Ujumbe kwa leo

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata…Kama umezungukwa na watu BASIC…
Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU..Fulani kamegwa na yule..halafu yule naniliu saivi anatembea na yule ex wa nanii…Asubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLE…Hawa ndio watu BASIC…Hata siku 1 hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHERE…NEVER

Na ukionekana unaanza kufanya vitu EPIC watakugeuka kwamba UNARINGA.. UNAJISIKIA.. UMEWATENGA…UNAJIDAI UNA HELA…and lots of bullshit…
Pengine ulipaswa kuwa mbaaalii kibiashara lakini HUWEZI coz umezungukwa n Mbaazi tupu…BASIC PEOPLE…Ukiwaambia umesikia Kiwanja kinauzwa Kigamboni wanakwambia Kigamboni watu wanatapeliwa kuna mradi wa Joji Bushi…Ukiwambia unataka kujiunga Forever Living wanakwambia UNALIWA HELA…Ukiwaambia kuna SACCOSS wanatoa mikopo unataka uchukue ujenge wanakwambia INTEREST ZAKE UTASHINDWA na kujenga sio mchezo shosti..Unaamini unaacha!…Nataka kufanya Kitu flani WANAKUKATISHA TAMAA
Unahitaji kuzungukwa na watu wenye POSITIVE ENERGY ambao ukiwambia unataka kwenda Mbinguni kwa kupitia Mkuranga wanakuchangia Nauli…Niliposema naacha kazi watu ohh utakula nini..utaishije…Mji Mgumu huu..Wenzio wanatafuta kazi we unaacha utalosti…WHO SAID??Nadunda kama kawa..NEGATIVE PEOPLE WILL BRING U DOWN….Ukitaka Kupaa kaa karibu na ndege…We unataka kupaa unakuwa rafiki wa Nyangumi…UNAZAMISHWA SASA HIVI!!
Tangu nianze kukaa na watu Positive I have changed a lot…Nikiwaza jambo wanauliza HOW DO WE ACHIEVE THIS na sio FULANI ALIWAHIFANYA HII AKAFELI..
Ikikusaidia Chukua..
KILL ALL NEGATIVE PEOPLE AROUND YOU kama unataka kufikia Malengo Makubwa, I will be ur Lawyer at the Court na mwambie Hakimu nilikutuma mimi!
TIME TO DELETE ALL BASIC PEOPLE who wait of option😜😜😉😉

Ushauri wangu kwa leo

Kuna watu wengi sana huwa wanani-challenge ninaposema kwamba ni muhimu sana mtu kuishi katika kusudi la maisha yake. Na moja kati ya hoja zao ni kwamba haya maisha ya sasa mtu akisema aanze kutafuta kusudi la maisha yake atakufa maskini. Hivyo wanaonelea ni bora kufanya chochote kitakachotokea mbele yake ilimradi mwisho wa siku anapata pesa. Yaani anachagua kuwa mtumwa wa Pesa

Kusudi la maisha ya mtu huwa halina ukomo na halibadiliki, kinachobadilika au kufikia ukomo ni malengo ya kuli-ishi kusudi hilo. Kwa hiyo unapopanga malengo yako au unapokuwa na ndoto zako ni lazima uweze kupambanua mwisho wa siku hizo ndoto au hayo malengo yanakwenda kukidhi kiu ya aina gani inayofukuta ndani yako.

Ukifanikiwa kulitambua kusudi la maisha yako na ukafanikiwa kuli-ishi kwa vitendo, ni dhahiri utakuwa maarufu kwenye mazingira yanayohusiana na maisha yako. Mazingira yanayohusiana na maisha yako yapo ndani ya kusudi la maisha yako.

Ni wakati gani mtu anaweza kusema amefanikiwa katika maisha yake? Ni pale ambapo tu mtu anapoweza kutatua tatizo fulani katika jamii; Kugundua uhitaji wa kutimizwa au kukamilishwa kwa jambo fulani katika jamii. Ukiweza kuziba pengo fulani. Ukiweza kupata ufumbuzi wa kukamilishwa kwa hilo jambo kwa faida ya jamii fulani au niseme ukiweza kutatua tatizo hilo hapo unaweza kusema umefanikiwa. Huwezi kutatua tatizo lolote katika jamii kama hujawekeza ndani yako.

Haijalishi ni jambo gani unafanya katika jamii na liko kwenye kiwango kipi ilimradi liko ndani ya mstari wa maisha yako. Kwa mfano, una kamtaji kadogo na unaamua kuanzisha genge la kuuza mahitaji madogo madogo ya nyumbani (hasa jikoni) naamini unakuwa umeanzisha kwa sababu umeona eneo hilo kuna uhitaji wa aina hiyo ya huduma. Wewe unaweza kuwa unafanya tu labda kwa sababu ya shida fulani za maisha lakini wakati huo huo moyo wako unafurahia kile unachokifanya na unajikuta kila siku unabuni mbinu mpya na mikakati wa kuboresha genge lako. Kidogo kidogo unafungua genge lingine sehemu nyingine, na lingine na lingine, nk. Mwishowe unajikuta unatamani kuwa na duka kubwa la vyakula na mahitaji mengine ya kila siku au supermarket. Ukijiona unang’ang’ana kwenye “line” moja ya shughuli (Biashara) basi tambua hilo ndio kusudi lako na ndani yako una zawadi kubwa sana ya kutoka kwa Mungu ya kuhudumia jamii kupitia uuzaji wa mahitaji ya nyumbani.

Lakini ukijiona unatanga tanga leo umefanya shughuli hii kesho umefanya shughuli ile ambazo mwisho wa siku hakuna mahali zinakutana kwa namna yoyote ile japo unapata pesa, basi wewe hujatambua kusudi la maisha yako na usipokuwa makini utakuwa mhangaikaji hadi mwisho.

Ukifanya jambo nje ya kusudi ya maisha yako hutakaa ulifurahie kamwe, litageuka kuwa mateso hata kama linakuingizia pesa nyingi. Unaweza ukawa unafanya kitu nje ya mstari wako wa maisha hata kama kinakulipa mabilioni yaani bado utakuwa kama SAMAKI ALIYETUPWA NJE YA MAJI. Samaki akiwa nje ya maji, zile dakika chache kabla hajafa huwa anahangaika sana na ukimmiminia tone moja la maji kwenye mkia utaona anavyojaribu kutaka kuogelea. Kale katone ka maji kwenye mkia wa samaki akiwa nchi kavu ni sawa na wewe unapokuwa unafanya shughuli nje ya kusudi la maisha yako inyokupa hela nyingi lakini ikatokea katika kuhangaika ukafanya ka-kitu kadogo ambako kako ndani ya kusudi la maisha yako – moyo waku unakuwa na amani sana na unafurahi sana. Lakini unajikuta huendelei kufanya hilo jambo kwa sababu halikuingizii hela nyingi kwa wakati huo ukilinganisha na lile lingine hivyo unaamua kuendelea kuishi nje ya kusudi la maisha yako ili upate mali za nje na kuunyanyasa moyo wako. Maana yake ni kwamba, kama unafanya shughuli inayokuingizia kipato iliyo nje ya kusudi la maisha yako, hutokaa uache kuhangaika kujaribisha vitu vya aina mbalimbali. Kwa sababu moyo wako hautotosheka wa kuridhika – HUWEZI KUKATA KIU YA MAJI KWA KUNYWA SODA AU JUISI JAPOKUWA VYOTE NI VIMIMINIKA. . Ndio sababu huwa napenda kusisitiza sana kupata muda kwa ajili ya maisha yako binafsi, hii inakusaidia kujitambua.

Tatizo wengi hatutaki kuanzia chini, tunapadharau huku chini lakini matajiri wakubwa duniani kama unafuatilia historia za maisha yao na jinsi walivyoanza utagundua kwamba walianza wengine wakiwa hawana kitu kabisa. Ukiwa na nidhamu ya maisha hasa kwa kufuata kanuni za maisha, kanuni za biashara/shughuli unayofanya na kanuni za maisha yako binafsi huwezi kuacha kufanikiwa. Mafanikio ni safari. Umaarufu hauji bila kuwa umefanikiwa kwenye jambo fulani hata kama ni ujinga utapata umaarufu kwa wajinga wenzako.

Mafanikio yanaanza kwa wewe kuweza kujitofautisha na maisha yako ya nyuma. Usiruhusu maisha yako ya nyuma kukuwinda na hivyo kuwa kikwazo cha maisha yako unayoyaendea. Usiishi kwa mazoea ya nyuma. Mafanikio ni pale unapoweza kujitambua na kusimama imara katika kanuni za maisha ulizojiwekea na kujitofautisha na watu wengine wote kwa sababu wewe ni wa tofauti, kila binadamu ni wa tofauti ndio mana kila mtu ana nafsi yake mwenyewe hata mkiwa mapacha mmeunganika viungo vya mwili.

MAFANIKIO YANAANZA NAWEWE

Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha

Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi.
Ebu jiulize ni watu wangapi ulikuwa unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda.

KWANINI WEWE NI MSHINDI

Wanasayansi wanasema wakati ujauzito wa binadamu unatungwa kunakua na mamilioni ya mbegu za kiume ambazo zinakua zinatoka ili kwenda kurutubisha yai ili azaliwe mtoto. Na kwa kawaida inatakiwa mbegu moja tu kati ya hizo milioni. Hivyo basi wewe ni mmoja wa pekee kati ya mbegu za kiume millioni moja zilizotoka siku ile ulipotungwa tumboni mwa mama yako.

JIPIGIE MAKOFI SEMA MIMI NI MSHINDI

Kabla hujazaliwa ingewezekana ujauzito wako ukaharibika, Ingewezekana labda ujauzito wako ungetolewa, lakini haikuwa hivyo ukatoka salama. Na ulipozaliwa kuna watoto wengi tunasikia wanafariki wakati wa kujifungua lakini hukuwa wewe. Tunasikia pia magonjwa mbalimbali yanaua watoto lakini hukuwa wewe. Umeyashinda yote hayo hivyo wewe ni MSHINDI usijidharau kwa hali uliyonayo sasa wewe ni mshindi. Kuwepo kwako hai leo ni kwa sababu maalumu.

Umekwenda shule, umekua ,wako waliokufa kwa ajali lakini wewe upo hai bado Mungu ana kusudi na wewe.

Usijidharau nipo hapa Leo kukonyesha jinsi wewe ulivyo wa thamani mbele za Mungu. Wako wenzako wamepitia hatari ngumu na mateso hadi wakafikia kujinyonga, kunywa sumu, kujiua, lakini wewe upo hai. Wewe ni mshindi.
Upo duniani sasa ili uendelee kushinda.

Umezaliwa na uwezo wa kipekee sana ndani yako unaokuwezesha wewe kushinda kila siku na ukiweza kuutambua uwezo huo ushindi ni lazima. Kabla ya kutambua uwezo huo lazima utambue kwanini wewe umezaliwa! Ulizaliwa kwa kusudi gani? Ili uelewe kwanini Mungu amekuacha hai mpaka sasa ni ili ulitimize kusudi lake.

Hayo Yote niliyokwambia yanaweza yasiwe na maana sana kwasababu yameshapita sasa nakwenda kuzungumza namna ya kuendelea kutengeneza ushindi mwingine kila siku kupitia kwenye kusudi lako!

UFANYEJE UENDELEE KUSHINDA?

Haijalishi hali gani unapitia sasa upo hai leo kwa sababu maalumu na ni ili uweze kuendelea kua mshindi kwa kuifanya dunia kuwa mahali bora zaidi kuliko ulivyoikuta. Hii dunia haikua hivi miaka 10 iliyopita ni watu wachache wametumia uwezo Mungu aliweka ndani yao na kuvumbua mambo mengi na ya ajabu tunayoyaona sasa. Ni nafasi yako wewe kutumia nafasi hii ya kuwa hai leo kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi naamini wewe una nafasi kubwa sana.

“You were born to win, but to be a winner, you must plan to win, prepare to win, and expect to win.” – Zig Ziglar

Zig Ziglar anasema ulizaliwa kushinda kama tulivyoelezana hapo awali, lakini ili uendelee kua mshindi, lazima ujipange kushinda, ujiandae kushinda, na utarajie kishinda

Timu ya mpira inapochukua kombe sio mwisho wa mchezo wanakwenda kujinoa zaidi ili waweze kushinda tena na tena. Wewe unajiandaa vipi na kuendelea kushinda?
Vipo Vitu vichache vya Muhimu unatakiwa uwe unavifanya ili kushinda kila siku.

(a)Jitambue.

Ili uendelee kushinda kila siku lazima ujitambue wewe ni nani! Najua unatambua kwamba wewe ni jinsia gani. Lakini kujua hivyo tu haitoshi.
Kwanini ulizaliwa mwanamke/mwanaume, mtu mweusi tena Tanzania na sio nchi nyingine?
Ukitambua hivyo lazima ukubali na uanze kufanyia kazi na uendelee kushinda kila siku, Tambua kusudi la wewe kuzaliwa na kwanini ukazaliwa kipindi hiki na sio wakati mwingine.

(b) Usiangalie nyuma.

