Je, Kuangalia Picha za Ngono ni dhambi?

Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
β€œSitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya “AIBU” wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni.
Wanaume wamejikuta wakipiga punyeto (Mastubation) na Wanawake wakijisaga ( wanatumia mikono yao na viungo vyao vingine kama njia ya kujikidhi hali zao za tamaa mbaya waliloziamsha wao wenyewe). Haipaswi kamwe kuwa hivyo. Biblia inasema tusiyachochee wala kuyaamsha “mapenzi” mpaka yatakavyoona yenyewe (Wimbo ulio bora 2:7, 3:5). Naomba tufuatane pamoja kwenye somo hili muhimu sana ambalo litakuweka huru mbali na “utumwa wa fikra za kingono”

1. MAANA YA PICHA ZA NGONO

Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako. NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama. Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama. Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya “AIBU” katika nyumba zao (Warumi 1:24-28). PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na “uchafu” wa namna hiyo. Wahindi wao picha za ngono huziita “kachumbali” na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia “kachumbali” wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani. Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25). Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia “PICHA LIVE” ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba (2Samweli 11:2-27).
β€œIkawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?”………..
Kile kitendo cha Daudi “kuona” lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate “UKICHAA” wa muda ukajikuta umeng’ang’ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.

2. JE! KUANGALIA PICHA ZA NGONO NI DHAMBI?

Kuangalia picha za ngono “NI DHAMBI” kwa herufi kubwa. Katika Sheria ya Musa ilikuwa mtu anahesabika kuwa ametenda dhambi pale ambapo atakutwa akifanya kitendo hicho au kukiwa na mashahidi wawili au watatu atatakiwa kuhukumiwa sawasawa na Sheria husika. Kwenye dhambi ya uzinzi mtu alitakiwa apigwe mawe hadi afe sivyo kwa Sheria ya Kristo yenyewe inazungumzia juu ya kitendo cha “kutamani” tu unahesabika kuwa umefanyika DHAMBI (Mathayo 6:27-29, Waebrania 10:28). Tamaa mbaya ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Kwa kawaida tamaa huja na ile tamaa huchukua mimba na baadaye huzaa dhambi (Yakobo 1:13-16). Kitendo cha kuangalia picha za ngono hupofusha “FIKRA” nzuri za mtu alizonazo. Mawazo machafu uanza kutawala katika ubongo wako hadi “USHUSHE” huo mzigo ulioko kwenye viungo vyako vya uzazi. Ahaaa ni hatari aiseeee. Wewe unayengalia picha za ngono Kama ndiyo starehe yako unaiharibi nafsi yako “unakuwa zezeta wa akili” Biblia inasema “taa ya Mwili jicho na jicho lako likiwa safi mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu mwili wako wote utakuwa na giza..”(Mathayo 6:22-23). Kwa wale wanandoa ni “MWIKO” kutumia picha za ngono ili kunogesha kufanya Tendo la Ndoa. Wewe mume unaye hapo “chombo” unakiona “live” na kimethibitishwa na Mungu mwenyewe sasa hiyo mipicha ya nini? Kila kiungo Mungu alikiweka kwa ajili ya kusudi maalum kama ni mdomo kwa ajili ya kuongea na kupitisha chakula na si kunyonya sehemu za Siri za mwenzi wako. Mungu ameweka sehemu ya “haja kubwa” kwa ajili ya kutolea uchafu uliotengenezwa na tumbo na si kiungo kingine kiende kukoroga “zege” hilo huo ni uchafu(Ufunuo 22:10-15).
Warumi 1:26:27
β€œHivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”

3. JINSI YA KUSHINDA DHAMBI YA KUANGALIA PICHA ZA NGONO

PICHA ZA NGONO zinavutia sana kuziangalia ila zina maangamizo makubwa sana katika maisha yako. Lazima ufikie mahali kukata shauri ndani ya Moyo wako kuambatana na Mungu. Kusudi kubwa la shetani kuachilia mambo yake ya NGONO kwenye mitandao ili apate wafuasi wengi zaidi. Hakuna kitu unachoweza kukifanya katika simu za Android wengine wasikitambue. Kila unalolipitia na kuliangalia kwa Siri siku ya siku litaletwa hukumuni na Mungu mwenyewe (Warumi 2:16, Mhubiri 12:14)

USHAURI WAKIVITENDO:

I) Yatie Nuru macho yako – Zaburi 13:3, 19:8 – Yaruhusu macho yako yaingiziwe nuru na Yesu. Chukua muda wa kutosha kuingiza PICHA zinazomhusu Mungu zaidi. Angalia wahubiri mbalimbali.
II) Tazama mambo ya Adili(mema) – Zaburi 17:2-3 – Kuna nguvu kubwa sana tunapokuwa tunaangalia mambo mema. Vipindi vizuri vya neno la Mungu. PICHA zinazojenga siyo zinazoharibu fikra zetu.
III) Kumuomba Mungu afumbue macho yako – Zaburi 119:18, 146:8- Maombi ni muhimu ili kufanya macho yako kuona kusudi la Mungu na Kutambua uwepo wa shetani katika PICHA ZA NGONO.
IV) Weka maneno ya Mungu Mbele za macho yako – Mithali 4:20-21
Wakati wote soma neno la Mungu kupitia kifaa chochote cha ki-electronic ili uweze kumjua Mungu zaidi.
V) Macho yako yatazame Mbele – Mithali 4:25-27
Kutazama Mbele maana yake uwe na maono. Maono ni PICHA au TASWIRA ya Mbele ya maisha yako. Yeremia aliulizwa unaona nini naye akasema “anaona ufito wa mlozi” anaona kitu kizuri (Yeremia 1:11-12).
VI) Pendezwa na njia za Mungu – Mithali 23:26
Kuanzia sasa anza kupendezwa na njia za Mungu katika maisha yako. Acha kuzifuata njia zako katika kuufurahisha mwili wako wa PICHA zisizofaa.
VII) Tafuta watumishi wa Mungu ili wakufundishe – Isaya 48:17, 30:20-21
Kuna mambo ambayo yanatupa shida katika maisha yetu ni vizuri kuwaona waalimu ili watusaidie jinsi ya kutoka katika mtego huo.
VIII) Omba rehema na neema ya Yesu – Waebrania 4:16
Tunahitaji neema ya Mungu ili kushinda Hali hiyo ya kupenda KUANGALIA PICHA ZA NGONO na pia kufunguliwa kutoka katika vifungo hivyo vya pepo wa tamaa na mahaba.
Mungu atakubariki ukipeleka ujumbe huu kwa wengine

Kama una miaka 24 hadi 29 huu ni ujumbe wako, Soma hii tafadhali

ITAKUSAIDIA KIJANA PLEASE ISOME NA UITAFAKARI

SINTOFAHAMU MAISHANI KATI YA MIAKA 24 HADI 29
1. Umri mgumu zaidi katika maisha yako ni kati ya miaka 24 hadi 29 hivi. Presha ya kuwa mtu wa aina fulani au levo fulani ya maisha katika umri huo ni kubwa sana.

2. Kila ukitazama unaona watu wengine wanaishi vizuri sana, tena maisha unayoyatamani na wanayafurahia. Wewe unahisi kama unasukuma siku tu.

3. Umeomba kazi sehemu kibao lakini kila ukijibiwa ni jibu la kwamba umekosa na tena sehemu nyingine hata jibu hupati.

4. Bahati mbaya sana huu ndio muda au umri ambao wengi wanachanganyikiwa kabisa. Muda ambao kama mtu hana subira au umakini wa kutosha anajikuta katika ulevi wa kupindukia au madawa ya kulevya au kilevi chochote.

5. Kwa sababu kukata tamaa kunakuwa kwingi unajikuta unatafuta njia mbadala za kukimbia uhalisia. Unatafuta ulevi wako. Pombe! Madawa! Bangi! Kamari! Mwanamke!

6. Mbaya zaidi unakuta baadhi ya watu uliosoma nao wamepata bahati ya kupata kazi nzuri. Jinsi muda unavyoenda unahisi idadi ya marafiki zako inapungua –

7. Sio kwamba marafiki wanakutenga lakini wewe mwenyewe tu unaona bora ujitenge kwa namna hali ilivyo.

8. Hebu fikiria utafanya nini ukiwa katika WhatsApp group na marafiki zako wanajadili kuhusu safari ya kula starehe Zanzibar wiki ya wiki iliyopita

9. na hapo wanaendelea kujadili mipango ya kuchagua wikiendi fulani wakavinjari Ngorongoro au Serengeti na wake au wapenzi wao. Wewe utachangia nini wakati hata hujui mlo wako kesho utatoka wapi?

10. Mara nyingi unajikuta chat za kwenye group WhatsApp kama hizo unazisoma kimyakimya mwenyewe kama msalaba kwenye kaburi.

11. Kidogo kidogo unagundua hao watu na hili group la WhatsApp sio saizi yangu

12. kwa sababu kadiri unavyokaa karibu na group kama hilo au watu wa aina hiyo ndivyo jinsi ambavyo unazidi kupata au kujipa presha.

13. Si unajua zile stori za kwenye magroup ya WhatsApp za house party zikianza inabidi ujifanye bubu maana unawaza ikifika zamu yako hili kundi la watu 15 litaenea wapi katika chumba chako kimoja ulichopanga Sinza kwa Remi.

14. Ushawahi kukaa kwenye kundi la watu wanajadili iPhone mpya au jinsi ambavyo Fastjet wanatoa huduma mbovu?

15. hapo unasikia moyo wako unakwambia β€œkijana, huu ni ule muda wa maumivu ya moyo, huwezi kutafuta group ambalo wanajadili bodaboda?

16. Ila unabaki tu katika hilo group, unatulia kimya unatazama raia wanavyojadili maisha yao bora na wewe unakuwa kama secretary anavyoandika summary za vikao.

17. Unasahaulika kabisa kama kilema aliyesinzia kwenye daladala (huwa hadi wanapitishwa vituo)

18. Mara moja moja unakuta mmoja ya marafiki zako anakuuliza kama unahitaji bia nyingine

19. unawaza sijui niseme hapana niondoke zangu niende home? Ila unawaza tena home nikafanye ishu gani mida hii?

20. Unajikuta unajibu: β€œYes kaka, ngoja ninywe moja ya mwisho”. Mwongo!

21. Kosa kubwa unaloweza kufanya kipindi kama hiki bro ni kujaribu kuwa na mpenzi.

22. ukweli ni kwamba mtu ambaye anapitia nyakati kama hizi kwenye mapenzi ataleta tafrani tu. Mapenzi ni furaha na ili umpe mtu furaha lazima kwanza wewe mwenyewe uwe na furaha. Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna.

23. Huu ndo ule wakati ambao utaona wasichana ambao ungetamani kuwa nao wanatoka au wanaolewa na wanaume waliokuzidi umri zaidi ya miaka 10.

24. Halafu ndugu yangu huwezi hata kuwalaumu. Ni kwamba tu spidi ya maisha yako haiendani na malengo yao. So inabidi tu uelewe.

25. Wasichana wengi ambao utakuta nao muda kama huu tena kama una bahati sana wanaweza kukuvumilia mpaka utimize miaka 28 au 29,

26. na ukitimiza 29 maisha yako bado hayasomeki jiandae kuachwa.

27. Lakini katika umri huu unajifunza mengi sana kuhusu maisha.

28. Maisha yanakufunza mengi kuhusu uvumilivu, na kushukuru Mungu wako kwa kile unachopata kila siku,

29. yanakufundisha kitu kuhusu urafiki, mapenzi, kazi na kujitambua mwenyewe.

30. Huu daima ndio wakati wako wa kuamka au kuanguka moja kwa moja kwenye maisha kutegemea nini utaamua kufanya.

31. Namna utakavyoishi maisha yako kati ya miaka 30 hadi 39 na kuendelea itategemea sana namna ambavyo utayashinda maisha haya ya majaribu mengi kati ya miaka 24 hadi 29.

Never giv up….

πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ™ˆ

Mambo yanayoweza kusababisha sala au maombi yako yasijibiwe

Mara nyingi tumekua tukiomba lakini hatupati, sababu zinaweza zikawa hizi ;

1. Mawazo na matarajio yetu

Mara nyingi tunajifunga kwenye maombi yetu pale tunapoomba na kisha kuanza kuwaza “hivi Mungu atanipa kikubwa au kidogo au atanisaidia sana au kidogo” Au tunaomba halafu tunakua na matarajio tofauti na kile tunachoomba. Aidha tunatarajia kupata kidogo au kikubwa.
Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu kizuizi kwenye maombi yako. Yaani kumuongoza Mungu afanye kwa kiasi kile unachofikiri.

2. Kulenga kutizamwa na watu.

Hii ni kuomba kwa majivuno yaani kuomba ili ukishapata watu waone kuwa umepata.
Jambo hili linamchukiza Mungu ndio maana unapoomba kupewa kitu au kusaidiwa kitu Mungu hafanyi /hakupi. Na Mara nyingine hata vile ulivyonavyo unanyan’ganywa kwa kuwa hauombi kwa utukufu wa Mungu bali kwa utukufu wako.
Hali hii ni sawa na kumuwekea Mungu ukuta kwenye maisha yako.

