “Nakupenda mwanangu😅😅😀😆😆😆😂😂😂😂😄

Kama Mwanamme Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Angalia binadamu walivyo

Angalia Binadamu walivyo!,

“Ukitafuta sana anakuita MCHAWI,”

Ukifanikiwa sio BURE,

“Ukitulia MVIVU,”,

Usipovaa vizuri MCHAFU,

Ukidili sana na masomo unajifanya MSOMI,

Usipodili nayo MJINGA,

Ukisema sana MBEA,

Ukiwa mkimya JEURI,

Ukiwasaidia watu UNATAKA SIFA,

Usipowasaidia ROHO MBAYA,

Ukiwa na kazi UNAJISIKIA,

Usipokua nayo MZEMBE.

Hivyo BINADAMU ndivyo walivyo wewe jali MAISHA YAKO TU NA MAENDELEO YAKO.

MUNGU akulinde na shari zao.

Ushauri kwa mwanamke anayetafuta Mwanaume ili upate Mume sahihi

Siku zote mwanamke hawezi pata mwanaume aliye sahihi,,,.

1. Ukimpata handsome,,kichwa yake ni empty.

2. Ukimpata genius…yuko serious masaa 24 na wengi huwa hawako romantic , hawajipendi kihiivyo, wako rafu mno

3. Ukimpata tajiri…hawezi kukuheshimu full madharau, utamwambia nini wakati hela anayo bana.

4. Ukimpata mfanyakazi hodari na mtafutaji…hana muda wa kuwa na wewe..muda wote anawaza kazi na kutafuta maisha

5. Ukimpata mnyenyekevu…mfukoni huwa 0%.

6. Ukimpata anayekupenda kwa dhati…anakuwa siyo type yako..hana pozi zile unazitaka.

7. Ukimpata msomi..hasikilizi ushauri wako..anakuona Boya tu.

8. Ukimpata yule smart…ni muongo to the maximum… na player

So listen to your heart…❤❤, na shukuruni kwa kila jambo, toka anguko la Adam hakuna mtu perfect..hata wewe hauko perfect.
Kwa nini kulilia watu perfect??

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa uwezo wa kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake baada ya kuona kile anachokitaka hakipati kwa mpenzi wake.

 

Yafuatayo ni mambo ambayo wanawake wanapenda wanaume wayajue hata kabla ya kuambiwa;

1. Wanawake wanapenda ufuate anachokitaka

Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu. Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanya vile wanavyovipenda.

2. Hupendelea tendo la ndoa lidumu muda mrefu

Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda kuungana na wewe kihisia kupitia kushikana, kubusu nakadhalika. Wakati wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka. Kwa hiyo wanapenda tendo la ndoa lidumu lakini lisichoshe.

 

3. Wanataka mwanaume jasiri sio anayetumia nguvu

Wanawake wanataka wanaume walio jasiri wa kufanya nasio wanaotumia nguvu na ubabe. Wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu na mwisho kuwaumiza wapenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. Wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri kwamba sio kutumia nguvu na ubabe.

4. Wanawake hawafanani

Wanawake wanapenda wanaume wajue kuwa sio wanawake wote hupenda vitu sawa. Wanaume wengine hufikiri kuwa kwa sababu mpenzi wake wa zamani alikua anapenda kufanyiwa alikuwa basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta njia ya kukukwepa. Kwa hiyo mwanamme anatakiwa amjue mpenzi wake kibinafsi yeye kama yeye na sio kumjua kwa kumfananisha na wanawake wengine. Mwanamme amfanyie mpenzi wake kama anavyopendelea na sio kama anavyofikiri wanawake wanapendelea.

 

5. Kumfurahisha mwanamke sio ufundi tuu bali ni mapenzi

Wanawake wanapenda kuonyeshwa upendo au mapenzi ya dhati. Wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi na uzoefu katika haya mapenzi, ila wanasema hiyo sio kitu bora zaidi, wanachokitaka ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Mapenzi ni kichocheo kikubwa cha kumridhisha mwanamke.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa mojakirahisi kabisa kwenye simu yako.

Shopping Cart