Haijalishi umepitia maisha ya namna gani umezaliwa kwenye mazingira ya namna gani, wewe jua kusudi la Mungu ndani yako na ulifanyie kazi, haijalishi jana umefanya vibaya kiasi gani, haijalishi pia ulifanya vizuri kiasi gani angalia mbele angalia kule unakokwenda.
Kule unakokwenda kuna maana zaidi ya unakotokea. Pia huwezi kwenda mbele huku umeangalia nyuma utajikwaa. Haijalishi ulikosea mara ngapi, umeua, umeachwa, umefeli, huna kazi, umefukuzwa, una madeni, usiyaangalie hayo.
Kama umeshajitambua liangalie kusudi na songa mbele.
“Adui wa mafanikio yako ya leo ni mafanikio yako ya jana, Adui wa mafanikio yako ya kesho ni mafanikio ya leo”

(c) Jua unapokwenda.

Hakikisha umetambua unapokwenda kama tayari umeshajitambua na umeacha kuangalia nyuma hakikisha sasa unajua unapoelekea. Kuwa na Maono, ndoto kubwa na kua na viongozi wanaokufundisha uelekee kwenye maono yako.Ukijua unapokwenda huwezi kupotea, Ukijua unapokwenda huwezi kufanya mambo ya ajabu ajabu, ukijua unapokwenda huwezi kuchukuliwa na kila mtu hovyo hovyo, Ukijua unapokwenda lazima utajisitiri, Biblia inasema pasipo maono watu huacha kujizuia.
Kama huna maono kulijua kusudi hakuna maana, kama huna maono utadondoka kila siku.

(d)Jifunze Kila Siku.

Umeshajitambua, ukaacha kuangalia nyuma, ukajua unapokwenda kwa kuwa na maono na ndoto kubwa, sasa huwezi kuvifikia vyote hivyo bila kujifunza. Huwezi kwenda kuwa mtu mkuu kwa ufahamu huo ulio nao sasa hivi, Inawezekana umesoma vyuoni una Degree au Masters lakini hiyo haionyeshi vyema kwamba wewe umesoma unajua kila kitu unaweza kuyabeba maono makubwa.
Soma vitabu vya uongozi, vitabu vya kuhamasiha jiendeleze binafsi, Jifunze kwa kupitia watu unaokutana nao kila siku, Jiunge na magroup kama ya whatsapp na ujifunze Makala kama hizi.

USHINDI UTAKUA WAKO KILA SIKU

“adui mkubwa wa kujifunza ni kujua” unapojiona wewe unajua kila kitu umesoma sana huwezi kujifunza kwa mtu mwingine alieko chini yako unakosea sana na hutaweza kufika popote kubali kujifunza kwa kila mtu haijalishi ni nani. Ushindi ni wako Na naamini kabisa kupitia makala hii kutatoka watu wakubwa sana katika Historia ya nchi hii na dunia.

(e) Jitengenezee tabia za Kushinda.

Unajitengenezeaje Tabia za kushinda? Jiambie maneno ya kushinda,huonagi wachezaji huwa wakiwa kwenye mazoezi wanashangilia kama vile tayari wana ushindi?
Jiambie maneno ya kujihamasisha mwenyewe. Mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda, Siziogopi changamoto, mimi ni wa thamani, Unaweza kuandika maneno mazuri ya kukuhamasisha ukutani ili unapolala na uamkapo asubuhi uyaone na kuyasoma.
Washindi wana amka mapema. Washindi wanajua ndoto zao vizuri. Hakikisha kile unachokitaka kimekaa kwenye akili yako yaani hata ukishtuliwa usingizini leo unakuwa na uwezo wa kukisema.
Anza kufanyia kazi yale unayojifunza kila siku.

(F) Usiogope Kushindwa.

Usiziangalie changamoto na kukata tamaa. Zitumie changamoto kama shule jifunze kwa kupitia hizo na utaendelea kushinda kila siku.
Changamoto zinakuja kwasababu njia unayoiendea ni nyembamba hujawahi kuipita kabla. Na pia bado uwezo wako haujakuwa vya kutosha tumia changamoto kama njia za kukuza uwezo wako ili siku moja ufikie kule unakotaka ukiwa imara na usitetereke.

(g) Fanya vitu unavyoviogopa.

Usikubali kila siku unafanya vitu vile vile. Hakikisha kila siku kuna kitu kipya umefanya. Hii itakuongezea wewe uwezo wa kushinda na ujasiri wa kupita sehemu za mbele zaidi.
Hakikisha inapokua jioni umeangalia ni vitu gani vipya umefanya. Ni hatua gani umepiga katika malengo yako. Ni kitu gani kipya umejifunza. Usikubali unakutana na mtu anakupita hivi .Hujaongeza kitu chochote kwenye ufahamu wako au yeye hajajifunza kitu kutoka kwako. Wewe una kitu cha pekee sana ndani yako ambacho Mungu kakiweka kwa ajili ya wengine.

(h) Fanya na fuatilia zaidi vitu vinavyoongeza thamani kwako, kwa wengine, kwenye roho yako, kwenye mahusiano yako, kwenye maono na malengo yako na kwenye kusudi lako.

Ukifanya nje ya hapo utakua unapoteza muda bure. usikubali kupoteza siku yako bure. Kumbuka tumepewa masaa 24 tu ya kuishi yatumie vyema masaa hayo.

UKIWEZA KUFUATILIA HAYA USHINDI NI WAKO KILA SIKU, NI MAMBO MADOGO MADOGO UTAPITIA TU NA YANAREKEBIKA.

“Hakuna kiumbe kingine kitakachozaliwa tena kifikiri kama wewe, kitembee kama wewe, kiongee kama wewe, Hakuna tena, wewe ni wa pekee sana usijidharau tumia upekee huo kufanya mambo makubwa katika dunia hii usikubali kuondoka hivi hivi.”

“Hamu Yangu Ni Kuona Unafanikiwa”.

JITAMBUE : Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana, Anza sasa

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST.** Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho.

Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako.

Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma.

Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo.

Tambua ya kuwa, “hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho”

Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma.

Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati.

“Habari njema ya siku ni leo, na siku nzuri yako ni ya kesho “

Ukiona umesononeka kwa maisha kuwa magumu jua unaumia kwaajili ya maisha yako ya nyuma, maana unawaza jinsi ulivyo shindwa kulipa kodi ya nyumba,ulivyoshindwa kulipa umeme, maji, ada za watoto na ulivyoshindwa kuendesha biashara yako au ulivyoshindwa kuitetea ajira yako. Usipoteze Muda wako kwa kuwaza yaliopita badala yake waza kesho yako itakuwaje.

Waswahili wanasema yaliopita si ndwele, tugange yajayo. Huwezi kubadilisha jana, Bali waweza kubadilisha kesho yako kwa kufanya maamuzi leo.

Usipoteze Muda kwa kugeuza shingo yako kutazama ya nyuma, utajikuta unadumbukia katika shimo la maisha magumu.

“You can’t have a better tomorrow if you are thinking about yesterday all the time “

Maisha yako ya kesho hayalingani na maisha yako ya jana. Anza sasa.

BADILIKA : huu ni mwaka mpya

**Badilika huu mwaka. Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii
Kipenga kimeshapulizwa wewe maliza bajet yote leo kwenye starehe alafu uanze kulalamika eti Mwezi wa kwanza Mgumu utadhani umeubonyeza

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda na kasi ya Magufuli, wewe bado unapiga vibomu alafu unalalamika uchumi mbovu

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda porini kutafuta pesa na kuja kuzitumia mjini wanaenzi ule msemo wa Mali utaipata shambani /porini wewe unatafuta pesa kati kati ya mji, my friend utapata nauli tu

Kipenga kimeshapulizwa wanasiasa wenzako wanaleta matokeo chanya kwenye jamii, wewe umekwama na siasa zako za Maigizo, utaisoma namba vizuri

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatengeneza ajira na kulipa mishahara, wewe umeajiriwa mwaka wa 10 unasubiri bonus, increment na kubagain ongezeko la mshahara alafu bado unataka kuwa celebrity, my friend labda celebrity wa mikopo

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta matatizo ili yawe fursa kwao, wewe ukiona changamoto unakimbia na kuilalamikia serikali, utasubiri sana

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta kazi kwa kufanya kazi za kujitolea kujenga nchi, wewe unasubiri interview, hiyo experience utaipata ndotoni

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wanahojiwa na forbes magazine wamewezaje kuleta impact Africa nzima, we unakazana kujisifu unafollowers wengi instagram alafu Huna hata mmoja ambae ni rafiki wa kusaidiana.

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii wanalipwa, wewe kazi yako ni kuretweet/kurepost na kulike siku nzima bila kupata faida yoyote

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaoipenda nchi yao wanachangia matembezi ya tembo na faru yatakayofanyika Morogoro kwa kununua tshirt, wewe bado unazungusha bia na nyama choma alafu unalalamika watalii wamepungua, unataka waje wakuangalie wewe?

BADILIKA my friend.
😹😹😹😹😹

Jaribu kufikiria haya

1. Uelekeo ni muhimu kuliko kasi. Ni heri kwenda taratibu katika Uelekeo sahihi, kuliko kwenda kwa kasi katika Uelekeo usio sahihi.

2. Kulalamika mambo hayaendi wakati wewe mwenyewe hujui unakokwenda ni kuwa na matatizo ya akili.

3. Kasi yako inaamuliwa sana na umbali unaoweza kuona. Kama huoni chochote mbele ya maisha yako, basi huna chochote.

4. Sayansi inadai kuwa kazi ni nguvu inayotumika kusukuma kitu kwa umbali fulani kwenye Uelekeo maalumu. Kwa hiyo kama unatumia nguvu kusukuma mambo, lakini hayana Uelekeo maalumu jua kwamba hufanyi kazi yoyote, unapoteza nguvu tu.

5. Masaa yanaenda, siku zinapita, miaka inaongezeka, umri wako ndio unaenda hivyo, unafanya nini katika maisha?

Wazo mbadala kuhusu ajira au kupata kazi

Katika mambo ambayo nadhani nimeshawahi kujidanganya ni kufikiri kwamba nikipata kazi ndiyo utakuwa mwisho wa matatizo yangu na kuwa huru kufanya kila kitu ninacho kitaka.
👇👇👇👇👇
Sasaa baada ya kuipata iyo kazi nimekuja kupata ukweli kwamba kumbe kazi ya kuajiriwa siyo Mwarobaini wa Yale niliyo Nayo kumbe ndiyo safari inaanza na siyo mwisho kama nilivyo dhani.

Kazi Mara nyingi napenda kuifananisha na Ndoa, watu wengi walio nje ya kazi wanataka sana kazi na wakidhani ndiyo itakuwa mwanzo wa mafanikio yao.

Vijana waliopo nje ya mfumo rasmi wa ajira wanatamani waingie huko, lakini kutokana na ukweli kwamba kuna vitu hawavijui katika kazi ya kuajiriwa na ndio maana wanajihisi Wanyonge kwa kuto kuajiriwa.

USHAURI
kwanza tambua kukosa ajira siyo mkosi, wala siyo kwamba huna bahati. Yawezekana kwakukosa kwako ajira ni mlango wa kuwa muajiri. Unachotakiwa usilalamike tafuta fursa hapo ulipo, ndipo pana utajiri.

1. Kama hujaariwa acha kutamani maisha ya watu walio ajiriwa, ikiwezekana sitisha hata kupiga misele kwenye ofisi, zao kugongea maji ya dispenser

Badala yake anza kutafiti kwakina ni kwa namna gani watu ambao hawajaariwa wanaishi mtaani. Kuwa na marafiki wengi zaidi wanao pambana mtaani ili ujue wao wamewezaje.
Tafuta ndege unao fanana nao

2. Usidanganye kwamba ajira ndiyo itajibu matatizo yako yote unajidanganya

Badala yake kama utafanikiwa kupata iyo ajira, hakikisha unaifanya mbegu. Anza kwakuwekeza kwenye miradi ya uzalishaji maana mshahara hauto kutosha kuishi maisha uliyo nayo kwenye akili yako.

Mwisho kabisa Nguvu na imani uliyoweka kwenye ajira iweke hivyo hivyo kwenye shughuli zako binafsi

Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako

20 – 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 – 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.

30 – 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.

35 – 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.

40 – 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.

50 – 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.

60 – 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 – 80 = kula matunda.

80 – n.k= unamsikilizia Mungu anasemaje

Jinsi ya kulima mahindi kitaalamu kama inavyotakiwa

Mahindi ni miongon mwa mazao makuu ya chakula hapa nchin Tanzania na ulimwa karibu kila mkoa. Ulimwa zaidi nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njimbe na Katavi. Pia mikoa ya Morogoro Mwanza Dodoma Shinyanga Arusha Tanga na mikoa mingine. Kwakua ni zao la biashara hivyo karibu kila mkoa unalima zao hili.

Matumizi.

Zao hili ulimwa na utumika kwa matumizi mbalimbali yakiwemo yafuatayo

★Chakula (stample food)
★Chakula kwa mifugo
★Nishati (biofuel)
☆Dawa za asiri(mbelewele zake)
☆kutengenezea mapambo.
☆mabaki utumika kama mbolea n.k.

Pia wapo wakulima waliojikita katika kulima zao hili kibiashara ambao uuza katika soko la ndani ya mkoa nje ya mkoa na nje ya nchi. Hapa itategemea uwekezaji wa mkulima husika.

MAZINGIRA NA HALI YA HEWA NZURI KWA MAHINDI

Mahindi uota vizuri katika jotoridi lenye wastani wa 20-30 nyuzi joto za centigradi. Pia linaitaji mvua hasa wakati wa uotaji na uotaji wa mbelewele.