Namna njema ya kuomba ni hii

1. Kutokuomba mambo makuu sana ambayo huna haja nayo na hayana maana katika maisha yako.
2. Kutokuomba mambo madogo kwa mawazo labda nikiomba makubwa Mungu hataweza
3. Kutokuomba kwa ajili ya kutaka kuonekana na watu.

Maana ya Kumuamini Mungu

Kumuamini Mungu ni kuwa na uhakika na uwepo na uwezo wa Mungu. Ni kutambua na kukubali kwa uhakika kuwa Mungu yupo na anaweza kutenda. Unaweza kuwa na Imani lakini ukakosa kuamini yaani unaamini kwa Mungu lakini huamini kama atakutendea.

Kuamini kunakua na sifa zifuatazo

1. Kutokuwa na mashaka kama Mungu atatenda au hatatenda

2. Kuwa na subira. Kusubiri Mungu atende wakati unaofaa

3. Kuwa na matumaini hata kama hujatendewa.

Mara nyingi watu wanakuwa na imani lakini hawaamini ndio maana wanashindwa kuelewa mapenzi ya Mungu, mipango na matendo yake.

Kuwa na Imani tuu bila Kuamini huwezi kuendelea mbele kiroho. Kukosa Kuamini ndiyo sababu inayokwamisha maendeleo ya kiroho kwa watu wenye imani.

Dalili za kukosa au kupungukiwa Kuamini ni kama ifuatavyo

1. Kutokuwa na uhakika kama sala zako zitajibiwa.

2. Kukosa subira na matumaini.

3. Kuwa na maswali kama, Hivi Mungu yupo na mimi au hayupo na mimi??. Kujiuliza Hivi Mungu amenisikia?, Ananikumbuka?, Atafanya kweli??

Kukosa Kuamini kukizidi kunaleta hali ya kuhisi kuwa Mungu yupo na anaweza kutenda chochote lakini hatendi. Utakua sasa unaanza Kujiuliza kwa nini. Mtu akifika katika hali hii, Imani huporomoka na kupotea Mara nyingine mtu hufikia Kukosa imani kabisa na Mungu japokuwa anajua yupo na anaweza.

Ili kuondokana na hali hii ya kuwa na Imani lakini unakua na Kukosa kuamini, jitahidi kusali /kuomba neema ya kuamini, Jitahidi kusoma Biblia itakujengea kuamini na pia omba ushauri kwa watu wenye imani na wanaoamini.

AHADI 15 ZA ROZARI TAKATIFU

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.

1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu
2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii
3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana
4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.
5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.
6. Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.
7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.
8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi
9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari
10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.
11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari
12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao
13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari takatifu watapata
waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.
14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO
15. Ibada kwa rozari takatifu ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

JE,SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili wakati fulani.Na jibu lake ni kama ifuayavyo:
Mtu anapouliza kila kitu kimeandikwa wapi katika Biblia ni kudhihirisha kutokuijua au kuielewa vizuri Biblia Takatifu na historia yake.Mtu anapong’ang’ania “nionyeshe kitu fulani kimeandikwa wapi kwenye Biblia”ni kutaka kujiona ya kwamba yeye anaielewa sana Biblia na ameisoma yote kwa hiyo kila kitu kilichopo kwenye Biblia anakifahamu kumbe haijui Biblia bali anakariri Biblia!
Na hili suala la kushupalia swala la kuoa linadhihirisha jinsi gani tulivyo kizazi cha zinaa,ni kama tunadhani kuwa UZIMA upo katika kujamiiana!La hasha.
Paulo anasema “Kwasababu ya zinaa ni bora kuoa na kuolewa”(1Wakorintho 7:2.9) haya sio maneno ya kufurahia na kuchekelea tu maana “YANAWALENGA WALE WALIOSHINDIKANA KATIKA YALE YAPENDEZAYO”(1Wakorintho 7:1.8)sasa ni lazima tujiulize je tumeshindikana kiasi hicho?,hiyo sio sifa!
1Wakorintho 7:1.8
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
Na Paulo Mtume anasema “Ni bora kuoa au kuolewa” lakini hakusema “Ni LAZIMA kuoa au kuolewa”
Suala la kutooa kwa mapadre kadiri ya historia lilianza tangu zamani kabisa mwanzoni mwa milenia ya pili katika mtagusi wa pili wa Laterani mwaka wa 1139 ili waweze kumtumikia Mungu kwa uhuru na bila mawaa wala pasipo vikwazo(1wakorintho 7:32-35)
1wakorintho 7:32-35
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
Maandiko hayo hapo juu yanajieleza wala sidhani kama yanahitaji kufafanuliwa zaidi ya yanavyojifafanua yenyewe.
Watu wengine wanafikiri kwamba kutooa ni dhambi,kama ni hivyo basi hata Yesu mwenyewe alikosa maana hata yeye mwenyewe hakuoa.
Yesu mwenyewe anafundisha kuhusu ubikira(Mathayo 19:10-12)
Mathayo 19:10-12,
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
Yesu mwenyewe analifafanua jambo hili kwa mapana,katika orodha ya matowashi Yesu aliowataja,Mapadre ni Matowashi waliojifanya hivyo kwaajili ya huduma ya kanisa na ufalme wa Mungu.
Tena Yesu anatuambia waziwazi kwamba”sio wote wawezao kulipokea neno hilo”yaani sasa sio wote wawezao kuwa Matowashi(Mapadre)bali ni wale tu waliojaliwa na Mungu neema hiyo.wale wasioweza kuishi upadre huoa na kuwa na familia.Tena Yesu anamalizia kwa kusema “Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee”,kwa maana nyingine ni kusema “Fundisho au Utowashi huu sio wa lazima”anayeweza kuishi maisha hayo basi na ayapokee na yule asiyeweza basi aache!
Vilevile Mitume ili kumfuata Yesu kikamilifu waliyaacha yote waliokuwa nayo ikiwepo familia zao ili wamtumikie Bwana(Mathayo 19:27.29)
Mathayo 19:27.29:
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
katika injili hiyo,Yesu anadhihirisha kwamba aliyeacha hayo yaliotajwa si kwasababu hawezi kuyapata la hasha,bali ameyaacha hayo yote KWAAJILI YA JINA LA YESU atapokea mengi hapa duniani halafu tena ataurithi ufalme wa mbinguni.
Mapadre wameyaacha hayo yote,wameacha nyumba,familia zao na kila kitu SIO KWASABABU HAWANA UWEZO AU HAWAWEZI KUPATA MAMBO HAYO bali WAMEACHA KWASABABU YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KADIRI YA MAANDIKO MATAKATIFU na kwakutaka kwao kuyaishi kimamilifu MASHAURI YA INJILI ikiwepo USEJA.
Maneno ya Paulo na yale ya Yesu mwenyewe kuhusu kumtumikia Mungu bila kuoa sio ya bahati mbaya bali ndiyo njia bora na inayofaa sana na kukubalika mbele ya Mungu.
Kwahiyo unapowaona mapadre hawaoi ujue sababu yake ni hiyo kwamba “Wamejitoa kwaajili ya kulihudumia kanisa”
(Na pia huwa nawashangaa mno watu wanaowapiga vita Mapadre kwamba kwanini hawaoi,najiuliza je,hao Mapadre wamewakataza wao kwamba wasioe?.)..na kama jibu ni hapana,sasa Je,”Pilipili ya shamba usiyoila inakuwashia nini?”
TUMSIFU YESU KRISTO!

Majivuno na Kujikweza Mbele ya Mungu

Rejea Luka 14:7-24 na Luka 18 :9-18
Mungu anakawaida ya kumkweza yoyote ajishushaye na kumshusha yule ajikwezaye. Vile unavyojiona bora mbele ya Mungu na mbele ya watu ndivyo na Mungu anatakavyokuonyesha kuwa wewe sio bora au wewe sio zaidi ya wengine.

Madhara ya Kujikweza au majivuno

1. Sala zako hazitajibiwa kwa kuwa mara zote nia ya sala zako zitakua ni za kujitakia makuu.
2. Kusahau nafasi ya Mungu katika maisha yako na kuhisi unajitosheleza kwa yote.
3.Kusahau nafasi na umuhimu wa wengine kwa kuhisi kuwa hawana thamani kama wewe.

Dalili za Kujikweza au majivuno

1.Kutaka au kupenda kuwa na nafasi ya kwanza kwenye kila kitu.
2. Kukosa uvumilivu
3. Kuwa na hofu ya kushindwa na kufedheheshwa
4.Kukosa upendo na kujali kwa wengine
5. Kupungua imani kwa Mungu. Yani kuhisi kama Mungu anaweza kufanya au hawezi.
6. Kupungua ukaribu wako kwa Mungu.
7.Kutokupenda kusali /kuomba Mungu.

Dawa ya majivuno au jinsi ya kujishusha

1.Kujifunza unyenyekevu.
2.Kujifunza upendo wa kweli kwa Mungu na wengine.
3. Jifunze kuwaombea wengine. Hii itasaidia kujenga unyenyekevu.
4. Kujifunza kuridhika
5. Jifunze kufurahia mafanikio ya wengine.
6. Usiwe muongeaji sana na mchunguzi wa mambo ya watu sana.

Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi

Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi ni kama Ifuatavyo;

Ibada

Ibada mara nyingi huusisha matendo ya kipekee. Ibada inaweza kuwa ya kuabudu, kusifu, kuomba toba na kushukuru

Mfano wa ibada ni, Ibada ya Ijumaa kuu, Ibada ya kuabudu sakramenti kuu

Sadaka

Ni majitoleo kwa Mungu kwa nia ya kuomba, kushukuru, zawadi au kutakasa.

Sadaka ninayoiongelea hapa ni sadaka tofauti na hela/pesa ambayo inapotolewa hupewa binadamu mwingine na sio Moja kwa moja kwa mlengwa (Mungu). Sadaka ninayoiongelea mimi ni sadaka mfano wa ile ya Kaini na Abeli, Mfano wa ile ya Ibrahimu, Mfano wa sadaka alizotoa Musa Jangwani. Naongelea sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya damu ya kuchinjwa.

Sadaka hii inatolewa knisani kwenye adhimisho la ibada ya misa takatifu pale padri anapotolea mkate na divai na kuigeuza kuwa mwili na damu ya kristu.

Kinachofanyika hapa ni matoleo ya sadaka ya mwili na damu ya Yesu aliyoitoa pale msalabani, Pale Mkate na divai vinapogeuzwa mwili na damu ya Yesu basi ni ishara ya Sadaka ya mwili na damu aliyoitoa Yesu.

Mfano wa sadaka ni inapofanyika mageuzi ya Ekaristi pekee bila kwenda na mtiririko wa Misa

Sala

Sala ni kuongea kwa sauti au kimya, kwa nia ya kuomba, kushukuru, kusifu au kutafakari.

Sala inaweza ikawa sala za maombi, shukrani, sifa au tafakari

Mfano wa sala ni, jumuiya za kikatoliki zinapokutana, Sala za kawaida za kila siku mfano Asubuhi, mchana, Jioni

Kumbuka: Sala sio maombi. Sala ni zaidi ya maombi. Sala inaweza ikawa tafakari, maombi, sifa au shukrani

Umuhimu wa Ibada ya misa ya kikatoliki

Ibada ya misa ya kikatoliki imechukua nafasi ya vyote hivi vitatu, sala/maombi, sadaka na ibada. Ukishiriki misa ya Katoliki ni sawa na umeshiriki Ibada, Sawa na umeshiriki maombi na ni Sawa na umeshiriki Sadaka.

Tofauti kati ya misa ya kikatoliki na ibada za madhehebu mengine

Madhehebu menginehayachukui yote mfano inaweza ikawa imefanyika ibada tuu, na maombi bila sadaka.

Kwa hiyo unapohudhuria na kushiriki ibada ambayo sio ya kikatoliki, unakua hujakamilisha misa bali ni ibada na maombi tuu. Unakua umekosa sadaka yani sadaka ya mwili na damu ya Kristu.

Ndiyo maana unatakiwa uudhurie Ibada ya Misa Takatifu ya Kikatoliki.

Tags: huusisha ibada ijumaa inaweza kati kipekee. kristu.. kuabudu kuomba kushukuru kusifu kuu kuwa mara matendo mfano na ni nyingi sadaka sakramenti sala/maombi toba tofauti tumsifu wa ya yesu.

Ahadi kumi na mbili za Moyo Mtakatfu wa Yesu

Bwana Yesu mwenyewe kwa kutumia kinywa cha Mtakatifu Margareta Maria Alakoki aliahidi Baraka na neema zifuatazo kwa wale wote watakaouheshimu Moyo wake Mtakatifu.