MBEGU ZA MAHINDI

Kuna aina nyingi za mbegu. Zipo za Asili na pia zipo mbegu chotara (Hybrid F1 & F2) kutoka makampuni mbalimbali, za mda mfupi na za mda mrefu kulingana na kipindi/vipindi vya mvua kwa mwaka kwa mkoa usika.

Kwakua Tanzania ina kanda tofauti za hali ta hewa ikiwemo nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini, nyanda za kati na maeneo mengine ya pwani na pia ndani ya mkoa mmoja panaweza pakawa na matabaka tofauti yakijografia (geographical/ecological zone).

Hivyo mbegu za mahindi zinazofanya vizuri mikoa ya Pwani Morogoro Arusha Mwanza haziwezi kufanya viruzi katika mikoa ya Njombe Iringa n.k kwakua utofautiana katika ukanda.
Mbegu zinazofanya vizuri Njombe mjini ama wanging’ombe zinaweza zisifanye vizuri Ludewa ama Makete wilaya tofauti lakini mkoa mmoja.

Hivyo ni vema kujua kua mbegu upandao inafaa kwa ukanda upi?? Wa mvua za mda mrefu! Mda mfupi! Ama sehemu zenye ukame!!.

NAFASI

Hii itategemea aina ya mbegu na pia namna ya utunzaji ambao utegemea sana kusudi la ulimaji (chakula ama biashara).

UPANDAJI WA MAHINDI

Mche hadi mche ni sm 30-40. Mstar hadi mstari ni sm 70-75.
Yaani sm 75X30, pia waweza tumia sm 80X25 punje moja moja za mbegu chotara ya mahindi.

Ni vema ukapanda siku moja ambayo utaweka na mbolea. Anza na mbolea 5g kwa shimo fukia kidogo kisha weka mbegu ( mbegu moja kama ni Hybrid).
Mbolea nzuri zaidi yenye maboresho na lishe linganifu kwa mmea (balanced nutrition) ni YaraMila Cereal, Yara Vera Amidas na YaraBela Sulfan kutoka kampuni ya Yara Tanzania ltd. Mfuko mmoja mmoja, utapandia, utakuzia mkuzio wa kwanza na utamalizia mkuzio wa pili kama zilivyo orodheshwa hapo.

PALIZI YA MAHINDI

Kuna aina tatu za kupambana na magugu.

1. Palizi la mkono/jembe.

Hili lina gharama zaidi na linachukua mda mwingi na pia SIO SAHIHI kwakua halireti majibu mazuri katika kuzuia magugu.

2. Mbinu za Asiri.

Hapa utumika matandazo kama majana makavu, majani ya mgomba, pumba za mpunga n.k ( Mulching). Huitaji kujipanga zaidi na piaupatikanaji wa matandizo wakati wakilimo unaweza ukawa ni shida.

3. Palizi la Dawa.

Hapa ndio upatikana suluhisho sahihi kwa mkulima ingawa changamoto zipo katika ubora wa dawa wingi wa madawa uwepo wa dawa feki na gharama.
Ni vema ukatumia dawa zinazotumika kuzuia magugu mara baada yakupanda kabla ya magugu kuota (somo la magugu litafuata sio mda).
Tumia PRIMAGRAM GOLD kutoka Syngenta Tanzania Ltd epuka palizi la mkono okoa mda pata faida pata mda wakupumzika na kujishughurisha na mambo mengine na uongeze kipato.

WADUDU NA MAGONJWA KWENYE MAHINDI

WADUDU WA MAHINDI

Maize aphids, African armyworms, Bollworm, Stalk borer, leaf hoppers.

Dawa nzuri kuzuai hili ni Match 050EC na Karate 5EC/Karate 5CS(Originali kutoka Syngenta epuka dawa feki ilikopiwa nembo/lebo)

MAGONJWA YA MAHINDI

Magonjwa ya ardhini (soil born disease), kutu ya majani n.k.
Magonjwa ya kuvu sio tatizo sana ktk kilimo hiki ingawa maeneo ya nyanda za juu kaskazini yameoneka.
Tumia Artea na Amistar Kutoka kampuni ya Syngenta.

UVUNAJI WA MAHINDI

Mda ambao mahindi uchukua kukaa shamban hadi kuvunwa inategemea na ukanda na pia na mbegu, mahindi ukaa wastan wa miezi mitano toka kupandwa shambani. Lakini ni tamaduni za wakulima wengi kuacha mahindi shambani kwa mda mrefu zaidi ili yakauke kwa matumizi ya biashara. Mahindi kwa ajiri ya gobo ukaa mda mfupi (sio kila mbegu ni ya gobo/mahind yakuchoma) zaidi uvunwa kabla yakukomaa.

Idadi ya gunia utazopata kwa ekari moja utegemea

→ utaratibu uliofuatwa wakitaalum (Agronomic practices)
→ aina ya mbegu
→mazingira (ukanda)-mvua ama umwagiliaji.
→mapambano dhidi ya wadudu magonjwa na magugu.
→ usimamizi/mbolea/rutuba ya udongo wako.
Kila mbegu hasa chotara zinakua na kiasi tajwa cha mavuno kwa ekari.
Mf. Gunia 30, 25-30, ama 40 n.k. (gunia tafsiri yake kitaalum ni 100kg.

SOKO LA MAHINDI

Soko utegemea sana wastani ama ungezeko la walimaji na uzalishaji. Soko lake utegemea sana watumiaji wa ndani.
Pia utokea soko katika mkampuni kama wanunuzi wadogo wadogo, kampuni ndogondogo za usagaji mahindi, taasis mbalimbali,Mohamed enterprise, Hifadhi ya taifa ya chakula, n.k na pia soko la nje ya nchi eg Kenya Uganda Sudani Ethiopia n.k

Yafahamu Mambo Mbalimbali ya muhimu kuhusu kilimo cha Mazao ya Mboga Mboga kwa Ku-Download Kitabu cha MBINU ZA KILIMO BORA CHA MBOGA

Ni kitabu kinachotoa elimu ya Kilimo Cha Mboga. Kipo katika Mfumo wa PDF (Soft copy).

Kina kurasa 100 na utaalamu wa mazao zaidi ya 10, ambayo ni nyanya, kabichi, bamia, vitunguu maji, vitunguu twaumu, hoho, matikiti, karoti, uyoga na matango. Bila kusahau kilimo cha mboga kama chainizi na mchicha.

Pia utaweza kufahamu mbinu mbalimbali za kilimo cha mboga kama vile kuandaa shamba na kitalu, udhibiti wa wadudu na magonjwa katika mboga, kuvuna na kuhifadhi mboga, vilevile utajifunza kuhusu kilimo cha matone.

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako.

Ni wakati mwingine tena tunaenda kujifunza pamoja juu ya mambo mbalimbali ili tuweze kufikia mafanikio kila siku. Leo tunakwenda kujifunza kuhusu pesa na utajua mambo mengi sana juu ya pesa.

Ni siri gani ipo ndani ya fedha na wengi hawaijui?

Kwanini watu wengi wanakua matajiri halafu wanapoteza utajiri wao wote na kuwa maskini tena?

Ulishawahi kuona watu maarufu wamekua na pesa nyingi lakini baada ya muda wanapotea na pesa zao zinapotea na kurudi kuwa watu wa kawaida kabisa?

Hujawahi kuona watu wakiuza mashamba ya urithi kwa mamilioni ya pesa na wakabadilisha aina ya maisha wanayoishi lakini baada ya muda pesa zinapotea na wanarudia hali yao ya zamani?

Hujakutana na vijana waliochimba madini wakajikuta wamepata mawe wakawa milionea lakini ghafla baada ya muda Fulani wanarudi kule kule walipokua?

Wengi wakiona hayo utawasikia wanasema pesa za mashamba hazika! Pesa za madini zina mashetani! Ni siri gani ipo kwenye hii pesa?

Inawezekana umeshajiuliza sana maswali haya na hata kuogopa kuwa nayo. Ukaamua kuwa mtu wa kawaida tu kwasababu ya hofu hizi zinazokujia unapofikiri kuwa tajiri kisha uje upoteze pesa zako zote!

Watu wengi wamekuwa na fikra kwamba pesa ni mbaya, zinaharibu watu, zinawafanya watu kuwa wachoyo, zinawafanya watu kuwa na tamaa pamoja na mengine mengi unayoyafahamu.

Ukweli ni kwamba pesa haina tatizo lolote pesa haina shetani wala pepo lolote linaloifanya imharibu mtu anapokuwa nayo nyingi. Pesa sio kiumbe hai. Pesa tunaitumia kununua bidhaa mbalimbali au kulipia huduma tunazozihitaji katika maisha yetu ya kila siku.

Ukweli kuhusu pesa ni huu hapa. Kwanza pesa haimbadilishi mtu bali inamfanya awe Zaidi ya vile alivyokuwa mwanzo yaani kama mtu alikuwa ni mchoyo akipata pesa atakuwa mchoyo maradufu, kama alikua mlevi akipata pesa anazidisha kuwa mlevi Zaidi.

Na wengine wakiwa hawana pesa kuna tabia nyingi wanakuwa nazo ndani zimejificha hawazionyeshi wakishapata pesa zile tabia zinafunguka na kuwa wazi.

Kama mtu alikuwa Malaya akipata pesa ndio utaona anaanza kubadilisha wanawake. Pesa zinabaki kuwa pesa na tabia za mtu zinabakia kuwa tabia za mtu.

Kama mtu alikua mtoaji akipata pesa atakuwa mtoaji Zaidi.
Kama alikua mcha Mungu akipata pesa atakwenda kuabudu Zaidi.
Hivyo pesa sio tatizo watu ndio wenye matatizo ndani yetu.

“Having more money won’t change you as a person. It will, however, magnify
the person you already are.” – Bob Proctor

Huwa napenda kuutumia mfano wa chombo. Watu wengi wanaopata pesa nyingi ghafla na kuzipoteza zote ni kama maji yaliyojaa kwenye ndoo utake kuyaweka yote kwenye kikombe cha chai.

Ukweli ni kwamba kikombe kitajaa lakini yale yaliyobaki yatamwagika yote chini hivyo hivyo na pesa zinazopatikana ghafla ni sawa na kuziweka kwenye kikombe ambacho ni uwezo wa akili yako.

Kama Akili yako bado haijaweza kupangilia milioni ishirini hivyo hata ukipewa leo zote zitapotea na zitabaki kile kiwango ambacho akili yako inaweza kutawala na kuendesha. Hivyo njia sahihi ya wewe kuweza kumiliki mamilioni ya shilingi na kubakia nayo ni kuanza kubadili ufahamu wako. Kuza ufahamu wako kidogo kidogo ili uweze kuendesha utajiri mkubwa. Na hili halitokei ndani ya siku moja ni kadiri unavyojifunza kila siku. Kwa kusoma vitabu na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Jambo moja na muhimu la kufanya ni kutokuweka akili yako yote kwenye pesa. Usiweke malengo yako kwenye pesa unapofanya biashara unafanya ili upate pesa lakini siku zote pesa hazikai huwa zinaisha hivyo badala ya wewe kuweka nguvu zako na mawazo yako kwenye pesa weka Zaidi katika kuwasaidia watu kama unauza nguo kazana Zaidi katika kuwafanya watu wafurahie huduma yako pesa zitakuja.

Kama unatoa huduma hakikisha unatoa huduma bora ili kuvutia wateja Zaidi kila siku. Pesa utaziona kwako na zitaongezeka kila wakati.

Wekeza pia muda wako kwenye kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itakuwa inakuingizia pesa bila kuwa na kikomo. Unapotegemea mfereji mmoja wa kipato lazima utabakia pale pale siku zote.

Jambo la muhimu la kufanya ili uweze kubakia juu kwenye mafanikio siku zote ni kujifunza na kujijengea misingi ambayo itakuwezesha wewe usiyumbe na ubakie na utajiri wako.

Kuwa mwaminifu, kua mtoaji, wapende wengine, kuwa muadilifu, usidhulumu mtu, kabla hujafanya lolote angalia lina manufaa gani kwako na kwa wengine.

Nikutakie wakati mwema Asante sana kwa kusoma Makala hii.

Mambo 13 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia

1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.

2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako.
Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.

Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako- Basi ww usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na ww umeahidiwa

3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia.

Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki.

4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa.
Omba maarifa ya kutengeneza pesa kama yeye, tena kwa mtaji mdogo.

Maarifa ndio mtaji wa kwanza.
Unaweza kupewa/kusaidiwa pesa iwapo una mawazo mazuri ya kuzalisha pesa. Baadhi husema, “Omba ndoano, usiombe samaki”

5. Usitunze mbegu badala ya kuipanda.
Watu wengi hufurahia pesa wanayolipwa/kuipata kisha wanaiweka bank au nyumbani bila kuiwekeza.
Wekeza pesa ili uzalishe zaidi. Usiogope kuingia hasara, kila aliefanikiwa alipoteza kwanza kabla hajafanikiwa.Wengi walipoteza muda, pesa, afya na hata matumaini ya kufanikiwa, ila kwa uthubutu wao, mwisho wa siku walifanikiwa”

6. Kamwe usimkopeshe mtu pesa ambayo unahisi hatorudisha.

Unapomkopesha mtu huyo pesa, jiridhishe mwenyewe moyoni kuwa kama hatoweza kulipa basi deni lake-halitoathiri urafiki wenu. Ukihisi kwamba kushindwa kwake kulipa kunaweza kuathiri urafiki wenu, basi mshauri aende bank akakope”

7. Usikubali kumdamini mtu ambae huna uhakika kuwa atalipa kile unachomdhamini.
Kumbuka- dhamana maana yake utawajibika iwapo atashindwa kulipa

8. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hata huna matumizi nazo wakati huo.
Unaweza kujikuta unafanya matumizi ambayo hayakuwa kwenye ratiba sababu ya ushawishi wa pesa ya mfukoni.
Ili kuepuka haya, tembea na pesa uliyopanga kuitumia katika safari yako.
Pesa nyingine itunze mahali pengine palipo salama”

9. Epuka kutunza pesa mahali pasipo sahihi.
Maeneo kama kwenye soksi, sidiria, chini ya mto wa kulalia, chini ya begi, kwenye kopo au hata kwenye begi la safari, si maeneo salama.
~Ni rahisi kusahau, kuibiwa au kupoteza pesa zako.

Ni bora ukatunza pesa kieletroniki; yaani bank au kwenye simu au kwenye pochi yenye kamba ngumu ya kuivaa mabegani au wallet ambayo inatosha kwenye mifuko imara na yenye vifungo kwenye nguo zako hasa uwapo safarini.

10. Usitumie pesa kwa kitu ambacho hakikuwa kwenye ratiba yako.

Jiulize kwanza kabla hujanunua,
“Bila kitu hiki, maisha yataenda au lah?”
Ukiona maisha yataenda bila kitu hicho, acha kukinunua. Tabasamu kisha ondoka.

12. Matumizi yako ya pesa yasizidi pato lako.

Unaweza kuwa una ndoto kubwa/matumizi makubwa ya pesa kuzidi pato lako.

Unapaswa kuwa bahili katika matumizi yako. Cheza na pato lako.
Fanya matumizi makubwa pale tu pato lako litakapoongezeka. Hii itakuepushia kushindwa kufanya baadhi ya mambo ya msingi na kisha ukajikuta unaishia kwenye madeni makubwa.
13. Una ndoto kubwa hapo baadae; labda kujenga nyumba, kununua gari, kununua kiwanja, simu nzuri hata pikipiki.

Usikurupuke, ukanunua kitu cha ndoto yako sasa eti tu sababu umekipata kwa bei ya punguzo.

Usichanganye kati ya mahitaji ya baadae na ya sasa.

Pesa unayotumia kutimizia ndoto sasa itumie kwa mahitaji ya sasa. Ndoto ibaki kuwa ndoto.

Hii itakuepushia kuingia katika madeni au kuishi kwa shida sababu ya tamaa.
Jipange taratibu kutimiza ndoto yako.

*Mwendo*

Tabia za kuepuka ili uweze kuwa tajiri

UKIWA NA HIZI TABIA 9, JIANDAE KUFA MASKINI…………
By Kashindi Edson

“Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu” (Nelson Mandela, R.I.P)

“Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio”(Mwl Nyerere, R.I.P).

“Kile unahokifanya muda huu ndicho kinachoashiria na kutoa picha kamili ya baadae yako”(Mahatma Gandhi, R.I.P)

“Ukizaliwa maskini sio kosa lako, ila ukifa maskini hilo ni kosa”(Bill Gate, The richest man in the world).

Mwalimu wangu wa chuo aliwahi kuniambia kuwa, “mstari unaomtenganisha maskini na tajiri ni mwembamba sana, kwa hiyo ni rahisi sana kuwa tajiri pia ni rahisi sana kuwa maskini”. Mpaka leo sijaelewa alimaanisha nini.

Watu wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali za maisha, kwenye uongozi, biashara, kilimo, elimu, siasa, michezo, uandishi, muziki, afya, imani, utangazaji, nk huwa hawana hizi tabia 9 nilizokuandalia leo, kwa hiyo kama una kiu ya mafanikio kwa hicho unachopambania, achana na haya mambo 9 yafuatayo;

1. KUTOKUJARIBU.

Katika kutafuta mafanikio huwa kuna vitu viwili tu vya kuchagua. Tambua kuwa maisha ni vita. “Chagua kufa, au kupambana”. “Siogopi kufa, naogopa kutokujaribu'(Jay Z). Hakuna alie zaliwa anajua, jiamini, jaribu utafanikiwa.

2. KUTOKUJIFUNZA.

Che Guava mpaka anafariki library yake ilikuwa na vitabu zaidi ya 2000, mwenzangu na Mimi sijui hata kama una Biblia au Quran ghetoni kwako. Nkwameh Nkrumah library yake ilikuwa na vitabu zaidia ya 3000, Obama anakuambia kila akiamka asbuhi lazima asome kitu kipya. “JOSEPH=Jifunze, Ona, Soma, Elimika, Pitia, Hamasika.(Prof Jay)

3. WOGA & WASIWASI.

“Tunaweza tukamsamehe mtoto anayeogopa gizani, lakini sio mtu mzima anaeogopa mchana”(Plato, R.I.P). Kitu cha kuogopa katika maisha ni woga wenyewe. Kama hujiamini hutakuja kuwa mshindi katika jambo lolote. Fanya hicho unachofikiria kukifanya kwa moyo wa dhati, kama unaamini ni cha harali na kia manufaa kwako na familia yako, na jamii nzima. Acha tabia ya kuogopa kitu ambacho hakijatokea.

4. KUJILINGANISHA.

Kuna baadhi ya watu, huwa wangetamani kuwa kama watu Fulani. Kuwa wewe pia jiamini. Usitamani kuwa Magufuli, Kassim Majaliwa au Paul Makonda. Kila mtu ni wa pekee na maalumu. Jikubali kwanza afu wengine ndo watakukubali wewe. Weka nguvu kwenye ubora wako na sio kwenye madhaifu yako. Ukijilinganisha sana utakosa furaha ya nafsi maisha yako yote.

*5. KUWEKA VINYONGO.**

“Kuweka chuki na konyongo moyoni ni sawa na kunywa sumu ukidhani atakufa mtu mwingine”. Onesha upendo, sambaza upendo, hayo ndo mafanikio ya kweli.

6. UONGO

“Uongo utakupa ushindi wa siku moja, ukweli utaishi milele”(WEUSI), “Muongo hata akiongoea ukweli usimuamini”(FID Q). Ukiwa muongo huwezi kufanikiwa hata siku moja. “Unaweza ukawadanganya watu, lakini huwezi kuwadanganya watu wote, wakati wote”(Bob Marley). Ukweli kama jua, katika safari ya mafanikio huwezi kuvificha.

7. UVIVU & UZEMBE

“Nyumba yenye njaa ukisizi unapata zero”(Fid Q). Mafanikio huja kwa kupenda unachokifanya. Neno “kazi” katika biblia limeandikwa mara 600. Dangote analala masaa 3 tu kila siku, Mohammed Dewj anaamka saa 11 asbuhi kila siku. We kwepa majukumu tu, kesho utakula magodoro. “Uvivu unalipa muda huu, bidii & juhudi vinalipa baadae”.

8. STAREHE & ANASA KUPINDUKIA

Pombe, sigara, ngono, unga, bange, shisha, cocaine, nk vitu vibaya sana. Ni ngumu sana kufikia mafanikio makubwa kama una tabia kama hizi. “Sisi ni kile tunacho kula”. Mafanikio ya kwanza huanzia kwenye afya yako”. Afya ni utajiri. Pia starehe hupoteza muda sana. “Mavuno ya uzee, ni swaga za ujana, kwa ukila ujana kumbuka kula kiungwana”(Nikki Mbishi,).

9. LAWAMA & UMBEA

“Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hujadili kuhusu mawazo, uwezo wa kati hujadili kuhusu matukio na wale wenye uwezo wa chini, hujadili kuhusu watu” We upo kwenye kundi gani? Bora ukawa kundi la kati kuliko hilo la chini kabisa, hilo ni la “wachawi”. Tusilamike, tupambane,lawama hazisaidii chochote.Ukiweka malengo yako, vizuri na ukaacha hizo tabia hapo juu, muda si mrefu itazifikia ndoto zako

FURSA HAIJI MARA MBILI: Jinsi unavyoweza kupata faida au hasara ukitumia Nafasi au fursa uliyonayo

Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.

Kufanikiwa kwenye maisha ni matokeo ya kujua
mambo sahihi ya kuyafanya.Ni kama ilivyo wakati
unapotaka kufungua mlango
uliofungwa,unachohitaji ni ufunguo sahihi wa
kutumia na sio vinginevyo.
Ili ufanikiwe lazima uwe mtu mwenye bidii na
ambaye unawathamini watu bila kujali hali zao za
sasa.Ili kutoka hapo ulipo na kwenda kule
unakotaka unahitaji watu wa kukuunganisha na
fursa mpya,kukuonyesha njia nzuri ya kufanya
mambo,wa kukurekebisha na watu ambao
unaweza kujifunza kwao.

Mwaka 2012 mmiliki wa kampuni kubwa ya vifaa
vya michezo ya Modell nchini marekani,bwana
Mitchell Modell alifanya tukio la ajabu sana lililotoa
funzo kubwa la mafanikio katika maisha yetu ya
kila siku.Aliamua kujibadilisha mwonekano wake
kwa kunyoa nywele zake zote na kuweka ndevu
nyingi sana za bandia na pia kuvaa hereni sikio
moja.Kisha baada ya hapo alienda kuomba kazi
kwenye kampuni yake na akaanza kufanya kazi ya
daraja la chini kabisa.
Akiwa ameajiriwa bila watu kujua kuwa ndiye
mmiliki alikutana na wafanyakazi wengi sana wa
aina mbalimbali.Kati ya wafanyakazi katika tawi lile
alikuwepo dada mmoja anayeitwa Angel ambaye
alikuwa ana watoto 3 ila hakuwa anakaa na mume
wake na kwa muda wa miaka 2.Lakini pia,Angel na
watoto wake wamekuwa wanaishi kwenye vibanda
kwani hakuweza kulipia pango kwenye nyumba
nzuri ya kuishi.Gharama zote za
chakula,ada,matibabu na mavazi ya watoto yote
ilikuwa juu yake.
Pamoja na hali yake hiyo,Angel alikuwa ni
mfanyakazi anayewahi kazini kila siku na alikuwa
anafanya kazi kwa bidii sana.Hata wakati wengine
walikuwa wanalamika juu ya mshahara,yeye kazi
yake ilikuwa ni kuwatia moyo na kuwahamasisha
wafanye kazi kwa bidii sana akiamini ipo siku
mambo yatakuwa mazuri.Kila wakati Bwana
Mitchell alipokuwa anamkuta Angel,alikuta
anafanya kazi zake kwa umakini na hata akikuta
anaongea na wenzake basi itakuwa ni kuwatia
moyo na kuwapa hamasa na kuwataka waaache
kulalamika.
Wakati Bwana Mitchell akiwa kama mfanyakazi
mpya alihitaji sana msaada wa kufundishwa jinsi
mfumo unavyofanya kazi na mambo mengine.Kila
mmoja alikuwa hayuko tayari kumfundisha,ila
Angel alikuwa tayari kumfundisha na kumsaidia
hata na kazi ambazo alikuwa hawezi kuzifanya
kutokana na ugeni wake.Na kwa sababu ya ukaribu
wake ndipo alipoweza kumfahamu Angel na
kuyajua maisha yake kwa undani.
Baada ya siku kadhaa za kufanya kazi bila mtu
yoyote kujua kuwa ndiye mmiliki,ndipo alipoamua
kufanya kitu kikubwa kwa Angel.Kwanza
alimpandisha cheo na kumfanya kuwa meneja
msaidizi na kisha alimpa zawadi ya dola laki mbili
na hamsini(Takribani shilingi milioni 500 za
kitanzania) ili aweze kupata nyumba nzuri ya
kuishi.
Baada ya tukio hili kutokea wafanyakazi wengi
sana walijilaumu na walitamani sana kupata fursa
upya kama wangejua kuwa yule alikuwa ni mmiliki.
Ndivyo maisha yalivyo na ndivyo safari ya
mafanikio ilivyo.mara zote huwezi kujua ni wakati
gani fursa kubwa inayohusu maisha yako
itakutokea.Kilichomfanya Angel kufanikiwa ni ile
hali ya kuwa ni mtu ambaye hakuruhusu jambo
lolote limzuie kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi
kila wakati hata kipindi ambacho maisha yake
yalikuwa magumu.
Mara nyingi unaweza kujikuta katika hali ambazo
zinakatisha tamaa na zinakupa uhalali wa kila
namna wa wewe kuwa mtu wa kulalamika na
kukata tamaa.Hebu fikiria mama wa watoto
watatu,analipwa mshahara mdogo lakini bado
anawahi ofisini na huwa halalamiki.Kuna fursa
nyingi kwenye maisha unazikosa kwa sababu ya
malalamiko juu ya hali inayokuzunguka.Kitu cha
msingi unachotakiwa kujua ni kuwa kulalamikia
kitu au mtu hakuwezi kubadilisha hali yako ya sasa
lakini kufanya kwa bidii kunaweza kufungua fursa
nyingi kubwa katika maisha yako.
Inawezekana kazi unayoifanya ni ndogo
ukilinganisha na ndoto kubwa
uliyonayo,inawezekana mshahara unaolipwa sio
mkubwa kama unavyotaka,inawezekana biashara
yako bado haifanyi vizuri kama mipango yako
ilivyo ama hauna mtaji kiwango
unachotaka.Katikati ya hali hii unachotakiwa
kufanya sio kuanza kulalamika na kukata
tamaa,unatakiwa kuwa kama Angel,weka kiwango
kikubwa cha bidii kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajifungulia milango mikubwa zaidi
katika maisha yako.
Kuanzia leo fanya maazimio katika maisha yako
kuwa utakuwa mtu wa kufanya kwa bidii kile
ambacho unakifanya hata kama itakuwa kwenye
mazingira magumu,kwani kwa kufanya hivyo
utakuwa unajitengenezea fursa kubwa sana mbele
yako.Ukiamua kuishi kwa mtazamo huu,muda
mfupi sana ujao utafanikiwa.
Kitu kingine cha msingi cha kukizingatia hapa ni
kuwa usidharau watu katika maisha yako.Kati ya
mafumbo makubwa ambayo Mungu ameyafumba
ni kuhusu hatima za watu ambao tunakutana nao
kila siku katika maisha yetu.Hakuna kitu kibaya
kama kumdharau mtu eti kwa sababu anaonekana
kwa wakati huo hawezi kukusaidia
chochote.Jifunze kumuheshimu na kumthamini
kila mtu.
Ilil ufanikiwe katika maisha yako jifunze kuishi
kama Angel,jifunze kuwa na bidii ya kazi hata
katika mazingira magumu lakini pia jifunze
kuthamini kila mtu ambaye unakutana naye-
Kuanzia mdada wa kazi
nyumbani,mlinzi,mfagizi,kondakta wa daladala
hadi dereva wako.Kila mtu ni muhimu na ana
mchango katika maisha yako.Kanuni ya maisha
inasema-“Husiana na watu kama wewe unavyotaka
watu wengine wahusiane na wewe pia”. Kuanzia leo
ishi na kila mtu kama “Mitshell wako” wa
kukuunganisha na fursa kubwa uliyokuwa
unaisubiria.
Sina shaka kuwa fursa yako kubwa iko njiani
inakuja,usikate tamaa.
Kumbuka kuwa ndoto Yako Inawezekana,
See You AT The Top.
©Joel Nanauka