Na kwa maneno yake mwenyewe, Bwana Yesu aliahidi:

1. β€œNitawajalia neema zote watakazozihitaji katika hali yao ya maisha

2. Nitawajalia amani katika familia zao

3. Nitawafariji katika magumu yao yote

4. Nitakuwa kimbilio lao salama wakati wa maisha yao, na zaidi sana katika saa yao ya kufa

5. Nitawapa baraka tele katika shughuli zao zote

6. Wakosefu watapata katika Moyo wangu chanzo na bahari ya huruma isiyo na mwisho

7. Waumini walio vuguvugu watakuwa na bidii

8. Waumini wenye bidii watakwea kwa upesi katika ngazi za juu za ukamilifu

9. Nitabariki kila mahali ambapo picha au sanamu ya Moyo wangu Mtakatifu itawekwa na kuheshimiwa

10. Nitawajalia mapadre karama ya kuigusa mioyo migumu

11. Wale wote watakaoeneza Ibada hii kwa wengine majina yao yataandikwa ndani ya Moyo wangu na sitawasahau kamwe

12. Wale wote watakaopokea Sakramenti ya Ekaristi kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa miezi tisa mfululizo wakiwa katika hali ya neema ya utakaso, hawatakufa wakiwa na uadui nami, nitawapa neema ya kudumu katika uaminifu hadi mwisho na hawatakufa bila kupokea Sakramenti za mwisho”.

Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye

Kwa hiyo Mitume na wakristu wa mwanzoni hawakuwa kumuomba wakati akiwa hai. Ila Baada ya Kifo chake na kupalizwa kwake Mbinguni walianza ibada kwake.

Kumbuka, Kifo cha Bikira Maria hakijaandikwa kwenye biblia kwa kua wakati anakufa vitabu vya biblia vilikua vimekwishaandikwa

Ndio maana anaitwa Mama wa Wakristu. Mama mbarikiwa

Rejea Ufunuo 12:1-17

Mafundisho (Dogma) ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho

Mkingiwa Dhambi ya Asili

Malaika alimsalimia Maria β€œumejaa neema” (Lk 1:28) maana ndiye tunda bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi dhambi ya asili na madonda yanayotokana nayo, wala asitende dhambi maisha yake yote. Kwa maneno mengine, Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna bora kushinda viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita β€œA Panagia” = β€œMtakatifu tu”. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira Maria alijitambulisha kama Mkingiwa kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi (Ufaransa). Tena mwaka 1917 huko Fatima (Ureno) aliwafunulia Lusia, Fransisko na Yasinta Marto moyo wake safi usio na doa.

Mama wa Mungu

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, β€œHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi katika yote isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu: akisema, β€˜Mimi’, ni kwa Nafsi yake hiyo. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, β€œKweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo” (Yoh 8:50). β€œKama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, β€œWakati maalumu ulipotimia Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika. β€œMalaika alimwambia, β€˜Hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’” (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa Efeso uliomuita β€œMzazi wa Mungu”, ukisema Maria anastahili kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: β€œUmebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” (Lk 1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti likakamilishwa na Mtume Thoma aliyemuambia Yesu mfufuka: β€œBwana wangu na Mungu wangu!” (Yoh 20:28).

Bikira na Mama

Wakristo na Waislamu wote wanakiri kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango wa mwanamume. La ajabu zaidi katika imani hiyo ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili inasita, ni lazima kukiri na malaika, β€œHakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:38). Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa.
Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa β€œBikira daima” kwa sababu alimchukua mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa inajitokeza katika jibu alilompa malaika aliyemtabiria mimba: β€œLitakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Lk 1:35). Ni kielelezo cha Wakristo ambao Mtume Paulo aliwaandikia: β€œNawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2Kor 11:2), β€œmpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine” (1Kor 7:35).
Wanaosemwa katika Injili β€œndugu zake Yesu” si watoto wa Bikira Maria, bali ndugu wa ukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, Yesu angekuwa amefanya kosa la kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, β€œβ€˜Mwana, tazama Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo β€œndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na mama yao kwenye Injili anaitwa β€œMaria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. β€œWalikuwepo pia wanawake waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue kuwatofautisha kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira Maria kama β€œMama wa Yesu”.

Kupalizwa Mbinguni mwili na roho

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya mwanamke mshindi. β€œIshara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio lake yametimia: Mungu β€œamewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza” (Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale, yanavyoshuhudiwa na Mababu wa Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius XII kwa niaba ya maaskofu wote mwaka 1950.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Heshima za Liturujia kwa Bikira Maria

Kuna ibada za Mama Bikira Maria zinazoadhimishwa katika liturujia ya Kiroma. Hapa zimepangwa kulingana na heshima zinavyozidiana:
Sherehe
8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili 1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu 25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari 15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni

Sikukuu

31 Mei – Maamkio ya Bikira Maria 8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria

Kumbukumbu

Juni – Moyo Safi wa Maria 15 Septemba – Mama Yetu wa Huzuni 22 Agosti – Bikira Maria Malkia 7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari 21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni

Kumbukumbu za Hiari

11 Februari – Bikira Maria wa Lurdi 13 Mei – Bikira Maria wa Fatima 16 Julai – Bikira Maria wa Mlima Karmeli 5 Agosti – Kutabaruku Kanisa la Bikira Maria 12 Septemba – Jina takatifu la Maria 12 Desemba – Bikira Maria wa Guadalupe
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria: mashariki zinatumika tenzi na nyimbo mbalimbali, k.mf. Akatistos inayomuita β€œdaraja linalounganisha dunia na mbingu”, β€œngazi aliyoiona Yakobo” β€œkina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Mwa 28:12); magharibi]] anaheshimiwa kwa rozari.
Wakristo wanaomheshimu Bikira Maria hawamuabudu hata kidogo, lakini wanamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Tofauti ni kwamba Mungu tu anastahili kuabudiwa (kwa Kigiriki, β€˜latria’) watakatifu wanapewa heshima (β€˜dulia’) na Bikira Maria heshima zaidi (β€˜yuper-dulia’). Kanisa Katoliki linakiri neema zote za Mungu zinampitia Maria.

Jinsi Bikira Maria anavyoelezwa Katika dini ya Kiislamu

Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili.
Hata hivyo anapewa heshima ya pekee, kama inavyoonekana katika sura ya 3:43: β€œNa kumbukeni malaika waliposema, β€˜Ewe Mariamu, kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa walimwengu”. Tena katika aya 3:46: β€œNa kumbukeni waliposema malaika: β€˜Ewe Mariamu, bila shaka Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za Neno litokalo kwake, jina lake Masihi Isa mwana wa Mariamu, mwenye heshima katika dunia na ahera, na yu miongoni mwa waliokaribishwa’”.
Aliambiwa amefanywa β€œishara” pamoja na mwanae, ingawa haisemwi ni ishara ya nini. Sura ya 19, yenye jina lake, inaeleza kwamba Malaika Jibrili (Gabrieli) akimpasha habari ya mimba alisema, β€˜Hakika mimi ni mjumbe wa Mola wako ili nikupe mwana mtakatifu’. Akasema, β€˜Ninawezaje kupata mtoto hali hajanigusa mwanamume yeyote, wala mimi si mwasherati?’ Akasema, β€˜Ni kama hivyo; Mola wako amesema: Haya ni rahisi kwangu, na ili tukufanya ishara kwa mwanadamu na rehema itokayo kwetu, na ni jambo lililokwisha hukumiwa’ ” (19:19-21). β€œNa mwanamke yule aliyejilinda tupu yake na tukampulizia roho yetu na tukamfanya yeye na mwanawe ishara kwa walimwengu” (21:91).
Pamoja na kusifiwa kwa usafi wake, anaongezewa sifa za imani na unyenyekevu: β€œNa Mariamu binti Imrani aliyejilinda uchi wake, na tukampulizia humo Roho yetu na kayasadikisha maneno ya Mola wake, na vitabu vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu” (66:12).

Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria

Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.
Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).
Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).
Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, β€œWala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12).
Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.
Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, β€œNi mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, β€œMama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).
Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: β€œTazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).
Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, β€œMtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27).
Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.

Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia

Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): β€œNitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: β€œAdamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. β€œPenye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, β€œMama, tazama, mwanao”. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, β€œTazama, mama yako”. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).
Utabiri mwingine ulisema, β€œTazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, β€œMariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. β€œImba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: β€œMalaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, β€˜Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe’”. β€œUmebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, β€œAkapaza sauti kwa nguvu akasema, β€˜Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa’”.
Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, β€œHeri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa β€œchombo” tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, β€œMimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).

Bikira Maria katika maisha ya Yesu

Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: β€œBasi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).
Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, β€œSiku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, β€˜Hawana divai’. Yesu akamwambia, β€˜Mama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia’. Mamaye akawaambia watumishi, β€˜Lo lote atakalowaambia, fanyeni’. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, β€˜Jalizeni mabalasi maji’. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, β€˜Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza’. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, β€˜Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa’. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).
Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. β€œBasi, mtu mmoja akamwambia, β€˜Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, β€˜Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, β€˜Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yangu’” (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia β€œmwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, β€˜Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, β€˜Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).

Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu

Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, β€œTazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, β€œHivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).
Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, β€œMsalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoni”. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.
Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, β€œNa sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). β€œβ€¦ maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b).
Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.

Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu

Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. β€œHao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).
Yesu alisema, β€œNinayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, β€œKwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).

Biblia inavyothibitisha kuwa Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote

Ufunuo 12:17
17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo.
Kwa hiyo Bikira Maria ni Mama wa Wakritu wote yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo

Ukisoma kwa urefu inasomeka hivi

Ufunuo 12:1-18

1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. 2Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa. 3Kisha ishara nyingine ikaonekana mbinguni: Likaonekana joka kubwa jekundu lenye vichwa saba na pembe kumi na taji saba katika vichwa vyake. 4Mkia wake ukakokota theluthi ya nyota zote angani na kuziangusha katika nchi. Ndipo lile joka likasimama mbele ya yule mwanamke aliyekuwa karibu kuzaa ili lipate kumla huyo mtoto mara tu atakapozaliwa. 5Yule mwanamke akazaa mtoto mwanamume, atakayeyatawala mataifa yote kwa fimbo yake ya utawala ya chuma. Lakini huyo mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu kwenye kiti Chake cha enzi. 6Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku 1,260. 7 Basi palikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na hilo joka, nalo joka pamoja na malaika zake likapigana nao. 8Lakini joka na malaika zake wakashindwa na hapakuwa tena na nafasi kwa ajili yao mbinguni. 9Lile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwenguni wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. Ushindi 10Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema, β€œSasa Wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za Mungu usiku na mchana. 11Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa. 12Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo Shetani ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!’ 13Lile joka lilipoona kuwa limetupwa chini duniani, lilimfuatilia yule mwanamke aliyekuwa amezaa mtoto mwanamume. 14Lakini huyo mwanamke akapewa mabawa mawili ya tai mkubwa, kusudi aweze kuruka mpaka mahali palipotayarishwa kwa ajili yake huko nyikani, ambako atatunzwa kwa wakati na nyakati na nusu wakatia ambako yule joka hawezi kufika. 15Ndipo lile joka likamwaga maji kama mto kutoka kinywani mwake, ili kumfikia huyo mwanamke na kumkumba kama mafuriko. 16Lakini nchi ikamsaidia huyo mwanamke kwa kufungua kinywa na kuumeza huo mto ambao huyo joka alikuwa ameutoa kinywani mwake. 17Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke, likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari. 18Yule joka akajikita katika mchanga ulioko ufuoni mwa bahari.

Tunajifunza nini

Mwanamke ni Bikira Maria

Mwanamke aliyetukuzwa Uf 12:1

1 Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua na mwezi ukiwa chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake.

Anamzaa mtoto

Analindwa nyoka asimdhuru

Nyoka anapambana na wanawe

IShara ya joka kama Shetani

Akisubiri kuzaliwa kwa mtoto ili amdhuru kisha alishindwa na kutupwa duniani na kutaka kupambana na yule mwanamke Akashindwa na kuishia kupambana na watoto wa Yule mwanamke yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo Uf 12:17

Mtoto Aliyezaliwa mwenye mamlaka

Ambaye ndiye Yesu Kristu

Kwa hiyo, Bikira Maria Aliwezeshwa kumshinda Shetani na ni Mama wa Wakristu wote

Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;
  1. Kifo
  2. Hukumu
  3. Mbinguni
  4. Motoni
Mambo haya yote yanaweza kutokea wakati wowote bila kujua wala kutarajia

Kifo

Kifo ni kitu ambacho kinaweza kumpata mtu yeyote wa umri wowote awe mtoto kijana au mzee na kwa wakati wowote.
Maranyingi watu hawapendi kuongelea kuhusu kifo kwakua ni kitu ambacho kinampata kila mtu na hakipingiki wala hakina mjadala.

Hukumu

Baada ya kifo, inafuata hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake kama ulitenda mema utaenda mbinguni, na kama umetenda mabaya utaenda motoni.

Mbingu

Kama mtu akifa akiwa katika hali usafi wa moyo anaelekea mbinguni. Haijalishi ni kwa kipindi gani aliishi hivyo. Ila ni kwa hali gani kifo kilimkuta. Kwa sababu hii kila mtu anatakiwa aishi katika hali ya usafi wa moyo kwani hajui ni wakati gani atakutwa na kifo.