Jinsi ya Kufuga vizuri kware Kwa Faida

Kware au Kwale au Kereng’ende ni jamii ya ndege ambao kwa sasa wanafugwa majumbani na wanaotaga mayai kama kuku ama bata na kwa wingi sana.

Ndege hawa ni wadogo 280gm – 300gm, rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano.

Chakula

1. Kware anakula chakula chochote anachoweza kula kuku ikiwemo chakula cha broiler. Kama utaamua kuwapa chakula cha broiler unawapa “starter” kware wenye umri kuanzia siku moja hadi wiki ya tatu baada ya hapo unawapa Falcon au hill.

2. Ukiweza kuwatengenezea chakula chako mwenye kutumia pumba nk. Ni vizuri zaidi kwa mayai yenye lishe 100%

3. Kware 100 wenye umri wa mwezi hutumia kiroba cha kilo 20 kwa wiki 3.

4. Kware hawamalizi chakula kama kuku.

5. Pia kware hupewa majani kama mchicha nk.

Kutaga na kuatamia kwa Kware

Kware dume humpanda jike kwa muda kidogo, Hapo jike anakuwa tayari kutaga na hutaga mayai 290 hadi 310 kwa mwaka (hii hulingana na lishe nzuri atakayopatiwa).

Mayai ya Kware huatamiwa kwa siku 18 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 2, kuanzia siku ya 18 na hadi 20.

Njia bora ya kutotolesha mayai ya Kware ni kwa kutumia incubator ambapo mayai huatamiwa kwa wingi ndani ya siku 18.

Utunzaji wa vifaranga vya kware na chakula

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 1 – 7

Vifaranga wapatiwe chakula “STARTER PELLET” na maji masafi ya kutosha. Siku ya 1 wawekee ‘GLUCOSE’ kwenye maji, Packet moja kwa lita 20 za maji, na siku ya pili hadi ya tano wawekee Amin Total kwenye maji, Wape maji pekee siku ya sita na siku ya saba wapatie chanjo ya Newcastle. Utawapatia joto kwa njia ya umeme kwa ‘BULB’ mbili (2) za 200watts kwa kila vifaranga 300, ama unaweza kuweka taa ya ‘Energy Server’ pamoja na jiko la mkaa uliofunikwa na majivu ambao utakidhi kuwapatia joto sawia kwa masaa 24 kwa siku 7. (Majivu yanasaidia moto kukaa kwa muda mrefu)

Banda/box lako liwe la ukubwa wa 1.5m x 1.5m (au eneo la ukubwa huo ndani mwa banda kubwa la kufugia kuku) lazima uzingatie usalama wa vifaranga dhidi ya panya, paka au vicheche. Unatakiwa kuweka magazeti au mabox chini kwenye sakafu yatakayosaidia usafi. Kwa week ya kwanza chakula kitawekwa chini na tunashauri utumie chakula cha pellet ili kusaidia vifaranga wasiteleze na kuathiri miguu. NOTE: Weka gololi au mawe kwenye drinkers zako ili kuzuia vifaranga wasizame ndani ya (drinkers) maji na kufa.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 8-14

Vifaranga wataendelea kupewa chakula “STARTER PELLET” na maji safi. Wataendelea kuhitaji ‘mwanga’ wa kutosha muda wote na joto la wastani bulb 2 za watts 100 au moja ya watts 200

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 15-21

Uhitaji wa joto utapungua, ila ni kipindi ambacho wanakula chakula zaidi kwa ajili ya kukua. Ni vizuri waendelee kupata taa ili kupata mwangaza utakayowawezesha kula mchana na usiku.

Utunzaji wa vifaranga vya kware Siku 21 na Kuendelea

Kware wako hawatahitaji joto tena wawekee taa tu za energy server kipindi cha usiku, wape chakula na maji ya kutosha zaidi kwa ajili ya kukua.

UTAGAJI WA KWARE

WIKI YA SITA

Wiki ya sita kuelekea ya saba Kware wako wataanza kutaga mayai kila siku, kwa wastani Kware mmoja hutaga mayai 300 kwa mwaka.

Magonjwa ya Kware

Kware ni ndege wenye kinga kubwa na ni vigumu sana kushambuliwa na magonjwa kama kuku na mara wanapougua ni rahisi sana kutibika. Magonjwa yanayoweza kuwapata Kware ni typhoid, mafua na kuharisha .

Tiba za asili za kware

Waweza kuwatibu vifaranga au Kware wako kwa kutumia njia ya asili ambayo pia ni rahisi, gharama nafuu na bora zaidi kuliko kutumia madawa yaliyochanganywa na kemikali na yenye gharama.

Vifuatazo ni vitu vya asili vinavyotumika kutibu magonjwa mbali mbali kwa Kware na yanayopatikana kwa wingi katika maeneo ya mfugaji. Madawa haya hutumika kwa kiwango cha wastani na hayana kipimo maalum kwani hata ukiyazidisha hayana madhara.

Mwarobaini na Aloe Vera:

Madawa haya hutumika kutibu kuharisha damu pamoja na mafua kwa vifaranga vya Kware. Chukua kiasi kidogo cha mwarubaini kisha twanga vizuri kupata maji maji. Kamua maji yale, kisha weka katika maji uliyoandaa kuwanywesha vifaranga wako. Kata vipande vidogovidogo vya aloe vera (jani moja laweza kutosha) na tia katika maji yaliyochanganywa na mwarobaini, kisha wapatie vifaranga wanywe (Aloe Vera itaendelea kujikamua yenyewe ikiwa ndani ya maji huku vifaranga wakiendele kunywa).

Kitunguu swaumu:

Hii hutumika kukinga na kutibu vifaranga vya kware wanaosumbuliwa na kuharisha damu. Unachukua kitunguu swaumu na kuondoa maganda ya nje kisha kusafisha na kukata vipande vidogo sana, na kuwawekea kama chakula. Vifaranga wanapenda sana vitunguu hivyo na watakula kwa kasi kama chakula lakini ni tiba tayari. Unaweza kuwapatia kila siku hadi watakapo pona.

Maziwa:

Maziwa yanayotokana na ng’ombe pia hutumika kutibu ugonjwa wa kuhara pamoja na kuwapa nguvu Kware waliolegea. Mnyweshwe maziwa hayo Kware anayeumwa bila kuyachemsha na umnyweshe maziwa ya kutosha kiasi cha kushiba. Unamnywesha mara tatu kwa siku. Hakikisha maziwa unayotumia yanatoka kwa ng’ombe wanaotibiwa kila mara.

Angalizo

Siyo lazima Kware waugue ndipo uwapatie tiba hizi. Hakikisha unawapa tiba kabla hata hawajaugua hivyo utawakinga na magonjwa hayo. Waweza kuchanganya madawa hayo yote kwa wakati mmoja kwani hayana madhara.

Endapo madawa ya asili hayapatikani katika eneo la mfugaji basi waweza kuwatibu Kware kwa madawa yafuatayo ambapo vipimo huelezwa moja kwa moja kwa maandishi katika madawa hayo au kuelezwa na muuzaji pale utakaponunulia; Amprolium kwa ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis), Fluban,Coridix au Doxyco kutibu mafua (Coryza) na Esb3,Trisulmycine au Trimazine hutumika kwa homa ya matumbo (Typhoid).

ZINGATIA:

Wanapokosa madini ya kutosha kwenye chakula huweza kupata madhara yafuatayo:-
1. Kuharisha
2. Kunyonyoka manyoya
3. Kupunguza kasi ya kutaga mayai.

Chanjo Ya kware

Siku ya 7 lazima vifaranga wapatiwe chanjo ya “kideri/mdondo”
(respiratory & digestive diseases) kwa dawa inayoitwa ‘newcastle’. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 14 lazima wapewe chanjo ya “gumboro”. Chanzo cha
maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 21 lazima warudie chanjo ya “Newcastle (aina ya IBDL)”. Chanzo cha maambukizi ni maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi na pia husababishwa na virusi kwa njia ya hewa.

Siku ya 35 lazima wapate chanjo ya “Ndui”.

Soko la kware

Mayai ya Kware ni bidhaa adimu sana hapa nchini kwa kuwa ni wafugaji wachache waliojikita katika ufugaji huu, Ufuatao ni muhtasari wa wastani wa bei ya bidhaa za Kware sokoni

1. Trei ya (mayai 30) ya KWALE inauzwa shilingi 30,000 .
2. Kifaranga wa Kware wa siku moja anauzwa shilingi 2500 – 3000
3. Kware wa week 4 (mwezi mmoja) anauzwa kwa shilingi 10,000– 12,000
4. Kware aliyeanza kutotoa (week 6) huuzwa shillingi 20,000 – 25,000
5. Kware kwa aliyekomaa kwa ajili ya kitoweo huuzwa kwa shilingi 25,000
6. DROPING za Kware huuzwa kwa shilingi 10,000 kwa 50kg kwa wafugaji wa samaki

Soko la KWALE liko juu sana kwa mayai na nyama. KWALE pia hutofautiana bei kwa jike na dume.

FAIDA ZA KUFUGA KWALE

Ufugaji wa kwale hua na faida ukilinganisha na ufugaji wa ndege wengine

· Chanzo cha kipato kwa wafugaji.
· Hawana gharama sana katika suala kufuga.
· Hawataji utaalam sana katika kuwafuga.
· Mayai yake ni tiba ya magonjwa mbalimbali.
· Mayai yake hayakosi soko.

SALA MBELE YA SAKRAMENTI KUU II

Yesu, Mungu wangu mpenzi,/ upo hapa katika Altare mbele yangu;/ na mimi napiga magoti mbele yako.// Waniangalia sana,/ siyo kwa kunipeleleza,/ lakini kwa sababu wapenda kuniona hivi karibu na wewe,/ wafurahiwa nikija kukuabudu./ Wayasikiliza maneno yangu yote/ yenye kutoka mdomoni mwangu,/ na zaidi wapokea maneno yangu yanayotoka moyoni./ Nataka kuzungumza na wewe peke yako,/ na kusahau mambo mengine yote/ na watu wengine walioko kanisani pamoja nami./

Yesu wangu,/ nakushukuru/ kwa sababu umekubali kutupa Sakramenti hii kuu kabisa,/ ukitaka kukaa pamoja na sisi,/ na hata ukakubali kuwa chakula chetu/ chenye nguvu ya ajabu./ Mfalme wangu Yesu,/ Sultani wangu Mkuu,/ naamini kabisa kwamba upo katika Altare/ na kwamba umejificha chini ya umbo la mkate./ Ulipokuwapo bado hapa duniani mbele za watu,/ ulikuwa hujifichi kama sasa;/ lakini hata siku zile/ watu hawakuweza kukuona vile ulivyo./ Hawakuweza kuutambua Umungu wako,/ ikalazimu kukuamini tu sawa kama sisi./ Wakainama kichwa wakisema,/ “Bwana wangu na Mungu wangu”./ Na mimi kadhalika naungama/ U Bwana wangu na Mungu wangu/ na Mkombozi wangu/ na salama yangu yote./ U Yesu wangu tu,/ siwezi kusema zaidi./ Nakuabudu ee Yesu./ Najua sana, mimi ni mdogo kabisa,/ sina maana hata kidogo./ Mimi ni dhaifu na maskini mno./ Lakini Wewe katika hruuma yako kubwa/ waniita nije kwako./ Wewe huuangalii umaskini wangu,/ bali wanivuta katika mapendo yako./

Nasikia maneno yako usemayo:/ “Njooni kwangu ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo/ nami nitawasaidia”./ Kwa ajili ya maneno hayo/ nakuja kwako bila hofu./ Najua kwamba wanipenda,/ najua wataka kunisaidia na kuniponya,/ najua kuwa wataka kunitakasa./

Nahitaji sana msaada wako, hakika./ Unaniona katika mwendo wangu wa kila siku,/ Jinsi ninavyohangaika na vishawishi mara nyingi;/ jinsi nilivyo na lazima ya kushindana kila siku/ nikitaka kukaa mwema na safi katika utumishi wako./ Naungama mbele yako Wewe Mkombozi wangu,/ kwamba sikukaa imara siku zote vile nilivyopaswa./ Naungama kwamba nimeshindwa mara nyingine/ na kwa hivi naomba toba./ Lakini kwa nini nimeshindwa mara nyingine?/ Kwa nini nikakosa?/ Ni kwa sababu nalikuwa nimekwenda mbali nawe;/ nalianza kujitegemea mwenyewe./ Katika majivuno yangu nikajisifu mwenyewe,/ nikajiona mwema,/ nikasahau udhaifu wangu./ Na kwa ajili hiyo nikajitia katika hatari bure,/ sikujilinda tena,/ nikampa shetani nafasi ya kunishambulia kwa hila zake zote./ Unihurumie ee Yesu wangu./

Sasa nafahamu jinsi nilivyokuwa mjinga kwelikweli./ Ndiyo maana nakuabudu kwa moyo wangu wote./ Najiweka mikononi mwako/ ufanye nami vile unavyotaka./ Wewe utanitunza;/ Wewe utanilinda vema;/ Wewe utaniongoza nijue namna ya kuepa hatari zote,/ na jinsi ya kufukuza kila kishawishi./ Chukua moyo wangu kabisa,/ kwa sababu ni mali yako kamili;/ Wewe ndiwe uliyeniumba,/ ndiwe uliyenipeleka katika Ukristo,/ nawe ndiwe utakayenihukumu siku ya mbele./ Ndivyo ninavyojitolea kwako./ Ndivyo ninavyokuabudu,/ wala sijui njia nyingine ya kukusifu zaidi./

Yesu wangu mpenzi,/ naomba upokee kwa uzuri heshima hiyo yangu./ Angalia: naitolea pamoja na heshima yote/ unayopewa daima na watakatifu wako/ na malaika wako./ Nikipiga magoti hapa mbele yako sasa,/ siko peke yangu,/ nakuabudu pamoja na Mama yako Bikira Maria,/ ambaye sala zake zinakupendeza kabisa./ Sala zangu naweka pamoja na sala zake yeye,/ uzipokee zote pamoja,/ zikupendeze zote sawa./ Ee Mama Maria!/ Nifundishe maneno ya kumsifu Mwanao Yesu vizuri./ Nipeleke kwa Yesu tumwabudu pamoja./ Nifunike na utakatifu wako/ kusudi Yesu asiangalie tena umaskini wangu/ na makosa yangu,/ aniponye katika huruma yake./

Sasa najisikia vizuri, Yesu wangu./ Sasa nina moyo wa kuweza kuendelea vema/ katika njia njema./ Sasa ninatumaini kwamba/ nitakaa mkristo mwema,/ nitakuwa mtumishi wako mwaminifu./ Nasikia amani kubwa sana moyoni mwangu,/ kwa kuwa nimo mikononi mwako./ Baada ya dakika chache/ nitaondoka tena kanisani,/ nitarudi nyumbani kwangu,/ lakini hatutaachana,/ hapana./ Mapendo yetu yatatuunganisha pamoja daima./ Wewe utanikumbuka nikiwa kazini,/ nikilala usingizi,/ nikienda njiani,/ kila mahali nilipo,/ Wewe utaniona,/ utafuatana na mimi./ Kadhalika nitakukumbuka tu./ Nitafanya bidii nisikuache kabisa./ Amina.

SALA YA KUMWABUDU BWANA YESU KATIKA SAKRAMENTI TAKATIFU

Ee Yesu Kristu,/ Bwana wangu na Mungu wangu/ ambaye ninasadiki kuwa upo hapa/ katika Sakramenti Takatifu ya Altare;/ pokea kitendo hiki cha kukuangukia kifudi fudi/ kama ishara ya tamaa niliyonayo ya kukuabudu Wewe/ bila kuchoka/ na kukushukuru kwa mapendo yako makubwa/ yasiyo na kipimo/ ambayo Moyo wako Mtakatifu sana/ unawaka katika Sakramenti Takatifu hii./ Siwezi kukushukuru vizuri zaidi/ kuliko kama ningetolea kwako/ matendo yangu yote ya kukuabudu/ unyenyekevu wangu/ uvumilivu na mapendo/ ambayo huu Moyo Mwabudiwa ulifanya,/ bado unafanya/ na utaendelea kufanya katika uzima wa milele mbinguni./ Ninaahidi kupitia Moyo huu,/ nitakupenda,/ nitakutukuza,/ na nitakuabudu kama nitakavyoweza./ Ninajiunganisha na hii Sadaka Takatifu/ ambayo unatoa kwa Baba Mungu/ na ninatolea kwako utu wangu./ Ninakuomba kuangamiza ndani yangu/ dhambi zote pamoja na majeraha yake/ na usikubali kunitenga nawe milele./ Amina.

(Na Mt. Margareta Maria Alakoki)

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU KWA SIKU ZOTE TISA

Ufuatao ni mtiririko wa Novena ya Roho Mtakatifu kwa siku zote tisa.

Kusali novena hii unaanza nia wimbo/nyimbo kisha unasali sala ya kila siku na kumalizia na litania na Atukuzwe Baba….x3 kwa siku zote tisa.

BAADHI YA NYIMBO KWA ROHO MTAKATIFU

NJOO WANGU MFARIJI

/Njoo wangu Mfariji
Yako shusha mapaji
Roho Mungu njoo/

1. Hekima nishushie, Mungu nimfuatie, Roho Mungu njoo
2. Akili nijalie, imani nizidie, Roho Mungu njoo
3. Nieneze shauri, imani nizidie, Roho Mungu njoo
4. Nizidishie nguvu, nsifanye ulegevu, Roho Mungu njoo
5. Elimu nieleze, hakika niongoze, Roho Mungu njoo
6. Ibada niwashie, Peke nikupupie, Roho Mungu njoo
7. Uchaji nitilie, dhambi nizichukie, Roho Mungu njoo.


NJOO ROHO MTAKATIFU

/Njoo Roho Mtakatifu, shusha mapaji (kweli) niwe imara x2
Leta nuru ya mwanga wako, ifikie moyoni mwangu x2/

1. Roho mwenye hekima, Roho wa shauri na nguvu
2. Nipatie elimu nitambue nafsi yako
3. Nipatie ibada nikusifu daima milele
4. Roho mwenye uchaji washa moto wako wa mapendo

UJE ROHO (SEKWENSIA)

1. Uje Roho Mtakatifu, tuangaze toka mbingu, roho zetu kwa mwangao
2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, uje mwanga wa mioyo
3. Ee Mfariji mwema sana, ee Rafiki Mwanana, ewe raha mustarehe
4. Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto burudisho, u mfutaji wa machozi
5. Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waumini, neema yako mioyoni
6. Bila nguvu yako Wewe, mwanadamu hana kitu, kwake yote yana kosa
7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, na kuponya majeraha
8. Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi, nyosha upotovu wote
9. Wape waamini wako, wenye tumaini kwako, paji zako zote saba
10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila hila, wape heri ya milele.
11. Amina aleluya, amina aleluya, amina aleluya.

NJOO ROHO MTAKATIFU

1. Njoo Roho Mtakatifu, angalia zetu nyoyo, waletee neema nguvu, wakosefu viumbevyo.
2. Majina yako Mfariji, shina la uzima pendo, wake Mwenyezi upaji, mafuta ya roho moto
3. Ndiwe mnye mapaji saba, wa Mungu kuume mkono, mshika uhadi wa Baba, mtoa kwa ndimi maneno
4. Angalo litung’arie, moyo kwa pendo tushushe, nguvu neema tujalie, wanyonge wasabilitishe
5. Shetani mbali mkimbize, amani utupatie, tukufuate tuongoze, maovu utukingie
6. Baba Mungu tujulishe, pia Mwana tumkubali, Roho tukuungamie, mtokea wao wawili.

NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA KWANZA, IJUMAA

ROHO MTAKATIFU ANATUFARIJI

Yesu alipokuwa akiagana na mitume wake, kabla ya kupaa mbinguni, aliwaambia wasiondoke Yerusalemu mpaka hapo watakapokuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Aliwaambia: “Wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni, mtajazwa nguvu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yuda na Samaria, hata kwenye mipaka yote ya dunia.” (Mdo.1:8)

Waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni mpaka siku ya Pentekoste. Waliomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze na mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho Mtakatifu aliwashukia hao kundi dogo nao wakawa chanzo cha Kanisa lililopata kuenea duniani kote.

Siku hizo tisa za kusali zinaitwa NOVENA; na kila mwaka wakati huu, wakristu wakifuata mfano wa mitume, wanasali muda wa siku tisa kabla ya Sikukuu ya Pentekoste. Wanamuomba Roho Mtakatifu awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake.

Wakati huu wa NOVENA , Tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na kujiombea sisi wenyewe. Kwa hiyo tumuombe Roho Mtakatifu atusaidie kusali vema na kuomba yale yote tunayohitaji kwa maslahi yetu ya roho na mwili.

Na kama mtume Paulo alivyowaambia wale waKristu wa kwanza, Roho Mtakatifu huja kutufatiji katika udhaifu wetu. Basi tumuombe atufariji kwa sala hizi za NOVENA, Atuwezeshe kusali na kuomba inavyotupasa kusali.

1. Ee Baba wa milele, tunakuomba umtume Roho Mtakatifu atushukie sisi taifa lako awashe ndani yetu moto wa upendo wako.
W. Twakuomba utusikie.

2. Ee Baba mwema, tunakuomba utujalie faraja ya Roho Mtakatifu sisi wana tulio katika dhiki na taabu nyingi mno hapa duniani.
W. Twakuomba utusikie.

3. Ulijalie Kanisa lako mapaji ya Roho wako Mtakatifu, liweze kutekeleza vema utume wake wa kuhudumia watu wote hapa duniani.
W. Twakuomba utusikie.

4. Utujalie sisi kudumu katika NOVENA hii mpaka mwisho kama Maria na mitume walivyodumu pamoja wakisali kabla ya Pentekoste ile ya kwanza.
W. Twakuomba utusikie.

5. Utujalie neema zote zinazohitajika ili tuweze kumshuhudia Kristu popote kwa mwenendo na matendo yetu ya kila siku, tukiongozwa na Roho Mtakatifu.
W. Twakuomba utusikie

6. Uzijalie familia zote za wakristu neema na nguvu za Roho Mtakatifu tupate kuendelea pasipo kuchoka katika sala na katika matendo mema siku zote.
W. Twakuomba utusikie

7. Ewe Roho Mtakatifu, uwajalie vijana wetu moyo wa ujasiri, wapate kulijenga kanisa lako na kueneza utawala wako katika jumuia zetu za Kikristu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Mungu, uliye muumba wa vitu vyote , tunakuomba utusikilize kwa wema sala zetu sisi taifa lako, utuongoze sote tufuate siku zote utaratibu wa mapenzi yako; naye Roho Mtakatifu atutegemeze mpaka mwisho wa novena hii. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu .
W. Amina.

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA PILI, JUMAMOSI

ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUENEZA INJILI

“Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika utawala wa Mungu,” (Yn. 3:5).

Kanisa limepewa na Yesu ujumbe wa kuwaletea watu wote uzima mpya, uzima wa Mungu. Yesu aliwaambia mitume wake: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni basi mkawafanye watu wa makabila yote kuwa wafuasi wangu. Wabatizeni kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Wafundisheni kuyashika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote mpaka mwisho wa nyakati (Mt.28: 18-20).

Sisi tuliobatizwa tumepata kuwa viungo vilivyo hai vya Mwili wa Fumbo wa Kristu; kwa Kipaimara tumeimarishwa na kuthibitishwa na Roho Mtakatifu. Tumekuwa taifa teule. Tumeshirikishwa ule ukuhani wa Kristu. Tumepokea ujumbe wa kueneza utawala wa Mungu.
Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakmenti ya Ekaristi, tunalisha imani na kuongeza mapendo, ambayo ni msingi wa utume wowote ule. Mapendo yanatuhimiza kueneza utawala wa Mungu na kumpenda Yesu Kristu aliyekuja kuwakomboa wanadamu wote.

Kila aliyebatizwa anao wajibu wa kueneza imani ya Mungu na utawala wake. Kwa hiyo tumuombe Roho Mtakatifu atuwezeshe kutimiza wito huo.

1. Ee Baba wa mbinguni tunakuomba umpeleke Roho Mtakatifu aliangaze kanisa na kuliongoza, liweze kuwafikishia mataifa yote habari njema ya wokovu.
W. Twakuomba utusikie

2. Ee Yesu Mkombozi wetu, umtume Roho Mtakatifu awahimize wakristu wapate kutimiza wajibu wao wa kueneza neno lako popote duniani
W. Twakuomba utusikie

3. Ewe Roho Mtakatifu Mfariji, uamshe katika mioyo ya vijana wengi hamu ya kupenda kulitumikia kanisa lako na kulihudumia taifa lako kwa uaminifu.
W. Twakuomba utusikie

4. Ewe mwanga wa mataifa , uwajalie wanafunzi wasikie sauti yako mioyoni mwao, nawe unapowaita wasikose kuisikia sauti yako, wawe tayari kujitoa kwa ajili ya ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie.