Motoni

Kama mtu akifa katika hali ya dhambi anaenda motoni. Kwa hiyo inatupasa tutumie vyema msamaa na huruma ya Mungu katika maisha yetu ili mwishi wetu uwe mzuri wakati bado tukiwa na muda.
Kila unapoishi ni lazima ufikirie mambo haya ukizingatia hujui wakati yanaweza kukupata. Kwa hiyo, nilazima uishi ukiwa unatafakari haya
ili uwe na mwisho mzuri.

Kwa nini Wakatoliki wanaungama dhambi kwa Padri?

KWANINI NYIE WAKATOLIKI MNAUNGAMA DHAMBI KWA PADRE AMBAYE NI MWANADAMU NA MDHAMBI BADALA YA KUUNGAMA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU?
Pengine umewahi kuulizwa swali hili au umewahi kujiuliza: hapa ni maelezo yatayokusaidia kuelewa sababu (japo sio zote) na uhalali wa jambo hilo.
Hapa tunaongozwa na maneno ya Bwana Yesu mwenyewe alipotoa amri hiyo kwa mitume wake akisema;
“Pokeeni Roho Mtakatifu.wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa na wowote mtakaowafungiwa dhambi wamefungiwa”(Yohane 20:22-23).
Na huo ndio utaratibu wetu tangu mwanzo wa kanisa wa mitume.
“Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana mpate kuponywa”(Yakobo 5:16a)
Ni miongoni mwa maagizo msingi kabisa ambayo hatuna mamlaka kuyabadili labda Yesu mwenyewe aliyeagiza hivyo aje mwenyewe kuyabadilisha.
Mungu anayesamehe dhambi ndiye aliyechagua njia ya kutoa msamaha huo,sisi tu nani tumpangie njia ya kutoa msamaha huo na kujipangia njia zetu?je tunamfundisha Mungu kazi?
Inashangaza siku hizi kusikia kwamba hata baadhi ya wakatoliki wameanguka katika mtego huu wa kutaka kubadilisha agizo hili la Yesu na inashangaza ni kwanini wanataka kurahisisha mambo kiasi hicho.
Mungu hafanyi kazi zake hewani bali huzifanya kupitia kwa watu wake.
Tunapoomba msamaha tunategemea kusikia maneno kama vile “nimekusamehe”,hutaka kuamini kwamba mtu akinyamaza au akiongea kimoyomoyo basi amekusamehe.
Yesu kwa kujua umuhimu na kazi ya neno hilo,alilitumia yeye mwenyewe akiwa binadamu(Luka 7:48).
Luka 7:48
“Naye Yesu akamwambia yule mwanamke,umesamehewa dhambi zako”
na alitaka aendelee kulitumia hata utimilifu wa dahari katika hali ya kibinadamu,ndio maana aliwaachia binadamu baada ya kifo chake ili waendeleze kazi hiyo.
Kuondolea watu dhambi ni moja ya utume wa Yesu(Marko 2:10),ni pamoja na kazi hiyo aliwaachia mitume wake(Yohane 20:23).
Tukilinganisha na mfano wa mtume Petro baada ya kumkana Bwana,tunaweza kujifunza kwamba tunapoongea na Mungu peke yetu ni katika hali ya toba na majuto(Luka 22:61-62).
Luka 22:61-62
“Bwana akageuka na kumtazama Petro,naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana ‘leo kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu’ hapo akatoka nje,akalia sana.”
Hivyo bado tunadaiwa kuungama iki kuondolewa dhambi zetu(Yohane 21:15-17)
Chakushangaza ni kwamba,Wakristo wote tunaamini kwamba Sakramenti ya ubatizo inatuondolea kabisa dhambi ya asili na dhambi zote zikizowahi kutendwa na yule anayebatizwa na kwa kawaida huwa hatujibatizi wenyewe wala hatubatizwi moja kwa moja na Mungu moja bali hubatizwa na wanadamu wenzetu.
Sasa kama huyu mwanadamu mwenzetu anatubatiza na anatuondolea dhambi ya asili na wote tunasadiki hivyo iweje tukija kwenye kitubio tunapinga ushiriki wa binadamu mwenzetu na wakati matokeo yanayotarajiwa katika sakramenti hizo ni yaleyale kama ya ubatizo.
Iweje aliyekubatiza na kukuondolea dhambi ya asili na ukaamini kwamba amekuondolea ashindwe au ushindwe kusadiki ushiriki wake katika kitubio?
Iweje akisema “Nakubatiza kwa JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU” hiyo iwe sahihi lakini akisema “Nakuondolea dhambi zako KWA JINA LA BABA NA LA MWANA NA LA ROHO MTAKATIFU” iwe sio sahihi?
Sasa huoni kama unajipinga na kujichanganya mwenyewe hapo?
Wapendwa,tuache kutafuta visingizio visivyo na ukweli kwaajili ya kutaka kupindisha ukweli.
Anayekuondolea dhambi ni Mungu mwenyewe kupitia kwa wapakwa mafuta wake yaani mapadre ambao amewaweka mwenyewe kwaajili ya huduma ya kanisa lake.
Wengine hudai pia kwamba ni watu wote waliopewa jukumu hilo na sio mapadre pekee,lakini ni vizuri kwanza kabla hujajitetea kwa msimamo huo dhaifu uchunguze tofauti iliyopo kati ya “Wanafunzi” na “wafuasi” kisha usome Biblia yako na kuona je jukumu hilo Yesu aliwatamkia wanafunzi wake au aliwatamkia wafuasi wake.
Wanafunzi wa Yesu ni wale kumi na wawili walioandamana naye.
Wafuasi ni wale makutano wengi waliokuwa wakimfuata kwaajili ya kusikiliza mafundisho yake.
Ikumbukwe kwamba Yesu hakusema mambo yote hadharani mbele ya makutano,baadhi ya maagizo msingi kama haya aliwachagua watu maalum kwaajili ya kuwapa kazi hizo na Biblia inasema aliwaita faragha peke yao na kuwapa maagizo hayo.

MITAGUSO MIKUU YA KANISA KATOLIKI

MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.

ORODHA YA MITAGUSO MIKUU

β€’ Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)
β€’ Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)

HISTORIA YA MITAGUSO MIKUU

Mitaguso mikuu ya kwanza ilifanyika hasa ili kubainisha katika mafundisho yaliyogongana yapi yanalingana na imani sahihi. Mwisho wake ulikuwa kutangaza dogma fulani na kutenga na Kanisa watakaokataa kuiamini na watakaofundisha tofauti.
Mitaguso iliyofanyika baada ya farakano la mwaka 1054 kati ya Kanisa la mashariki na la magharibi, pamoja na kulenga umoja uliovunjika na kufundisha dogma mpya, ilishughulikia zaidi urekebisho wa Kanisa katika ngazi na nyanja zote. Kwa namna ya pekee Mtaguso II wa Vatikano tangu uitishwe ulijulikana kuwa wa kichungaji, yaani usio na lengo la kufundisha dogma mpya wala kulaani mafundisho mengine.

Mtaguso I wa Nisea (325)

Mtaguso I wa Nisea ndio mtaguso wa kwanza kuitwa (tangu mwaka 338) mtaguso wa kiekumeni, yaani mtaguso wa dunia yote au mtaguso mkuu. Ndiyo sababu inashika nafasi ya pekee kati ya mitaguso yote.
Uliitishwa na kusimamiwa na kaisari Konstantino Mkuu, aliyehofia mabishano kati ya raia wake Wakristo kuhusu Yesu Kristo, ambayo yalihatarisha umoja na usalama wa Dola la Roma lililoanza kuelekea kusambaratika. Yeye aliwaalika maaskofu wote wa dola, waliokuwa kama 1000 mashariki na kama 800 magharibi. Washiriki walitokea hata nje ya dola hilo, kama vile Persia na Armenia. 2
Katika hali hiyo mtaguso ulianza tarehe 20 Mei 325; washiriki walikuwa kama 318, wengi wao wakitokea upande wa mashariki wa dola hilo. Upande wa magharibi uliwakilishwa na watu 4 kutoka Ulaya na 1 kutoka Afrika. Papa Silvesta I (314-335) aliwakilishwa na mapadri wawili.
Asili ya mabishano ilitokea katika Kanisa la Aleksandria (Misri), ambapo kasisi Arios alikuwa amekanusha umungu wa Yesu, na hivyo alihukumiwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 321, iliyoitishwa na askofu Aleksanda wa Aleksandria. Hata hivyo Arios hakuacha mafundisho yake, akakimbilia Palestina kwa rafiki yake Eusebio wa Nikomedia.
Basi, mtaguso ulikiri karibu kwa kauli moja kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu kwa maana ana ousìa (yaani dhati) ileile ya Kimungu aliyonayo Baba. Ndiyo kiini cha Kanuni ya imani ya Nisea iliyopitishwa na mtaguso.
Uamuzi mwingine wa mtaguso ulikuwa kupanga siku ya Pasaka, sherehe kuu ya Kanisa, iwe Jumapili inayofuata mbalamwezi ya kwanza ya majira ya Springi, tofauti na kalenda ya Kiyahudi. Pia zilitungwa kanuni 20 kuratibu mambo mbalimbali.
Mtaguso ulipomalizika tarehe 25 Julai 325, Konstantino alifikiri uamuzi juu ya dogma utamaliza mabishano, lakini haikuwa hivyo, kwa sababu Wagiriki wengi, ingawa hawakukubaliana na Arios, hawakuridhika na msamiati uliotumika kuelezea uhusiano wa Baba na Mwana.

Mtaguso I wa Konstantinopoli (381)

Mtaguso I wa Konstantinopoli ndio wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene yaliyofanyika wakati wa mababu wa Kanisa. Uliitishwa na kaisari Theodosius I ukafanyika Konstantinopoli mwaka 381.
Maaskofu 150 waliohudhuria walilaani aina mbalimbali za uzushi, hasa ule wa Masedoni wa Konstantinopoli aliyekanusha umungu wa Roho Mtakatifu, wakathibitisha maamuzi ya mtaguso mkuu wa kwanza (Mtaguso I wa Nisea), uliofanyika mwaka 325.
Hivyo walikiri kwamba Roho Mtakatifu pia, kama vile Yesu Mwana wa Mungu, anachanga dhati ileile ya Baba.
Pamoja na hayo, walikamilisha kanuni ya imani ya Nisea ambayo kwa sababu hiyo inaitwa sasa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli na ambayo inatumika sana hata leo katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, hasa katika liturujia.

Mtaguso wa Efeso (431)

Mtaguso wa Efeso unahesabiwa na Wakristo walio wengi kama mtaguso mkuu wa tatu. Ulifanyika Efeso katika mkoa wa Asia Ndogo, kwa amri ya kaisari Theodosi II; Papa Selestini I (422-432) alimteua Sirili wa Aleksandria kuuendesha; washiriki walikuwa zaidi ya 150 na kujadili vikali hasa uzushi wa Nestori wa Konstantinopoli.
Patriarki huyo alikuwa anasisitiza ubinadamu wa Yesu Kristo kuliko umungu wake, akisema Bikira Maria alimzaa mtu Yesu, si Mungu, wala si Neno wa Mungu aliyehifadhiwa ndani ya nafsi ya Kristo kama hekaluni. Kwa hiyo Kristo alikuwa Theophoros, yaani “mbeba Mungu”, na Maria Christotokos, “Mama wa Kristo” si Theotokos, “Mama wa Mungu”.
Mtaguso huo ulilaani haraka mafundisho hayo ukikiri kwamba nafsi ya Yesu Kristo ni moja tu, ile ya milele ya Mwana wa Mungu, na kwamba nafsi hiyo ilitwaa ubinadamu kamili wenye mwili na roho. Hivyo Maria ni Theotokos kwa kuwa alimzaa Mungu kama binadamu.
Wajumbe wa Papa walipofika walithibitisha uamuzi huo, lakini maaskofu kutoka Antiokia hawakuridhika, na uzushi huo uliendelea Mesopotamia na kuenea hata Asia mashariki.
Mtaguso ulitangaza kuwa Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ni kamili ukakataza isibadilishwe kwa namna yoyote. Pia ulilaani Upelaji, uzushi kutoka Ulaya magharibi kuhusu uwezo wa binadamu kutenda mema bila kusaidiwa na neema ya Mungu.

Mtaguso wa Kalsedonia (451)

Mtaguso wa Kalsedonia (leo katika nchi ya Uturuki) unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa nne kati ya mitaguso ya kiekumeni iliyofanyika katika historia ya Kanisa.
Mtaguso huo uliitishwa na kaisari Marcianus wa Dola la Roma Mashariki pamoja na mke wake Pulkeria wa Bizanti miaka 20 baada ya Mtaguso wa Efeso.
Hao waliona haja ya kudumisha umoja wa Wakristo, uliokuwa msingi wa uimara wa dola hilo, hasa wakati huo ambapo makabila yasiyo na ustaarabu kutoka Asia yalikuwa yanajaribu kuteka Ulaya.
Umoja huo uliingia hatari ya kuvunjika kutokana na uamuzi wa mtaguso mkuu wa Efeso kuhusu imani sahihi juu ya Yesu Kristo kutoeleweka kwa namna moja.
Hasa baadhi ya walioshinda mtaguso huo walionekana kusisitiza mno umungu wake hata kutia shaka kama wanaamini sawasawa ubinadamu wake.
Vikao vilianza tarehe 8 Oktoba 451 vikiwa na washiriki zaidi ya 350: mara nyingi inatajwa idadi ya 600 hivi. Hatimaye mafundisho ya Eutike na Dioskoro wa Aleksandria yalilaaniwa.
Ufanisi wa mtaguso ulichangiwa na msimamo wa kaisari Valentiniano III wa Dola la Roma Magharibi, binamu wa Pulkeria. Kaisari huyo alimuunga mkono Papa Leo I (440-461) aliyekuwa ametoa msimamo wake na wa Kanisa la Roma tangu mwaka 449 katika Tomus ad Flavianum, yaani Waraka kwa Flaviano, Patriarki wa Konstantinopoli aliyeuawa na wafuasi wa Eutike. 3
Ingawa msimamo huo wa kati ulikubaliwa na wengi, wengine waliuona ni kinyume cha uamuzi wa Efeso, hivyo walishikilia sana mtazamo hao hata walipodhulumiwa na serikali. Ndiyo asili ya farakano la Misri, Syria, Armenia n.k. linalodumu hata leo.
Mtaguso huo ulitunga pia kanuni mbalimbali, kama vile kwa kumpatia Patriarki wa Konstantinopoli nafasi ya pili kati ya maaskofu wote.

Mtaguso II wa Konstantinopoli (553)

Mtaguso II wa Konstantinopoli uliitishwa na kaisari Justiniani I mwaka 553 kwa lengo la kupatanisha tena na Kanisa Katoliki Wakristo wote wa Misri, Syria n.k. waliojitenga miaka 100 iliyopita kufuatana na Mtaguso wa Kalsedonia.
Kwa ajili hiyo kaisari huyo alifanya yalaaniwe maandishi ya Wanestori watatu (Teodoro wa Mopsuestia, Teodoreto wa Kiro na Iba wa Edesa) yaliyochukiwa sana na Wamisri.
Pia mtaguso mkuu huo ulilaani baadhi ya mafundisho wa Origene.
Walihudhuria maaskofu 168; kati yao 11 walitokea magharibi. Kumbe Papa Vigili (537-555) na maaskofu wengine 12 wa magharibi walikataa kuhudhuria ingawa walikuwepo Konstantinopoli, ila mwaka uliofuata alikubali maamuzi ya mtaguso.
Hatimaye Papa Gregori I (590-604) aliutambua kama mtaguso mkuu kwa sababu haukuharibu kitu. Hivyo Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa tano kati ya mitaguso ya kiekumeni, ingawa lengo halikufikiwa, kwa kuwa Wamisri waliendelea kukataa Mtaguso wa Kalsedonia.

Mtaguso III wa Konstantinopoli (680-681)

Mtaguso III wa Konstantinopoli unahesabiwa na Wakristo wengi kuwa wa sita kati ya Mitaguso ya kiekumeni.
Kaisari Konstantino IV wa Konstantinopoli ndiye aliyeuitisha na kuuendesha kuanzia tarehe 7 Novemba 680 hadi tarehe 16 Septemba 681.
Suala kuu lililosumbua Wakristo wa karne VII lilimhusu Yesu Kristo upande wa utashi. Ulikuwa unaenea mtazamo wa kwamba hakuwa na utashi wa kibinadamu, bali ule wa Kimungu tu.
Lakini wamonaki Sofronio wa Yerusalemu na Maksimo Muungamadini walipinga vikali jaribio hilo la kuleta upatanisho wa Waorthodoksi wa Mashariki (Wamisri n.k.) kwa kumpunguza Yesu katika ubinadamu wake kamili uliosisitizwa na Mtaguso wa Kalsedonia (451).
Vilevile Papa Martin I (649-655), katika mtaguso uliofanyika Laterani, alilaani mtazamo huo, kinyume cha Kaisari na Patriarki wa Konstantinopoli.
Konstantino IV alikubaliana na Papa Agatoni (678-681), na hivyo Mtaguso III wa Konstantinopoli ulilaani rasmi mtazamo wa kwamba Yesu hakuwa na utashi wa kibinadamu.

Mtaguso II wa Nisea (787)

Mtaguso II wa Nisea uliitishwa na malkia Irene wa Bizanti mwaka 787 ili kujadili matumizi ya sanamu katika Ukristo, kutokana na ombi la Papa Adrian I (772-795).
Wakristo wengi wanauhesabu kuwa wa saba kati ya Mitaguso ya kiekumeni. Ni wa mwisho kufanyika wakati wa mababu wa Kanisa.
Mtaguso mkuu huo ulihitajika ili kumaliza mabishano makali kuhusu sanamu za Kikristo yaliyochukua zaidi ya miaka 100 hasa katika Dola la Roma Mashariki yakimalizika mwaka 843 tu.
Chanzo ni uamuzi wa kaisari Leo III wa Konstantinopoli (717-741) wa kuteketeza sanamu zote ili kujilinganisha na Waislamu waliotishia utawala wake.
Patriarki wa Konstantinopoli alilazimika kujiuzulu, lakini uamuzi wa kaisari ulizidi kupingwa hasa na wamonaki na mwanateolojia Yohane wa Damasko. Mapapa wa Roma pia walipinga uamuzi huo.
Sera ya dola ilibadilika aliposhika uongozi Irene kwa niaba ya mtoto wake mdogo Konstantino VI.
Mtaguso ulianza Konstantinopoli mwaka 786, lakini ulipoingiliwa na jeshi waliowaunga mkono maaskofu wengi waliopinga sanamu, Irene aliuhamishia Nisea ambapo vilifanyika vikao 7 kuanzia tarehe 28 Septemba 787. Cha mwisho kilifanyika katika ikulu tarehe 23 Oktoba 787.
Pamoja na maaskofu 300 hivi wa dola hilo, walihudhuria wamonaki wengi. Papa alituma mabalozi wake wawili na barua moja.
Mtaguso ulitofautisha heshima inayokubalika kwa sanamu na ibada isiyovumilika. Hoja kuu ni kwamba sanamu si kitu, ila inamwakilisha yule aliyechorwa ndani yake. Kimsingi sanamu zinakubalika kutokana na umwilisho wa Mwana wa Mungu uliomfanya atwae sura na kuonekana.
Mtaguso ulichukua pia maamuzi mbalimbali ili kurekebisha Kanisa.

Mtaguso IV wa Konstantinopoli (869-870)

Mtaguso IV wa Konstantinopoli ni jina linalotumiwa na Wakristo kwa namna tofauti, kadiri wanavyokubali au kukataa uhalali na uekumeni wa mitaguso fulanifulani.
Kanisa Katoliki linahesabu kuwa Mtaguso Mkuu IV wa Konstantinopoli ule uliofanyika tangu tarehe 5 Oktoba 869 hadi 28 Februari 870.
Uliitishwa na Kaisari Basili I wa Konstantinopoli na Papa Adrian II (867-872), kwa sababu mwisho wa ikonoklastia katika sinodi ya mwaka 843 ulikuwa umeacha athari kubwa katika Kanisa la Mashariki. 4
Patriarki Metodi wa Konstantinopoli (843-847) alijitahidi kutuliza pande zote, lakini hakufaulu.
Alipofariki, malkia Teodora, akitawala kwa niaba ya mtoto Mikaeli III, alilazimisha nafasi yake ishikwe na Ignas I, mmonaki mwenye msimamo mkali, ambaye hatimaye aliondoshwa.
Badala yake alichaguliwa mlei msomi Fosyo ambaye kwa siku chache alipewa daraja na kutawazwa, lakini kufikia Februari 859 lililotea farakano kati ya waliomkubali yeye na waliomkubali Ignas I.
Ndipo Fosyo alipojitahidi kuungwa mkono na Papa Nikolaus I (858-867), ambaye kwanza alimkubali pamoja na pendekezo la Kaisari Mikaeli III la kuitisha mtaguso uliofanyika Konstantinopoli kati ya Aprili na Agosti 861 wakihudhuria maaskofu zaidi ya 300.
Papa hakupendezwa na maamuzi ya mtaguso huo, akashindana na Kaisari kimaandishi kwa sababu za kiutamaduni na za kisiasa pia.
Hapo Fosyo alipata nguvu dhidi ya Papa akaitisha mtaguso uliovunja umoja kati ya Makanisa ya Mashariki na yale ya Magharibi mwaka 867, akithubutu kwa mara ya kwanza kumhukumu Papa kama mzushi na kutaka kumuondoa madarakani.
Kumbe Kaisari mpya alimrudisha Ignas I kuwa Patriarki na pamoja naye akamuomba Papa atume mabalozi kwa mtaguso mwingine wa kufanyika Konstantinopoli.
Mtaguso ulipoanza tarehe 5 Oktoba 869 walikuwepo tu maaskofu wakuu 5 na maaskofu wengine 7, lakini walikuwepo mabalozi wa Mapatriarki wa Antiokia na Yerusalemu (wale wa Aleksandria walifika baadaye).
Waliokuwa upande wa Fosyo walikubaliwa kuhudhuria kuanzia tarehe 7 Oktoba wakamtetea sana dhidi ya msimamo wa Papa, lakini wakashindwa na kutengwa (29 Oktoba).
Baada ya miezi mitatu mtaguso uliendelea tarehe 12 Februari 870, wakiwepo maaskofu 67 walioongezeka tena hadi kufikia 103 siku ya mwisho (28 Februari), lilipotolewa tamko la imani pamoja na kanuni 26 kuhusu teolojia na sheria, bila kutoa mafundisho mapya. Pamoja na idadi yenyewe kutokuwa kubwa sana, ni muhimu kwamba walikuwepo maaskofu wakuu 37 kati ya 40.
Kwa kuwa mtaguso huu haukukubaliwa sana huko Konstantinopoli (hasa baada ya Fosyo kurudia Upatriarki mwaka 877), na pande mbili zilishindwa zaidi na zaidi kuelewana, uliitishwa mtaguso mwingine, ambapo wafuasi wa Fosyo walikuwa ndio wengi.
Baadhi ya Waorthodoksi wanahesabu mtaguso huo mpya (879-880), uliofuta maamuzi dhidi ya Fosyo, kuwa wa kiekumeni na kuukataa ule wa miaka 10 ya nyuma. Lakini wengine hawakubali kuwa wa kiekumeni kwa sababu haukutoa mafundisho ya imani.
Ingawa wajumbe wa Papa Yohane VIII (872-882) walikubali kwanza maamuzi wa mtaguso huo ili kudumisha amani, na labda hata yeye mwenyewe, waandamizi wake waliukataa, na Fosyo mwenyewe aliondoshwa tena mwaka 886.

Mtaguso I wa Laterano (1123)

Mtaguso I wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki mtaguso mkuu wa tisa katika historia yake, wa kwanza kufanyika Magharibi. Ulianza tarehe 18 Machi ukamalizika tarehe 11 Aprili 1123.
Mahali pake ni kwenye Kanisa Kuu la Roma (Italia) katika mtaa wa Laterano, alipokuwa anaishi askofu wake. Hukohuko baadaye ilifanyika mitaguso mingine minne ya Karne za Kati, halafu umuhimu wake ukapungua Papa alipohamia Vatikano.
Mtaguso uliitishwa na Papa Kalisti II (1119-1124) mnamo Desemba 1122, mara baada ya Mapatano ya Worms, ya kwanza kufanyika kati ya Papa na Dola Takatifu la Kirumi, iliyofurahisha sana wanakanisa, hata mwaka huo ulitajwa kuwa mwanzo wa kipindi kipya.
Mapatano hayo yalikomesha desturi ya walei kuteua viongozi wa Kanisa na wa utawa, yakitenganisha shughuli za kiserikali na zile za kidini, na kukubali kwamba mamlaka ya kiroho inatokana na daraja takatifu.
Ili kuthibitisha mapatano hayo, Papa alialika Roma maaskofu wote wa Magharibi. Waliohudhuria kweli walikuwa zaidi ya 900 kati ya maaskofu zaidi ya 300 na maabati 600 hivi). Papa mwenyewe aliendesha vikao.
Hakuna hati za mtaguso, ila matunda yake. Tunachojua ni kwamba Mapatano hayo yalisomwa yakapitishwa rasmi, pamoja na kanuni 22 au 25, ambazo nyingi zilikuwa zimeshapitishwa zamani.