5. Uwasaidie wazazi wawalee vema watoto wao; uwatie moyo katika wito wao, wapate pia kuishiriki vema ile kazi ya kueneza neno lako kwa jirani zao.
W. Twakuomba utusikie

6. Ewe Roho Mtakatifu, uwasaidie wakristu wote kueneza habari njema ya wokovu, kwa sala, kwa sadaka na kwa mifano ya maisha yao ya uchaji.
W. Twakuomba utusikie

7. Ewe mpaji wa mema, uwajalie waumini mapaji yako saba, wasichoke kulieneza neno lako kwa hekima pasipo hofu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Mungu, unapenda watu wote waokoke, waifikie kweli yako. Tunakuomba uwapeleke wafanyakazi walio wengi na wema katika shamba lako. Uwajalie kulihubiri neno lako kwa imani kuu ili neno lako lienee na kupokewa na mataifa yote, wapate nao kukujua wewe peke yako Mungu wao, Mungu wa kweli. Tunaomba hayo kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeliongoza kanisa lako sasa na milele.
W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TATU, JUMAPILI

ROHO MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME

Bwana alisema kwa kinywa cha nabii Yoeli; “Katika siku zile za mwisho asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu. Watoto wenu, waume kwa wake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto….hata watumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika siku zile, nao watautangaza ujumbe wangu. (Mdo.2:17-21)

Siku ile ya Pentekoste, bada ya Roho Mtakatifu kulishukia kanisa, mitume waliwakumbusha watu maneno haya ya nabii Yoeli, na miaka mingi baadae, Petro aliwaandikia barua Wakristu wa kwanza akawaambia; kila mmoja anapaswa kutumia kipaji alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili mwema wa zawadi mbali mbali za Mungu. Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele (Pet 4;10-11).

Mtaguso wa Pili wa Vatikano ulitukumbusha jambo hilo hilo uliposema; “Roho Mtakatifu anayetakasa taifa la Mungu kwa njia ya Sakramenti amewapa waumini mapaji ya pekee na kumjalia kila mmoja kadiri apendavyo. Kwa hiyo kila mmoja amgawie mwenzake kadiri ya vipawa alivyopewa, awe mgawaji mwaminifu wa neema ya Mungu, alijenge kanisa zima katika upendo.

Tunao wajibu wa kutumia vipawa tulivyojaliwa na Roho Mtakatifu kwa manufaa ya kanisa zima, na kwa faida ya watu wote. Tuunganike sote pamoja na wachungaji wote katika kazi hiyo ya utume. Tumuombe basi Roho Mtakatifu atusaidie kutumia vema vipawa vyake alivyotujalia.

1. Ewe Roho Mtakatifu uwape wakristu neema na nguvu za kutumia vema vipaji ulivyowajalia kwa ajili ya kujenga kanisa lako popote duniani, kwa ajili ya wokovu wa watu wote
W. Twakuomba utusikie

2. Utujalie sisi sote mapaji yako saba, tupate kukutumikia kwa uchaji
W. Twakuomba utusikie

3. Utujalie tuwe mitume wa kweli wa wenzetu, tushirikiane na wachungaji wetu katika huduma za kuwaongoza watu wote na kuwafikisha mbinguni
W. Twakuomba utusikie.

4. Utujalie hekima na nguvu za kuwahudumia watu wote kwa mapendo ya kweli yasiyo na kinyume
W. Twakuomba utusikie

5. Utujalie neema ya kumpenda Mungu kwa moyo wote na kuwapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe
W. Twakuomba utusikie

6. Utupe neema ya kulisikia neno lako na kulifuata, nayo mawazo yetu na matendo yetu yafuate daima mwongozo wako mtakatifu
W. Twakuomba utusikie

7. Uwazidishie mapaji yako wale wote wanaotumia vyema vipawa vyao, uwarudishe na wale wanaotumia vibaya rehema zako

W. Twakuomba utusikie

=== TUOMBE;
Ewe Roho Mungu ndiwe uliyewapa waumini vipawa vyako kwa kadiri unavyotaka. Utujalie tuyapokee na kuyatumia vyema mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina lako na kwa ajili ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
W. Amina

Litania ya Roho Mtakatifu …. (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NNE, JUMATATU

ROHO MTAKATIFU ANALIUNGANISHA KANISA

“Atakapokuja huyu Roho wa kweli , atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yn 16:13)

Baada ya kusema hayo, Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni akasema “Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba Wewe ulinituma (Yn 17:4,21).

Nasi twamuomba Mungu Mwenyezi alijalie kanisa lake umoja wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote katika zizi moja chini ya mchungaji mmoja.

Popote duniani watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa Kanisa. Hata ndugu zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho Mtakatifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja chini ya mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona kwamba kwa namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu, naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kumshuhudia hata kwa kumwaga damu yao.

Tena katika hao ndugu zetu waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha katika mioyo yao ile ya imani inayowaunganisha wafuasi wote wa Kristu. Tumwombe basi Mwenyezi Mungu atujalie hima huo umoja wa Kanisa lake tunaouania mno.

1. Ee Yesu Bwana wetu wewe umetuombea kwa Mungu Baba tuwe itu kimoja kama Wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie huo umoja, ili ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana na Mkombozi wa watu wote
W. Twakuomba utusikie

2. Ee Yesu utujalie moyo wa kulishika neno lako kwa uaminifu, wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
W. Twakuomba utusikie

3. Ee Yesu uliye Mchungaji wetu mwema, ondoa ndani yetu ile tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako wewe uliye mchungaji wetu mmoja.
W. Twakuomba utusikie

4. Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie wachungaji wetu wawe siku zote na upendo wa Jina lako, wasichoke kulichunga vema kundi lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane
W. Twakuombaa utusikie

5. Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za watu wote, wapende siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano
W. Twakuomba utusikie

6. Ee Mungu, utufungulie …… wa muungano wako wa kweli sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
W. Twakuomba utusikie

7. Utujalie mapatano na amani, tudumu tumeungana katika familia zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Mungu, utuunganishe sisi kondoo wako tuliotawanyika, tuwe chini ya Mwanao mpenzi, tupate sote kuushiriki ule utawala wako wa kweli na haki, utawala wa neema na amani, utawala wa upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu

W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU …. (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TANO, JUMANNE

ROHO MTAKATIFU ANAWATAKASA WAUMINI

Walio wa Mungu watafuata yaliyo ya Mungu, na walio wa dunia hufuata yaliyo ya dunia,. Ni mauti kutosheka na mambo yaliyo ya dunia. Uzima na faraja ya kweli hupatikana tu katika mambo ya Mungu.

Kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote jema. Kuweza kwetu kwatoka kwa Mungu, kwatoka kwa Yeye anayetupa kujua, kupenda na kutenda.

Mtu anapotenda dhambi, hawezi kuongoka ila kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ndiye anayempa mkosefu neema ya kutambua ubaya wa kosa lakena kuamua kuliacha. Ndiye anayempa pia mkosefu kutambua uzuri wa neema aliyoipoteza na kumrudishia neema hiyo. Ndiye anayempa nguvu za kuidumisha neema hiyo na kuiongeza.

Isitoshe, Roho Mtakatifu ndiye anayemuwezesha mtu kuwa na maendeleo katika fadhila na utakatifu. Ndiye anayemjalia imani iliyo msingi wa maisha ya kiKristu. Ndie anayetujalia akili ya kushika mafumbo ya dini yetu na kuishi imani yetu mpaka kufa.

Lakini imani peke yake haimtoshi mtu aokoke. Imani pasipo matendo haifai kitu; imani bila matendo imekufa (Yak 2:28) Roho Mtakatifu anamuwezesha mtu kumuamini Mungu na kumenda kuliko vitu vyote na kumpenda jirani kama kujipenda mwenyewe. Ndiyo maana Roho Mtakatifu huitwa chanzo cha matendo yetu yote yaliyo mema. Basi, tumuombe Roho Mtakatifu aitakase mioyo yetu sisi waumini wake, atuzidishie imani, atuwezeshe kutenda matendo yaliyojaa imani.

1. Ewe Roho Mtakatifu, utudumishie imani, uyatakase mawazo ya mioyo yetu yafuate daima maongozi yako na amri zako
W. Twakuomba utusikie

2. Uzigeuze nia zetu zipate kumuelekea daima Mungu
W. Twakuomba utusikie

3. Utuwezeshe kuelekea katika utakatifu na kutenda mema kwa imani siku zote za maisha yetu
W. Twakuomba utusikie

4. Utuzidishie imani matumaini na mapendo, tuweze kushika kwa moyo thabiti yale yote tunayofundishwa na kanisa lako takatifu
W. Twakuomba utusikie

5. Uiwashe mioyo yetu na moto wa mapendo yako, tupate kumpenda Mungu kweli na kumpenda jirani yetu pasipo unafiki.
W. Twakuomba utusikie

6. Utusaidie tuishi vema kwa imani na matumaini siku zote za maisha yetu
W. Twakuomba utusikie

7. Utujalie kudumisha mioyoni mwetu ile neema ya utakaso tuliyoipata mwanzo katika ubatizo wetu
W. Twakuomba utusikie

TUOMBE;

Ee Mungu, mbele yako mioyo yetu i wazi; wewe wayajua yote, wala hakuna siri iliyofichika mbele yako. Uyatakase mawazo ya mioyo yetu kwa kutupelekea Roho Mtakatifu, ili tuweze kukupenda na kukutukuza kama inavyostahili. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu

W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SITA, JUMATANO

ROHO MTAKATIFU ANATUPA NGUVU

“Nitamuomba Baba , naye atawapelekea Mfariji mwingine atakaye kaa nanyi siku zote”. Katika maisha yenu hapa duniani tunahitaji mno kitulizo cha Mungu. Ni jambo la hekima kutafuta kitulizo hicho kwa Mungu wala si kwa viumbe; maana kitulizo kinachopatikana kwa viumbe hapa duniani hakidumu; bali kitulizo kitokacho kwa Mungu ni cha kudumu.

Roho Mtakatifu ndio kitulizo chetu cha kweli. Baba ndiye aliyetuumba, Mwana ndiye aliyetukomboa, Roho Mtakatifu ndiye aliyetutakasa mioyo yetu na kutufariji.

Kazi ya Roho Mtakatifu sio tu kuwatuliza wale walio na huzuni, bali pia kuwapa moyo wa kuvumilia taabu zozote kwa saburi.

Tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi maisha mema ya kikristu. Katika juhudi zetu za kumtumikia Mungu mara nyingi tunakutana na shida; naye Roho Mtakatifu ndie anayetufariji kwa kutupa nguvu za kupambana na matatizo yote. Maisha yetu hapa duniani yamejaa misalaba. Na misalaba hiyo hatuwezi kuichukua kwa nguvu zetu wenyewe. Roho Mtakatifu ndie anayetupa nguvu za kuvumilia. Basi, tumuombe aje kutufariji na kutupa nguvu za kuchukua msalaba wetu kwa saburi kila siku.

1. Ee Yesu Bwana wetu, tunakusihi Wewe na Baba mumtume Roho Mtakatifu atufariji, awajalie kitulizo wale wote walio katika taabu na majonzi
W. Twakuomba utusikie

2. Ewe Roho Mtakatifu, uwafariji wale walio katika tabu za namna zozote ili waweze kuvumilia kwa saburi mateso yao kwa faida ya Roho zao na roho za ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie

3. Uwafariji wale walio wagonjwa, uwajalie afya ya roho na ya mwili
W. Twakuomba utusikie

4. Uwasaidie yatima, wajane na wote walioachwa, wasikose kupata siku kwa siku mahitaji yao ya lazima
W. Twakuomba utusikie

5. Wajalie wale wote walio walegevu na wakosefu neema ya kuongoka na kurejea hima katika amani ya upendo wako
W. Twakuomba utusikie

6. Uwaimarishe wale walio wema, uwajalie neema ya kudumu wasilegee katika kutenda mema leo na kesho na siku zote za maisha yao.
W. Twakuomba utusikie

7. Utujalie nguvu za kutafuta na kudumisha amani ya kweli katika mioyo yetu na kati ya ndugu zetu katika jumuia zetu za kikristu
W. Twakuomba utusikie

TUOMBE;

Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba neema ya Roho Mtakatifu ituangaze akili na mioyo yetu na kutujaza nguvu ya upendo wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA SABA, ALHAMISI

ROHO MTAKATIFU ANATUPA HEKIMA

Hekima tunayopewa na Roho Mtakatifu si sawa kama hekima inayopatikana katika ulimwengu huu.

Hekima ya Roho Mtakatifu ni ile Mtk. Paulo aliyowaambia Wakorintho ya kuwa; ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana kama wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo maandiko; mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio kuyasikia mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni, hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao (1Kor 2;8-9).

Mtk. Paulo alisema kama vile roho ya mtu ndiyo yenye kufahamu na kutambua yaliyo ndani yake; hivyo pia Roho Mtakatifu ndiye anayefahamu mambo ya Mungu na kutufumbulia sisi mioyoni mwetu.