Mtaguso II wa Laterano (1139)

Mtaguso II wa Laterano, uliofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 11 Aprili 1139 chini ya Papa Inosenti II (1130-1143), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi. Ni wa pili kufanyika Magharibi, kwenye Kanisa kuu la Roma (Italia).
Mtaguso ulihitajika kutokana na farakano lililotokea mwaka 1130 alipofariki Papa Honori II (1124-1130): hapo makardinali waligawanyika kuhusu Mapatano ya Worms, ambayo mwaka 1122 yalikuwa yamekomesha mashindano kuhusu uteuzi wa maaskofu.
Isitoshe, kulikuwa na ushindani kati ya koo mbili za Roma, yaani Frangipane na Pierleoni.
Tarehe 14 Februari 1130, makardinali 16 waliosimama upande wa familia ya Frangipane walimchagua Gregorio Papareschi, aliyejiita Papa Inosenti II. Saa chache baadaye, Pietro Pierleoni alichaguliwa na makardinali wengine na kujiita Anakleti II.
Hatimaye, kwa msaada wa Bernardo wa Clairvaux, Inosenti II alishinda na kukubaliwa na wengi, ingawa hakuweza kuhamia Roma mpaka baada ya mpinzani wake kufa (1138). 5
Mtaguso ulipaswa kurekebisha matokeo ya farakano hilo. Basi, Inosenti II alifungua kikao na kuondoa madarakani maaskofu waliomfuata mpinzani wake.
Halafu papa alikusudia kuendeleza juhudi za urekebisho za Mtaguso I wa Laterano. Hivyo zikapitishwa kanuni 30, ambazo nyingi kati yake zilikuwa za kurudia zile za zamani kuhusu usimoni, mapadri wenye wake n.k.

Mtaguso III wa Laterano (1179)

Mtaguso III wa Laterano uliitishwa na Papa Aleksanda III (1159-1181) ufanyike huko Roma mwaka 1179, kutokana na Amani ya Venezia kati ya Kaisari Federiko I wa Ujerumani na Lega Lombarda ya Italia kaskazini.
Unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na moja. Ulijadili masuala mbalimbali na kuyatungia kanuni. Kati ya maamuzi muhimu zaidi, mmojawapo ulihusu uchaguzi wa Papa, ukidai thuluthi mbili za kura za makardinali wote, bila kutofautisha haki za makundi yao matatu.

Mtaguso IV wa Laterano (1215)

Mtaguso IV wa Laterano unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na mbili.
Uliitishwa na Papa Inosenti III (1198-1216) kama kilele cha kazi yake.
Ulihudhuriwa na maaskofu zaidi ya 400 (wakiwemo mapatriarki wa Kilatini wa Konstantinopoli na Yerusalemu na wawakilishi wa wale wa Antiokia na Aleksandria), na wakuu wa watawa zaidi ya 800, mbali na mabalozi wa watawala wa nchi mbalimbali.
Mada kuu zilikuwa Vita vya msalaba, Mashindano kuhusu uteuzi wa viongozi wa Kanisa, mamlaka ya Papa, mwenendo wa makleri, mashirika ya kitawa, imani (kuhusu ekaristi n.k.) na wajibu wa Wakristo wote kupokea sakramenti ya kitubio walau mara moja kwa mwaka.
Kutokana na wingi na umuhimu wa mafundisho na maamuzi yaliyotolewa, mtaguso huo unahesabiwa kuwa kati ya ile iliyoathiri zaidi Kanisa hadi leo.

Mtaguso I wa Lyon (1245)

Mtaguso I wa Lyon uliitishwa na Papa Inosenti IV (1243-1254) tarehe 24 Juni 1245 akiwa huko Lyon (Ufaransa), alipokimbilia usalama. Waliushiriki karibu viongozi 150 wa Kanisa Katoliki, ambalo linauhesabu kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tatu.
Baada ya mashindano makali kati ya mamlaka ya kiroho ya Papa na ile ya kisiasa ya kaisari huko Ulaya, mtaguso huo uliitishwa ili kumhukumu moja kwa moja kaisari Federiko II kuwa Mpinga Kristo.
Mtaguso ulianza tarehe 28 Juni 1245 wakiwepo maaskofu 144, halafu ukawa na vikao viwili vingine tena tarehe 5 Julai na 17 Julai. Hatimaye maaskofu walikuwa 225.
Mwanzoni papa alitangaza matatizo 5 yanayotesa Kanisa:
β€’ kuharibika kwa imani na maadili;
β€’ kushindwa kuikomboa Nchi takatifu (Yerusalemu ulitekwa tena na Waturuki mwaka 1244);
β€’ kudumu kwa farakano la Waorthodoksi;
β€’ kujitokeza hatari ya kuvamiwa na Watartari;
β€’ kupambana na Federiko II.
Maamuzi yalitangazwa tarehe 25 Agosti tu, baada ya papa na wasaidizi wake kurekebisha miswada, yakapokewa na kufafanuliwa na vyuo vikuu. Lakini uamuzi wa kumuondoa madarakani kaisari haukuweza kutekelezwa hata kwa vita.

Mtaguso II wa Lyon (1274)

Mtaguso II wa Lyon unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na nne. Ulikusudiwa hasa kurudisha umoja kamili kati ya Wakatoliki na Waorthodoksi, uliotafutwa katika karne XIII yote.
Mnamo Februari 1274, katika ikulu ya Konstantinopoli, kaisari Mikaeli VIII ilifaulu kufanya maaskofu wengi wakiri ungamo la imani lililodaiwa na Papa Klementi IV (1265-1268).
Ndipo Papa Gregori X (1271-1276) alipoitisha mtaguso huko Lyon, ambao uhudhuriwe na wawakilishi wa Waorthodoksi ili kukamilisha umoja.
Papa Gregori X alifungua mtaguso tarehe 7 Mei 1274 akitangaza tena malengo yake matatu:
β€’ kusaidia Wakristo wa Nchi takatifu,
β€’ kuungana tena na Waorthodoksi,
β€’ kurekebisha maadili ndani ya Kanisa.
Vilifuata vikao viwili tarehe 18 Mei na 4 Juni. Halafu tarehe 24 Juni ulifika na kupokewa kwa shangwe ujumbe kutoka Ugiriki, ukiundwa na maaskofu 2 na katibu wa kaisari.
Tarehe 6 Julai kilifanyika kikao cha nne kwa ajili ya muungano na hatimaye tarehe 16 Julai kile cha mwisho kilichopitisha hati mbalimbali za urekebisho. Kesho yake mtaguso ulifungwa.
Muungano haukuweza kudumu, kwa sababu, alivyoandika Papa Paulo VI (1963-1978) tarehe 19 Oktoba 1974, ulifanyika Β«bila kulipatia Kanisa la Kigiriki nafasi ya kutokeza kwa hiari mtazamo wake kuhusu jambo hilo. Wakristo wa Kilatini ndio waliotunga hati na matamko kufuatana na mafundisho juu ya Kanisa yaliyofafanuliwa na kupangwa magharibiΒ». 6
Mikaeli VIII alijaribu kulazimisha raia zake wapokee mambo wasiyoyakubali kwa moyo, hata akatumia nguvu kuwadhulumu waliokataa; akilaumiwa na watu wa Roma kwa kushindwa kufanikisha muungano, akaja kutengwa na Kanisa. Alipokufa (1282), mwanae Androniko II aliyemrithi, alifuta maamuzi ya baba yake kwa ajili ya muungano.
Vilevile mipango kwa ajili ya vita vya msalaba haikutekelezwa, na hatimaye (1291) Waturuki waliteka Akri, mji wa mwisho kubaki mikononi mwa Wakristo huko Mashariki ya Kati.
Maamuzi mengine yalihusu utaratibu mpya wa kumchagua Papa kwa lengo la kuzuia uchelewaji uliojitokeza hapo nyuma, na katazo la mashirika mapya ya kitawa.

Mtaguso wa Vienne (1311-1312)

Mtaguso wa Vienne unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na tano.
Mtaguso huu ulifanyika Vienne (Ufaransa) baada ya mashindano kati ya Papa Bonifas VIII (1294-1303) na mfalme wa Ufaransa Filipo IV.
Hatimaye mwaka 1309 mwandamizi wake, Papa Klementi V (1305-1314) alikubali kubaki Avignon (leo nchini Ufaransa), karibu na himaya ya mfalme huyo.
Mapapa walibaki huko hadi mwaka 1377, waliporudi Roma.
Kwa shinikizo la mfalme, Papa alitoa hati Regnans in excelsis (12 Agosti 1308) ili kuitisha mtaguso mkuu huko Vienne tarehe 1 Novemba 1310, kwa lengo la kujadili mada 4:
β€’ suala la Wahekalu;
β€’ vita vya msalaba;
β€’ hali ya imani na Kanisa kwa jumla;
β€’ urekebisho wa Kanisa.
Mtaguso ulichelewa kuanza hadi tarehe 16 Oktoba 1311, walipokuwepo washiriki 170 hivi, ambao kati yao Wafaransa walikuwa zaidi ya thuluthi moja. Wengine walizuiwa na mfalme wa Ufaransa.
Vikao rasmi vikawa vitatu hadi Machi 1312.
Kuhusu Wahekalu, mtaguso uliamua kufuta shirika lao kama alivyopenda mfalme, bila kulifanyia utafiti wala kulitolea hukumu.
Kuhusu Vita vya Msalaba, uliamua kuvianza upya na kwa ajili hiyo kutoza zaka kwa miaka sita, lakini mfalme alijitwalia hizo pesa bila kutekeleza ahadi yake ya kuongoza vita hivyo.
Kuhusu imani, ulijadili baadhi ya mafundisho hasa ya makundi kadhaa ya watawa, lakini uamuzi ulichukuliwa baadaye tu.
Kuhusu urekebisho, ulidai haki za Kanisa ziheshimiwe na serikali za nchi. Pia ulijadili kirefu mahusiano ya ndani, hasa kati ya maaskofu, maparoko na watawa.

Mtaguso wa Konstanz (1414-1418)

Mtaguso wa Konstanz (Ujerumani) unahesabiwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa kumi na sita. Uliitishwa na antipapa Yohane XXIII kwa ombi la kaisari Sigismund wa Ujerumani ukathibitishwa na Papa Gregori XII (1406-1415).
Lengo kuu lilikuwa kumaliza Farakano la Magharibi lililofikia hatua ya kuona maaskofu watatu kujidai Papa kwa wakati mmoja. Malengo mengine yalikuwa kung’oa uzushi na kurekebisha Kanisa β€œkatika kichwa na viungo vyake”.
Hatimaye Papa Gregori XII alikubali kujiuzulu, wapinzani wake wawili waliondolewa, na Papa Martin V akachaguliwa.
Ulikuwa mtaguso muhimu kwa wingi wa waliohudhuria (makardinali 29, maaskofu 186, maabati zaidi ya 100 na wataalamu 300 hivi), muda (vikao 55) na mafanikio, ingawa majaribio yake ya mapinduzi yalishindikana, hasa ulipodai kuwa na mamlaka ya juu kuliko Papa.
Kati ya maamuzi mengine kuna hukumu dhidi ya John Wyclif na Jan Hus kama wazushi.

Mtaguso wa Firenze (1431-1445)

Mtaguso wa Firenze uliitishwa na Papa Martin V (1417-1431) mwaka wa mwisho wa uongozi wake ili kutekeleza shingo upande agizo la Mtaguso wa Konstanz la kwamba mtaguso ufanyike mara kwa mara.
Mtaguso ulianza Basel (Uswisi) chini ya Papa Eugenio IV (1431-1447), ukiwa na maaskofu wachache kulingana na mapadri na walei wenye haki ya kupiga kura.
Ingawa mtaguso ulifaulu kupatanisha wafuasi wa Hus na Kanisa, na kutoa sheria kadhaa za urekebisho kwa kibali cha Papa, baadaye ulianza kumshambulia yeye pamoja na makardinali, ukionyesha wazi wengi waliuona una mamlaka ya juu kuliko Papa, kinyume cha mapokeo.
Hapo Eugenio IV aliuvunja halafu akauhamishia Ferrara (Italia), ulipokutanika tarehe 8-1-1438, bila kujali upinzani wa wale ambao walibaki Basel na kumchagua antipapa wa mwisho, Felix V.
Huko Italia ulifika ujumbe mkubwa kutoka Konstantinopoli kwa ajili ya kurudisha umoja kati ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi. Kati ya wajumbe 700 kulikuwa na kaisari na patriarki wa Konstantinopoli, walioogopa Waturuki watateka mji wao (kama ilivyotokea kweli tarehe 29 Mei 1453); hivyo walihitaji msaada wa Wakristo wenzao wa magharibi.
Ferrara iliachwa kutokana na uhaba wa majengo na hofu ya tauni. 7
Mwaka 1439 mtaguso ulihamia Firenze ukafikia makubaliano ya kurudisha umoja (6-7-1439), ingawa uamuzi ukashindwa kutekelezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na upinzani wa waumini wa Konstantinopoli.
Vilevile tarehe 22-11-1439 yalifikiwa makubaliano na Waarmenia na tarehe 4-2-1440 yale na Wamisri.
Hatimaye tarehe 24-9-1443 mtaguso ulihamia Roma kwenye Laterano. Huko yalifikiwa makubaliano ya kurudisha umoja na Wasiria kadhaa (30-4-1444) na Wakaldayo na Wamaroni wa Kupro (7-8-1445).
Hakuna hati kuhusu mwisho wa mtaguso. Lakini waliobaki Basel na kujitenga na Papa, kufikia tarehe 19-4-1449 walimkubali Nikolaus V na siku sita baadaye walifunga mkutano wao.
Mtaguso huo ulichochea Wakristo wa magharibi kutamani mawasiliano na wenzao wa Ethiopia na India, jambo lililowafanya waanze zile safari za mbali kupitia baharini zilizowafikisha Afrika Kusini na Mashariki, China na Amerika.

Mtaguso V wa Laterano (1512-1517)

Mtaguso V wa Laterano ulifanyika kuanzia mwaka 1512 hadi 1517 huko Roma. Kanisa Katoliki linauhesabu kama mtaguso mkuu wa kumi na nane.
Uliitishwa na Papa Julius II (1503-1513) ambaye alianza kuusimamia tarehe 3 Mei 1512. Baada ya kifo chake, uliendelezwa na Papa Leo X (1513-1521) hadi kikao cha 12 na cha mwisho kilichofanyika tarehe 16 Machi 1517.
Ulihudhuriwa na maaskofu 100 hivi, wengi wao wakitokea Italia. Kutofika kwa wajumbe kutoka nchi nyingine, pamoja na wengi kukosa nia ya kujirekebisha, kulichangia kufanya utekelezaji wa maamuzi ya mtaguso ushindikane.
Maamuzi hayo yalitolewa kwa hati za Papa. Mengine yanahusu mafundisho ya imani, mengine maagizo ya urekebisho wa Kanisa.
Kabla yake kilifanyika “Kitaguso” cha Pisa: kwa kuwa Papa Julius II alikuwa hatekelezi kiapo chake cha kuitisha mtaguso kwa ajili ya urekebisho, baadhi ya makardinali, wakihimizwa na watawala wa Ujerumani na Ufaransa, waliuitisha huko Pisa (Italia) kuanzia tarehe 1 Septemba 1511. Walikusanyika wachache tarehe 1 Oktoba, halafu katika kikao cha nane walimsimamisha Papa wakahamia Lyon (Ufaransa).
Papa aliitikia β€œkitaguso” hicho kwa hati ya tarehe 18 Julai 1511, ambayo pamoja na kukipinga na kujitetea aliitisha mtaguso mkuu ukusanyike tarehe 19 Aprili 1512 huko Laterano.
Vita vilichelewesha mwanzo wa mtaguso wenyewe hadi tarehe 3 Mei 1512, walipokusanyika katika basilika la Laterano makardinali 15, mapatriarki 2, maaskofu wakuu 10, maaskofu 56, maabati na wakuu wa mashirika ya kitawa wachache pamoja na mabalozi wa nchi 3. Mwisho walikuwepo makardinali 23 na maaskofu 122.
Upande wa matokeo, utekelezaji wa maagizo ya mtaguso ulikuwa mdogo sana, la sivyo pengine Matengenezo ya Kiprotestanti yasingetokea. Ukweli ni kwamba Martin Luther aliyaanzisha miezi sita tu baada ya mtaguso kwisha.

Mtaguso wa Trento (1545-1563)

Mtaguso wa Trento (uliofanyika kwa kwikwi kuanzia mwaka 1545 hadi 1563), unahesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mtaguso mkuu wa kumi na tisa.
Mtaguso huo, uliochukua muda mrefu kuliko yote ya historia, ulieneza urekebisho wa Kanisa na kuchukua msimamo kuhusu mafundisho ya Waprotestanti waliojitokeza katika hiyo karne XVI.
Mtu wa kwanza kulilia mtaguso ambao uamue kati yake na papa alikuwa Martin Luther (1517): huko Ujerumani ombi lake liliungwa mkono na wengi, pamoja na kaisari Karolo V aliyeuona kuwa njia ya kurekebisha Kanisa lakini pia ya kujiimarisha kimamlaka. Ndiyo sababu kuu iliyomfanya Papa Klementi VII (1523-1534), aliyesimama upande wa Ufaransa, kukataa kabisa kuuitisha.
Wazo hilo lilipata nguvu tena chini ya mwandamizi wake, Papa Paulo III (1534-1549), ambaye mwaka 1536 aliitia kwanza Mantova halafu Vicenza maaskofu na maabati wote, pamoja na wafalme wadogo wengi wa Dola takatifu la Kijerumani.
Baada ya juhudi mbalimbali kushindikana, mwaka 1542 uamuzi ulifikiwa wa kuitisha mtaguso huko Trento kwa sababu ni mji wa Italia lakini ulikuwa ndani ya mipaka ya dola hilo. Hatimaye (Novemba 1544) papa aliweza kutoa hati ya kuitisha mtaguso inayoitwa Laetare Jerusalem.
Mtaguso ulifunguliwa rasmi tarehe 13 Desemba 1545 katika kanisa kuu la Mt. Vigilio.
Mwanzoni mtaguso ulikuwa na maaskofu wachache, karibu wote kutoka Italia, ukatawaliwa na wajumbe wa papa. Kati ya makardinali wapya (Contarini, Sadoleto, Carafa, Fisher na huyo Pole) wengi walipenda urekebisho.
Zilijadiliwa na kupitishwa hasa dogma dhidi ya mafundisho ya Waprotestanti, kama vile kuhusu utakaso na wokovu. Pamoja na kupitisha tafsiri rasmi ya Biblia katika Kilatini iliyo maarufu kwa jina la Vulgata, kati ya maamuzi muhimu zaidi upo ule wa kudai maaskofu waishi katika majimbo yao ili kufanya uchungaji uliowapasa.
Baada ya mtaguso kuhamishiwa Bologna, Papa Paulo III aliusimamisha mnamo Septemba 1549.
Papa Julius III (1550-1555) aliuitisha tena kuanzia tarehe 1 Mei 1551 na zikatolewa hati juu ya sakramenti za Ekaristi, Kitubio na Mpako wa wagonjwa. Polepole waliohudhuria waliongozeka, 8
wakiwemo Waprotestanti wengi pia, wakidai wanateolojia wao wawe na haki ya kupiga kura na hati zilizokwishatolewa zifutwe. Ndipo ilipoonekana wazi kwamba tofauti katika imani ni kubwa mno.
Majeshi ya Kiprotestanti yalipokaribia Trento, Papa alikubali kusimamisha tena mtaguso tarehe 28 Aprili 1552.
Sehemu ya mwisho ya mtaguso baada ya kuitishwa ilichelewa kuanza hadi tarehe 18 Januari 1562, tena ilikabili matatizo mengi, lakini iliokolewa na kutawaliwa na askofu wa Milano Karolo Borromeo, mpwa wa Papa Pius IV (1559-1565) aliyemalizia haraka mtaguso wakiwemo wajumbe 255.
Katika sehemu hiyo yalitolewa mafundisho rasmi kuhusu Misa, Daraja takatifu na Ndoa, Toharani, sala kwa watakatifu, heshima kwa masalia na rehema. Pia Kanisa la Roma lilikubaliwa kama mama na mwalimu wa makanisa yote. Maaskofu wote walitakiwa kuahidia utiifu kwa Papa, ambaye peke yake ana haki ya kuitisha mtaguso mkuu. Kwa msingi huo, mtaguso ulimuachia Papa kuthibitisha maamuzi yote, naye alifanya hivyo bila kujali upinzani wa maofisa wake huko Roma.
Isitoshe, mwishoni, maamuzi mbalimbali yaliachwa mikononi mwa Papa na ofisi zake, yakachukuliwa miaka iliyofuata; kati yake, urekebisho wa Breviari na Misale, kwa kusawazisha liturujia za majimbo ya magharibi (isipokuwa chache, kama ya Milano na Lyon) kulingana na mapokeo ya Roma. Halafu ikatolewa Katekisimu ya Trento na Orodha ya vitabu vilivyokatazwa (Index librorum prohibitorum).

Mtaguso I wa Vatikano (1869-1870)

Mtaguso I wa Vatikano unatazamwa na Kanisa Katoliki kama mtaguso mkuu wa ishirini katika historia yake.
Uliitishwa rasmi na Papa Pius IX (1846-1878) mnamo 29 Juni 1867 na vikao vyake viliendelea katika Basilika la Mt. Petro huko Vatikano mjini Roma kuanzia tarehe 8 Desemba 1869 hadi vilipokatika mnamo 1870, kutokana na jeshi la Italia kuteka Roma tarehe 20 Septemba.
Walishiriki maaskofu na mapadri 774 (kati ya 1050 wenye haki ya kuhudhuria), ambao kwa mara ya kwanza walitokea mabara yote. Pia ilikuwa mara ya kwanza ya kutokuwepo wawakilishi wa serikali. Kumbe wajumbe wa Waorthodoksi na wa Waprotestanti walialikwa pia, lakini hawakufika.
Tarehe 24 Aprili 1870, baada ya majadiliano mengi, ilipitishwa hati Dei Filius juu ya Mungu, ufunuo, imani, na uhusiano kati ya imani na akili.
Ingawa lengo halikuwa hilo, tokeo kuu la kazi ya mtaguso huo ni tangazo la dogma ya Papa kuwa na karama ya kutokosea katika mafundisho ya imani na maadili anayoyatoa ili yadumu moja kwa moja pale anapotimiza masharti fulani (kwa kifupi: akisema “ex cathedra”, yaani “kutoka ukulu).
Dogma hiyo iliimarisha mamlaka ya Papa na umoja wa Kanisa dhidi ya maelekeo ya kitaifa ambayo yalitawala karne zilizotangulia yakisababisha matatizo mengi.

Mtaguso II wa Vatikano (1962-1965)

Malengo ya Mtaguso II wa Vatikano

Muda mfupi baada ya kuchaguliwa Papa, mwenye heri Yohane XXIII alitangaza uamuzi wake wa kuitisha mtaguso mkuu akiamini kwamba utaweza kuandaa na kusababisha ustawi mpya wa maisha ya Kanisa. Lengo kuu la mtaguso lilikuwa kuliamsha Kanisa likumbuke wito wake na kwa kujifanya upya kwa ndani lipate msukumo mpya wa kimisionari ili kuwatangazia watu wote ujumbe wa milele wa wokovu, amani na umoja.
Tangazo hilo lilitolewa tarehe 25-1-1959. Baada ya maandalizi, Mtaguso II wa Vatikano ulifunguliwa tarehe 11-10-1962. Vikao vinne vikafanyika mpaka ulipofungwa tarehe 8-12-1965. Kila kikao kilianza Oktoba na kumalizika Desemba ya miaka hiyo.
Kwa kuwa Yohane XXIII alifariki tarehe 2-6-1963, vikao vitatu vya mwisho viliongozwa na mwandamizi wake, Paulo VI, na hati zote kumi na sita zikatolewa chini yake pia kwa kupigiwa kura ya ndiyo karibu kwa kauli moja. Maaskofu na wakuu wa mashirika kadhaa wenye haki ya kupiga kura walikuwa kama elfu tatu, wakiwakilisha karibu Kanisa lote duniani, isipokuwa nchi zile zenye kuwadhulumu Wakristo.

Mafundisho makubwa ya Yesu Kristo

Heri

Basi Yesu alipoona makutano, alipanda
mlimani akaketi chini, nao wanafunzi
wake wakamjia. 2Ndipo akaanza kuwafundisha,
akisema:
3 β€œWana heri walio masikini wa roho,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
4Wana heri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.
5Wana heri walio wapole,
maana hao watairithi nchi.
6Wana heri wenye njaa na kiu ya haki,
maana hao watatoshelezwa.
7Wana heri wenye huruma,
maana hao watapata rehema.
8Wana heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
9Wana heri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10Wana heri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana hao Ufalme wa Mbinguni ni wao.
11Mna heri ninyi watu watakapowashutumu
na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya
aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. 12Furahini
na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni
kuu.