Katika Sikukuu hii ya Pentekoste tunatazamia kumpokea Roho Mtakatifu. Yeye aliye hekima ya Mungu atatufumbulia siri za Mungu na ukweli wake. Ndiye atakayeamsha ndani yetu mapendo ya Yesu Msulibiwa , Mkombozi wetu. Ni yeye atakayetuongoza kutenda mema na kuacha mabaya; tunahitaji sana Roho Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku, tupate hekima ya kuchagua na kutenda daima yaliyo mema. Katika novena hii tuzidi kumuomba Mungu atushushie Roho Mtakatifu, atujaze na hekima yake.

1. Ee Mungu, uwabariki viongozi wa dini na wasaidizi wao, wapate kutuongoza kwa hekima na mapendo
W. Twakuomba utusikie

2. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie hekima ya kutambua Mambo ya Mungu na kuyatekeleza kwa uchaji
W. Twakuomba utusikie

3. Utujalie kuyajua mapenzi ya Mungu na kuyapokea kwa furaha
W. Twakuomba utusikie

4. Uamshe ndani yetu mapendo ya Yesu msulibiwa , utuwezeshe kutimiza vema wajibu wetu kama wafuasi wa kweli wa Kristu Bwana wetu
W. Twakuomba utusikie

5. Utuwezeshe kuchagua daima yaliyo mema na kuyatekeleza, tupate kulijenga na kulidumisha kanisa lako hapa duniani
W. Twakuomba utusikie

6. Utuepushe na mafundisho yoyote yaliyo na upotovu, utujalie hekima ya kuzidi kutambua ukweli wako na mafundisho yako yaletayo wokovu
W. Twakuomba utusikie

7. Hekima ya Roho Mtakatifu ituongoze katika satfari ya maisha yetu hapa duniani, tupate mwishowe kukurudi Wewe Muumba wetu uliye mwanzo wetu na mwisho wetu
W. Twakuomba utusiki

TUOMBE;

Ee Mungu, Baba wa utukufu, tunakuomba utupe Roho wako wa hekima, atuwezeshe kukufahamu vema, atuongoze kuishi maisha yenye kukupendeza. Utusaidie kupambana na matatizo ya maisha, tupate kuishi maisha mema hapa duniani na mwisho tupate tunzo la heri na furaha yako huko mbinguni. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

W. Amina.

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA NANE, IJUMAA

ROHO MTAKATIFU ANATUPA MWANGA.

Roho Mtakatifu anaangaza akili zetu tuweze kuona ukweli wa Mungu na kuufata. Bila Roho Mtakatifu akili zetu zimo katika giza nene, wala hatuwezi kuona njia ya kutuelekeza kwa Mungu.

Mungu alipoumba ulimwengu, dunia ilikuwa giza tupu, haina kitu. Mungu alisema; “Iwe nuru”, ikawa nuru, Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema (Mwa 1;3-4) vivyo hivyo akili ya binadamu bila nuru ya mwanga wa Roho Mtakatifu, ni tupu, ina giza, haiwezi kuona mambo yanayotuelekeza kwa Mungu. Tukiwa na nuru ya Roho Mtakatifu tunaona ukweli wa Mungu jinsi ulivyo.

Roho Mtakatifu anapoijia roho ya mtu, anaiangaza akili yake iweze kuona mambo yanayofaa kwa wokovu. Naye akiisha kuiangaza akili ya mtu huimarisha utashi wake na kumwezesha kuchagua daima yaliyo mema.

Roho Mtakatifu huiangaza akili iweze kuona ukweli. Kabla ya kuwaaga mitume, Yesu aliwaambia kuwa atawapelekea mfariji mwingine atakayekaa nao siku zote. Roho wa kweli ambaye dunia haiwezi kumpokea kwa sababu hawakumfahamu, lakini wao mitume watamfahamu kwa maana atakaa nao siku zote. Yesu ametuahidi pia sisi Roho huyo akae nasi
Leo hivi duniani kuna uwongo na udanganyifu mwingi; kuna dhuluma, vita, na maovu ya kila namna. Hii ni kwa sababu dunia haijamtambua bado Roho Mtakatifu na kumpokea Yeye aliye mwanga wa dunia na asili ya kweli yote.

Mtaguso wa Pili wa Vatikano watambua ya kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika kanisa na katika mioyo ya waumini kama katika hekalu. Roho Mtakatifu analiongoza kanisa na kulifanya liwe na umoja; analipamba na mapaji yake mabalimbali.

Tumuombe Mungu Baba ampeleke huyo Roho Mtakatifu katika kanisa lake, aliongoze na kulilinda lisipate kutengana, bali lisaidie kueneza utawala wa Mungu popote duniani.

1. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie kuona mwanga wa kweli yako na kuifuata
W. Twakuomba utusikie

2. Uwape waregevu neema ya kuirudia tena njia ya kweli yako
W. Twakuomba utusikie

3. Utuwezeshe sisi sote waamini wako tutembee siku zote katika nuru ya kweli yako na sheria zako
W. Twakuomba utusikie

4. Utuangazie akili ya mioyo yetu tuchague daima yale yanayakupendeza
W. Twakuomba utusikie

5. Uwape mwanga wako viongozi wetu wa dini na serikali, wapate kutuongoza kwa hekima na uchaji, wasisahau kamwe kwamba uwezo walionao unatoka kwa Mungu.
W. Twakuomba utusikie

6. Utupe mwanga wako tuwaone watu wote kama ndugu zetu. Tuishi kindugu na kusaidiana kindugu
W. Twakuomba utusikie

7. Ewe Roho Mtakatifu ndiwe mpatanishi wa mioyo,; tunakuomba uondoe udhalimu, uonevu, udanganyifu na maovu yote katika mioyo ya watu wote.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Yesu Bwana wetu, uliyesema “Pasipo Mimi hamuwezi kitu” umpeleke Roho Mtakatifu atuangaze akili zetu, tupate kufahamu mapenzi yako na kuyatimiza kwa imani na uchaji. Roho Mtakatifu atuongoze katika mambo yote, yeye anayeishi na kutawala nawe pamoja na Baba daima na milele.

W. Amina

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


NOVENA YA ROHO MTAKATIFU SIKU YA TISA, JUMAMOSI

ROHO MTAKATIFU ANATUPA MAPENDO

Maandiko Matakatifu yanatuambia ya kuwa, Roho Mtakatifu, Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ndiye Upendo katika Baba na Mwana. Upendo hujieneza. Naye Roho Mtakatifu aliye pendo lenyewe la Mungu, hupenda kujieneza na kujishirikisha nasi, na kuwasha ndani yetu moto wa mapendo yake.

Roho Mtakatifu ndiye mwenye kutakatifuza roho zetu kwa neema ya utakaso. Neema hiyo ni uzima wa Mungu, ndio huo upendo wa Mungu tunaoshirikishwa. Roho isiyo na neema ya utakaso imetengana na Mungu, haina uzima wake, haina upendo wake, kwa hiyo haiwezi pia kuwa na mapendo ya kweli ya jirani.

Ingawa tunaona ishara nyingi za watu kupendana kidugu hapa duniani, mapendo hayo si mapendo ya kweli wala si kamili kama hayatokani na neema ya utakaso rohoni mwa mtu. Kama hakuna neema ya utakaso ndani yetu, Mungu pia hayupo kati yetu.

Roho Mtakatifu anatuunganisha na Mungu katika upendo. Pasipo na mapendo hapana mapatano, hapana masikilizano wala mwungano. Watu wanaopendana wanaungana na kulingana katika fikra zao na nia zao. Roho Mtakatifu anayetutia mapendo rohoni na kutuwashia moto wa mapendo, ndiye anayetuwezesha kuwa na mawazo ya namna moja na nia moja.

Watu wanaopendana hupenda kukaa pamoja, kuishi pamoja na kusaidiana. Roho Mtakatifu aliye chanzo cha mapendo ya kweli hutuweka pamoja katika Kanisa lake. Hukaa ndani yetu, hukaa katika Kanisa na kuwasha moto wa mapendo yake ndani yetu. Roho Mtakatifu anatuwezesha kukaa kwa amani nyumbani, kazini na katika jumuiya zetu. Basi, tumwombe sasa Roho Mtakatifu atuongezee hayo mapendo yake ndani yetu.

1. Ewe Roho Mtakatifu, uwashe mioyoni mwetu moto wa mapendo yako, tupate kuwapenda jirani zetu kama tunavyotaka kupendwa nao.
W. Twakuomba utusikie

2. Udumishe ndani yetu neema hiyo ya mapendo yako, tuwezeshe kuishi kwa amani leo na siku zote za maisha yetu.
W. Twakuomba utusikie

3. Utujalie neema na nguvu za kutekeleza mema yote tunayokusudia kuyatenda siku hii ya leo
W. Twakuomba utusikie

4. Uongoze nia zetu na maazimio yetu, yalingane na juhudi zetu za kutaka kuleta mafanikio ya roho na mwili kati yetu
W. Twakuomba utusikie

5. Utubariki, ili baada ya maombi haya, tuwe na juhudi ya kutimiza vema zaidi wajibu wetu wa kikristu kwa moyo mkuu
W. Twakuomba utusikie

6. Utuwezeshe kueneza mapendo na amani kati yetu na katika jumuiya zetu za kikristu
W. Twakuomba utusikie

7. Utuwezeshe kuwa kweli chachu ya wema na mapendano kati ya watu, ili nao wapate rehema zako kwa maombezi yetu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE;

Ee Mungu, tunakushukuru kwa neema ulizotujalia, hata tukaweza kuifanya ibada hii ya Novena takatifu mpaka mwisho. Utujalie mema yote tuliyoomba; utusaidie kutekeleza yote yale tuliyokusudia kutenda. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

W. Amina.

LITANIA YA ROHO MTAKATIFU … (soma hapo chini)


LITANIA YA ROHO MTAKATIFU

  • Bwana Utuhurumie………Utuhurumie
  • Kristu utuhurumie……..….Utuhurumie
  • Bwana utuhurumie….. Utuhurumie
  • Baba mweza wa vyote….. Utuhurumie

  • Yesu Mwana wa Pekee wa Baba na Mwokozi wa Dunia……..Utuokoe
  • Roho wa Baba na Mwana aunganishaye maisha ndani ya Baba na Mwana………….Ututakatifuze
  • Roho Mtakatifu……….Utusikie

  • Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana…………..Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Ahadi ya Mungu Baba……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Mionzi ya Mwanga kutoka Mbinguni……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Mwandishi wa vyote vilivyo vizuri……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Chanzo cha Maji ya Uzima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Moto utumikao daima……………… Njoo ndani ya mioyo yetu
  • Muungano Mtakatifu……………… Njoo ndani ya mioyo yetu

  • Roho wa ukweli na upendo……………………Utuhurumie
  • Roho wa hekima na elimu……………………Utuhurumie
  • Roho wa shauri na nguvu……………………Utuhurumie
  • Roho wa akili na neema ya kumtumikia Mungu……………………Utuhurumie
  • Roho wa neema na sala……………………Utuhurumie
  • Roho wa amani na subira……………………Utuhurumie
  • Roho wa usafi na uaminifu……………………Utuhurumie
  • Kitulizo cha Roho……………………Utuhurumie
  • Roho aletaye Utakatifu……………………Utuhurumie
  • Roho uongozaye Kanisa……………………Utuhurumie
  • Zawadi kutoka kwa Mungu juu Mbinguni……………………Utuhurumie
  • Roho ajazaye ulimwengu……………………Utuhurumie

  • Roho Mtakatifu…………………..tupe neema ya kuchukia dhambi
  • Roho Mtakatifu…………………..njoo ufanye upya sura ya ulimwengu
  • Roho Mtakatifu…………………..jaza roho zetu kwa mwanga wako
  • Roho Mtakatifu…………………..ifuraishe mioyo yetu kwa sheria yako
  • Roho Mtakatifu…………………..washa moto wa mapendo ndani yetu
  • Roho Mtakatifu…………………..jaza mioyo yetu na hazina ya neema yako
  • Roho Mtakatifu…………………..tufundishe kusali vyema
  • Roho Mtakatifu…………………..tuangaze kwa nguvu zako za Ki-Mungu zitupatiazo moyo wa kutenda daima yaliyo mema
  • Roho Mtakatifu…………………..tuongoze Kwenye njia ya wokovu
  • Roho Mtakatifu…………………..tuweze kufahamu yale ya muhimu tu
  • Roho Mtakatifu…………………..tupe hamu ya kuitafuta fadhila yako
  • Roho Mtakatifu…………………..tusaidie tuweze Kupata fadhila zote
  • Roho Mtakatifu…………………..tupe uvumilivu tuweze kutenda yaliyo mema tu.
  • Roho Mtakatifu…………………..tunaomba uwe zawadi ya uzima wetu

  • Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………….Tushushie Roho wako Mtakatifu
  • Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………….jaza mioyo yetu kwa mapaji yako ya Roho Mtakatifu
  • Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia…………….tupe roho ya hekima na neema ya kumsifu Mungu.
  • Njoo Roho Mtakatifu uzijaze roho za waumini wako uwashe moto wa mapendo yako ndani ya mioyo yetu (W)

TUOMBE

Ee Mungu Baba mwenye huruma tujalie Roho wako alete Mwanga kwetu ili apate kututakasa na kuingiza ndani ya mioyo yetu Baraka za kuweza kutenda yale yaliyo mema.
Tunaomba hayo kupitia kwa Mwanao Mpendwa Bwana wetu Yesu Kristo, anbaye anaishi na kutawala pamoja nawe katika Umoja wa Roho Mtakatifu. AMINA

Atukuzwe Baba…..x3

Shopping Cart
3
    3
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About