Chumvi na Nuru

13β€˜β€˜Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini
chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje
kurudishiwa ladha yake tena ? Haifai tena kwa
kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na
watu.
14β€˜β€˜Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji
uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. 15Wala
watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli.
Badala yake, huiweka kwenye kinara chake,
nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani
ya ile nyumba. 16Vivyo hivyo, nuru yenu iangaze
mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu
mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kutimiza Sheria

17β€œMsidhani kwamba nimekuja kuondoa
Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.
18Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu
na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja
ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo
yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe
kimetimia. 19Kwa hiyo, ye yote atakayevunja
mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri
hizi, naye akawafundisha wengine kufanya
hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa
Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na
kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika
Ufalme ya Mbinguni. 20Kwa maana nawaambia,
haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria
na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika
Ufalme wa Mbinguni.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Hasira

21β€œMmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, β€˜Usiue, ye yote atakayeua
atapasiwa hukumu.’ 22Lakini mimi nawaambia
kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake
wa kiume au wa kike, atapasiwa hukumu. Tena,
ye yote atakayemwambia ndugu yake wa kiume
au wa kike, β€˜Raca’a, yaani kumdharau na
kumdhihaki, atapasiwa kufanyiwa baraza. Lakini
ye yote atakayesema β€˜We mpumbavu ulaaniwe!’
Atapasiwa hukumu ya moto wa jehanam.
23β€œKwa hiyo, kama unatoa sadaka yako
madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako
ana kitu dhidi yako, 24iache sadaka yako hapo
hapo, mbele ya madhabahu, uende kwanza
ukapatane na ndugu yako wa kiume au wa kike,
kisha urudi na ukatoe sadaka yako.
25β€œPatana na mshtaki wako upesi wakati
uwapo njiani pamoja naye kwenda
mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia
mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia
mikononi mwa walinzi, nawe ukatupwa
gerezani. 26Amin, nakuambia, hutatoka humo
mpaka umelipa hadi senti ya mwisho”

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Uzinzi

27β€œMmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Usizini’.
28Lakini mimi nawaambia: kwamba ye yote
amtazamaye mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29Jicho
lako la kuume likikufanya utende dhambi, ling’oe
ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam. 30Kama mkono wako
wa kuume ukikufanya utende dhambi, ukate
uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza
kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako
mzima utupwe jehanam.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Talaka

31β€˜β€˜Pia ilinenwa kwamba, β€˜Mtu ye yote
amwachaye mkewe na ampe hati ya talaka.’
32Lakini mimi nawaambia, ye yote amwachaye
mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati,
amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na ye yote
amwoaye yule mwanamke aliyeachwa azini.’’

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kuapa

33β€œTena mmesikia walivyoambiwa watu wa
zamani kwamba, β€˜Usiape kwa uongo, bali
timizeni, nadhiri zile ulizofanya kwa Bwana’
34Lakini mimi nawaambia,’’Msiape kabisa, ama
kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha
Mungu, 35au kwa nchi, kwa kuwa ndipo mahali
pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu,
kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36Nanyi
msiape kwa vichwa vyenu kwa kuwa hamwezi
kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe
au mweusi. 37β€˜Ndiyo,’ yenu iwe β€˜Ndiyo’ na
β€˜Hapana’, yenu iwe β€˜Hapana.’ Lo lote zaidi ya hili
latoka kwa yule mwovu.’’

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kulipiza Kisasi

38β€œMmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Jicho kwa
jicho na jino kwa jino.’ 39Lakini mimi nawaambia,
msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu
akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na
la pili pia, 40Kama mtu akitaka kukushtaki na
kuchukua shati lako, mwachie achukue na koti
pia. 41Kama mtu akikulazimisha kwenda
kilometa moja, nenda naye kilometa mbili.
42Mpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie
kisogo yeye atakaye kukukopa.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Upendo Kwa Adui

43β€˜β€˜Mmesikia kwamba ilinenwa, β€˜Mpende
jirani yako na umchukie adui yako.’ 44Lakini
mimi ninawaambia : Wapendeni adui zenu na
waombeeni wanaowatesa ninyi, 45ili mpate
kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa
maana Yeye huwaangazia jua lake watu waovu
na watu wema, naye huwanyeshea mvua
wenye haki na wasio haki. 46Kama mkiwapenda
wale wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani?
Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo?
47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je,
mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu
wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 48Kwa hiyo
iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni
alivyo mkamilifu.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwapa Wahitaji

β€˜β€˜Angalieni msitende wema wenu mbele ya
watu ili wawaone. Kwa maana mkifanya
hivyo, hamna thawabu kutoka kwa Baba yenu
aliye mbinguni.
2β€˜β€˜Hivyo mnapowapa wahitaji, msipige
panda mbele yenu kama wafanyavyo wanafiki
katika masinagogi na mitaani, ili wasifiwe na
watu. Amin, amin nawaambia wao wamekwisha
kupokea thawabu yao. 3Lakini ninyi mtoapo
sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa
kushoto usijue mkono wako wa kuume
unachofanya, 4ili sadaka yako iwe ni siri. Ndipo
Baba yako wa mbinguni, Yeye aonaye sirini
atakupa thawabu kwa wazi.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu kusali

5β€œNanyi msalipo, msiwe kama wanafiki,
maana wao hupenda kusali wakiwa
wamesimama katika masinagogi na kando ya
barabara ili waonekane na watu. Amin, amin
nawaambieni, wao wamekwisha kupata
thawabu yao. 6Lakini wewe unaposali, ingia
chumbani mwako, funga mlango na umwombe
Baba yako aliye sirini. Naye Baba yako aonaye
sirini atakupa thawabu yako. 7β€œNanyi mnaposali
msiseme maneno kama wafanyavyo watu
wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani
kwamba watasikiwa kwa sababu ya wingi wa
maneno yao. 8Msiwe kama wao, kwa sababu
Baba yenu anajua kile mnachohitaji kabla
hamjamwomba.’’
9β€˜β€˜Hivi basi, ndivyo iwapasavyo kuomba :
β€œBaba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
10Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa duniani
kama huko mbinguni.
11Utupatie leo riziki zetu za kila siku.
12Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tulivyokwisha
kuwasamehe wadeni wetu.
13 Usitutie majaribuni,
bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu,
kwa kuwa Ufalme ni Wako na nguvu
na utukufu hata milele. Amen.”
14Kwa kuwa kama mkiwasamehe watu wengine
wanapowakosea, Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe pia na ninyi. 15Lakini
msipowasamehe watu wengine makosa yao,
wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa
yenu.

Mafundisho ya Yesu Kuhusu Kufunga

16β€œMnapofunga, msiwe wenye huzuni kama
wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja
nyuso zao ili kuwaonyesha wengine kwamba
wamefunga. Amin, amin nawaambia wao
wamekwisha kupata thawabu yao kamilifu.
17Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani
na kunawa nyuso zenu 18ili kufunga kwenu
kusionekane na watu wengine ila Baba yenu
aliye sirini, naye Baba yenu aonaye sirini
atawapa thawabu yenu kwa wazi.”

Akiba Ya Mbinguni

19β€œMsijiwekee hazina duniani, mahali
ambapo nondo na kutu huharibu, nao wevi
huvunja na kuiba. 20Lakini jiwekeeni hazina
mbinguni, mahali ambapo nondo na kutu
haviharibu, wala wevi hawavunji na kuiba.
21Kwa sababu mahali akiba yako ilipo, hapo
ndipo pia moyo wako utakapokuwa.’’

Jicho Ni Taa Ya Mwili

22β€˜β€˜Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni
nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru.
23Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote
utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru
iliyomo ndani yako ikiwa giza, hilo ni giza kuu
namna gani ! ”

Mungu Na Mali

24β€˜β€˜Hakuna mtu ye yote awezaye
kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama
atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine,
au atashikamana sana na huyu na kumdharau
huyu mwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia
Mungu na malia.’’

Msiwe Na Wasiwasi

25β€˜β€˜Kwa hiyo nawaambia, msiwe na
wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au
mtakunywa nini, au kuhusu miili yenu, mtavaa
nini. Je, maisha si zaidi ya chakula na mwili
zaidi ya mavazi? 26Waangalieni ndege wa
angani, wao hawapandi wala hawavuni au
kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni
huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi
kuliko hao ndege? 27Ni nani miongoni mwenu
ambaye kwa kujitaabisha kwake aweza
kujiongezea hata saa moja zaidi katika maisha
yake au kuongeza dhiraa mojab kwenye kimo
chake ?
28β€˜β€˜Nanyi kwa nini kujitaabisha kwa ajili ya
mavazi? Fikirini maua ya shambani yameavyo.
Hayafanyi kazi wala hayafumi. 29Lakini
nawaambia, hata mfalme Solomoni katika fahari
yake yote hakuvikwa kama mojawapo ya hayo
maua. 30Lakini ikiwa Mungu anayavika hivi
majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho
yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri
zaidi, enyi wa imani haba? 31Kwa hiyo msiwe na
wasiwasi, mkisema, β€˜Tutakula nini?’ Au
β€˜Tutakunywa nini?’ Au β€˜Tutavaa nini?’ 32Kwa
maana watu wasiomjua Mungu ndio
wanaoshindania hayo, lakini Baba yenu wa
mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji hayo
yote. 33Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa
Mungu na haki yake na haya yote
mtaongezewa. 34Kwa hiyo msiwe na wasi wasi
kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajitaabikia
yenyewe. Yatosha kwa siku masumbufu yake.’’

Mafundisho ya Yesu kuhusu Kuwahukumu Wengine

β€œUsihukumu ili usije ukahukumiwa. 2Kwa
maana kwa jinsi ile unavyowahukumu
wengine, ndivyo utakavyohukumiwa na kwa
kipimo kile utakachotoa ndicho utakachopokea.
3β€˜β€˜Kwa nini unatazama kibanzi kidogo
kilichomo kwenye jicho la ndugu yako na wala
huoni boriti iliyoko kwenye jicho lako? 4Au
unawezaje kumwambia ndugu yako, β€˜Acha nitoe
kibanzi kwenye jicho lako wakati kuna boriti
kwenye jicho lako mwenyewe ?’ 5Ewe mnafiki,
toa kwanza boriti kwenye jicho lako mwenyewe,
nawe ndipo utakapoona wazi ili kuondoa kibanzi
kilichoko kwenye jicho la ndugu yako.
6β€˜β€˜Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu, wala
msitupie nguruwe lulu zenu. Kama mkifanya
hivyo, watazikanyaga kanyaga na kisha
watawageukia na kuwararua vipande vipande. ”

Omba, Tafuta, Bisha

7β€œOmbeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi
mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
8Kwa maana kila aombaye hupewa, naye
atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa
mlango.
9β€˜β€˜Au ni nani miongoni mwenu ambaye
mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe?
10Au mwanawe akimwomba samaki atampa
nyoka? 11Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua
jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi
sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu
vizuri wale wamwombao ? 12Kwa hiyo cho chote
ambacho mngetaka mtendewe na watu, ninyi
nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii
ndiyo Torati na Manabii.’’

Njia Nyembamba Na Njia Pana

13β€˜β€˜Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba,
kwa maana lango ni pana na njia ni pana
ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa
kupitia lango hilo. 14Lakini mlango ni
mwembamba na njia ni finyo ielekayo kwenye
uzima, nao ni wachache tu waionao.’’

Mti na Tunda lake

15β€œJihadharini na manabii wa uongo,
wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya
kondoo, lakini ndani wao ni mbwa mwitu
wakali.16Mtawatambua kwa matunda yao. Je,
watu huchuma zabibu kwenye miiba au tini
kwenye michongoma? 17Vivyo hivyo, mti
mwema huzaa matunda mazuri na mti mbaya
huzaa matunda mabaya. 18Mti mwema hauwezi
kuzaa matunda mabaya wala mti mbaya
hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19Kila mti
usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa
motoni. 20Hivyo, kwa matunda yao,
mtawatambua.’

Mwanafunzi Wa Kweli

21β€œSi kila mtu aniambiaye, β€˜Bwana, Bwana,’
atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni
yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye
mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile,
β€˜Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako
na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza
mingi? 23Ndipo nitakapowaambia wazi,
`’Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi
watenda maovu!’

Msikiaji Na Mtendaji

24β€˜β€˜Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya
maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu
mwenye busara aliyejenga nyumba yake
kwenye mwamba. 25Mvua ikanyesha, mafuriko
yakaja na upepo ukavuma ukaipiga hiyo
nyumba, lakini haikuanguka kwa sababu msingi
wake ulikuwa kwenye mwamba. 26Naye kila
anayesikia haya maneno yangu wala
asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga
nyumba yake kwenye mchanga. 27Mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo
ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo
ikaanguka kwa kishindo kikubwa.’’
28Yesu alipomaliza kusema maneno haya,
makutano ya watu wakashangazwa sana na
mafundisho yake, 29kwa sababu alifundisha
kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama
walimu wao wa sheria.

Zaburi ya Toba, Zaburi ya 51

Hii ndiyo Sala ya Toba
Zaburi 51
1 Ee Mungu, unirehemu,Sawasawa na fadhili zako.Kiasi cha wingi wa rehema zako,Uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa na uovu wangu,Unitakase dhambi zangu.
3 Maana nimejua mimi makosa yanguNa dhambi yangu i mbele yangu daima.
4 Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,Na kufanya maovu mbele za macho yako.Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,Na kuwa safi utoapo hukumu.
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6 Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7 Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe,Mifupa uliyoiponda ifurahi.
9 Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;Uzifute hatia zangu zote.
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
11 Usinitenge na uso wako,Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako;Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13 Nitawafundisha wakosaji njia zako,Na wenye dhambi watarejea kwako.
14 Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,Uniponye na damu za watu,Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
15 Ee Bwana, uifumbue midomo yangu,Na kinywa changu kitazinena sifa zako.
16 Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
17 Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;Moyo uliovunjika na kupondeka,Ee Mungu, hutaudharau.
18 Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,Uzijenge kuta za Yerusalemu.
19 Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,Na sadaka za kuteketezwa, na kafara.Ndipo watakapotoa ng’ombeJuu ya madhabahu yako.
Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About